John Legend, mwanamuziki(Three times Grammy Award Winner) wa Kimataifa ametoa Albam yake mpya inatwa Once Again, kwenye hii Albam kuna wimbo umewika sana unaitwa Show Me, Video ya huu wimbo imefanywa Zanzibar Tanzania na kumuonyesha kijana wa Kizanzibar na maisha anayoishi mwenye ndoto za kwenda nje na jinsi alivyoondoka kwa kudandia Ndege si Meli kama ilivyozoeleka.


Imenivutia kwa kweli kwani inaonyesha maisha halisi ya huko nyumbani kwa vijana na wale waliopoteza matumaini. Hebu icheki hapa http://www.youtube.com/watch?v=Bd_-ainw7g8


Mdau PiusKuala Lumpur.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Ndugu msomaji wa blog hii
    Kuna blogger Mzungu ni mchangiaji katika kijiji hiki jina lake la blogging ni marque kwa kifini ni Marko.
    Binaadamu huyu ana hulka zooote za kibaguzi,ni muandishi anayejifunza lugha ya kiswahili kupitia Chuo kikuu cha Tumaini Tanzania anatuchafulia Jina la nchi yetu kama utapata mtafsiri wa lugha ya kifin "Finnish" soma habari zake kuhusu Wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini, generalisation yake kuhusu mikoa yetu ,Utamaduni wetu na mengineyo hii ndio link http://helloafricatellmehowyourdoing.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. Video imetulia mno na ujumbe umefikishwa, huu ni utundu bunifu wa wasanii wenye vipaji vya kuzaliwa sio kugeza,nimeipenda mno...huu uwe mfano kwa wanaojiita masupa staa wa bongo badala ya kupeleka ujumbe muhimu, nyimbo zao ni za kushangilia mapenzi tuuu wakati hali ngumu za maisha ya watu ndio muhimu kupigia kelele kama wanamuziki waliotangulia, kizazi kipya kinajali pombe, ngono na kutanua bila ya kujishughulisha. uvivu wa vitendo pia uvivu wa fikra ndio umewaandama.

    ReplyDelete
  3. We Pius, ni nini kilichokufurahisha kwenye hii video? unafurahi nchi yenu kuonyeshwa kwa ulimwengu kuwa ni masikini? hujiulizi kuwa mbona wakionyesha Afrika huwa wanaonyesha umasikini, lakini wakionyesha Ughaibhuni wanaonyesha utajiri? hebu jiulize kwanza. Acha ulimbukeni wewe Pius.

    ReplyDelete
  4. Nyimbo imetulia sana hii huwezi kuilinganisha na ya Roony sijui Loony, kiukweli ukiingalia hata huelewi maneno unapata ujume.

    ReplyDelete
  5. mdau hapo juu, video iko katika dedication waliofanyiwa watoto wawili kutoka Guinea walio stowaway kwenye ndege iliyokuwa inaeleka france na siyo kwamba inongelea kijana wa zanzibar mwenye ndoto za kudandia ndege, kwa habari zaidi angalia www.showmecampaign.org kwa maelezo zaidi, asante..

    ReplyDelete
  6. Nyimbo imeenda shule na dhumuni limefahamika,inasikitisha lakini ndio reality ya maisha yetu Tanzania na Afrika nzima kwa ujumla.Sijui lini tutajikwamua na njaa tuliyonayo na maisha magumu tuweze kuishi kwenye bara letu bila kutegemea nchi za nje kama mfano wa huyu mtoto jinsi alivyo piga hesabu kaona hali nyumbani ni ngumu katafuta solution pamoja zinakua tragic lakini desperation inampeleka mtu pabaya hatari haioni.Mungu ibariki Afrika

    ReplyDelete
  7. Watu wengine wanapenda ubishi sana,sasa wewe anon wa 8:56pm,unabisha nini?kuna tofauti gani ya ujumbe uliokua potrayed kwenye hiyo nyimbo na hao watoto walio kufa.Ni ndoto kama hizo za huyo mtoto ndio ziliwaponza wakafa.Yes video imetengenezwa Zanzibar yes kijana wa kizanzibari au hata wakinyalu katumika ku play hiyo part mradi ujumbe ufike asante mdau Pius ni issue ya watanzania na waafrika wote.Zanzibar ina beach nzuri na hotel nzuri lakini faida yake wakaaji wa zanzibar hawaijui,ukiingia mitaani hali ya kwenye video ilivyopigwa ndio hali halisi ilivyo.Fikiria huu ujumbe unge fika vipi endapo wangepiga video kwenye hayo mahoteli yakifahari yaliyo jengwa kwenye fukwe za zanzibar.It wont make sense.Ilivyo chukuliwa ndivyo haswa,unajua vipi watu wanakua driven to find fertile land.

