Taarifa ya Mhe Profesa Lipumba juu ya Uteuzi wa Mhe Jakaya Kikwete kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa AU


Directorate of Information and Policy Dissemination

The Civic United Front (CUF)

Party Headquarters

P.O. Box 3637

Zanzibar

Tanzania

Tel. (+)255 (0)747 414100

(+)255 (0)741 257 665

E-mail:
cufhabari@yahoo.com
Website: www.cuftz.org

Kufuatia kuchaguliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Mheshimiwa Prof. Ibrahim Lipumba, ametoa taarifa ifuatayo:

“Nachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Jakaya Kikwete kwa heshima kubwa aliyopewa na viongozi wenzake wa nchi za Afrika waliyomchagua kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa mwaka huu wa 2008.

Chama Cha Wananchi (CUF) kimezipokea habari hizo kwa furaha kubwa na kinaiona heshima hiyo ni ya Tanzania na Watanzania wote kama Taifa bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa. Hapana shaka kwamba kuchaguliwa kwa Rais Kikwete kuuongoza Umoja huo kutasaidia kuzidi kuipandisha chati Tanzania na kuitangaza kimataifa.

Pamoja na kuwa ni heshima kubwa kwa Rais wetu na kwa nchi yetu, hatua hii inatupa changamoto zaidi kuzidi kuling’arisha jina la Tanzania katika bara la Afrika na ulimwengu wa kimataifa kupitia nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Natoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa mfano katika ujenzi wa demokrasia ya kweli kwa kujenga taasisi imara zitakazohakikisha sauti ya wananchi inasikika, maamuzi yao yanaheshimiwa na uwajibikaji unaimarika.

Katika uchumi, Tanzania iwe mfano katika kuhakikisha tunatumia rasilimali zetu nyingi na za kutosha kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake kwa kujenga uchumi imara wa soko huria linalotoa ajira, tija na neema kwa wananchi wote. Na katika masuala ya kijamii, Tanzania iwe mfano katika kufikia malengo ya milenia.

Hii pia ni nafasi adhimu ya kukamilisha mazungumzo ya CCM na CUF ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar ili kumpa nafasi Rais Kikwete ya kushughulikia vyema migogoro mingine ya kisiasa barani Afrika, ambalo litakuwa sehemu muhimu ya majukumu yake akiwa Mwenyekiti wa AU.

Namhakikishia Rais kuwa mimi binafsi na Chama cha CUF tutampa kila ushirikiano na msaada anaouhitaji katika kutimiza matumaini ya Waafrika wenzetu waliotuamini kuuongoza Umoja wa Afrika. Kwa mara nyengine tena, tunasema hongera Rais Kikwete.


DAR ES SALAAM
1 Februari, 2008

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. We Lipumba naona unaanza kutapika Pumba...Unamfagilia JK ua ndo kujigonga......???

    ReplyDelete
  2. Mzee,hebu acha hizo pongezi dururu!
    Heshima ni yake bwana kwani taifa litanufaika nini?Kitu ambacho sasa kitawasumbua raia ni kuona ziara za nje za Mheshimiwa JK sasa zitashika kasi ambazo zitaifirisha hazina ya taifa...labda ndio hilo mlichunguze kwa makini!!!

    ReplyDelete
  3. Nikiwa kama kada wa CCM,kwa moyo wa dhati kabisa napenda kumpongeza Mh.Lipumba na chama chake cha CUF kwa taarifa hii iliyojaa ukomavu wa hali ya juu kisiasa.Ni taarifa ambayo kwa kweli imejali utaifa na uzalendo zaidi ya tofauti itikadi za kisiasa tofauti kabisa na nilivyomsikia Mh. Mrema alipokuwa anahojiwa na BBC kuhusu uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete na Tanzania kwa ujumla kuwa Mwenyekiti wa umoja wa Afrika.Naheshimu maoni ya kila mtu maana hiyo ndiyo demokrasia.Lakini nadhani demokrasia inahitaji hekima na busara pia inayozingatia hali halisi na wala sio kupinga kila jambo.Naungana na Mh.Profesa Lipumba kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa huu ni uteuzi wetu sote bila kujali itikadi zetu.Mafanikio yake ni mafanikio ya watanzania wote halikadhalika kushindwa kwake ni kushindwa kwa watanzania wote.Kwa maana hiyo tuna kila wajibu wa kumpa ushirikiano wa kila hali Mh.JK katika kutekeleza majukumu yake katika kipindi chote cha uongozi wake kama mwenyekiti wa AU.
    Mungu ibariki Tanzania.

