IFUATAYO ni hotuba fupi aliyoitoa Waziri Mkuu Edward Lowassa katika Bunge mjini Dodoma leo (Alhamisi Feb. 7, 2008) asubuhi, wakati wa mjadala wa Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi "Richmond Development Company LLC" ya Huston, Texas, Marekani mwaka 2006:

"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.


Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli.


Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".
Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.

Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.
Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili.
Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. aaaah anajitetea nini hapa, tumechoka na mambo wanayoyafanya kwenye nchi yetu, hawa ndo wanafanya tuliopo nje tusiwe na hamu hata ya kurudi nyumbani.. ila kwa upande mwingine nao kina mwakyembe walitakiwa wamuulize huyu bwana, kwa jinsi alivyolalamika! hahhah utasema hajala hizo hela..

    ReplyDelete
  2. Mhishimiwa sana tumesoma ujumbe wako.Lakini bila kukuonea wewe wala tume,maswali ni mengi kuliko majibu hapa. Nina maana hasi zimezidi chanya,hisababti haijakaa sawa.
    Why don`t you do a gentlemen thing here for the sake of your constituency and the national as well.Can you please,honorably resign your parliament membership too !! Then and only then ,you can come back and complain like a crying baby on the streets !!
    Unachoshindwa kukubali hapa nikuwa,hata kama hujakatiwa panga,ilikuwa incompetent enough kuachia hali hiyo ifike hapo.Wewe si msimamizi mkuu wa serikali daily ?Au hilo kidogo ulisahau ?
    Haya bwana Lowasa,karibu mtaani tuongozane kwenye foleni na uone how beatiful three lanes work !!
    Wala sikusikitikii chochote,ila naomba wale wote wa aina yako wafichuliwe,waondolewe,ili tupate unafuu kidogo,jamani.
    Ooh, by the way,ukija mtaani watch out,sababu kipindupindu hakichezi mbali sana,kinaweza kikakupindua na hicho.
    Wanaokupenda na wakukaribishe majumbani mwao sasa ili ukwanywe nao chai !
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  3. HAIKUWA LAZIMA KWA WAZIRI MKUU KUISHUTUMU TUME KWAMBA HAIKUSEMA UKWELI JUU YAKE. ALICHOTAKIWA MUHESHIMIWA NI KUBWAGA MANYANGA BILA KUZUA MJADALA MWINGINE UNAOMKABILI WA KUTHIBITISHIA BUNGE KWAMBA KAMATI YA MWAKYEMBE ILIMVUMISHIA UONGO JUU YA TUHUMA DHIDI YAKE , HATAIVYO HATIMA YA TANZANIA AMBAYO WANANCHI WAKE WATAJIVUNIA MATUNDA YA UHURU BAADA YA KIKWETE KUINGIA NDANI YA NYUMBA WADAU WEMGI WANAOTUMIKIA NCHI ZA WATU WENGINE WAKATI WANADENI NA NCHI YAO WAMETIWA MOYO SANA NA SEREKAI YA MHESHIMIWA.NA WALE WALIOKUWA WANOOGOPA KUNANIHIWA KWA SABABU YA KUSEMA UKWELI WAFUFUKE HUU NDIO WAKATI NAMUONA DADA ANA ANAONYESHA USHUPAVU WA HALI YA JUU ANASEMA HATA JOHN AKICHEMSHA HAMUONEI HURUMA KWASABABU YA MASLAHI YA WANA WA NCHI. KWELI TANZANIA ILIYOKUWA INAOTWA SASA INA KUWA YA KWELI.SASA HICHI KIZAZI CHA MAZOEA YA UTENDAJI KWA WAKUU WA SERIKALI ULIOKITHIRI USANII UNAELEKEA KUINGIA MITINI INGAWA BADO KUTA KUWA NA NGUVU MBADALA YA KUHAKIKISHA MAZOEA YANAENDELEA LAKINI HISIA ZINAONYESHA LAZIMA WASANII WATANYEA KWA MUDA HUKU WAPENDA HAKI WAKIFANYA KAZI ANGALAU HATA KIDOGO KUTAKUWA NA MWANYA KIDOGO.

    ReplyDelete
  4. I am suprise that an issue of this magnitude was thrown at you and the office of the prime minister and you could not see it coming. I say the office of prime minister because the office is not an individual entity its there to represent the people so you are just an employee.

