kadau destiny (kati) ka shule ya vidudu ya st. florence academy ya dar kalipomaliza pre unit hivi karibuni kakiwa kameshika zawadi ya kuwa mshindi wa tatu darasani. shoto ni ashley na kulia ni trinity ambao nim washkaji zake wakubwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hebu someni majina ya hao watoto kwanza.
    Wadau naomba niwaulize swali:Hivi baada ya miaka kama 20 ijayo tutakuwa na majina ya kiswahili kweli? Kama utabili wangu ni sahihi nadhani majina yote ya kiswahili kama masumbuko, mateso, mkandawile n.k. yatakuwa yameishapukutika ktk historia ya mswahili.

    Waswahili kwa kuiga hatujambo. Mara utasikia waswahili wanawaita watoto wao majina ya kizungu kama Moore, McFallen, Washington n.k. Hivi ni lini tutaacha huu ulimbukeni wa kuiga kila kitu kwa mzungu. Ina maana sie majina yetu hayana mvuto au ni ulimbukeni tu wa kuigaiga kila kitu cha mzungu?

    Mbona hatujawahi kusikia wazungu wakijiita majina ya kiswahili? Ulishawahi kusikia wazungu wanaoitwa majina kama Maganga, Mwanahawa,Msemakweli n.k? Na kwanini sie tu ndio tuige kutoka kwao? Hebu tuamshe akili zetu tusiwe wavivu wa kufikiri!

    ReplyDelete
  2. Mie mwenyewe nimeshangazwa na hayo majina. Waafrika tunapenda sana uzungu. Yaani sie tunafikiri kuendelea ni lazima kufanana na wazungu :)

    SAC

    ReplyDelete
  3. Wewe nawe, wenzio majina siku hizi wanatoa kwenye internet, utandawazi huo, sasa hayo majina ya Kaundime, Nyangere, Kichiku, Manka, Tatu, Pili, Mwanahoja, Semeni, Bahati, Amani, Imani, Furaha, watayatoa wapi wakati kwenye internet hayapo?

    Mtoto Destiny, hongera kwa kumaliza chekechea na kujiandaa kuingia darasa la kwanza au grade 1.
    Ili suala la majina watu turuhusiwe tukiwa wakubwa kuchagua na kubadilisha majina unavyotaka, si unajua mtu unajikuta umeshapewa jina tayari hata kama hulipendi lishaluwa lako

    ReplyDelete
  4. KWELI INATISHA SANA MAANA HATUWEZI
    THAMINI TENA TAMADUNI ZETU.DUH KWELI TUMEKWISHA KABSAAAA.YANI
    WANATUONA KAMA KATUNI SASA

    ReplyDelete
  5. wewe hapo juu hiyo ni yako wewe jina lako nani...Mbona kuna wazungu wengi wanaitwa changu, kenya, keita etc

    mambo ya kukandia majina ya watu sio vizuri ..jina ni jina na paul ni jina la kiswahili...?

    Globolization muhimu...nyie kaeni tu na majina wachina sasa hivi wana majina mawili ya kichina na ya kiiternational...wanajua watatembea ulimwenguni kumake it easy ....kupita popote bila kuulizwa mara mbili mbili what ...what....


    Ndio yale kiswahili tuuuu watu wanatoka nje ya nchi wanashindwa kucommunicate......
    Kma uko sawa na jina la kiafrica ni wewe kama ni la kizaramo ni wewe kama kila mtu ana freedom ya kuita jina analopenda

    Mimi mwanangu jina la kiswahili litakua middle name akienda kijijini watamwita hilo akienda mahali wanataka jina easy watamwita hilo...I have been there and I know what I am talikng about....

    oh well....

    Hey Kadau ...hongera sana kwa mwendo huo tunakusubiri Harvard...

    ReplyDelete
  6. Jamani watoto wadogo kama hao mimi nisingeona sababu ya kutoa zawadi kwa walioshinda. Wote ni washindi. Kuamka asubuhi kwenda shule ukiwa mtoto sio rahisi. Na hao wasio na zawadi wataanza kuwa waoga na kujiona wao hawana akili...psychological unadestroy the ability ya hao watoto toka wadogo ya kupenda shule. mimi kwa upande wangu ningewapa wote zawadi kuwamotivate wapende shule zaidi.