    ReplyDelete
  8. Wewe anon wa kwanza kwanini usiseme haswa mzungu anachoandika? Unafikiri mtafsiri atatoka wapi? He who aledges must prove, kha! Au unategemea mtasha ajisemee?? Fichua ufisadi mwanangu!

    ReplyDelete
  9. SASA KMK UNACHOBISHA HAPO NI NINI?
    MIMI NIMESEMA IMENIFURAHISHA IMEGUSA NDOTO WALIZONAZO WENGE NA KUONYESHA SAFARI NDEFU YA KUTAFUTA MAISHA AMBAVYO WENGI HUTAKA KUIKATIA DENGE MDAU HAPO JUU AMEJARIBU KUKUONYESHA NI JINSI GANI HIZI NCHI ZETU ZENYE UTAJIRI MKUBWA WATU WAKE WANAVYOTAABIKA, ULITAKAJE WAONYESHE SHERATON AMA BWAWANI HOTEL? WAKKATI KUNA WATU WANASHINDIA VICHWA NA UTUMBO WA KUKU? NDIO MNAVYOSEMA HUKO KWAMBA KILA KITU NI TAMBARARE? CHINI NIMESEMA HALI HALISI YA VIJANA NA WALE WOTE WALIOKATA TAMAA YA MAISHA NYUMBANI.

    Sio kila waliokwenda nje wamefanikiwa na ndio maana huyu aka dedicate kwa hao wawili lakini kuna zaidi ya hao ambao wanakimbia kwenda nje na safari yao inaishia njiani? kila siku unasikia boti zinatoka Morocco kwenda Spain na kwingineko na zinaishia njiani, Hao ndio ninaowaongelea mimi.

    Wabillah Tawfiq

    ReplyDelete
  10. Hii video ni mbaya kwetu, kwa nini asiende Guinea kutengeneza video kama hii? mtoto wa kizanzibari hawi vile ni kinyumme kabisa na reality. inaonesha udhaifu kila sehemu hata airport imekosa usalama? i wonder who gave the permission to shoot such video.

    ReplyDelete
  11. Amijeee Mzanzibar acha ubishiiii yakhe!! Haya Ntoto wa Kizanzibar akoje? kwani huoni bibi akilima Mwani pale? huoni mtu akivua samaki, huoni Chai Maharage weye? maisha yepi hasa ya Kizanzibar zaidi ya haya, sema hawajaeka chapati nchuzi tuu!!
    Ila kwa mi ninayeijua vizuri Zanzibar tena humu ineonyesha si ile hasa ya kiswahili kwani hii ni maisha ya Mzanzibar wa kawaida tuu, je utalinganisha hii na ya Mapunk?
    Yakhe angalia uzuri utaniambia.

    ReplyDelete
  12. Hakuna Mzanzibari yoyote aliezaliwa au kukulia Zanzibar akabisha kwamba this is not the reality! hapo jamaa kaonyesha kile ambacho watu wengi hasa viongozi wamekuwa wakijaribu kukificha .Lakini utafanyaje ndo unacho tu! ukitaka usitake!

    ReplyDelete
  13. its a very nice muziq, well done john, and there is nothing to be ashamed of!! the boy really did acted well, we indeed have good coming up actors in tz, znz.
    nana

    ReplyDelete
  14. Duh! kali kichizi imetulia hasa! mpaka Maalim SEIF ndani! hebu ichekini fresh wadau.

    ReplyDelete
  15. I dont know sisi watanzania tunataka kuonyeshwa nini? Huyu Mdau kaleta hii muone na kaandika maelezo yake eti jitu oooh umefurahishwa na nini we ulitakaje aonyeshwe BALALI pale akila pesa ama?
    Acha ushwaini....
    Hebu soma baadhi tu ya maneno yake hapa chini ujue umuhimu wa hii Campaign

    "Our specific goal is to fund the village in Tanzania and others that we're visiting," he said, "and the program is a five-year program to raise $1.5 million to fund it, and we've already raised a few hundred thousand dollars."