    And just like the fact you were quick to highlight the professional qualifications of Dk. Harrison Mkwakyembe, I fail to understand how ignorant were you to the suffering of the people you are suppose to represent.
    You claim to hear about all this issues through the streets, through the newspapers and other media and blame the fact that they did not come to consult you (so I guess you could cover your tracks or the tracks of your friends well.)Now tell me who did you expect was to come running to you and tell you that the office failed during your watch". You were place incharge and you slept!

    Arrogant as you are, you could see the people suffering and yet did not set out to clear the office of the PM from such allegations nor investigate the plight of the mass.It did not bother you since it does not effect your household. You were selected in that esteem office to help the people and as the executive head for the ministers, I guess you are responsible for their failure. Belive me your resignation is not comparable to the suffering of an ordinarly Tanzania.
    The nation is not young! Don't fool the people with such remark, it's politicians like you who lie to people and think they are stupid. We should be ashamed that for four decades, this is the best we can do????

    I advise you as a final gesture to the people of Tanzania, provide all the support you can as an ordinarly tanzanian you are now, to facilitate the solution to this problem.The mass deserve at least that!
    May this event set a precedent to all future leaders maybe its time to owe up to the people who were responsible to put you up there.

    ReplyDelete
  5. Wajameni,
    Pamoja na wizi wote wa Lowasa inaonekana pia kamati haikuwa makini ilijaa chuki za binafsi. Which means Dr. Mwakyembe naye ana matatizo anataka umaarufu katika cheap politics. Tuwe wakweli ukisoma maelezo ya Lowasa kuna maswali mengi

    ReplyDelete
  6. Ilitolewa nafasi kwa Mtz yeyote anayejua chochote kuhusu Richmond awasiliane na tume, ili ahojiwe au atoe maelezo yake. Mbona Mhesh. hukwenda, je si ulijua kuhusu hiyo kampuni kimeo. Sasa unasemaje hukupataiwa nafasi wakati unajua fika kuwa ulihusika, na vimemo uliandika. Acha kutuzuga wewe.. Kituo cha pilie KEKO....

    ReplyDelete
  7. Lowassa amefanya vizuri kujitoa maana sasa hata kama ni kushtakiwa itakuwa rahisi zaidi.JK tunajua Edo ni rafiki yako lakini kama amehusika usiishie kukubali kujiuzulu kwake ruhusu sheria ifuaate mkondo wake na kumshitaki kama amehusika

    ReplyDelete
  8. Lowassa ahsante kwa kujiuzulu maana atleast hautakuwa kama ndugu yetu Sumaye

    ReplyDelete
  9. Atasingiziwaje bwana!hebu aache hiyo maneno huyu vipi?alale mbelezake yaani majina ya hawa waizi ni kila siku hawa hawa kudadadeki alaa!

    ReplyDelete
  10. KWA UPANDE MWINGINE BINAFSI NITAMISS SANA MISIMAMO YAKO KWA MASLAHI YA TAIFA NA UKALI WA USIMAMIZI WA MAAGIZO NA HASA ILANI ZA CHAMA NAKUMBUKA MSIMAMO WA SUALA KAMA LA UJENZI WA MAHOTELI UKANDA WA UTALII NA MENGINEYO.... HAYA BWANA USIFE MOYO MKO WENGI MKUMBO HUU WENZIO WANAKUJA BADO BUZWAGI, BADO MADINI YETU MACHO

    ReplyDelete
  11. Speech ya muheshimiwa Lowassa imeandaliwa na mtu mwenye kipau cha juu sana cha saikolojia ya watu. Siku zote watu wana muhurumia mtu ambae ajatendewa haki.

    Muheshimiwa alitakiwa ajiuzuru any way, no matter anahusika au hausiki. The main reason ni kwamba muheshimiwa alisha itetea sana Richmond kwamba ni kampuni safi, so akiwa kama waziri mkuu alifanya maamuzi ya kihayawani kuitetea kampuni hewa, ambayo wengi wetu tuishio Marekani knew everything about this company.

    So, bye bye Mr Lowassa, we are going to miss you, but you need to GO

    ReplyDelete
  12. Lowassa anakosea sana anaposema kuwa nchi yetu ni changa...hawa hawa ndio kila siku wana wimbo wa nchi yetu ni maskini wakati wao ni mabilionea. Wana tabia ya kuupotosha umma wakati wao wanafaidi.

