oyaaa...mjomba mbona unaturuka???

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Duuh hii kizamani kweli siku hizi mtu plate wali maua.

    ReplyDelete
  2. Hayo mamabo yenu ya wali maua zungumzia huko kwenu Tabata, Mbezi Beach, Masaki, Sinza labda.

    Sie kwetu tuachieni na masania yetu ya pilau. Hivi unafikiri hiyo ni shughuli ya kualikwa kwa kadi mpaka ujue ni sahani ngapi utapika au utagawa kama shughuli zenu za kichoyo za uzunguni?

    Hapo mguu wako tu na mkono wako nawa ule, sahani utaweka ngapi? Na hapo kila mtu anakuja mpaka kibaka, wakati mwingine hata hayo masinia yenyewe yanaidisapia.

    Peleka mambo ya uzungu uzunguni tuachieni tartibu zetu za kujichana bila kubaguana.Upooo!!

    Mswahili!

    ReplyDelete
  3. Mambo tambarrraaarrreeeeee....

    ReplyDelete
  4. Duh hii ni noma inanikumbushia nilipokuwa Bongo mtaani kwetu Mwananyamala kukiwa na hitma,harusi au msiba sehemu watu walikuwa wakialikana na pozi hizo zilikukuwa kawaida kabisa.

    ReplyDelete
  5. Yap!! hii bomba sana, siku hizi watu hawana ushirikiano na wachoyo, hata shughuli kama hizi wanatoa kadi!!!??? zamani tulikuwa twataarifiana mtaa mzima na mitaa ya jirani hata washkaji wa mbali, unakuja na ndizi yako mbivu ya kushushia!! Shaba tatu au nne mnajichana na kubeba.

    ReplyDelete
  6. Du washikaji kweli wali waliwa.

    ReplyDelete
  7. Duuh sura zao zimedata kusubiri wali wa bure!!halafu mwasema turudi bongo? sirudi wacha nibebe mabox yangu kujichana mabugger kwa sanaaaa. Ha ha haa..eti bongo TAMBARAREEEE.. mnacheza

    ReplyDelete
  8. we anony hapo juu unaigiza wa mwananyamala jongo kweli!nimekudetect nimeona post iliandikwa saa moja na dakika thelathini na moja, na upo tz, mbona wengine mnapenda sana kuwaiga wabeba boksi?tutawageuza keyboard!wabonyezwa mwaka mzima!

    ReplyDelete
  9. Kwanza Muandazi anatangaza "Waungwana watatu watatu na Watwana Watano watano"

    Pili sinia zinpita kweda kwa Waungwana kwanza (si unaona jamaa mwenye Tshirt la mistari anavyomeza mate)

    Tatu zinakwenda kwa watwana hapo sinia ikishuka tuu hukuti nyama vidole vina Auto search.
    Watu huja na pilipili, Tomato Source kwenye kifuko, Ndimu na Ndizi kabisa...

    Hehehehe hii kali kaka.

    ReplyDelete
  10. mswahili elewa hapo mmoja akiwa na ugonjwa wa kuambukiza,banda lote la kuku linateketea

    ReplyDelete
  11. Duh hii kali ...inanikumbusha masinia ya pilauz huko Tanga- pangani na bweni enzi zetu tukisoma Boza.... akina msingapore....petertosh....galusi....kasix...akina window...chilewaz...kamna....nk cjui washkaji mpo wapi?? tulikuwa tunakula na kubeba kwenye majumu, mashati.....kaaaazikwelikweli

    ReplyDelete
  12. hawa jamaa wa bongo wanaotuita wabeba box ni wivu tuu unawasumbua na wanatamani sana kiwanja ila basi tuu uwezo hawana,na box sijui maana yake nini? wanafikiri kila mtu ni kubeba box tuu na hata kama unabeba box hawajui kama ni kazi tuu na unalipwa vizuri kuliko CEO wa bongo....acheni wivu utawaua na njaa zenu ,na kila siku kazi kupiga mizinga tuu kwenye email,eti mshikaji nisaidie dola ishirini nimepungukiwa,hatuna roho mbaya tutasaidia sana tunajua mna njaa sana,ila acheni wivu,sisi tunaendelea kutesa huku kwa sana na maneno yenu ni kumpigia mbuzi gitaa tuu,tutawaona tukija vacation

    ReplyDelete
  13. Baaaaaaaaaaaab kubwa...hiyo ndiyo yenyewe...

