kuna mdau anaomba msaada wa kusaidiwa kuona mchemsho fulani katika hii picha. tarishi hauwawi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Kwenye hundi sehemu ya maandishi kumeandikwa "two hundred thousand" wakati kwenye sehemu ya namba kumeandikwa 300,000...kaazi kweli kweli kweli

    ReplyDelete
  2. Eti hyo ni jk, na hiyo hawala ya fedha ni ya kwake binafsi au ya huyo mdhungu?
    mh, mbona sielewi?

    ReplyDelete
  3. hawa jamaa hawajaenda shule,yaani hata kuandika check hawajui?Pili hii check imeandikwa kwa malipo ya scholarship fund(Pay to scholarship fun) na wala si kama madai ya Tanzania na uganda kama chanzo fulani(tz) cha habari kilivyosema.Sasa JK aliipokea hii check katika misingi gani?

    ReplyDelete
  4. E bwana hii kali si mbaya jamaa alitakiwa aandike 200 nyngine atie mfukoni akajisahau akakoroga mambo

    ReplyDelete
  5. unajua wanataka kutufanya sisi sote vihio! basi hata muheshimiwa nae hakuisoma au kusikiliza (maana lazima wakati anakabidhiwa yuko aliesema 'Hii hundi ya $ flani namkabidhi mtu flani' !)
    Haiwezekani jamani eeh, kumtenda hivi mwenzao!!!

    ReplyDelete
  6. Dah! Jamaa kapigwa changa la macho laiv!!!

    ReplyDelete
  7. Najua katika benki kibao , cheki ikikosewa hivyo, haikubaliki.
    Ukikosea hivyo na kumuingiza Raisi katika PR dizaini namna hiyo, hukawii kufukuzwa kazi na muajiri wako.
    Lakini kama aliyekosea kuandika ndio mfadhili mwenyewe, rahisi kusamehewa!

    ReplyDelete
  8. UZURI NI KWMABA HIO SI CHEQUE YA UKWELI UKWELI NI YA KUPIGIA PICHA TU

    ReplyDelete
  9. Rais wetu wa safari hii anasikitisha sana! Yaani hana kazi ya kufanya, mara kahudhuria sherehe ya chekechea, mara kaenda kupokea cheki! Sasa hiyo scholorship fund si angepokea waziri wa elimu ya juu tu! Yaani kama hajui, watu wanamtumia ili kujipatia umaarufu usiokuwa na maana! Na yeye yumo tu, as if hana kazi zingine za maana za kufanya! Huo muda anaupata wapi?

    Mbona nchi hii ina mambo mengi sana tu ya kutatuliwa jamani? Halafu wapinzani wanapanda chati haraka haraka sana katika kipindi hiki kifupi cha serikali ya awamu ya nne kwa sababu ya udhaifu wa serikali yeneyewe katika utendaji kazi! Eti mawaziri wanazunguka nchi nzima kuelezea "uzuri wa bajeti"...........Duh!

    ReplyDelete
  10. dah! hiyo balaa maana mbili na tatu hata hazifanani sielewi huyu alieandika cheki alikuwa anawaza kitu gani. tuwe makini washkaji.

    Thanx michu for the alert.

    ReplyDelete
  11. hapo JK kapatikana ikienda benki lazima ataambiwa RETURN IT TO THE DRAWER au YOUR CHEQUE IS DIISHONOURED la sivyo atapokea malipo yaliyoandikwa kwa MAANDISHI yaani dola laki mbili.Mjini shule bwana mpaka raisi kapelekwa chaka.

    ReplyDelete
  12. Payee nadhani ni sawa ni huo mfuko ulianzinshwa kwa ajili ya Ma-CEO's. Shida ni amount. Kama mimi JK wasaidizi wote, watu wa protocal wote wabadilishwe ofisi. Labda wapewe ofisi nyingine kama Bandarini.

    ReplyDelete
  13. Jamani mbona wazungu wamezidi KUMTAPELI raisi wetu? Ama wanadhani raisi wetu HAJUI KUSOMA au KILA KIKU ANAKICHUKULIA JUU JUU TU!