    Kamati alijua inafanya kazi na yeye kama raia mwema hata bila ya kuitwa angetembea tu kwa mguu kama anavyosema na kuiona kamati kama walivyofanya raia wengine wema.

    Memo zimetoka ofisini kwake na yeye alikuwa na habari kabisa kuwa kuna uchunguzi wa namna hiyo unaendelea na amekuwa akiitetea Richmond mara kwa mara alishindwa nini kwenda kwenye kamati na kuitetea zaidi?

    ReplyDelete
  13. Lowassa resignation come little bit too late, he should go on the very first day when he was appointed as PM. The issue here is the intergrity of the gov as whole.But gee! you dont have to be a rocket scientist to tell this people they run this scum while leaving behind mountains of finger prints. Mr Lowassa, as it stood, there is no defence on what you have done to the country. If I were your advisor, I could ask you to be a gentleman and apologise to wakulima for letting them down. Your friends Nazir who is arrogants run his office like his kitchen.Are we heading to the Man eat MAn Society? Hope not!!!

    ReplyDelete
  14. Kwani KAMATI ilikufukuza kazi?
    Mtu kukutuhumu si hoja, wangapi wanatuhumiwa lakini wako innocent?
    Yesu mwenyewe alituhumiwa kuzuia watu wasilipe kodi ya kaisari n.k je ilikuwa kweli?

    Mwanaume na Mwanasiasa makini ungekuwa ngangari umwage manyanga with concrete evidence na wewe unayoyajua juu ya actually muhusika wa ubadhilifu juu ya tenda ya richmond hapo ndo ungeona moto unawaka Bungeni ungetusaidia wasikilizaji na sisi mahakimu wa umma kujua nani mwizi kweli.

    Kitendo cha kujiuzulu tu kimya kimya na kubaki kulalama juu ya kutoitwa kimefanya ni cha kitoto. Sasa kila mtu amejiuzuru na kukana kuwa hakuhusika utafikiri kuwa Richmond ilitelemshwa na Mungu toka Houston au ilijitokeza tu kutokana na mabadiliko ya ulimwengu ya the big bang!.

    Ungemtaja waziwazi unayojua nakwambia mbona sasa hivi tungekuwa hakika tuna mnyororo mzuri wa jinsi 10% ilivyotembea!

    Zaidi ya yote mbona sasa bungeni ulikuwepo na ulikuwa na nafasi ya kujitetea? na hapo wewe mwenyewe si haba maana ulikuwa mkuu katika shughuli za serikali? Kama kweli ulijua hukuhusika basi wabunge wa CCM ambao ndio wengi wangekutetea tu!

    Pia, hivi ni wapi panasema kuwa matokeo ya tume maalumu ya Bunge ni FINAL!

    Kama unasoma hapa au jamaa yako nakuuliza yafuatayo:

    1.WEWE na Rais mlijadiliana kuhusu Dk.Balali mkamfuta kazi (sio tu kumtuhumu kama tume ilivyofanya juu yako) je ni lini mlimwita mkamuoji? Mbona Rais asingesema kuwa moja ya rejea ya taarifa ya ubadhilifu wa BOT ni maelezo yake mwenyewe Balali? Tena mmemfukuza akiwa nje ya nchi tena mgonjwa (according to what you told us) je hiyo ndiyo natural Justice? Au unataka common sense yetu iendelee kuamini kuwa ni nyie mlipanga huo mchezo wa kumtoa halafu ndio mjirushe na mistari ya ki-boyz II men???

    2. Nakumbuka kukuona ukimtuhumu na kuagiza mhandisi afutwe kazi(si kumtuhumu tu) ukiwa kwenye sight ya kifusi lilipoanguka lile ghorofa. Wewe ulikuwa umemwita au kukaka na uongozi mzima wa Manispaa na kujua kuwa engineer ndiye muhisika mkuu? Where was that natural justice at that groud zero?

    USHAURI WA NGUVU:


    KWA VILE WEWE NI MWANA SIASA NA BADO UNA MOTO WA KUENDELEA KUONGOZA NA KUISHI KUPITIA SIASA THIS IS WHAT YOU CAN DO EFFICIENTLY NA MSINISAHAU MAANA NA MIMI NI MWANA SIASA AMBAYE SIJARIDHIKA NA MAHALA NILIPO.

