wadau nimeletewa huu mchongo sasa hivi. sasa kiinglishi changu kama mjuavyo kiko ugokoni. ila hayo masifulisifuli yananipa mshawasha pamoja na neno coca cola. naomba msaada kwenye tuta hili, mnitafsirie na kunipa ushauri nifanyeje...

coca-cola-promo <lott_info01@bellsouth.net>
13:50 (5 minutes ago)
ATTENTION WINNER

This is to inform you that you have been selected for a cash prize of £1,000,000(One million, pounds sterling) in cash.held on the 18th november,2007 in Ireland.
The selection process was carried out through random selection in Our computerized email selection system (ess) from a database of over 250,000 email Addresses drawn from which you were selected. Contact our fiduciary agent for claims with:

Name: Mr. Kenneth Smith,
Email:mr_kenneth_smith02@hotmail.com
Fill the below:1. Name: 2. Address 3. Marital Status: 4. Occupation: 5. Age:6. Sex: 7. Nationality: 8. Country of Residence: 9. Telephone Number:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Michuzi,

    Mimi nakaa Ireland, na habari hizi sijazisikia/au kuziona, kwenye local news au media za hapa.

    Kwa hiyo huo ni utapeli. na kama sivyo, nikisikia umetangazwa mshindi nitakujulisha.

    Hata hivyo, Ireland wanatumia Euro na siyo English Pounds, kama itakua ni Northen Ireland, hilo litakua swala jingine, and I am definitely would advice you to keep you dreams alive. NEVER say NEVER.

    Ha ha ha..

    ReplyDelete
  2. Hello Michuzi,
    Hao ni wezi wakubwa, wanachotaka ni kupata data zako za uhakika, na baadae wanakuibia, watataka wapate jina lako na taarifa zako muhimu kama jina, kazi, vitambulisho vyako, na baada ya hapo watakueleza uwape akaunt namb yako na iwe na kiasi fulani cha pesa ili wakutumie hizo pesa na baada ya hapo wanakuibia, na wao watakuelekeza kwamba hizo pesa zipo katika akaunti fulani, na ukiiangalia katika mtandao ni kweli utaiona, lakini ukweli wa mambo hicho kitu hakipo.

    Pia hata kama hawatafanikiwa kukuibia pesa, lakini wakipata taarifa zako kamili hawa watu wanaweza kuzitumia kufanya uhalifu, hivyo wanaweza kufanya wizi kwa jina lako, au ugaidi kwa jina lako na usishangae siku moja utajikuta upo matatizoni kwa kosa ambalo hujalifanya. hawa ni watu hatari sana, ndugu yangu.

    unajua hakuna kampuni inayoweza kufanya kitu kama hicho hasa kama hujawahi kushiriki katika bahati nasibu kama hizo, hawawezi kufanya kitu kama hicho, na pia haya makampuni yanayochezesha bahati nasibu huwa hawafanyi mawasiliano na wateja kwa kutumia email, pia hawawezi kukutajia kiwango ulichoshinda mapema hivyo tena kwa email. hao jamaa wapo tu wametulia zao hotelini au kijiweni wanafanya mambo kama hayo. yaani hupaswi hata kuwajibu email yao.

    Halafu uliona wapi mfanyakazi wa kampuni kubwa anatumia anwani kama hiyo hotmail.com kwa mawasiliano ya kiofisi? hakuna kitu kama hicho, kwani hata akina sisi anwani zetu za ofisi hatuzitumii kwa kila jambo.

    remmygama@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. Heee kuwa macho. ikifikia wakati watakuomba credit card,tia mbano.watakuibia