    Tumsifu,Bowling Green State University,Ohio-USA

    ReplyDelete
  4. Kiss Ass At It's Best !

    ReplyDelete
  5. Kweli Lipumbu unaonyeha umekomaa kisiasa. Nakupongeza kwa hilo kweli wewe ni kiongozi unayejali sana utaifa wetu kama Wa-TZ.Heko CUF pia.

    ReplyDelete
  6. michuzi unapenda sana habari za kusifia ccm ,ukiletewa habari za ufisadi wa bot roho inakudunda utasema na wewe ulikula hela kumbe unafanya kazi kwenye gazeti la serikali.usiogope kukosoa makosa kaka .wananchi tunaweza kusikika kupitia nyinyi waandishi wa habari uwezi kukuwepa makosa yote ya serikali.unakimbia sana hoja ya kwa nini dk.balali asiletwe nchini kujibu mashitaka/

    ReplyDelete
  7. anon 3:20:00 nakupa 5 m2 wangu....ebwana ehe unakumbuka enzi za mwl nyerere mapumziko anenda kujiachia butiama,mzee ruksa alikuwa anenda znz au mwanalumango, big ben mjasiliamali alikuwa anenda masasi au ukweni kujiachia, lkn inakuwaje jk mapumziko ya 2006 alikuwa zamani kempisiki znz amekula zaidi ya 800m za kibongo na 2007 kala kama 950 m huko ngurudoto atwn, maisha bora kwa kila mtz yatakuwepo au ndio longolongo za bongo flavor????

    ReplyDelete
  8. ...Hivi mazungumzo ya CUF na CCM kutafuta ufumbuzi wa mpasuko bado yanaendelea tuu??? KKkaaaazz, kwel kwel!!!

    ReplyDelete
  9. Sidhani kama JK anahitaji pongezi kwa kuchaguli kuwa mwenyekiti wa AU kwani nafasi hiyo ilikuwa ni obvious kwa Tz kwani nchi nyingi za mashariki mwa Afrika hazikuw na sifa ya kutoa kiongozi aliyetakiwa.

    ReplyDelete
  10. Naona kuna ugonjwa mpya umeingia TZ, unaitwa ugonjwa wa SONONI watu kila kukicha sononi, panapo baya sononi mahala pake kama huumwi ugonjwa huu, lakini kama hata yakitokea mazuri basi wewe unaendelea kusononeka, wahi hospitaki haraka. Sononi inaua. Na dalili zake ni hizo mgonjwa husononekea kila kitu kinachopita mbele ya macho yake kiwe kizuri kiwe kibaya.

    Hongera Mhe. Mwenyekiti wangu wa CUF kwa kuonyesha ukomavu wa kiakili na kisiasa kwa kumpongeza Rais Kikwete kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa AU. Wanaofikiri kuwa siasa ni kupinga tu kila kitu wanaumwa SONONI.

    ReplyDelete
  11. Wewe bwana Lipumba ni mtu safi sana pongezi hizi najua unazitoa moyoni mwako na si vinginevyo wewe ni msomi safi muadilifu huna jazba unakila aina ya sifa za kuwa kiongozi wa nchi tatizo lako ni chama ulichojiunga nacho hao jamaa hawabebeki ,hawakupendi wanafiki kwelikweli ufanyapo vikao na wao pia huenda kufanya vya kwao kisiri kujadili mliyoyasema wakati ule nakuambia hizo ni habari nyeti amini usiamini hawakupendi wanakufanya tingatinga uwasafishie njia wapite mnyamwezi na wapemba wapi na wapi ukisoma nakuwasikiliza wanachama wako wengi wao hawakuamini wanasema wewe ni ccm hasa unapopata safari za nje wanawasiwasi na safari zako,ushauri wangu kwako achana nao lasivyo utapoteza heshima yako kama mapalala na sisi wanyonge tunakuhitaji sana kwa mawazo yako mazuri na hotuba zako zilizojaa mafunzo hasa kuhusu uchumi huyo katibu mkuu wako ndio nyoka kabisa kama hujui bro take care nawasilisha tafadhali yafanyie kazi maneno yangu unachelewa kupata ridhaa zetu kama kiongozi wa nchi kwa sababu ya chama unachokiongoza kwa bendera tu wenye chama wapo pemba kweli unaweza kusoma ukakosa elimu wewe ni profesa hujui kinachoendelea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...