Kwa niaba ya kanisa la watu wote wanaotumia lugha ya kiswahili katika hili jiji la Dallas, ninapenda kuwakaribisha wa Tanzania wote katika ibada maalumu ya kuombea ndugu zetu wa Kenya ambao wako katika machafuko ya kisiasa.
Kanisa la umoja limeona ni vema kuungana na watu mbali mbali ambao wamekuwa wakiombea amani ya majirani zetu. Tukumbuke kwamba, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hivi "Tanzania haiwezi kuwa huru mpaka Africa yote iwe uhuru".
Kwa msingi huo hatuwezi kuwa na amani ya kweli mpaka ndugu zetu wawe na amani ya kweli. Hali ya Kenya imeathiri sana watoto wa kitanzania wanaosoma huko, imeathiri biashara kati ya nchi hizi mbili na hali ya wasi wasi miongoni mwa majirani zetu imekuwa ya kutisha sana.
Ilikuhakikisha ibada hii inakwenda vizuri, kanisa lako la Umoja limekuandalia muhubiri machachari anaheshimika ndani na nje ya Tanzania pastor NAAMAN SHAURI kutoka Tanga.
Ibada hii itaanza saa moja kamili jioni siku ya jumamosi tarehe 25.1.2008 katika kanisa la Umoja liliko katika makutano ya 635 na Hillcrest.
Direction: 635w exit Hillcrest, make right on Hillcrest and church will be the second building on your right hand.
Contacts: 214 554 7381,
469 487 9953,
469 279 1762.
Karibuni sana.
Mdau-Dallas Texas
Sasa jamani sie tusio waumini je,si tukija tutaangaliana visura tu...kwa hiyo labda tuwe na mapochopocho na ngoma chakacha manaake wanasema'music is the language of love' mwasemaje wadau?
ReplyDelete