    1. JIUZURU PIA HUO UBUNGE ULIONAO NA UTULIE TU NYUMBANI.

    2. MWAKA 2009 WEWE NA AKINA MAREGESI NA TIMU YAKE YA EX- WAZAZI NA HATA AKINA SALIM AHMED NA ZITO NA PROF.LIPUMBA NA HATA ADUI YAKO MWANAKIJIJI (MAANA SIASA HAINA PERMANENT ADUI) MJIUNGE PAMOJA NAKWAMBIA HIYO ITAKUWA THE ORANGE MOVEMENT MAANA MNAJUA INN AND OUT YA SIRI ZAO. DON'T GO FOR PRESIDENTIAL POSITION! UNAMUACHIA MWINGINE TU ANAGOMBEA BAADA YA HAPO ANAKUPA UWAZIRI MKUU AU UWAZIRI WA FEDHA AU MAMBO YA NJE NA FAME YAKO NA KAZI YAKO YA SIASA INABAKI PALEPALE NA WAPINZANI WOTE NA WATANZANIA WENGI WATAKUWA WAMEWAUNGA MKONO SO LONGO AS CCM IS NOT IN POWER AGAIN.

    NITAFUTENI TU MIMI NAITWA OBWATASYO
    TUANZE MIKAKATI. NANI ALIJUA KUWA MOI AU KIBAKI ATAANGUSHWA?

    ReplyDelete
  15. Mimi nafikiri sio wazo zuli alivyojiuzulu. Moja la jukumu lake ni kuwaangaliwa watu wa chini yake wanafanya kazi vyema. Nahilo ameshindwa kwahiyo aanze. Kiongozi sio kazi yake kupokea mshahara tu. tatizo nikuwa labda hizo hela wametumia pia kwa uchanguzi, sasa nafikiri kurudisha itakuwa issue.

    ReplyDelete
  16. Nimefurahishwa na uwazi kidogo ukionyeshwa na watanzania wa kuonyesha furaha yao kwa viongozi wabovo, lakini ningependa kusema waswahili wanasema kufanya kosa si kosa lakini kurudia kosa, Mheshimiwa JK anakubalika sana lakini Tukubaliane ki msingi alifanya kosa kumpa Uwaziri Mkuu Mh, Lowasa, nadhani watanzania wanakumbuka historia yao, Lakini la msingi lililonikera leo ni hotuba ya Mheshimiwa (X WAZIRI MKUU)Waingereza walituachia nchi miaka zaidi ya 40 iliyopita ingekuwa ni binadamu ana wajukuu, lakini cha kushangaza Mheshimiwa anasema nchi yetu bado ni changa swali lini nchi yetu itakomaa? wanasiasa wa Kitanzania achani kutupiga michanga ya macho rekebisheni mambo, kuweni wahaminifu, kubalini kuelezwa ukweli, mambo mnayofanya yamepitiwa na wakati, Mwisho Mh, JK ULIFANYA KOSA KWA LOWASA TAFADHALI USIFANYE KOSA HILO TENA, MUNGU AKUSAIDIE, GOD BLESS AMERICA GOD BLESS TANZANIA. MR VITA

