HAYATI SALOME MBATIA ANATARAJIWA KUZIKWA KESHO NYUMBANI KWAO MOSHI, MKOA WA KILIMANJARO, NA KWA MUJIBU WA RATIBA ILIYOTOLEWA, WAOMBOLEZAJI WA DAR WATATOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO NYUMBANI KWAKE MTAA WA UGANDA, OYSTERBAY, ASUBUHI HII KABLA SAFARI YA KUELEKEA KILIMANJARO HAIJAANZA MARA TU BAADA YA ZOEZI HILO KUKAMILIKA.
Home
Unlabelled
SALOME MBATIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Mungu akulaze mahali pema peponi mama. Huyu mama alikuwa mwadilifu na mwenye upendo. Si unaona hata alikuwa anatumia gari yake binafsi kwa sababu alikuwa kwenye campaign za NEC mabazo hazihusiani na majukumu yake ya kiserikali. Hii ni tofauti na mafisadi mengine ambayo bila aibu yanatumia rasilimali za serikali kwenye campaign za chama. Angekuwa anatumia gari yake ya serikali huenda airbags zingemnusuru, ila yote ni mipango ya mungu, siku yako ikifika hakuna kuchomoa.
ReplyDeletewww.makeroadssafe.org/
ReplyDeleteThis is a webiste for global campaign for road safety in the world. Tuangalia the way we can adapt it in our country. Parliamentarians please take note - opposition parties and NGOs and all the Michuzi Stakeholders. Also I have posted something to the wananchi website to request Mheshimiwa raisi avalie njuga hili tatizo kama HIV/AIDS CAMPAIGN. NTW
Michu tumuvuzishie picha za Oysterbay Msibani nyumbani kwa marehemu Salome Mbatia fasta plizzzzzzzzzzz
ReplyDeleteAhsante kwako weye uliyiandika hiyo website ya makeroadssafe.org. Bila glogu ya kaka Michuzi ningeipata wapi?? Be blessed
ReplyDeleteMama ninakulilia,
ReplyDeleteMungu kakukimbilia,
Sasa umetangulia,
Mema tunakusalia
Sifa nilizisikia,
Watu wakihadithia,
La sikufuatilia,
Undani kuulizia.
Jamii yaugulia,
Pengo lilisalia,
Waiombea familia,
Faraja kuijazia.
Hakika nafikiria,
Dira ulishikilia,
Katu hukuichia,
Chombo kikatulia
Tutakuenzi asilia,
Kwa zako nadharia,
Mema umetuachia,
Ni budi kushikilia.
Kubwa ya asilimia,
Utu wa kutojisikia,
Mungu alikujalia,
Sote twalishuhudia.
Baraka twakutakia,
Rabana wa mizania,
Ukweli anausikia
Sala ataitikia.
Kalale pema peponi
“Amen”