Wadau,
While I feel I need to congratulate Br. Nundu, I am not surprised to see a Tanzanian excelling on international circles. That has been the case with many before. The big question is why these people who do wonders outside are not mobilised to help our country to be an international pride as well. Is it because we do not appreciate their roles or is it sheer selfishness on the part of those who dominate the local political hegemony?
As ever,
Concerned Mdau
---------------------------------------------------------------------------------------------
The Council of the International Civil Aviation Organisation has appointed a Tanzanian Aeronautical Engineer Omari Rashid Nundu as President of its technical body, the Air Navigation Commission for the year 2008.

The Commission consists of distinguished experts nominated by ICAO Contracting States and appointed on a highly competitive basis by the ICAO Council to serve in the Commission for a period of three years.

The Commission is the technical source of all standards, rules and procedures for the design of aircraft, airports and aeronautical equipment; and for the safe conduct of international air transportation.

Omari Nundu who was born in Tanga 59 years ago triumphed against Carlos Cirilo of Brazil to serve in the top seat of the high profile international body as far as air transport is concerned.

Engineer Nundu’s journey to the Presidency of the Commission started in 2005 when the number of seats on the Commission was increased from 15 to 19 and he was nominated by Tanzanian Government to contest for the additional seat. He began to serve in the Commission in 2006 and in the same year his colleagues in the Commission unanimously elected him to be their First Vice President for 2007.


It is not customary or assurance that the First Vice President becomes the next President and this has never happened before but on 14th December 2007 the Council of ICAO elected Engineer Nundu the President of the Commission for 2008.

The commission is currently served by only 2 Africans amongst its 19 commissioners. Each Commissioner must have excelled outstanding qualifications and experience in the science and practice of aeronautics to be considered for appointment and since there are always more candidates than seats appointment is through serious competition.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. hii kali michuzi,huyu mbongo ina maana ana uwezo wa kudizaini maboing na ma eabasi na mamig na ma b52?mmmmmmmmmmmmmmmh,kama kweli basi he is my man of the year 2007!

    ReplyDelete
  2. Mdau nadhani ni combination ya vyote viwili..ie selfishness ya wahusika na system isiyotaka new ideas. selfishness kwa kuwa wengi walio huko majuu hawataki au hawako tayari kupokea compensation ya mboga wakati wanajua fika kwamba skills zao ziko on demand na wanaweza pata whatever they want. Sasa kama wakifanya hivyo ni dhahiri kwamba hawawezi kufanya kazi katika mazingira ya kitanzania yetu ambayo wote tunayajua.

    La pili kuhusu system, wote tunajua Tanzania yetu viongozi wetu ni wanafiki, wazandiki na wanaotaka waabudiwe. Unakuta kiongozi ni form four au hata ana degree lakini ndo hivyo anamnyanyasa mtu mwenye elimu yake. angalia wabunge walipwa kiasi gani na maprofesa waliobobea katika fani zao wanalipwa nini. we need coherence. Na hili Serikali haiko tayari...you can go on an on..

