Muasisi wa reggae bongo Jah Kimbute amefungua mwaka na majarida ya kimataifa. Katika jarida la African News linalochapishwa nchini Uholanzi limeandika ziara yaSuper Star huyo wa Reggae toka bongo kuwa atafanya ziara nchini Uganda mwaka huu wa 2008 ambapo mashabiki wa reggae nchini Uganda wataburudika na moto mkali wa mziki huo.
Gazeti hilo linapatikana kwa kukong'oli hapa www.africanews.com/site/list_messages/14799
Simba huyo wa reggae kutoka bongoland anaonyesha dalili za kuwasha moto tena baadaya mapuziko ya muda ya kutokupanda jukwaani mara kwa mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Doh!kaka,punguza hizo nywele,zinakunyonya dam,humuoni mwenzio Dk Remmy Ongara, sasa anaonekana kijana?utamaduni mwingine jamani!!!

    ReplyDelete
  2. Ahhh uchafu wa aina gani huo???

    ReplyDelete
  3. Waswaili bwana! wat is human rights to you anons? tofautisha nywele nyingi na nywele chafu! hivi wenye vipara hawaitaji kuosha vichwa!!

    ReplyDelete
  4. Hiyo dental formular kweli ina-balance na je ni ya binadamu au predator?Ukiongeza na hizo nywele utadhani VODOO.Ukileta posa kwetu hukubaliwi mjomba.

    ReplyDelete
  5. mmh huyu nadhani he needs to invest in braces...info zaidi ni hii link http://www.minarsortho.com/
    good luck

    ReplyDelete
  6. Ni mwamini wa “variety is the spice of life” kulingana na taratibu zetu tulizojiwekea.

    Nachukia mvunja sheria au mwenye kuvunja sheria iliyopo, kwa makusudi, hata kama inaiona ni mbaya (two wrongs do not ordain a right)! Ni vizuri kukaa chini na kujaribu kuirekebisha sheria hiyo mbovu.

    Kuna baadhi yetu wanaoshangaa kwa kuibuka kwa kile nitakachoita, “utamaduni wa ‘kabila/din’ wa u-Rasta (Rastafarians)” nchini.

    Utamaduni wa “kabila/dini” huo ulitokana na Weusi wa Kisiwa cha Jamaika na kujikita miongoni mwa walalahoi wa kitongoji cha Dungle cha mji mkuu na bandari ya Kingston – wengine sehemu kama hizo huziita za “ghetto”.

    Katika sehemu hizo za mji wa Kingston kulizaliwa muziki wa staili au aina za mento, ska, rock steady hadi kukua na kufikia staili ya reggae.

    Muziki wa “rege” ulienezwa sana na Mjamaika mwimbaji mashuhuri Robert “Bob” Nesta Marley (marehemu)na wengineo.

    Wafuasi wa mwanamuziki mashuhuri marehemu Bob Marley, ambaye wa “kabila/dini” hiyo ya u-Rasta wanamfikiria kuwa ni “ nabii” wao.

    Ma-Rasta wa Jamaika walijitambulisha na nchi ya Ethiopia. Kutokana na kujitambua kuwa huko, ndio maana wa-Rasta wengine wa Jamaika hivi karibuni walipendekeza (bila kufanikiwa) maiti ya Bob Marley ipelekwe kuzikwa huko Ethiopia.

    Wa-Rasta wa Jamaika walivutiwa na historia ya ukoo wa ki-falme wa Ethiopia wenye damu ya Malkia wa Sheba, mmojawapo wa wake za m-falme “mwenye hekima” Sulemani wa Uyahudi, aliyekuwa na wake kama elfu moja hivi, licha ya makahaba au vimada wake.

    Walijivunia kutawazwa kwa m-falme mpya kijana, Haile Selassie (Ras Tafari Markonnen) waliyemfikiria kuwa ni “Masiya” wa kuwakomboa kutokana na dunia hii yenye dhambi (Babylon) na kujenga dunia “tambarare” (Yerusalemi), kurejeshwa kwa heshima ya Afrika, umoja wa Afrika na dini za ki-Afrika. Wakachukua jina lake, Rastafarians!

    Kisiwa cha Jamaika kilikuwa na watumwa wengi sana kutoka sehemu mbali mbali za magharibi ya Afrika.

    Kwa nini hao wa Kisiwa cha Jamaika walijitambua kuwa wanatokana na Malkia wa Sheba?

    Je, walikuwa wanaifahamu Afrika kweli? Au ni kwa sababu ya sifa za Ethiopia? Ethiopia ni Afrika. Lakini Afrika sio lazima iwe Ethiopia.

    Mara nyingi huwa nafikiria kuwa ndugu zetu waliouzwa utumwani huku katika nchi zilizojulikana kama “Dunia Mpya” (New World) walitoka sehemu za magharibi ya Afrika pamoja na sehemu za Msumbiji.

    Labda, kulikuwa na ndugu zetu waliotoka Ethiopia walioletwa huku!

    Kujitambua katika u-Ethiopia kunazalisha fikra za kujiona kuwa ni wa damu “teule” (the chosen).

    Sifikirii kuwa u-Rasta ni kujiona kuwa bora zaidi kushinda wengine. Kama sentenso yangu iliyopita haina uzito wowote, basi huo “uteule” ni ubaguzi!

