AISEE BROTHER MICHUZI NAOMBA KUWAKILISHA HOJA HII KWA WADAU WOTE WA BLOG YETU YA JAMII ILI WATOWE MAWAZO YAO.

HOJA NI KWAMBA, LEO HII SERIKALI KUPITIA KWA WAZIRI WAKE MHESHIMIWA A. CHENGE AMEKARIRIWA NA VYOMBO VYA HABARI AKISEMA “ SERIKALI ITAWAPATIA KIFUTA MACHOZI MAHUJAJI WALIOKWAMA HAPO DAR KWA NIA YA KUPUNGUZA AU KUPOOZA GHARAMA WALIZO INGIA KUTOKANA NA KUCHELEWESHEWA SAFARI YAO NA ATCL”.

HAPO MIMI NIMESHINDWA KUELEWA JAMBO MOJA NALO NI HIVI NI NANI HASWA ANAWAJIBIKA KULIPIA AU KUFIDIA HASARA HIYO YA MAHUJAJI ? NI SERIKALI KUPITIA WAZIRI CHENGE KAMA ALIVYOELEZA, AU SERIKALI KUPITIA SHIRIKA LA NDEGE LA ATCL? MIMI NAONA SERIKALI KUPITIA WIZARA ZAKE IMESHAMALIZA JUKUMU LAO NA HILO WANALOTAKA KULIBEBA NAFIKIRI HALIWAHUSU NA BADALA YAKE WAIACHIE ATCL. AU WADAU MNAIONAJE HIYO???

NI MIMI MDAU TOKA UGHAIBUNI CANADA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. you are right mdau wa canada, the government has nothing to do with it so far, since they flew safely, but the one responsible for their refunding is none other than shirika la ndege. maybe the government just wants to look good, but whose money are they going to use if not our taxes!! wawaachie hao shirika la ndege, they can as well help ´build schools with that money.

    ReplyDelete
  2. ATC ni kampuni ambayo ni LTD.inayosimama kwa kujitegemea.Kwa nini ATC isiwajibike? Chenge ni mwanashera anajua anachosema.Lakini uzuri si mwanasheria peke yake nchi na wanasheria wengine pia tunajua anachosema na kwa nini angependa serikali ilipe ili ionekane moja kwa moja serikali ni mhusika mkuu kwenye hilo sakata badala ya ATC

    Naona kuna ujanja hapo.

    Chenge anataka aiingize serikali kusudi waislamu waishtaki serikali na siyo ATC.Wakiishtaki serikali na kuidai mabilioni basi Mawakili watachota mabilioni toka serikalini ili kuitetea ATC.Inawezekana pengine kuna mawakili wameshapangwa tayari ili wachote hela za walipa kodi kiulaini.Na hii ya kuiingiza Serikalli ni kitendo cha makusudi cha kufikia azma hiyo.Ukiishitaki serikali lazima ilipe wote mahujaji na mawakili.Atakayeumia ni mlipa kodi shauri yake.

    Lakini kuna minong`ono kuwa Chenge na Mwenyekiti wa Bodi ya ATC walihusika moja kwa moja katika hilo.Kuna minong`ono kuwa kulikuwa na maslahi katika kukodi ndege nje ya nchi watu walikuwa wanataka waponee hapo kwenye kukodi bahati mbaya bomu likafyatuka.Sasa sijui ni nani alitaka kuponea hapo je Ni Chenge,Mwenyekiti wa Bodi Nnyang`anyi au Mataka mkurugenzi wa ATC au ni nani ukweli UTAJULIKANA TU.

    ATC ndiyo ilitakiwa iwajibike.Maana ni shirika LTD.
    Chenge ni mwanasheria kuna mahali analenga hizo semi zake za kuitaja serikali kama mlipa fidia badala ya ATC si bure zinalenga mahali.

    KIKWETE KAZI UNAYO.

    ReplyDelete
  3. Wazo la jamaa huyu hapo juu ni zito sana kwa maslahi ya tz yetu
    Mtoa hoja elewa kuwa ktk nchi inayofata Unicameral legislature kama hii TZ suala la kidini na gharama zake haiihusu hata kidogo serikali
    suala la dini kwa nchi un religious allign kama TZ suala la kuhijj na gharama zake wanaachiwa waliopewa tenda na dini husika,serikali haipo hapo
    Chenge elewa kuwa ukiwalipa gharama watu hawa,nao Roma Catholic walipwe kwani hata nao wanakwenda kuhijj huko Vatican na huwa hata wao wanahangaishwa sana na usafiri,kama tu waislam hawa!
    Chenge ajue kuwa,watz sasa sio wapuuzi kama anavyofikiri,na wanajua kuwa hapo kuna mkono wa mzee JK,lkn he has to be smart to swim on strong current winds as that as we're Tanzanians we notice
    ACHENI UDINI

    ReplyDelete
  4. Labda tuulize nani ni mwenye hilo shirika? Who is the owner of ATCL, hapo ndipo huwezi kuchanganyikiwa kuhusu serikali kulipa gharama.

