PONGEZI KWA MH RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE


Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza rais wetu Mh Kikwete kuchaguliwa kwake na umoja wa Afrika kuwa mwenyeketi kwa kipindi cha mwaka mmoja,mh rais nakupongeza sana na ninakutakia kila la kheri katika kazi hii nyeti .pili nakupongeza kwa hotuba yako nzuri ya mwisho wa mwezi wa kwanza(january) mh ,hotuba yako ni ndefu na nzuri sana na ziara yako ya mkoa wa kagera.
Nikianza na hili la umoja wa afrika ,hili litasaidia katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kisiasa ,kiuchumi na kijamii,kwani naamini kabisa katika safari zote za kikazi mh rais atakuwa akitumia kofia zote mbili katika kuitangaza afrika na Tanzania kiujumla. Afrika imefika mahali ambapo inahitaji kuwa na misingi mizuri ambayo itasaidia nchi zake kujikwamua kiuchumi,kisiasana kijamii ,misingi hiyo ndio imesaidia jumuiya kama za asia(India,Srilanka,maldives,pakistan),asia ya kati kama Thailand,Singapore,Malyasia,Indonesaia nk ,jumuiya hizi zimefikia mahali ambapo nchi za kibepari zimekuwa hazi lali usingizi kutokana na maendeleo yake yanayopatikana kila kukicha,
Leo, London stock exchange inajiuliza what happen at Mumbai stock exchange to day?,zamani ikiitwa Bombay,(India) shangai,hongkong,tunahitaji nasi tufike mahali wajiuleze what happen at D’salaam,Cairo,Lagos,Johanesburg, ?na nk,tukiweza kufika hapo basi yale yote wanayofikiri kuhusu Afrika yatakuwa yakiwasuta wao wenyewe kama yanavyowasuta yale yanayotokea Mumbai,Hongkong,,Bangkok na nk
Pili nakupongeza Mh rais ktk hotuba yako ya mwisho wa mwezi wa kwanza(january),ktk hotuba yako jambo la mwisho ndilo ambalo naamini limewavutia wengi na mimi binafsi,kuhusu maadili ya viongozi na uongozi ,hili ni jambo kubwa sana katika kuhakikisha nchi inasonga mbele, ni lazima ;wala si hiari kwa wale wote wanaopenda kutumikia uma wa nchi zao kuachana na biashara ya aina yeyote kama wanazo ,hili litasaidia kupunguza rushwa ,umimi,usisi,uwao katika maslahi ya Taifa,Mh rais naamini hii ni ishara kwamba what next after that………………….,na kwa kuwa limejadiliwa na kamati kuu ya CCM,litafika serikalini muda si mrefu na kupelekwa bungeni kama muswada,ili lipitishwe kuwa sheria,mh rais nakuombea kwa mwenyezi mungu maisha marefu,afya njema ili uweze kulisimamia hili kwa uadilifu,nchi kama India zaidi ya hili haihitaji raisi,waziri mkuu,mbunge,waziri kiongozi,katibu mkuu na nk kuwa na nyadhifa mbili zaidi ya ile moja aliyokuwa nayo(hili lipo katika katiba yao)tunafaham katiba ya India ndio kubwa kuliko zote duniani,nchi za kibepari katiba zao zinaingia kwa India ..,kama ifuatavyo….marekani mara saba,France mara tano,Australia mara sita na nk
Katika hili la maadili ya viongozi na uongozi, ndio linalotokea leo hii kwa mfanyabiashara maarufu na mmliki wa manchester city ya uingereza(football club) Dr Thaksin shinawatra alipokuwa waziri mkuu wa Thailand siku za nyuma ,leo hii ana kesi ya kuhusiana na rushwa alipokuwa waziri mkuu,japo alikuwa ni mfanyabiashara hata kabla hajawa waziri mkuu wa Thailand.