    Hapo ni mwendo wa kujisongeza na ndizi mbivu na kapilipili...

    Ndio kwetu ndio kwetu...asikwambie mtu...kwetu hatuna mambo ya INVITESHENI KADI...mguu wako tu...

    ReplyDelete
  14. Haya mambo tuulizeni sisi watoto wa uswazi kule kule kunako, hapo tunajuana kwamba ukikaa na fulani sinia moja umeumia lazima utoke hujashiba, hii imetulia sana

    ReplyDelete
  15. wee any. wa 6:33, mambo ya wabeba mabox hapa yamekujaje?
    Watu wanazungumzia msosi wewe unaleta frustration zako za kubeba maboksi hapa? Jamani mbona hii mambo ya maboksi kila mahali ukiingia hata pasipokuwa na hiyo mada watu wanaileta.

    Mimi nahisi hiyo ni dalili ya kutoa kinachomsibu mtu kumoyo, sasa watu wanajadili na kukumbuka mambo ya shughuli zetu za uswahilini wewe unaleta manung'uniko yako ya maboxi? Yanahusianaje?

    Halafu usifikiri kukaa ulaya ni utajiri au kukaa uswahilini ni umaskini. Watu wametoka uswahilini na wako majuu na wanasafiri kuliko wewe unayejidai. Mwenye nazo hajigambi wala humsikii ila sie tunaozishikashikaa??!!

    Bwana hapo umetukumbusha mbali kweli na huyo anayesema kuambikazana maradhi umekula wee utotono kwako mbona mpaka leo umzima na hukuambukizwa maradhi yoyote. Kula kwenye siniaambako kila mtu anakula kwa mkono wake ni maradhi lakini kunywa kwenye chupa moja ya wine watu kibao sio maradhi. Na ku.... basi naishia hapa nimekuwa sensored.

    Ndio jadi yetu shughuli mguu wako na hatumuombi mtu mchango pamoja na umaskini wetu, nyie matajiri wa meza na masahani mpaka watu wachangie ndio shughuli iwe na asiye changa haruhusiwi kutia mguu wake. Tena sahani moja yenye kijiko kimoja cha wali vinjegere, kiazi kimoja kipande kimoja cha nyama na kipapatikio cha kuku mnamuuzia mtu elfu kumi (chini ya elfu kumi hupewi kadi)

    Njooni muone ukarimu wa kiswahili!!

    Mswahili

    ReplyDelete
  16. Du huyo mkambungu mwenye shati flana nyeusi na nistari meupe katoa mimacho utafikili hajala miaka kumi au kama anataka kumlukia huyo mjomba aliyebeba sahani!Michuzi hii ishu ilikuwa wapi? na nini kilitokea nikiwa na maana harusi,matanga,kipaimala,au ninini? Maana inaonekana hiyo timu iliyokuwepo hapo sio mchezo da!huyo mwandaaji anaonekana kaharibu pesa nyingi kulisha masela lakini poa waswahili wanaamini ni thawabu kwa Mungu ata kama ukilisha then unanasa poa tu thawabu!!!!!hao wajomba mstari utafikili wanasubilia kukatwa majando!!!!

    ReplyDelete
  17. hEEEEWAAAAAAA!! Yap ustaadh hii imenikumbusha sana Tanga(Kisoso, Chumbageni) enzi za maulidi. yaaa, huko ndo uswaz!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...