    Angalia Mashirika yote ambayo bado yanamilikiwa na Serikali, mfano Tanesco. Je hujawahi kusikia serikali kuingilia kati hapo mara kadhaa ima kwa kutoa ruzuku au kwa kuiingiza tanesco kwenye mikataba.

    Hivyo hakuna cha ajabu hapo kwa mwenye chake kukiendesha atakavyo. Kumbuka na ATCL nao wanadai fidia kule walikokodi ndege ya kwanza ambako haikuja siku waliyopanga safari iwe. Kwa mfano ingekuwa wewe Mdau wa Canada ATCL ni shirika lako unalimiki 100% ungefanyaje? Ungesubiri waende Mahakamani wakadai fidia ambayo itaamuliwa na Mahakama au?

    ReplyDelete
  5. NAUNGA MKONO HOJA YAKO ASILIMIA MIA KWA MIA!!!

    ReplyDelete
  6. kATIKA KUCHANGIA HII MAADA NADHANI WAZIRI CHENGE YUPO SAWA KWA SABABU HIYO NDIO WIZARA MAMA NA ANAJARIBU KUEPUSHA OTHER CIVIL CHARGES KUTOKA KWA MAHUJAJI KISHERIA MAHUJAJI WAKILETA ANY CLAIMS LAZIMA IPITE KWANI NI KWELI WAMELIPA NAULI KAMA ATCL WAYOWAAMBIA NA NI ATCL NDIO WALIOSABABISHA HUO USUMBUFU WEWE MWENYEWE UTAFAHAMU SHUSHULI NA COST YA CIVIL CHARGES HATA HUKU NJE KAMA PROBLEM IMETOKEA NOT YOUR FAULT YOUR ENTITLED FOR COMPENSATION NASASA WAKIWAACHIA ATCL MEANS KAMPUNI BASI TENA NA HIZO TUNDEGE TWAO CHA MWAKA 47

    ReplyDelete
  7. Mdau wa Canada, nashukuru kwa hoja yako nzuri uliyoitoa yenye kuhitaji upembuzi yakinifu.Nadhani kabla ya kuzama ndani ya hoja ni vyema ukachanganua Serikali ni nani na ATCL ni nani.Je Serikali ina hisa ngapi katika ATCL.What is the role of the government on the Public Company like ATCL.

    Who is directing and controlling the ATCL,mbali ya hapo inatakiwa pia kuangalia kwa kina sheria iliyoinzanisha ATCL inasemaje katika mgawanyo wa mamlaka ya kiutendaji.Inawezekana ikawa ni joint contributions from Government,ATCL na waliokuwa wanahusika na utoaji wa vibali na ndege pia,lakini serikali ndiyo msemaji mkuu.

    Mimi nadhani bado serikali ni mdau mkuu wa ATCL,ni suala lillitokea pale linahusu pia ITIFAKI ya hali ya juu kwani linapita nje ya mipaka ya Tanzania na linajumuisha wananchi wa nje ya Tanzania,kwani kuna mahujaji wengine walikuwa wanatokea nje ya Tanzania.


    Tatu nadhani pia watu walikuwa wanapaswa kuondoka huenda kuna baadhi ya matukio muhimu kwenye ibada yao waliyakosa ama watayakosa,hivyo inabidi serikali kama ndiye mhimili mkuu iweze kwafidia kwqa usumbufu huo.


    Labda suala kuu ni kwamba what is the expected value of compensation, which formula will be used to compensate the affected part, this will be main obstacle, labda watawalipa substance allowance base on delay and make the standard cost of meals: Breakfast, Lunch and Supper!!

    Ila kwa swali kuu la hoja hii nadhani Chenge yuko sahihi kabisa,ingawaje sasa wanatakiwa wawe fair kwenye kutoa maamuzi kama haya,siyo wafanye kwa kumfurahisha mtu ama jamii fulani tu,maana naona kwenye msafara kulikuwa na familia inayotoka kwenye nasaba yenye mamalaka nadani ya nchi

    ReplyDelete
  8. Hata ikilipia serikali au atcl ni kitu kilex2 kwa sababu hizo zote ni pesa za mlalahoi ndio zina chezewa. Mishirika yenyewe inajiendesha kihasarahasara na kishkaji unadhani hapo kuna chochote cha maana.
    Hiyo atcl ni njia tu inayotumika kuhamisha pesa za umma kuzipeleka kwenye matumbo ya walafi. Hao mahujaji wametumiwa kama chambo tu.
    Kwa muda mrefu sasa kumekuwa hakuna kisingizio cha kutoroshea pesa za umma kwenda matumboni mwa wachache.
    Ilimradi sasa kisingizio kishapatikana sasa kazi kwenu kufuja!sisi walalahoi yetu macho.