    Msimamo huu wa “kujiona bora” unawakumba pia baadhi ya Weusi wa Amerika ambao huwa wanajigamba kuwa wanatokana na falme mashuhuri za Afrika kuliko kujitambua kuwa walitokana na “walalahoi” wa Afrika!

    Wana-Rasta wengi ni watu makini sana wenye maadili mema na nidhamu ya hali ya juu. Wana historia ya kuheshimu uzawa (indigenity and existentiality) wa ki-Afrika.

    Hii yagusa sana akili yangu kwani kuna tabia nyingi ninazopenda za “kabila/dini” hili/hii ya u-Rasta, ikiwa ni pamoja na kupenda rangi nyekundu, nyeusi, na kijani, na nywele ndefu zilizosokotwa.

    Mwanablogu mmoja aliandika yafuatayo kuhusu Wamaasai kupata soko la kusuka nywele za mtindo wa ki-”rasta”:

    “Staili ya nywele za rasta imejipatia umaarufu sana siku hizi. Ghafla, vijana wa kimasai wamejikuta wakiingia sokoni kwa vile wana ujuzi mkubwa wa kusuka nywele hizo. Kichwa kimoja inaanzia elfu mbili hadi tano kulingana na staili na uwingi wa rasta!”

    Tabia nyingine zinivutazo ni wapenda amani na maadili mema, alama ya Simba wa Yuda ya Mfalme Haile Selassie na hawavutwi sana na vya utajiri wa duniani (Babylon); wanategemea vya milele (Yerusalemi).

    Kwa wale wanaojua mambo ya bailojia, nguvu za muziki (strong solution) huo ilikuwa na mvuto kwa baadhi yetu (weak solution) na kupenyeza mipaka yetu ya kimataifa, ambayo leo hii inavukika kwa urahisi (very permeable) shauri ya vya kisasa.

    Kuna tabia moja ya wa-Rasta wengine inayonikera. Sana sana wa-Jamaika waumini wa “kabila/dini” la/ya u-Rasta wanaita bangi, “ganja”.

    Wanavuta na kuitumia kwa mambo mengine; ni “mmea mtakatifu” (holy weed) unaomfanya muumini kujitambua halisi na kumtukuza “Jah” (Muumba).

    Sivuti sigara na situmii bangi ingawa wataalamu wa madawa wanasema kuwa bangi inapunguza pia makali ya maumivu ya saratani.

    Matumizi ya bangi, hata kama ni kwa matibabu, yanaweza kuleta madhara pale yasipodhibitiwa na daktari mtaalamu!

    Lakini ninatoka kabila la Wajita, huko Mashariki ya Ziwa Victoria, ambalo baadhi yao huvuta bangi au “lirongo” (limestone). Huko kwetu bangi inaitwa, “injaga”.

    Kidogo neno hilo liko sawa na linavyoandikwa kinyume nyume huko Jamaika: “ganja”!

    Wajita wangu huvuta bangi kwa kuliweka kwanza ndani ya kidawi cha “lirongo” (na kuliwasha kwa moto wa mkaa) chenye tundu chini kinachosimikwa ndani ya kijibuyu chenye mkia kilichojazwa maji.

    Kabla ya kuingiliwa na u-Kristu wa ki-Sabato na u-Koloni, natumaini wavuta bangi wa kabila langu walikuwa lukuki! Serikali ya wa-Koloni ilipiga marufuku uzalishaji na utumiaji wa bangi bila kufaulu. Toka wakati huo hadi leo hii, vita dhidi ya bangi inaendelea.

    Hao wavuta bangi wa kabila langu walikuwa ni wazee – wengi wenye wajukuu. Ulikuwa ni mwiko kwa vijana kuvuta bangi!

    Hata kwa wazee, uvutaji wa bangi ulikuwa wa siri siri, na ulikuwa “functional”, kijamii na kiuchumi.

    Kijamii, kwa sababu wazee walikutana kubadilishana mawazo kuhusu ujirani wao wakati wa majira ya kumalizia adhuhuri.

    Kiuchumi, baada ya kuvuta, walichukua zana zao kwenda kutayarisha sehemu za mashamba za kulima keshoye. Walikwenda kukata miti na kuchimba visiki ili kurahisiha ulimaji, na kuwakomboa akina mama kupambana na visiki hivyo!

    Bangi ni bangi tu hata kama inatumika kwa matibabu ya saratani; wengi wanaotumia bangi nchini mwetu hawana saratani!

    ReplyDelete
  7. thela wee avae !!!!

    ReplyDelete
  8. Jah kimbute is a good person with beautiful music.For those who insult his hair or teeth ,you don't have brain at all.You realy think people wear brace in Africa??? rasta is a black thing so don't be too westernized and forget your home baby.And who the F.. told you that he doesn't wash his hair? shut your crutch up cross your leg,lean back and let the brother drop his music,don't hate because you don't have a life.Love you too heffer...

    ReplyDelete
  9. NINAMKUMBUKA HUYU MTU, ALICHANGQANYIKIWA MIAKA MINGI SANA, HUYO MTU NI YULE ALIYEMUAMBIA LUCKY DUBE KUWA HAJUI KUPIGA REGGAE WAKATI DUBE ALIPOTEMBELEA TANZANIA, KISA ALIKATALIWA KUINGIA BURE KWENYE ONESHO. MWISHO, HAILE SELASSIE HAKUWA MCHAFU HIVYO WAKATI YEYE NDIYE MWENYE ASILI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...