    Angalia lile tangazo la mama Ghasia kwamba nafasi kubwa serikalini hazitatangazwa tena..bali watakua wanateuana. Sasa kama sio unafiki na ubinafsi ingekuwaje? Tanzania yetu inasikitisha lakini ndo hivyo.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na anony wa Monday, December 17, 2007 10:05:00 AM EAT, kwa yote uliyosema. Nabii huwa hakosi heshima, isipokuwa kijijini kwake na nyumbani kwake mwenyewe. Kuna vichwa vingi sana vya kibongo vipo sehemu mbali mbali duniani vikifanya maajabu katika nchi za wengine, kwani havithaminiwi nyumbani kwao. Kuna Bwana mmoja anaheshimika sana pale katika taasisi ya mambo ya anga ya NASA (Marekani), na jamaa hawako tayari kumuachia kwa gharama yoyote ile. Nakumbuka kuwa Waziri Mkuu mstaafu Bw F T Sumaye alikutana na hali ya namna hiyo nchini Namibia, kwamba zaidi ya wabongo 80 walikuwa wameshika nafasi nyeti nchini kule, na akawauliza wale "Wadanganyika", kwamba kwa nini hawarudi kwao kuijenga nchi yao? Alijibiwa kuwa mazingira ya wasomi kwa Tanzania hayakuwa mazuri kuwafanya wao kurejea, hivyo asihangaishe kichwa chake kuwashawishi warejee makwao. Sijajua alichukua hatua gani baada ya hapo, ila nina uhakika kuwa hakufanya lolote kuwashawishi jamaa warudi kuijenga nchi yao! Hatua wanazochukua akina "Ghasia" na wenzake katika kukumbatia ajira chache ambazo nazo zimejaa wenye majina makubwa ndizo zinafanya watu wawe wagumu kurejea makwao mara baada ya masomo nje ya nchi. Sio kwamba watu wanapenda kujilipua, ila ni mazingira ya namna hii ndio yanawafanya wasiipende nchi yao ki-ajira, ingawa huwa wanaikumbuka wakipata vijisenti.
    Something needs to be done in the govt in Tanzania!
    Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Uongozi mbaya na usio na malengo ndio unawafanya watu waikimbie nchi...ingawaje kuna chembe za ubinafsi vile vile kwa wanaokimbia.

    Serikali yetu inasomesha tu watu bila kuwa na malengo na wala haifuatilii kuwa tuna wataalamu wangapi katika fani mbali mbali....kila mtu anahitaji kutambulika kama amesomea kitu fulani.

    Siasa ni mbaya sana na hususan ikiwa chini ya watu wachache ambao hawakusoma!

    ReplyDelete
  5. Kusema ukweli, naona hili swala serikali yetu inalifanyia utani na nina uhakika wanajua kwamba nchi haiwezi kufika popote kama wataalamu kama hawa hawarudi nyumbani na kupewa msaada katika kutumia vipaji vyao. Unaweza ukalaumu pande zote; lakini nani ana ubavu wa kugongana na 'wazee wa nchi'? Nchi imeshikwa na Waasia wenye hela...Jiulizeni, mabilioni ya hela za kampeni hupatikana wapi? Unadhani ni hela kutoka bus terminal ya Ubungo??

    Kwanza, kabla hujaanza kuwarushia mawe watu ambao hawarudi, jiulize wewe, kama kuna sehemu ambayo unathaminiwa na unatunzwa (pamoja na familia yako), je, utarudi Bongo?

    Waafrika huwa wanalalamika kuhusu ubaguzi wa rangi - kweli, upo hadi leo. Lakini waulize wale ambao wameshikiliwa na nchi zinazoendelea. Watakwambia, upo lakini akitaja kazi anayofanya tu heshima hurudi.

    Kwa kifupi, watu wanaotengeneza hela, hawajali kuwa wewe ni Muafrika, Mmatumbi au Michuzi. Kama una uwezo wa kuendeleza walichonacho na kuwawezesha kupata hela zaidi, watakuchukua.

    Jana kulikuwa na interview moja - CEO wa AMD alikuwa anahojiwa. Kama ungepata nafasi ya kumsikiliza ninachosema kingeeleweka vizuri zaidi.

    Kuna baadhi ya nchi, kama una profession fulani fulani, basi wanakupa na uraia kabisa au kibali cha kuishi (permanent).

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Bw. Nundu! Nivizuri sana kuona watu kama wewe uliofanya kazi maisha yako yote ili kuisaidia nchi yetu. Watu ambao hawaelewi kuwa mtanzania yeyote anaweza kuendeleza nchi yetu hata akifanya kazi nje ya nchi wananisikitisha sana. Ndio maana nchi yetu haiendelei.
    Wivu ni kitu kibaya sana!
    Mungu akubariki Bw. Nundu!
    Hongera sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...