    ReplyDelete
  9. Hii yote ni uoga na unafiki tu, kujaribu kupoza mambo kutokana na ukweli kwamba walioguswa ni sehemu ya jamii za kidini kubwa nchini tena zenye kelele, la msingi ni serikali kuwa makini kwa huduma zake kwa jumla na kuhakikisha uwajibikaji ambao ungeanzia kwa waziri husika ili wengine waone mfano. Mbona abiria wa kawaida(walalahoi)wanapokwamwa kwenye stesheni za treni bila chakula na hali mbaya ya mazigira hamna hata kiongozi (hata mwenyekiti wa mtaa)anayekwenda kuwapa pole achilia hilo la kuwapa kifuta machozi, haya yote ni matunda ya tawala mbovu tunazozidi kuziendekeza.

    ReplyDelete
  10. Michuzi, huyu jamaa hajui uhusiano kati ya ATCL na Wizara ya Chenge, na hili ndio limekuwa tatizo kubwa kwa watanzania walio wengi, nashindwa kuelewa ni ujinga, ni mfumo tuliokulia au nini.
    Kwa nini nasema hivi, unaweza kuta huyu jamaa aliyeleta hii mada kamaliza kati ya moja ya vyuo vyetu muhimu, hasa ndani ya nchi mana siamini mtu aliyesoma nje kama anaweza kuuliza swali kama hili, nadhani huu ndio wazungu wanasema umasikini unatusumbua.
    Kumsaidia Chenge ni waziri wa nini, na ATCL iko chini ya usimamizi wa nani?? Lakini pia inawezekana sio kosa la mshikaji, unajua hata mshikaji wako JK ame i dilute sana nafasi yake ya urais! Unajua why nasema hivi? Mana sasa imekuwa hata wachimba mitaro hawataki kumsikiliza mtu, lazima JK ndio aseme, kwani Chenge ni waziri wa nani kama sio Govt, sasa kwa nini asiongee, mi nadhani tafuta mtaalamu siku moja atuandikie humu jinsi Govt invyofanya kazi, na uhusiano kati ya idara mbali X 2 za govt.
    Poa,

    ReplyDelete
  11. Duh hii hoja iko moto.Ukweli uko palepale ATCL ndio wa kuwajibika na sio serikali kwani ya serikali yametosha. Au labda kuna ndugu wa kiongozi katika msafara?

    ReplyDelete
  12. kwakweli hata mimi nashangaa inakuaje serikali inaingia gharama kama hizo, ki vipi hasa, inamaana sasa hivi kila atakaekwama airport alipwe??? au ni aje hapo mbona nakuwa sielewi, serikali ya Tanzania haiendi mbele ila inaenda backward, na wananchi watanzania tumekaa kimya tu, tunaongelea kwenye michuzi no one is doing anything about anything happening to that country, jamani upendeleo umezidi, Mungu aione Tanzania, na wachomwe moto hapa hapa duniani tuone, watu wengi wanateseka ile nchi ila watu wanalipwa watu wenye uwezo wa kwenda kuhiji, hivi hata huyo Mungu anaenda kuombwa anafurahia haya kweli, mwingine afe na njaa kwakuwa kuna watu wanaenda kuhiji, jamani muogopeni Mungu hata kidogo, msiwe maselfish kiasi hicho, sidhani hata kama hizo sala zitafika wakati mmeacha watu wengine wanakufa, mmeambiwa saidieni watu na nyie Mungu atatwasaidia. Tanzania haina dawa ile, utafikiri viongozi wote ni matahaira. MUNGU IONE TANZANIA. AMINA

    ReplyDelete
  13. Mimi Ninashanga kama wewe...
    Je ni Watanzania wangapi wamecheleweshewa haki zao za msingi na wengine bado kupata na hakuna anayewajali??? Je nao nani awasemee ama nani atawalipa na kwa kiasi gani kwa kadiri wao na jamii zao walivyoumia/athirika??? Hapo kipimio ni nini???
    Mi naona waliosababbisha kadhia hii ama wajiondoe kazini ama waondolewe na haki zao wapewe waathirika...hii inaudhi sana

    ReplyDelete
  14. YAPO MENGI ZAIDI YA HILI HUMU NJINI...NI KUWA TU HILI LIMITUKIA HUKO DAR... huku kwetu yapo mengi tumwone nani atulipe???

    ReplyDelete
  15. Hilo ni jukumu la ATC na Insurance. Kwa nini Serikali?

    ReplyDelete
  16. man,thats cray and rediculous I think there s no reason for doing that its the flight company responsibilities to pay the loss suffered

    ReplyDelete
  17. Jamani mi sioni cha ajabu hiyo ndio SIRIKALI sio SERIKALI wanajua wayatendayo.


    Ukiona hivyo tayari kuna hekali linaenda kumaliziwa.Hapo wanaweza kuandikwa hadi MAHUJAJI HEWA....

    Kweli bongo nawakubali

    ReplyDelete
  18. Kwa kweli hapo Chenge ametuacha hoi! labda kama hatujamwelewa! Yaani wamepewa kifuta jasho, kwa lipi ambalo serikali inahusika? hatuelewi kama hizi ni POLITICS au kiini macho. Waislamu wengi tu huko Nigeria, Ghana na sehemu nyingi wamekwama. Iweje fedha ambazo kila siku tunaambiwa hazipo au hazitoshi, leo ati wengine wapewe kifuta jasho!