    ReplyDelete
  17. Ndugu Lowassa hakutegemea hilo lilotokea kwani imekua kawaida kwa ka utawala uliopo kila inapotokea kashfa za ufisadi ujaribu kuzifukia kwa kwa kuunda kamati za uchunguzi au kupitia Takukuru au mwanasheria mkuu vyombo hivi vimekua kama taasisi za kuwalinda MAFISADI badala ya kulinda masilahi ya wananchi.Kutokana na shinikizo la wapinzani,wananchi,wafadhili na wabunge wengi wa CCM kuona chama chao kinaelekea ukingoni na kutumiwa na wajanja wachache kutimiza ufisandi wao this time mazingaombwe hayo sasa yamegonga mwamba.Nd.Lowassa ,Rais,Spika baaada ya kuipata taarifa hiyo na kugundua kua ni vitu vya kweli wakaanza kufanya jitiahada zote kuizima lakini kutokana na mazingira niliyo yataja hapo juu ilishindikana hivyo kujikuta ana kwa ana na ukweli.Hotuba yake kabla ya kujiuzulu naifananisha na maneno ya mtapa maji .Uongo,sikuitwa na kamati ,kunamkono wa mtu n.kSawa ukuitwa na kamati kutoa maelezo,kwanini ukutumia muda huo katika hotuba yako ya kujiuzulu katika bunge kuiumbua kamati kwa kusema ukweli na uongo ni upi?Hii naifananisha na mtu aliyefumaniwa akitembea na mke wa mtu kwa vile akulitegemea kauli inayozunguka ulimini ni waongo,sio kweli.Bwana we uko uchi mke wa mtu yuko uchi ndani ya nyumba ya kulala wageni ulikua unafanya nini ?upi uongo?Badala yake ndg.Lowassa anatoa hotuba zisizokua wala kichwa wala miguu.Huyu ndg kwanza anabidi aseme uongo ni upi katika taarifa hiyo na athibitishe .Kama atathibitisha hivyo basi kamati ichuliwe hatua na kama atashindwa kufanya hivyo basi Spika amburuze mahakamani kwa kulikashifu bunge.y
    Yafuatayo ni ushauri wangu kwa Mh.Rais kama kweli amepania kupambana na ufisadi na rushwa;
    1.Washukiwa wote wanapaswa kukamatwa mara moja,akaunt na mali zao kuzuiwa wakati mkondo wa sheria ukichukua nafasi yake.Kwanini?Nafafanua kwanza ili wasikimbia au kuingilia au kuaribu ushahidi,Pili ni kwa ajiri ya usalama wao pamoja na mali zaokwani chuki ya Wananchi kwa mafisadi imefikia kiwango kikubwa katika hali hiyo kua kwao huru na mali zao kutolindwa na serikali ni hatari kwao.
    2.Viongozi wa Takukuru na mwanasheria mkuu wawajibishe mara moja.
    3.Bunge livunjjwe na kutangaza uchaguzi mara moja ili wabunge wakapime imani zao kwa wananchi kwani bunge ili la CCM limechangia kwa kiasi kikubwa kufikia katika hali hii tuliyofikia bunge lisilolinda masilahi ya walala hoi bali masilahi yao wabunge ukiondoa wapinzani hambao ndio wameibua kashfa zote za ufisadi.
    4.Uundaji wa baraza la mawaziri usifate itikadi za kichama bali sifa na uwezo wa mtu .
    5.Watuhumiwa wate pindi mkondo wa sheria utakapogundua kuwa wakosaji walipe gharama zote zilizotumika kuchunguza uozo huo.
    5.Kujiuzulu sio wakati wote nia adhabu,kitendo cha busara au ushujaa.Kama waziri wa mambo ya ndani na miundo mbinu akijiuzulu kufuatia ajari zinazotekea na kupotza maisha ya watu kila siku ambapo mambo mengi yako nje ya uwezo wake kitendo hiki tunaweza kukiita cha kishujaa na cha busara na kumpa Mh.Rais nafasi ya kutafuta mchakato wa kuimarisha sekta hiyo.Lakini kama waziri mkuu,waziri au kiongozi yeyote atakapochota pesa za walalahoi kwa ufisadi na rushwa na kujiuzulu na kwenda kutumia pesa zake kwa njia ya ufisadi huyu sio shujaa ni fisadi na mahala pake ni gerezani.Kwani kumekua kunawatu wanaosema hatua ya kujiuzulu ni za kishujaa na za busara ni ushujaa gain aliofanya ndg.Lowassa kuwabebesha wananchi gharama za umeme zisizo na msingi?Anaweza kua Shujaa mbele ya Richimud lakini mbele ya walala hoi ni FISADI.
    Hatua nilizozitaja hapo juu ziwe kwa viongozi wote kwa kufanya hivo, ile kauli ambayo imesahalikakaUONGOZI NI DHAMANA.Mh.Rais kama hayo niliyoyataja hayatatekelezwa .Yotea hayo yatakua mazingaombwe na hatutasita kukushirikisha na yote yanayotokea na tutachukulia kujiuzulu kwa Lowassa ni mbuzi wa kafara.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  18. Nakukumbusha kuwa usisahau kutaja majumba iliyo nayo ili vipigwe mnada, wananchi wasikeshe visimani wanangoja maji, wewe una kula maraha tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...