    ReplyDelete
  4. Michuzi,

    Hii ni ujanja ambao unatumika miaka mingi sana kuwaibia hela watu ambao ni maskini na wana tamaa ya kupata hela haraka haraka na wanapenda sana kuwatafuta watu wenye majina yanayotoka nchi maskini kama Africa,Asia na ata America na Ulaya kwenyewe,kitu watakacho kufanyia ni kwenda na wewe sambamba kwa emails watakuomba iki mara kile,watakupa document hii mara ile lakini mwisho wa siku watakuomba hela kwa jina lolote like fee ya processing or consultation etc ambayo huwa mara nyingi ni from 100$ onwards na ukisha wapa ndo hutowasikia tena!!!!!wao biashara yao wanalenga millions of desperate people sasa we zidisha dollar mia moja mara elfu kadhaa ni hela nyingi sana....mi mwenyewe binafsi walinitumia na tulipofika kwenye mshiko nikawaambia kateni kwenye iyo million niliyoshinda then nitumieni changu wakagoma eti hawana iyo ruksa na hawawezi gusa hela zangu,pili walitaka niwatumie kwa njia ya western union na mi nikawabana kwanini hamtaki tutumie benki wakashindwa majibu ya akili,c unajua western union huwezi kum trace...so wewe kula nao sahani mola kama unapenda kupata jua janja yao itaishia wapi and let us know...ICT

    ReplyDelete
  5. kwahiyo michu umeamua kutuonyesha kuwa upo kwenye list ya wabongo wenye bahati ya kufunga mwaka. hongera kama ni kweli

    ReplyDelete
  6. MMMMMHHHHHHHH
    I'm sure hawa ni POPOZZZZZZ!(NIGERIANS.)
    Ni uwongo tu hamna ishu kaka michuzi, wanataka kujua Bank details zako waibe pesa zako zoteeeeee.

    Hata mm nazipataga emails kama hizi, ni MATAPELI TU. Dont try to give them your Bank details! dont ever

    Dada T

    ReplyDelete
  7. Kwa kukusaidia nenda kwenye link hii
    http://www.sophos.com/pressoffice/news/articles/2006/06/colascam.html

    Nadhani hii yote ni ule muendelezo wa utapeli. Hakuna vya bure ndugu yangu!! Kuweni waangalifu.

    ReplyDelete
  8. Ndugu yangu Michuzi huu ni mchezo wa matapeli, wala hiyo cocacola haihusiki. Jiulize mwenyewe, hiyo bahati nasibu ya kukupatia pauni milioni moja (bil 2 ya kwetu) bila kuchangia chochote katika kununua tiketi, itashuka kutoka mbinguni? Hizo hela za kuwalipa washindi watakuwa wanazitoa wapi?

    Hawa ni matapeli, hapo wanakusanya taarifa zako, na kitakachofuata watakuambia uwatumie details za akaunti yako ya benki, kisha wanakomba kila senti iliyomo humo! Njia nyingine ni kukudanganya utume kiasi fulani cha hela ili kushughulikia malipo yako, sasa wakikutajia pauni 10,000 utaona ni asilimia 1 tu ya pesa unayotarajia kupata, kwa hiyo it is worth it! Ukituma hizo ndo zimekwenda hivyo! Wengi wamelizwa na hawa jamaa.

    Ushauri ni kwamba mtu yeyote akipata email ya namna hii, uamuzi wa kuchukua ni kuifuta mara, wala usihangaike kuijibu.

    Asante ndugu Michuzi.

    B.J.Y Kithuku

    ReplyDelete
  9. Kaka Michuzi, kwa maoni yangu, nafikiri ni SCAM. Kitakacho fuata, watataka information yako kisha waitumie kwa manufaa yao. Ushauri wangu: Proceed with caution.

    ReplyDelete
  10. Kaka Michuzi, kwa maoni yangu, nafikiri ni SCAM. Kitakacho fuata, watataka information yako kisha waitumie kwa manufaa yao. Ushauri wangu: Proceed with caution.

    ReplyDelete
  11. Duhhhhhhhh!! Aisee Michuzi naona washindi wa "Sindano ya coca cola" tumefungana hapa. Maana hata na mimi nimepata email kama hiyo, yenye maelezo yanayofanana kabisa!! Sasa tumpigie simu basi huyo Mr. Smith ili tupate hayo mamilioni na kumpiga bao RICHARD!!LOL!!!
    Yaani hawa matapeli wana fikiri watu wamelala kabisa!