    Kwa kweli African Countries, ni mwisho!

    ReplyDelete
  19. Hapa ndugu wadau mimi naona kama kawaida ya viongozi wetu wa serikali, wamejaa ubabaishaji tu.Mimi binafsi nilimsikiliza Mh Chenge kwenye TV akisema hawalipa fidia, ila kifutajasho.sababu ya kutolipa fidia ni kwa vile ATCL walifanya jitihada zikashindikana.
    Kama kweli walifanya jitihada kwa umakini bila uzembe wowote wasingekosa slot huko Arabuni.Kukosa slot sio force
    majeure labda kama Mh Chenge anataka kuleta shule mpya ya mawazo(A new school of thought)Kukosa slot au kutapeliwa wanakodai ni matokeo ya mchakato hafifu wa kuandaa safari hii ya mahujaji.Maoni yangu ni kuwa Mh Chenge na Bodi ya ATCL hwatakiwi kuendelea kuwa ofisini.Ni vema tu wakaona aibu na kujiuzulu.

    Hivi kweli watu 1000 wanalala chini pale airport kwa siku 10, waziri asione aibu?.Kwa mtu kama mimi ninayeamini katika utawala bora naona ni sawa na kijana kuona mama mkwe gagulo limemvuka na wewe ukaendelea kutumbua mimacho ukizistadi nyeti za mama mkwe.Ni aibu, halafu tunaenda ulaya kila siku wa development partner kujidai tunafanya utawala bora.Utawala bora kwa watu incompetent kama hawa?, unless uniambie kuwa this wa strategic kuwakomoa mahujaji, but again bado it is not expected.

    ReplyDelete
  20. Jenga picha mtoto mejiingiza kwenye gari mwenyewe kwa bahati hajaumia saaaana lakini kavunja kioo cha gari mtoto hana uwezo wa kukinunua kile kioo na baba pia ana majukumu mengi maana ada za shule, maji, matibabu na mengine mengi yanamngojea. Baba anatokea anataka kuchangia nusu hasara na yule mwenye gari maana mtoto hana uwezo wa kulipa kioo kilichovunjwa!

    Hapo juu nimejitahidi kutumia mfano au lugha ya picha. Ukweli ni kwamba Serikali inamiliki hisa 100% za ATCL kwa vyovyote vile Serikali inawazibika moja kwa moja na kadhia iliyotokea kupitia wizara ya Miundombinu. Kwa nchi zilizo komaa kidemokrasia sasa hivi ninapo andika comment hii Chenge angekuwa amemwaga unga au kwa lugha nyepesi kibarua kingekua kimesha ota nyasi na bodi nzima ya ATCL ingekuwa likizo ya muda mrefu kama si kungoja kupangiwa kazi nyingine.
    ATCL ni mali ya Serikali mtu anapokosa safari kwa sababu ambazo zimesababishwa na air line anatakiwa kulipiwa 5 au 4 star hotel na dola 100 mpaka 150 kwa siku mpaka atakapo pata safari rates hizo juu zinategemea na class ya ticket yako kama ni 1st class unaweza kulala mpaka 7 star hotel. Hizi ni sheria za kimataifa za Civil Aviation sasa ATCL haikufanya hivyo inamaana imekuika taratibu! na hii inatokana na ukweli kwamba ATCL isingezewa kumudu kuwalipia Breckfast,Lunch and dinner mahujaji zaidi ya elfu moja kila mmoja akitumia dola 20 kwa siku kwa milo mitatu mara 1000 ni $ 20,000 mara siku kumi na mbili $240,000 na pesa za kujikimu tuseme wawalipe $ 100 na sio 150 mara 1000 ni sawa na $ 100,000 mara siku kumi na mbili $1,200,000 + 240,000 = $ 1,440,000 hiyo ni hesabu ya watu elfu moja na wale waliokwama walikuwa ni zaidi ya elfu moja! Hapo ndio maana Serikali inataka kuwapa kifuta jasho maana kama wakiwasongesha front watalipa zaidi ya hiyo hapo juu! Je ATCL itakuwepo tena?na hata ikiuza ndege zote na lile jengo la Ohio hawata pata hiyo CASH! wanatalkiwa waonewe hurumu maana waliutaka mfupa kumbe hawana meno sasa umewashinda!

    ReplyDelete
  21. Nchi yetu nzuri haijui sheria.
    Sioni kwanini serikali iwalipe watu wakati wao walinunua ticket kwa kampuni binafi. Je hii ndege ni ya serikali?

    Basi tulipwe fidia wote tunaouziwa bidhaa au huduma mbovu na makampuni hapa bongo...

    Au kwa vile ni watu wa dini ndio maana wanapewa special treatments?