    The project has been funded with income from charity events and online donations from fans.

    Legend says the money will flow to the right resources.

    "It doesn't give cash," he said. "It does things like buy fertilizer, or set up Internet connections or buy malaria bed nets or have scientists come in and help them clean their drinking water and make sure it's healthy."

    He says giving services rather than cash leaves less room for corruption. "It's very traceable and the results have been very good," said Legend

    Big Up Michuzi
    Big Up Mdau wa Kuala Lumpur

    ReplyDelete
  16. Tena ningependa hii video ionekane mpaka kwa hao mataliano shwain wanaosaidiana na watanzania wengine kujinufaisha wao wakati nchi inadidimia. Hivi hako ka kisiwa ka Unguja unaweza kukimaliza kukizunguka kwa siku moja tu choote bado maendeleo yanayotokana na pesa za utalii yanashindikana? Pesa zenda wapii? Hebu tuangalie nchi zinazotegemea utalii kwa uchumi wake kama Tunisia kulivyoendelea. Pesa za utalii zimekuwa invested humo humo Tunisia kwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa mbali mbali na ndio watalii wanatumia hawaimport vitu ka siye. Na mapesa yotee yanaishia huko kwa wazungu wacheni ukweli usemwe. Pengine watasusia wakijua utalii wao hausaidii kuondoa umaskini!

    ReplyDelete
  17. sasa wewe anon wa kwanza kabisa, unamaana gani kutuletea hiyo habari halafu hutuambii kaweka nini kwenye hiyo blog yake?
    sisi tutapata wapi mtu wa kututafsiria hicho kifini
    wewe tuambie tu kasemaje ili tumcharure humu, hana adabu kabisa
    please let us know, hata kama ni ndefu wewe itume kwa michuzi halafu tucomment.
    thanks in advance

    mdau Canada

    ReplyDelete
  18. Jamani, pia tukumbuke kwamba watu wasije wagaiga kudandia ndege kama huyo mtoto alivyofanya (kujificha kwenye tires) kwani hapo ndani kunabaridi sana wakati ndege ikiwa angani, na hiyo inaatarisha maisha yako KIFO BABA!

    ReplyDelete
  19. Kuna usemi wa kiswahili unaosema mficha uchi hazai, nahii video John Legend ameonyesha hali halisi ya Zanzibar kwamba sio tende na halua, huyo anayetaka Zanzibar ionyeshwe sehemu nzuri sijui kama amamfahamu John alivyosema au sijui ameshaijua nia ya John, unafikiri kama angeonyesha hali ya maisha mazuri Tanzania/zanzibar hao wahisani wanaotoa msaada kwenye kijiji cha Mbola wangepatikana? pamoja kwamba dedication ilikua kwa vijana wa afrika ya magharibi lakini ujumbe kwa watu wa mbola kusaidiwa umefanya kazi.
    Zanzibar sio tende na halua na watu kama nyie mnaosema kwamba tumedhalilishwa kuonyeshwa kwenye dunia kwamba ni masikini, basi mujue kwamba hio ndio hali yenyewe, ndio nyie mnaowadanganya mademu kwamba mnaishi masaki kumbe mnaishi uswahilini.

    Big up mdau wa kuala lumpar

    ReplyDelete
  20. HIVI HUYU MDAU WA KUALA LUMPER KAIPATA WAPI HII VIDEO MIMI NIKO USA SIJAONA NIMEKUJA KUIONEA HUMU?

    HUKO SIKUTEGEMEA KAMA KUNA WATANZANIA. JAMANI WABONGO KWA KUNUSA HAYA NYIE MNAFANYA NINI HUKO?

    ReplyDelete
  21. Wewe hapo juu unaulizia watanzania walifikaje kuala lumpur Malasia, kwani wanaopanda mameli wanajua kwamba meli itatua wapi? inaweza kua meli ya wagiriki lakini inapiga masafa ya Malasia, wewe shangaa tu hapo, watu wanautoroka ufisadi bwana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...