    ReplyDelete
  7. ama kweli nyani haoni kundule ,kwani we jina lako hulioni au

    ReplyDelete
  8. hata mimi naku support wa hapo juu sana sana huyo anayeitwa t paul sasa sijui paul ni la kiswahili angeitwa kabisa paulo tujue kweli jina lake la kiswahili waosha vinywa bwana hawakosi lakusema.
    hongera destiny im proud of ya so as ur parents.
    majina yakiswahili siku gizi hamna dili utaonekana wa kuja this is a new century with new names sasa ukimuita mtoto wako masumbuko na kweli atasumbuka kweli.basi mpe jina mtoto wako chausiku
    yours mamacita

    ReplyDelete
  9. hey anon wa "globalization" hivi majina ya international yakoje?Kwani ukiitwa Kipanga huwezi ku-communicate na wazungu,wa-asia nk?Mimi majina yangu yote ni ya kilugha na naweza kucommunicate na kila mtu wa hapa nilipo na wao hawapati shida kulitamka jina langu na wanapopata ugumu kulitamka wananiuliza jinsi ya kutalitamka.
    Hivi unajuwa kuwa kila lugha ina a,b,c,... na hakuna lugha isiyowezwa kufundishika na kuongeleka?
    Inaelekea una self-esteem issues mkuu,ama sivyo umekuwa brainwashed kupindukia.

    ReplyDelete
  10. ACHENI USHAMBA KILA MTU ANA HAKI YA KUMPA MTOTO WAKE JINA ANAVYOJISIKIA SII UZUNGU PENGINE NI KUMBUKUMBU YA KITU, AU RAFIKI AU MAANA FULANI KWA INAVYOMFURAHISHA YEYE KWA UTASHI WAKE YEYE, KAMA UNA ISSUE NALO NI KIVYAKO... BIG UP DESTINY, ASHLEY AND TRINITY NICE NAMES ..........

    ReplyDelete
  11. Kwa mtazamo wangu, jina ni mojawapo ya utambulisho wa mtu. Majina mengi hutolewa kutokana sababu maalumu na zamani mabibi kwa kushauriana na mababu pamoja na shangazi na ndugu wengine wa upande wa baba ndio waliokuwa wakitoa jina kwa mtoto anayezaliwa na siku ya kupewa jina hilo kwa mtoto, sherehe ilikuwa ikifanyika kubariki jina pamoja na tukio zima kwa ujumla. Baada ya kuingia kwa dini/imani za kigeni walioleta dini/imani hizo pamoja na mambo mengine walileta majina kutoka katika lugha zao. Walitoa majina haya kutoka katika vitabu vyao vitakatifu pamoja na historia zao. Hapo ndipo na sisi tukaanza taratibu kuacha matumizi ya lugha zetu za kibantu pamoja na kiswahili katika kupata majina yetu na kuingiza majina kutoka katika lugha za historia zao. Majina hayo ya kwao yanatafsirika na mengine yametoholewa na kuwekwa katika lugha zetu za kibantu na Kiswahili.

    Kama nilivyosema awali majina hutolewa kwa sababu maalumu kama vile kuenzi mtu, kudumisha undugu/urafiki/ujamaa. Binti yangu anaitwa Nadia, jina hili ni la rafiki yangu ambaye ni Mrusi, alipokuja hapa Tanzania alipenda kuitwa Tumaini na hata sasa Tumaini ni jina linalotumika zaidi kumuita yeye huko Urusi. Sasa ili kuuenzi urafiki wetu, binti yangu nimempa jina lake na yeye anatumia Tumaini "Hope".

    Naomba kuwasilisha

    ReplyDelete
  12. Bwana majina magumu bora uwe mtu mzima ndio utoke nje ya nchi. Ukiwa mtoto mwanafunzi na jina lako gumu utashangaa na roho yako. Kila ukitamka watu wanakuangalia tu wewe. Yaani wanakujudge kabla hata hujafungua mdomo. Halafu unaulizwa tena na tena na tena. What ....??

    Bwana hata survey imeonyesha kuwa watoto wenye majina magumu (hapa USA) hawajibu maswali sana na pia walimu hawawaulizi maswali sana kuogopa au kutokutaka kukosea kutamka majina yao ..hivyo inaonyesha wanakua wanaachwa nyuma kuliko wale watoto wengine ambao ni wakitaifa lakini wamepewa majina common.

    Kama unajua mtoto wako hataenda ulimwengu wakimataifa muite kalumakenge au wagagagigikoko.

    Kuna kijana mjapani nilisoma naye alikua anaitwa K**a sasa hebu niambie kama angekua mtoto baba yake amehamia bongo kufanya kazi halafu umweke kwenye shule mtoto mwenye jina hilo si itakua tabu kweli huko shuleni...hatafanya vizuri kabisa na kuichukia shule... ???

    Kwa watoto ni shida sana kama wewe ni mkubwa umekuja huku na jina lako poa... you can tolerate being unique lakini kwa mtoto haelewi kwa nini anaulizwa jina lake mara tatu tatu au kila siku...how do you pronouce that...

    Ni vizuri kuwaandaa watoto kwa ulimwengu huu. Sasa kama unaita jina gani lakini sio ujifuraishe wewe...fikiria kama ni wewe ukiitwa hilo jina ingekuaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...