    ReplyDelete
  22. Kuhusu hoja hii SERIKALI inachemka.Kwa nini....! Serikali inatakiwa kuendesha mambo yake kila siku kwa kufuata katiba ya nchi!Kwa hili...Katiba inasema Serikali haina DINI na kwamba kila Ria anao uhuru wa kuabudu na kuwa na Imani yake...SASA Watu wameamua wenyewe kuabudu na kuwa na imani yao, wakapanga safari zao na vikundi vyao kwa kadiri ya Imani yao na watu wanaowajua wenyewe na kwa gharama zao wenyewe.Ikafika mahali sasa wakatapeliwa na hao watu wao wanaowajua wao na wakakwama kusafiri...SERIKALI NA WANASIASA WAKE WANAHUSIKA JE HAPO? KIONGOZI WA SERIKALI ANAACHA KUFANYA SHUGHULI NYINGINE ZA UMA ANAKWENDA AIRPORT KUFUATILIA WATU WENYE SAFARI ZAO BINAFSI KULINGANA NA IMANI ZAO WENYEWE...SASA TUNAAMBIWA SERIKALI INATAKA KUWALIPA KIFUTA JASHO....KWA KAZI GANI YA SERIKALI WALIYOIFANYA? NA JE BUDGET YA HAO NDUGU ILITARAJIWA NA KUTENGWA? HAYA NI MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA SERIKALI....MKITOA HATA SENT ITABIDI MJIELEZE KWA WANANCHI KWA KINAGA UBAGA....!!! ALAH MAMBO GANI HAYA.

    ReplyDelete
  23. Mimi naona
    hilo tatizo sio la serikali bali ni la Atc unless kuna walakini some where.

    ReplyDelete
  24. Kukusaidia tu, muundo wa ATc na umiliki wake unatoa mwanya kwa serikali kuwa wajibu wa kutatua baadhi ya matatizo ya ATC. Aidha kutokana na unyeti wa suala lenyewe, serikali haina budi kuwahi haraka ili lisije likawa tatizo la kisiasa na kidini, hasa katika zama hizi ambapo watu hawana haya. Ni heri serikali iwalipe fidia halafu ikafanye mahesabu nao pembeni kuliko kung'ang'ania kuwa ATC ilipe fidia au chochote, halafu ikashindwa, ikapelekwa mahakamani, mali zake zikapigwa mnada, halafu serikali ikarejea pale pale kwenye kuikomboa. Ni heri kutibu muwasho kuliko ukurutu.

    ReplyDelete
  25. Jamani, hizo ni pesa za wavujajasho. Ni pesa za kodi. Siyo halali kwa serikali kutoa hela zetu na kuwafidia watu waliokuwa na safari zao binafsi. Lini tutaelewa tofauti kati ya serikali na mambo binafsi? Shirika la ndege linatakiwa lifidie hao watu kibiashara kutokana na policies walizonazo za compensation. Siyo serikali kutoa fedha zake kuwafidia watu waliokuwa na safari za kidini. Hilo halikubaliki. Wewe Chenge unatakiwa uachie ngazi hujui unachokifanya...hujui kazi kabisaaa...!!! Unamuogopa nani? Au unajipendekeza kwa nani?

    ReplyDelete
  26. Misupu, blog ya mdogo wako inaitwje? Weka link basi, au hamuivi?

    ReplyDelete
  27. Mambo kadhaa ya kusahihisha:

    1. Simply kwa sababu watu wengi wanaohangaishwa kutokana na kutoajibika au uzembe Tanzania hawalipwi fidia si tiketi ya watu wengine kuzuwiwa kudai haki zao. Ni wajibu wa kila mtu kujua na kudai inapobidi haki yake!

    2. Simply kwa sababu ATC ni shirika ambalo serikali yetu ndo ina hisa kubwa kiasi cha kuliita shirika la serikali haihalalishi Waziri kusimama moja kwa moja na kutamka aina ya malipo yatakayotolewa tokana na makosa yaliyofanywa na uongozi wa shirika.
    Taratibu za utendaji zinajulikana na ni lazima zifuatwe vinginevyo hata mwanafunzi aliyechapwa fimbo akaumia katika shule ya serikali basi inabidi waziri wa elimu asimame na kutamka kifuta jasho kwa wazazi wa mtoto au na kwa mtoto mwenyewe. Hesabu za kipuuzi za kusema kuwa shirika la serikali ya JMT ni sawasawa na serikali ya JMT zinatufikisha ambapo tunasema watu wa serikali ya JMT ni serikali ya JMT; hivyo utapigwa ngumi kwenye disco na mlevi mmoja usiku na asubuhi yake unakwenda kukaa mbele ya Luninga ukiwa umetune stesheni ya TVT kusubiri Waziri wa usalama wa raia atangaze kifuta jasho chako na kwa DJ aliyesumbuka kusimamisha muziki tokana na yule MTU WA SERIKAlI ALIYESABABISHA FUJO!!

    Hakika binasfi nawapa pole sana Mahujaji walivyosumbuka lakini niseme kuwa wao kama wasafiri binafsi au kundi waachiwe nafasi kwa kadri ya utambuzi wao na kwa uzito wa usumbufu walioupata kupeleka malalamiko yao kwa mmiliki wa shirika la ndege walilyokuwa wamekubaliana hatujui kama ni kwa Mkurugenzi wa ATC au mwenyekiti wa Bodi ATC wanajua wao vyema. Na sisi hatujui makubaliano yao yalikuwa ni nini maana hii ni biashara yenye makubaliano na kama kuna nafasi ya Bima sisi hatujui.