Nampongeza Mh raisi pia katika ziara yake ile ya mkoa ule wa kagera ,pale alipozungumza na wananchi wa muleba/Biharamuro na kusisitiza katika suala lile la ujambazi ,kwa kuwataka wanaowafaham majambazi hayo wayataje ,ama yajisalimishe yenyewe,ni kweli wananchi wanawafaham,kwani ni wajomba,mtoto wa kaka,dada,binamu,nakuunga mkono 100% kuweka mikakati mipya ambayo itasidia kulikomesha hili,ambalo limekuwa sugu sana kwa sasa,wenzetu wanasheria inayosema “shoot order to kill” hii ikiwa na maana ukihisiwa tu kuwa wewe ni jambazi basi unauwawa,hakuna mahakamani wala gerezani nchi kama Brazil,Nigeria,Amerika ,Afrika ya kusini hili linafanyika na nchi nyingine nyingi tu duniani , hata jirani zetu Kenya ilikuwepo wakati wa utawala wa Moi miaka fulani fulani, sijui kama bado iko au la...,lakini mm nasema iliwasaidia jirani zetu naamini kwa Tanzania tunahitaji mbadala wa hili ,ambalo litawezesha kumaliza suala la ujambazi nchini.
Napenda kumtakia Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete afya njema,maisha marefu na vilevile naitaki a nchi yangu ya Jamuhuri ya muungano waTanzaia amani na upendo na afrika kwa ujumla.


Ni mtanzaia mwenzenu Baraka Abdallah kange,Bangalore,India.nikiwanafanya shahada ya kwanza ya uongozi wa biashara na fedha.


BARAKA ABDALLAH KANGE,
M/KITI JUMUIYA YA WANAFUNZI WA TANZANIA,
BANGALORE,

INDIA.
MOBILE: +91-9886933877,
EMAIL:barakakange@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

 1. Bwana mdogo, this is not the best way ya kujiwekea mambo safi.. Mpaka watoto woote wa wateule watakapopata ulaji ndio laaabda na wewe utaweza kuwekwa kwenye picha. Tafuta another alternative dogo

  ReplyDelete
 2. oooh jamaa analazimisha tabasamu lakini hakika kachoka na maisha ya india, maana yake hata shati lina muelemea!

  ReplyDelete
 3. Mi naona unanizingua tu na lihotuba lako lisilo na mwanzo wala mwisho.... Kama ulitaka kujulikana ungetuma tu picha na salam zako siyo kutuandikia hotuba na kuorodhesha cheo chako hapa....

  ReplyDelete
 4. Sawa mkuu tumekupata....

  ReplyDelete
 5. Sawa mzee kwa pongezi zako kwa Muheshimiwa.Kidumu

  ReplyDelete
 6. We zoba kweli, unazani umaarufu wa kujulikana unakuja kwa kuandika lihotuba lilefu hivi? au ndiyo staili yako ya kuomba kazi ccm na hilo shati lako la njano na kijani lililo kuvaa.
  hakika huko India kumekuchosha.

  ReplyDelete
 7. bro michu naomba kuuliza..hivi rais wetu JK anasoma hii blog yako kweli? ashakum si matusi ila nafikiri hizo pongezi hapa sio mahali pake. kwanini mdau asingepost kwenye blog ya serikali au aandike barua rasmi kwa rais na aipeleke ubalozini huko India. ameniboa..

  ReplyDelete
 8. Yakhe hebu acha kupka siagi na kulamba viatu mpaka rangi idondoke!!!ukitaka kurudi nyumbani njoo tu na sie tutakufikisha ikulu kumsalimia mama Ridhuani!!!!!

  ReplyDelete
 9. mwacheni mkereketwa wa watu jamani

  Yaani kanichekesha sana...kaandika vitu vingi kama geek vile lakini hajakaa kigeekgeek huyu...hawa ni wale....too much know...humwoni ni mwenyekiti wa international student...ha ha ha ha ha....

  Atakua naye mbunge sooon

  Kweli mshikaji hotuba yako refu saaana

  kaka michuzi kazi unayo...naona unapokeaga vingi sana tu...Sasa huo mda wa kusoma hiyo hotuba kabla hujaibandika huko....mhhhh...bora tukulipe siku hizi au tukutafutie assistant

  ReplyDelete
 10. This guy, like to promote himself, like to b' praised, etc.
  This is not the right place

  ReplyDelete
 11. Hawa watu wa namna hii ndio waliojaa serikalini nakwambia, watu wa kujikomba komba kwa wakubwa...watu wa NDIO MZEEE..