    ReplyDelete
  14. Duh, hata kwenye mikataba ya madini, huwa wanasaini bila kuisoma.

    ReplyDelete
  15. Matatizo ya kupeana kazi Ikulu kiushikaji badala ya uwezo.

    Hii picha inaidhalilisha nchi nzima.

    Rais gani huyu ambaye ana wasaidizi fake hivyo?

    Hivi mikataba ya madini kweli watu kama hawa wataisoma? Ndio maana tunafungwa bao kila siku kwenye madini.

    ReplyDelete
  16. Hii ndiyo hali ya benki nyingi lakini mie nadhani hapa kuna udalali fulani umefanyika haiwezekani tarakimu zitofautiane na maneno kazi kweli kweli nilipolisoma gazeti moja leo asubuhi baada ya kushtuliwa na jamaa yangu sikuamini macho yangu. eti naye Mheshimiwa hakuliona hilo hata jamaa wa usalama nao hawakulishtukia, kweli tunachezewa sana Wadanganyika

    ReplyDelete
  17. Yaani usanii anafanyiwa hadi Rais hii sasa kali, lakini mie nadhani kuna mtu amekula cha juu akasahau kurekebisha tarakimu zake na muda ukawa umekwisha hivi ina maana hata wapambe wa Rais hawajaliona hili kama yeye hakupitia kwanza cheki hiyo?? inaonesha ni namna gani tunavoishi katika nji ya Wadanganyika

    ReplyDelete
  18. naona hapo JK kapewa kanyaboya.

    ReplyDelete
  19. hii inaonyesha ni kiasi gani watz ni wakuburuzwa kuanzia gazi kuu hadi ndogo. hapo mkwere karizika kabisa kwani ashapata cha kudanganya kirudi hata kuangalia na kusoma maandishi hakua na muda. hivi jamani tutafika kweli???? misupu usiniweke kapuni na ww

    ReplyDelete
  20. INAONYESHA NI JINSI GANI TUNA UTAMADUNI WA KUTOKUJALI AMA KUTOKUFANYA HOMEWORK ZETU NA NI UZEMBE WA HALI YA JUU WA EXIM BANK. WATU WAO WA MASOKO WALIKUWA WAPI KOSA HILO LIKITOKEA NA BADO WAKARUHUSI BOSI WAO A POZE KWA PICHA NA MKUU WA NCHI? HIZI HELA ZA SCHOLARSHIP ZINAENDA KUWASAIDIA AKINA NANI? AMA NI KA-MRADI KA MKE WA MMOJA WA "MASHARE HOLDERS" WA AWAMU YA NNE??
    MICHUZI NAOMBA UPOST HII COMMENT

    ReplyDelete
  21. hahahahah...hawa watu waliwaomba wabongo wawatengenezee check na hela wamepewa...commission 100,000 wameshaondoka nayo. Mungu akawapiga kibao wakasahau kufuta....hahahah ...hilo ni big check namna hiyo wamekosea na hivyo vitabu vinabalance kweli tusivyoviona.........

    ReplyDelete
  22. Du!
    Bongo kweli kasheshe, yaani huyu Mzungu tulikuwa tunabeba nae maboksi hapa, akapotea ghafla.Hivi sasa mtu mkubwa Bongo!!1?Ama ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni.

    ReplyDelete
  23. Wandugu hivi mnajua kibenki amount iliyoandikwa kimaandishi ndio amaount halali? kwa hiyo inamaana mzungu amemetapeli JK kuwa anatoa laki tatu kumbe kitakacho tolewa ni lakimbili haki ya mungu mpaka dakika hii huyo jamaa wa PR hana kazi

    ReplyDelete
  24. Jamaa walitaka kupima uwezo na umakini wa viongozi wetu.Kama unaweza usitambue kosa lililoko kwenye cheki moja itakuaje katika mikataba yenye msuru wa namba kama wa BUZWAGI.Katika picha hii nimegundua mambo mawili.Viongozi wetu katika function nyingi wanakuwepo kama Formality hawajui kinachoendelea usubiri kusoma hotuba zilizoandaliwa mapema.Na kwa upande mwingine waandishi wetu wa habari hawawezi kumkosoa rais au kiongozi wa juu na CCM bali wa upinzani.Hapo wangelimwambia mtukufu rais cheki hii inamakosa!kukaa kwao kimya kunamwaibisha rais wetu .Hivi ndivyo nchi inavyoongozwa.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  25. aaa hii sasa too much ina maana waandaaji hawa kuangalia kabla hawajaifikisha mbele ya kadamnasi jamaniii....hii ndo inaonyesha jinsi ambavyo watu wengine hawako makini na kazi zao kweli