    Mimi nawaunga mkono waliosumbuliwa wachukue hata mawakili na wahusika wafikishwe mbele ya haki na malipo yatatolewa kwa haki tu kama ni kutoka katika faida/ hasara ya ATC au ni kutoka katika kiinua mgongo cha Mkurugenzi mkuu au ni mshahara na marupurupu ya Mwenyekiti wa Bodi aliyejitangulizia pasi ya dili au ni kutoka kwa kiongozi wao wa Kidini aliyeingia dili feki na Tapeli sisi hatukui lakini Sheria ndio kazi yake hiyo. Mbona ushahidi ukianza kumwagwa mbele ya baraza somo litaeleweka kwa haraka?

    Unajua hili suala linaweza kuwa baya sana siku za usoni (kijamii, kiutendaji, kisiasa na hata kidini) si kwa sababu eti ya serikali kunyamaza bali kwa sababu ya serikali kukurupuka na vitulizo ambavyo vinaleta maswali mengi kuliko majibu!!
    Waziri anapojitanguliza na kutamka aina ya fidia yeye anaitoa wapi hiyo? Nini maana ya kifuta jasho kwa raia aliyepata hasara tokana na uzembe wa mtu? Je anatoa wapi base (kiini) cha malipo ya namna hiyo. Yaani tosomewe hiyo sheria au hiyo kanuni ili tuichambue hapa.
    Maana lazima iwe na maelezo kuwa iko applicable kwa kundi la Waislamu wenye idadi fulani (maana nina imani kuwa Waislamu wengi walishawahi kusumbuka katika usafiri siku za nyuma lakini hawakufutwa jasho, au sheria inatamka kuwa lazima wawe wanakwenda nje ya nchi maana Waislamu kibao tumewahi kusumbuka wakati tunasafiri hata toka Zanzibar kwenda Dar. Au sheria ieleze kuwa ni lazima iwe ni katika usafiri wa anga maana kwa mabasi mbona tumeshasota mpaka ikabidi tununue tiketi nyingine kwenye mabasi mengine na bila maelezo wala hata mtu wa kuupa pole na au eti mpka ukapangiwa hoteli ya kulala wakati unasubii usafiri. Kwa Waziri kukurupuka ndiye anataka kutuletea udini maana kwa kweli atahitaji kukumbushwa jinsi Wakristo wa Sabato Marejeo na wengine wengi walivyokwisha pata karaha wakiwa wanasafiri kuhudhuria makambi yao!.

    Mambo ya dini ni sensitive sana, lakini hii si tiketi ya kuibuka toka katika ofisi ya Waziri na kwenda kwenye TV na kutamka yasiyotarajiwa. Ni vema serikali ikaacha taratibu ziongozazo zikachukua mkondo wake wa uwajibikaji. Mtu mwenye malalamiko ana haki yake ya kulalamika na akaipata kwa utaratibu mzuri tu pasipo kuamsha hisia za watu wengine kufikiri kuwa kuna double standards hapa!

    ReplyDelete
  28. wake up wa Bongo Please... kwanini Serikali ilipe kama wabongo tupo macho? wabongo kibao hawasaidiwi JE hawa sababu kuna Ndugu zake Raisi? Nakumbuka kuna Mzee Mmoja kati ya wale wazee wanaodai mafao alifia station ya Reli ktk sehemu aliyokuwa akijistili andthen Serikali ikajidai toa mchango wakumsafirisha hadi Mbeya.sasa wenye akili waka hoji kwanini wasingemsaidia akiwa hai?

    ReplyDelete
  29. 1. Serikali ya Tanzania ina hisa aslimia 49% katika ATCL. Na pia inajulikana kama "Parent Company" 2. Pili, ATCL ni "National Carrier" amabyo inabeba "Nationbal Flag", Ukiachilia mbali kuwa Serikali ni parent company, pia inawajibika kulinda heshima ya "National Flag" popote pale duniani bila ya kujali abiria ni nani ilimradi ni abria halali. Viongozi wote wa juu, Mwenyekiti (Nyalali) na CEO (David Mataka) wamechanguliwa na rais (presidential appointees) na wanajibika kwa serikali kupitia kwa Waziri kama majority share holder. Kwa bahati mbaya shirika linaendeshwa kwa hasara miaka mingi, lau kama lingeingiza faida basi faida (dividends) zingeenda serikalini kupitia hazina. Na ndiyo pesa hizo hizo ambazo serikali ingetakiwa kutoa fidia. Msiwe na jazba bila ya kuangalia miundo mbinu ya "Parastatals" (SU) na jinsi yanavyowajibika. Usisahau pia kuwa ni serikali iliyotoa pesa hazina kununua (kurudisha) hisa 49%kutoka SAA (therefore it is a major stake holder!!!) Ningetegemea na kushauri watu kuzungumzia zaidi uwajibikaji na siyo nani alipe au walikuwa ni abiria aina gani. 3. Kwa kuishia , Chenge kama major stake holder, hakusema hajatuambia atalipa fidia kupitia mfuko upi, jee haifai kuuliza hilo kabla ya kusema mengi .Tahadhari, Tanzania tupo njia panda......