  Honestly huwa wananikera sana!

  ReplyDelete
 12. hiyo kozi ndio kama BBA?anasomea shahada ya kwanza mwenyewe!

  ReplyDelete
 13. Huyo India atakuwa anasomea zile digrii za sanaa zenye mamneno mengi angekuwa anasomea digrii kali zile za sayansi asingekuwa na muda wa kuwaza na kuandika hayo maneno.

  Halafu mhurumieni si mnaona kavaa shati la kitenge la shilingi Elfu tatu kwenye maduka Manzese.

  ReplyDelete
 14. i have never seen such a stupid guy in my entire life! Unadhani kujikomba komba kwa rais ndo na wewe utapata kaulaji? Hivi unasoma nini huko halafu unaonekana huelewi.. Siku nyingine reserve mipongezi yako! UMENIBOA SANA!!!

  ReplyDelete
 15. Too much maelezo, mwenyekiti na hawo wenzio wako wapi? Ungeweka picha ya pamoja.

  ReplyDelete
 16. hivi wewe hujaona yaliyompata mwenzio Chibiliti ?
  haya we weka picha yako tu humu ndani
  unawatafuta watu uchokozi
  mmmmmmmmmhh

  ReplyDelete
 17. Huyu mtoto wa Mwalimu Kange naye. Wewe mtoto unataka sifa tu ya kujipendekeza kwa JK. Vipi mwalimu Kange yupo wapi siku hizi?

  ReplyDelete
 18. wabongo hamna dogo jamani, kama aliamua kujieleza mwacheni, na pili bora aweke ujumbe kwa michuzi baadhi ya balozi uko ulaya hazina huduma nzuri kwa wananchi, haswa uko america, sijui kikwete anapohamisha watu, anafanyaga uchunguzi, bora mwenzenu kajiwekea kwa michuzi.

  ReplyDelete
 19. jamani nyie wabongo vinawaumeni nn? mwenzenu katoa hutuba je nyie za kweni zikuwapi !!!!! wabongo bwana uswaili amuachi. tuacheni tabia za majungu

  ReplyDelete
 20. MH! KWANI WEWE NI NANI?
  YAANI BADO SIELEWI...HIVI WEWE NANIIIII? KILOBOTO, CHAWA, MZEE JONGO, TAMBALA, CHENGA...KAMA MSANII VILEEEE
  KWANI WEWE NI NANI WEWEEEE MBONA HUJIBUUUUUU?


  fsyuuuuuuuuuuuuuu )sonyo hiloooo)

  ReplyDelete
 21. who the hell do u think you are?au ndio umeambiwa ukianza hivyoo nawe utafikia stage za uccm at higher stages?? shwenzy taipuuuu wee subiria watoto wa wenzio wenye majina makubwa wapewe vyeo then ndio na wewe wafikirie ka waweza fit kwenye kazi ya ufagia ofisi za hiyo sisiemu yako wanaoji rich mondisha mifuko yao kwanza

  ReplyDelete
 22. jamani jamani nyie watu mwadiriki kumtusi hivi huyu kaka wa watu mjue labda ndio kikwete wenu wa bidae??!!mtakuja kumbuka matusi na kejeli mlizompa mjue eti kashati ka elfu tatu (kama ni that expensive), mie nasave hii page kwenye email yangu akiwa raisi nije muonyesha anipe cheo na mie maana naona na yeye ndio anajitahidi kuanza tafuta kujulikana kwa njia hiyo

  ReplyDelete
 23. wewe bwana hatuendi hivyo,kama wataka ujulikane who you are na vitu kama hivyo tafuta njia nyingine sio kwa kutuboa na speech lako yaani umenikera wewe mtu hivi wasoma kweli huko uliko?waonekana mtu mzimaaa lakini umedumaa nini tatizo?

  ReplyDelete
 24. eeh..yani wabongo,hamna dogo,mmezidi jamani kama hamtaki kuisoma hotuba yake si muache?mnachonga kama sio Mtanzania mwenzenu vile..mmesahau Watanzania wote ni ndugu?

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...