Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema shein akiwa amevalia vazi la asili ya kichagga alilovishwa na jumuiya ya umoja wa wazee wa kike wa moshi wakati Makamu wa rais Dk Ali mohamed shein alipokuwa katika ziara ya kukagua na kuangalia miradi ya maendeleo katika mkoa wa kilimanjaro leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. toba nilikua sijui tuna vasi la asili wachagga

    ReplyDelete
  2. Da! Sijui Michu umechemsha au mimi ndo nachemka...Kwetu kwa wachagga sjawahi kuona vazi la namna hiyo!!! Hebu waambie wakuambie vizuri, ni nini hiko??

    Kavishe Massawe

    ReplyDelete
  3. Naona ndo tume gundua vazi la asili kama kila kabila linalo na sisi inabidi tuwe nalo. Pamoja na kukulia uchagani maisha yangu yote haki sijawahi kuona hili vazi. Embu niambieni wadu ku "aia sari" au kufagia mbolea na hiyo nguo inawezekana!!!!!

    ReplyDelete
  4. Wamachame wajanja, wanajikomba tu kwa huyo mama na mumewe, kuna kitu wanatafuta hapo. Hakuna vazi la asili la wachaga linalojulikana, wachaga huwa wanachangamkia nguo yoyote ya bei nafuu inayodumu bila kujali ni ya fasheni gani au asili ya wapi.

    ReplyDelete
  5. AISEEE MREMA HUKO HUPATI KITU, KUMBE WASHAGHA WOTE NI CCM VASI LENU LINA RANGI ZA CCM HATA KABLA YA UHURU! KWELI NYIE WAJANJA SIJUI MLIJUAJE KUWA CCM ITAKUJASALIWA AU USOMI WENU! BRO MICHU KADI YAKO YA CCM NAMBA NGAPI?

    ReplyDelete
  6. Safi sana kusoma na kumwona mama mwenye jina jema la Mwanamwema. Tunahitaji balansidi kavaleji za namna hii si kila siku wale wale tu mpaka wanachuja!

    Rusha snap la Mrs. Slaa hapa tujue ushujaa wa mumewe unapoanzia, Leta hapa Mrs. Balali tumpe mawazo ya namna ya kumshauri mumewe KUJA TANZANIA NA KUKIRI MAPUNGUFU YOTE YANAYOMUHUSU NA LOLOTE ANALOLIFAHAMU JUU YA UFISADI NDANI YA BOT ili aingie katika rekodi ya mbingu isiyo na mfano wala kutengenezwa na mwanadamu mwenye mapungufu kama ile ya ginesi.

    ReplyDelete
  7. Hebu angalieni hiyo picha kwa makini sana. Munamuona Mhe. Dr. Shein anavyocheka huko kwenye picha yuko mbali lakini iangalieni hiyo picha vizuri. Anacheka kweli kweli, maana hili vazi na yeye limemchekesha kweli kweli.

    Lakini nyie msibishe wala msicheke,hili vazi huyu Mama amevalishwa na Wasee wa Kichaga, hao wanajua mila na desturi za kichaga kuliko sie. Pengine kabla makanisa hayajaja kutufundisha kuvaa magauni ya kuendea kanisani ndio walikuwa wanavaa hivi sasa wacha tujifunze mamaangu tujue asili yetu mbe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...