    ReplyDelete
  30. serikali inabidi ijitoe katika kufanya biashara, kazi ya serikali ni kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa na sio kutoa maamuzi ya jinsi kuendesha biashara

    ReplyDelete
  31. Hakuna hoja hapa. Owner wa ATCL ni serikali. ATCL kama inapata faida katika operations zake hiyo faida yote inaingia katika mfuko wa hazina ambao unamilikiwa na serikali.

    Hivyo kama ATCL au serikali (kupitia wizara) ikilipa fidia hiyo, bado pesa inatoka katika mfuko ule ule mmoja unaochangiwa na kodi wa walala hoi.

    ReplyDelete
  32. http://www.globalpublisherstz.com/2007/12/12/ndoa_ya_faraja_kotta_aibu_tupu.html

    Basi naomba mtembelee hapo juu ili mpunguze hasira watansania!! Najua jinsi gani linatuumiza kichwa hilo swala, ila wale wanyalu waangalie wasijejitundika, ha ha....

    ReplyDelete
  33. Jamani mimi nadhani ni umasikini tu wa mashirika yetu, lakini kulipwa fidia ni kitu cha kawaida kama ukicheleweshwa safari. nakumbuka nilicheleweshwa siku moja tu na KLM walinilipa kwa pesa za kibongo sh Laki nne na nusu hivi, nilala 5 star Hotel kula na kunywa free, kwa kuwa nikuwa sina haraka nilitamani wangeni chelewesha siku hata siku 10. kwa kifupi kulipwa kupo iwe serikali au shirika kwa Ulaya ni kawaida.

    ReplyDelete
  34. Kulipwa fidia ni haki ya mtu na siyo hicho kiini macho wanachokiita kifuta machozi. Labda ilikuwa zamani, lakini sasa hivi watoto wao tupo na tumesoma hasa hiyo fani ya sheria. Tutaiburuza ATCL mahakamani ikawalipe wazee wetu haki yao inayostahili kwa kuwachelewesha safari na kuwapa mateso ya kisaikologia kwa kutowaambia kitu kinachoendelea wakati wakisubiri hiyo safari.

    Na wale wanaolalamika kuwa kwa nini hawa walipwe fidia na wasafiri wengine wanaokwama hawalipwi fidia, hakuna mtu anayemzuia mtu mwingine kudai haki yake, sheria ziko wazi kama hukudai haki yao utapewaje?

    Msilete kisingizio cha dini ili kutaka kuwanyima watu haki zao, kama mtu ana tatizo na uislam atafute njia ya kulitatua, sijui kodi sijui nini, kodi inalipwa na watu wote haichagui kuwa huyu ni mwislamu asilipe kodi.

    Kwa kifupi tunawasubiri warudi kutoa Hijja, na Mwenyezi Mungu awajaalie Hijja ya salama na warudi salama, halafu tutaona taratibu za kisheria zinasemaje kuhusu madai ya fidia. Kama watalipa ATCL kama mwenye mtoto atambeba mwanae hatuangalii makunyanzi tunachotaka haki, kuwepo baba yake Bi Salma na nduguze kwenye safari kisiwe kisingizio cha kutaka kukosesha watu haki zao.

    Kodi zenu zinaliwa kwa mambo mengine ya kipuuzi hampigi kelele hili la waislam kusemwa tu watalipwa kifuta jasho sijui kifuta machozi na sio fidia imekuwa mwao!! Sasa bora tudai hiyo fidia ya mamilioni kabisa tena kwa kufuata taratibu za kisheria ili mnyamaze!!!!Daah!!

    Na anayeona kuwa hawafai kulipwa akasimame na wakili wa serikali mahakamani hapo kesi itakapofunguliwa.

    ReplyDelete
  35. Du watu wanaona mbali kweli na wanaandika haswa. Nimefurahishwa sana na huyo anony aliyetoa mfano wa mwanafunzi kuuumizwa na mwalimu na mlevi kupiga mtu disco. Yaani jamaa anachambua kama yule jamaa ambaye huwa anajiita MkataIssue.
    Kwa kifupi hakuna mwenye busara anayepinga madai au watu kulipwa fidia; issue ni je ni lazima waziri ndiye atangaze na tena atamke malipo yaitwayo KIFUTA JASHO??? Tusijikanyage wala tusilete hapa habari za kuonyesha hisa au mmiliki wa ATC. Hilo linajulikana lakini taratibu zifuatwe period.
    *************
    Michu mwaka unakwisha hivyo labda uorodheshe majina ya watu waliokuwa wachangiaji wakuu ktk blogu hii tuwapigie kura kupata the best 3 kwa kuchangia si mara nyingi bali substance yaani wanaotoa maoni yaliyokwenda shule na yenye busara hata kama ni mara chache na wakawa wameweka utambulisho wao fulani mwanzoni au mwishoni.