    ReplyDelete
  12. Kuwa mwangalifu maana hao ni wanigeria ni hatari sana wanweza kuzama kweneye mifukop yako na kukandamiza mafweza yote uliyonayo so kuwa mwangalifu.

    ReplyDelete
  13. mgosi kuwa mwangalifu ni utapeli hou hat hapa msufini jamaa mmoja kalizwa hivyo hivyo.take care bro!!! "Dunia hii cha bure kafariki, kabaki .....kazi kwako mgosi.

    ReplyDelete
  14. Habari yako. Mimi nilikua nasoma lile ombi lako pale kwa Issa michuzi. Ile Email nadhani imejia njia ya Inbox yako. Lakini ngoja nikwambie wanasemaje kisha nikwambie kuhusu mambo hayo. Wanasema umeshinda one million pounds in cash, ambayo mchezo huo ulichezwa leo hii na wewe ukawa mshindi katika draw yao hiyo. Kwa hiyo wewe umeshinda sababu walikua na email yako wakachanga mpaka wewe ukatokea mshindaji. Sasa wanataka wewe uwandikie email uwatumie jina lako, address yako, wanataka kujua kama umeowa ama umeolewa (sijui gender yako), wanataka kujua kama wewe ni male au female, wataka jua kazi ufanyayo, wanataka age,wanataka kujua wewe mtu wa wapi, wanataka jua jinsia yako, unaishi wapi na simu yako. Sasa mie nakwambia hivi ukiwatumia hivi vyoote ndugu yangu umeula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua. Sasa ngoja nikueleze

    Hawa watu wanao kutumia mambo hayo ni wanageria. Wapo kila nchi wana ibia watu na emails zao za kusema umeshinda. Ni hivi wanakutumia email (nimepata emails kama 100 so far) wanasema umeshind akitu flani na wanataka uwape contact wao ili wakupe info nyingine ambayo si yakweli. Ukishawapa numeber yako na hayo yoote walio kueleza basi wewe jua huyo ishi kwa privacy sababu hawa watu ni wezi na wanakusanya info nyingi tuu kwa watu kama wewe. Sasa wakipata info zako wanaweza kueka online watu wazione au wanaweza tumia jina lako na email yako na info zako nyingine zoooote wawe wanafanya mchezo wa kutumia watu email kuwambia wameshinda. Ama laa wanaweza kukupigia simu wanataka uwape bank account number yako ili wakuekee hizo hela. Sasa here is the catch, wao hawaeki hela bali wanachukua hela zilizo kwenye account yako. Hiyo ndo kazi yao. Hao ni nagerian people wanao fanya hivo hadi kwenye news huku majuu walikuepo. Kazi yako ni kuwaongopea watu. Na mie ilishanitoke waliniambia nimeshinda 3 million us dollars. Sasa mie nikawa najibishana nao back to back nawauliza wamepata vp info zangu na kila kitu changu. Nikawambia siwezi kuwapa kitu changu chochote adi waongee na lawyer wangu na pia waongee na polisi. Basi walinijibu na " We're sorry we wont bother u again". Nikawauliza why r u sorry when i wan claim my price fairly. Basi hiyo ndo ilikua email yao ya mwisho sababu wanajua ilikua uongo na kama ninge involve polisi basi wangekamatwa. Mimi nakwambia hivi sababu yashatutokea sie huku, saa nyingine wana fake kuhusu mtu kufa na jina lako. Mfano we jina lako ni Yusuf alafu kuna mtu mwingine anaitwa Yusuf amefariki ameacha mali (fake ones remember its fraud), basi watakutumia email na kama sio makini unawapa info zako wanakupigia simu basi wanakwambia uwape bank info watakuekea hela. Nakwambia kama haupo makini utachukuliwa hela zako na jela utaenda sababu polisi hawajali hayo watakuliza kwa nini usinge piga simu polisi ? Kua makini sana na vitu kama hivi ndugu yangu. Hawa watu wanatafuta adi na ma FBI . Wapo kila dunia,nchi,mkoa. Wamejaa tele kuwaibia watu kama nyie. Basi ukipata email kama hii usichukulie kweli sababu ni wezi na tena ni watu wa NIGERIA HAO kua makini nao. adi kwenye news walikuepooooo. Usiwape INFO zako zozote nakwambia. Basi kama unaona mie muongo natunga haya yoote. Kaa ufikirie lakini mwisho usije lia kilio.