    ReplyDelete
  26. Kwa kawaida cheki kama hiyo haiwezi kulipwa kama itapelekwa benki. Itarudishwa kwa reason kwamba "amountin words and figures differs".Lakini sheria za benki zinaruhusu cheki hiyo inaweza kulipwa kwa kutumia amounts in words tu na siyo amount in figures

    ReplyDelete
  27. MTIKILA!!! Mtikila Baba uko wapi???

    Kuna Kesi hapa. Mtikila akiishtukia na anavopenda kesi basi lazima ale fungu la kutosha hapo.

    Mtikila;tafuta kipengele cha "kumdhihaki Raisi wa jamuhuri hadharani"

    Pia Bank wawajibishwe kwa huduma duni. Kimsingi cheque inakuwa na two signatories to make it worth. sasa hao wote pamoja na mwandishi wa hiyo hundi hawafai.Kwa hiyo Exim wako chini ya kiwango cha kuhudumia jamii.Tunataka fidia.

    Jamani mlioko Bongo plz mtafuteni Mtikila!

    ReplyDelete
  28. Naomba mpigaji wa picha hii apewe pongezi kwani aliligundua kosa hilo ndiyo maana hata viongozi hakuwafocus vizuri. Pamoja na kwa kuwa Ndugu yetu Michuzi uliwapamba sana kwa kufyatua jengo kubwa pale posta lakini usione haya kuwaambia waombe radhi walao kupitia tztimes kimya kimya. Kumbuka pilipili hata ikikauka inawasha!! Kesho mzee mzima atashtuka!!

    ReplyDelete
  29. Hakuna cha kushangaa katika nchi hii, kwamba viongozi wetu ni bongo lala!!!

    ReplyDelete
  30. Kweli hapa MTIKILA ameula!

    Kesi imesimama wima hiyo;
    "Raisi kudhalilishwa hadharani"
    "Exim Bank hawana sifa za kuhudumia"

    ReplyDelete
  31. Jamani hii cheque ni kichekesho cha hali ya juu... Watu wasoni mnamwita Rais wa nchi halafu mnafanya mambo ya kitoto namna hii???? Acheni hizo jamani

    ReplyDelete
  32. Kweli wemakosea - kiasi cha fedha kwa maandishi na tarakimu vinatofautiana. Mimi sioni kwamba hawajaenda shule kama mmoja wa wadau alivyohoji.

    Tunatakiwa tujifunze kuwa kwenye shughuli za uzito huu makosa kama hayo yanaonyesha labda wengi wetu hatuna umakini.

    LAZIMA MWAANDAAJI AWE NA CHECKLIST INAYOLENGA KUHAKIKI VIPENGELE VYOTE VIKO PROPER KABLA YA SHUGHULI.

    Hebu Imagine kama Balozi Cisco na waandaaji wenzake wangefanya makosa kama haya wakati wa ule mkutano mkubwa wa SADC miaka michache iliyopita.... yaani kibao cha nchi Kenya kiwekwe mbele ya Rais wa Malawi???

    ReplyDelete
  33. Baada ya kugundua kosa kumefanyika nini? Nauliza tu mana hiyo ni aibu kubwa.

    ReplyDelete
  34. Katika hilo hiyo benki waombe msamaha si kwa Rais tu, kwa Watanzania wote. Hicho kitendo kinamchafua Rais na Watanzania wote kwamba hatuko makini. Ndo maana baadhi ya annon wanakifananisha kitendo hicho na jinsi viongozi wetu wasivyosoma kwa umakini mikataba ya madini au masuala mengine hivyo kutuacha tukiendelea kunyonywa vibaya! Tuweni MAKINI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...