    Jonathan - Morogoro

    ReplyDelete
  36. KILA SIKU WAPO WATANZANIA WENGI WANAOKWAMA KUSAFIRI LAKINI HAWA HAWAJULIKANI KWANI HAWAMO WAKWE KWENYE KUNDI LAO, HAPA KINACHOENDELEA NI KUWAPENDEZESHA WAKWE ILI WAONE FAIDA YA WAKWE, HII SI MARA YA KWANZA MAHUJAJI KUKWAMA LAKINI HUKO NYUMA HAWAKUWAHI KULIPWA KIFUTA JASHO. HATA HIVYO WANANCHI TUELEZWE PESA HIZO ZITATOKA KWENYE FUNGU LIPI.

    ReplyDelete
  37. ABIRIA AKICHELEWA NDEGE KOKOTE KULE HAPA DUNIANI, WAHUDUMU WANAVYOFURAHIAAAAA NA KUKUTUKANA MATUSI YOOOTE YA REJA REJA HATA KAMA UKICHELEWA DAKIKA TATU AU TANO UTAAMBIWA..."UNATAKIWA KURIPOTI UWANJANI MASAA MAWILI AU MATATU KABLA YA SAFARI".
    HAPO NDUGU YANGU UJUE HAKUNA SAFARI VINGINEVYO UONGEZE UCHACHE WA NGUVU ILI TIKETI YAKO IPATIWE NAFASI KWENYE NDEGE INAYOFUATA! III WAJAMENI
    LAKINI KIBAO KIKIGEUKA MWANAWANE NA WAO NDIYO WAWE WAMECHELESHA NDEGE AU KUVUNJA SAFARI, EEE BWANA WEEEE. WALIVYO WAGUMU KULIPA FIDIA SIAJAPA KUONA.
    WATAKUDANGANYA NA KIJIFADHILA CHA KUKUWEKA MALAPA INN AU KIJIHOTELI NJAA ILI MRADI UGHAIBIKE NA KUSAHAU HAKI YAO.
    SI HAO TU. MAKAMPUNI YOTE YANAYOHUSIKA NA MAMBO YA USAFIRI WANADHANI WAO NDIYO WENYE HAKI. LAKINI HIVI SASA WANAKIONA CHA MOTO KILA MTU MJANJA KWENYE HAKI YAKE. ANAYETENDA KOSA AADHIBIWE KWA KULIPA FIDIA.
    KWA NINI WANANCHI WADAIWE FIDIA WACHELEWA USAFIRI WAKATI WANAOTOA HUDUMA HIYO HAWATAKI KULIPA FIDIA? NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  38. serikali ni atc

    ReplyDelete
  39. ATC ni nani na serikali ni nani? wacheni kujitoa fahamu mahujaji wanahitaji kulipwa fidia yao, hao munaowapigia debe wameachwa hawakulipwa walifata taratibu za kudai haki zao?Au sababu yamewakuta waisilamu ndio munaumia na hela za walipa kodi,na muna uha kika gani hela itatoka katika mfuko wa walipa kodi?Wacheni chuki binafsi, watanzania sote ni kitu kimoja ingawa kila mtu ana imani tafauti.

    ReplyDelete
  40. jamani naona mnapoteza dira!hakuna aliyesema wasilipwe,wala waziri kutangaza sio issue sana. Swala ni nani alipe fidia????? period*****

    Mi nashindwa kuchangia kwa kuwa watu wawili wamenchanganya hapa,mmoja anasema serikali ina 100% hisa za ATCL mwingine anasema 49%. Kama ina 100% then naona ni sawa waziri kuresque hisa za serikali kwa kuingilia kati. Kama ni 49% jamaniiii ipo waziiiii, wanahisa ndo waku-share faida na hasara,serikali haitakiwi kulipa fidia yote,inatakiwa washirikiane ma-share holders wote,ipo waziiii kampuni yoyote duniani jamaaaaaaniiiiii mpaka nataka kulia. Na kama account ya ATCL hazina itakua haina hiyo amount basi inadeclare mufilisi !!! hakuna swala la kwenda kuchukua kodi za wananchi hapo serikali itakosea kabisaaaaaaa. Na kama kawaida viongozi wa shirika hilo nashangaa wapo mpaka sasa mi ndo maana sirudi bora nifie huku hata nikichomwa moto,nikija huko ntakua napata presha kila siku.

    ReplyDelete
  41. Wadanganyika Bwana,
    Mmesahau ya TVT kuhusu kuonyesha LIVE michuano mbalimbali??

    ReplyDelete
  42. Hii mada nzito sana watu wangu, cha msingi ni kumwomba Mungu afanye njia katika hili kwani inakatisha tamaa kuona mambo kama ya udini udini na uwoga wa ndugu wa wakubwa fulani wanataka kutuchafulia amani ya nchi kwa kuona kila mtu atasema mimi nilifanyiwa hiki sikulipwa mbona yule hata hajadhurika analipwa???!!!

    Kumbukeni issue ya Muhimbili 'UPASUAJI TATA'!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...