    ReplyDelete
  15. Michuzi mi naomba uachane na hawa matapeli kabisa. Yaani inakuwaje mtu mwenye dhamana kubwa hivyo kutoka kwenye conglomerate kama Coca Cola ana tumia yahoo address kwa ajili ya official correspondences. Mimi unaniboa sana ukiweka vitu kama hivi maana vinatupotezea muda tu. Please brother!

    ReplyDelete
  16. Umeliwa kinoma wapopo hawo. Kwani ulicheza bahati nasibu.

    ReplyDelete
  17. we michuzi unachokoza uone tutasema nini! Lkn nijuavyo mimi usilogwe ukatoa detail zako utajuta! watakusumbua na hiyo namba ya simu uliyowapa,pili wataingilia na kuikorofisha namba yako endapo hutakubaliana nao kile watakachokuambia (sijui ni nini ila usijaribu na wala yeyote usomaye msg hii)tatu utaombwa kutoa pesa kidogo ili kuwezesha upatikanaji wa huo mshiko na ndio utapeli!
    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  18. Sikupi tafsiri, ila ninachotaka kukuambia, these are POPOZ, ha ha ha ha. Unajua who are popoz?

    Jaribu wasiliana nao uone utakavyolizwa.

    ReplyDelete
  19. CHANGA LA MACHO HILO !!

    ALSO CHECK FOLLOWING HUMOROUS PAGE

    http://j-walk.com/other/conf/index.htm

    ReplyDelete
  20. aaaa kaka hawa ni matapeli wala usiwajibu. mwisho wa yote watakwambia wewe uwalipe ili washughulikie malipo yako!

    ReplyDelete
  21. coca wanafanya open promotions na wanatoa post ads kabla ya promo zao kwa maana hiyo huo mtungo hapo ni fekiiiiiiiiiiiiiii,usipoteze muda wako hao ni wanaigeria matepeli waloshindikana dunia nzima

    ReplyDelete
  22. Michuzi husiingie kichwa kichwa hiyo ni "scam" au utapeli hiyo email address ukkiangalia vizuri inajionyesha kuwa ni typical kama matapeli wengi wanavyofanya. Mimi ni mtaalam wa "cyber fraud prevention" niko ughaibuni naktahadharisha husiingie kichwa kichwa...

    Mengi tutwasiliana nikirudi Bongoland... Lazima nikutafute mshikaji.

    ReplyDelete
  23. Hata miye nilitumiwa email kama hiyo last week. Baada ya kuishtukia, niliamua kuifuta. So please bro Michu, hawa jamaa ni POPOZ, achana nao!!!!! watakuliza yakhe.

    ReplyDelete
  24. Cha Muhimu kwa wa Tanganyika na Wa Zanzibar wote hakuna msosi wa bure hapa duniani "NO FREE LUNCH" kwa hiyo huu ulimwengu wa utandawazi na TEKNOHAMA ukiona free seminar,scholarhip,bursary etc tafakuri mara mia kabla ya kufanya maamuzi.

    Mfano hiyo email tayari imewaliza watu wengi na wameshalipo kuwa ni SCAM.
    Bofya hii link kwa darasa zaidi
    http://lottoscams.blogspot.com/2007/08/contact-mr-kenneth-smith.html

    ReplyDelete
  25. Ebana Huo ni Uzushi, achana nao, Utaumia bureeeee....ila wape address ya pale mwananyamala kwa kopa waseme nayo,

    BooSt3D

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...