PAMOJA NA KWAMBA WAZIRI MKUU MH. LOWASSA, WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MH. NAZI KARAMAGI NA WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI MH. DK MSABAHA KUTANGAZA NIA ZAO ZA KUJIUZURU NYADHIFA ZAO, BADO WANAENDELEA KUWA VIONGOZI KATIKA NAFASI HIZO HADI HAPO JK ATAKAPOJIBU MAOMBI YAO. KWA LUGHA INGINE NI KWAMBA MPIRA UKO GOLINI KWA RAIS NA YEYE NDIYE ATAKAYETOA UAMUZI WA MWISHO KWAMBA WAACHIE NGAZI AMA LA. NAOMBA WADAU TUWE NA SUBIRA. HIVI SASA MJADALA UNAENDELEA NA HAKUNA NENO TOKA KWA JK HADI DAKIKA HII

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kaka pole na kunguru wa z'bar. Nasikia kuna nyumba za polisi moshi zimeungua (kama Nyumba 27) kama ni kweli nawapa pole sana waliounguliwa na nyumba zao

    ReplyDelete
  2. Michuzi kulingana na katiba Rais halazimiki kukubaliana na ombi la kujiuzulu la waziri mkuu..akishasema amejiuzulu, ndo imetoka iyo

    ReplyDelete
  3. Kaka michu,hawa watu kwanza wanyang'anywe passport maana hawachelewi kusema wanaumwa wanaenda kwenye matibabu..pili,tunaomba hizo hela walizoziiba warudishe kwa wananchi...tatu,kikwete anatakiwa hili swala aliamulie vizuri,pamoja shoga yake yupo matatizoni..asante

    ReplyDelete
  4. twasubiri kwa hamu isiyo na kifani kusikia toka kwa JK!...

    ReplyDelete
  5. Na JK naye inabidi ajiuzuru.. Sasa nani atakayetoa statement?

    ReplyDelete
  6. JK anawakati mgumu sana kuamua hili;
    sitamlaumu kwa uamuzi wowote atakao utoa; kupoteza viongoz wakubwa watatu ni hatari sana;
    Ila litakuwa Fundisho hata kwa viongoz wengine wajao,
    Hii ndio Siasa inayotakiwa ya kufichua madhambi yootee.

    Mungu mbariki Jakaya Kikwete;
    Mungu Ibariki Tanzania.

    Tuombe na kusali Wezii woote wa mali ya umma wawajibishe kwani siku za mwizi ni arubaini;
    Ingekuwa kwetu Migo migo hakuna kukatiza angeshachomwa moto hapo!!

    ReplyDelete
  7. Hivi unafikiri kujiuzulu kwa hao mawaziri ndio kutawaweka Chadema madarakani? Mbona kuna wabunge kibao wa CCM ambao watachukua nafasi zao bila hofu na JK hajiuzulu ng'oo. Ukisikia ukubwa dawa ndio huo umeshutumiwa bila ushahidi unakaa pembeni kupisha uchunguzi.

    ReplyDelete
  8. Kwanza natoa pongezi kwa kamati hii[naiita kamati bora].Namsifu mwenyekiti wa kamati na bunge la Tanzania.Kwa kuona kuna tatizo na kulifuatilia[Richmond company].Sasa hakuna la ziada hapo kama wamejiuzuru,inayofuatwa ni kufilisiwa kila kitu hadi mbwa wake au kuku wachukuliwe.Hatuwezi kulea watu wezi namna hii.TANZANIA TUAMKE NATUSIMWOGOPE MTU,ILA SEMA KWELI PALE KWENYE UKWELI.NINAONA TANZANIA INAKWENDA CANAN[NCHI YA AHADI]MUNGU IBARIKI TANZANIA NA AFRICA KWA UJUMLA.

    ReplyDelete
  9. Tanzanian PM to resign over graft

    Tanzania's Prime Minister Edward Lowassa has tendered his resignation after being implicated in an energy deal corruption scandal.
    He has denied that his office was involved in improperly awarding a contract to US-based electricity company Richmond Development in 2006.

    The firm failed to provide emergency power during a power crisis in 2006.

    Following Mr Lowassa's announcement to parliament, two other ministers linked to the scandal resigned.

    The BBC's Africa analyst Mary Harper says the offer of resignation from such a senior member of government for alleged links with corruption is unprecedented in Tanzania, and unusual in Africa.

    But Tanzania has been getting more serious about corruption since President Jakaya Kikwete was elected in 2005.

    Just last month, the governor of the central bank was sacked following the disappearance of public funds from the bank.

    'Lacked expertise'

    The BBC's Vicky Ntetema in Dar es Salaam says Richmond was contracted to bring in generators to provide 100 megawatts of electricity each day after a drought early in 2006 left low water levels in dams leading to severe power cuts.


    I've offered my resignation... to register my disagreement with the manner in which the committee misled parliament
    Edward Lowassa
    Tanzanian prime minister

    But a parliamentary inquiry, launched in November, found that the generators failed to arrive on time and when they did, they did not work as required.

    By the time the company was ready to start operations, Tanzania's power problems had been resolved.

    Despite these failings, the government was contracted to pay Richmond more than $100,000 a day.

    Mr Lowassa's office later influenced the government's decision to extend Richmond's contract despite advice to the contrary from the state-run energy company Tanesco, the inquiry alleges.

    Richmond "lacked experience, expertise and was financially incapacitated", ruling party MP Harrison Mwakyembe, who headed the investigation, is quoted by Tanzania's Guardian newspaper as telling parliament on Wednesday.

    Richmond transferred its tender to another company, Dowans, last year.

    Emotion

    Mr Lowassa, who has denied any links to the scandal, has suggested the parliamentary committee investigating the energy deal was given the wrong information.

    "I've thought long and hard about this issue. I've offered my resignation without any ill motive," he said in an emotional speech to parliament on Thursday morning.

    "I've done it to as a sign of my responsibility and to register my disagreement with the manner in which the committee misled parliament."

    Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi and Ibrahim Msabaha - a former energy minister and now in the East African Community ministry - resigned on Thursday afternoon.

    Our correspondent says Mr Lowassa, who entered politics in the 1980s, is a very close ally of President Kikwete.

    But the president is likely to accept his resignation in light of public anger over the scandal, she says.

    This is not Mr Lowassa's first brush with controversy.

    Under President Ali Mwinyi, he was relieved of his duties as a land minister because of allegations of corruption - a scandal that reportedly infuriated Julius Nyerere, Tanzania's respected independence leader.

    ReplyDelete
  10. Mimi naelewa mtu ukishajiuzulu ndio basi, haitegemewi kukubaliwa au kukataliwa. Kumkatalia mtu kujiuzulu ni sawa na kumlazimishia kazi ambayo ni kinyume na utashi wake. Nikitamka nimejiuzulu kazi, ni wajibu wa mwajiri wangu kutafuta mtu mwingine wa kufanya kazi hiyo. Ingekuwa kustaafu au kumaliza mkataba, hapo ni tofauti, inajadilika mwajiri anaweza kukuambia muda wako wa kustaafu bado, au akakuomba uongeze mkataba. Lakini kujiuzulu ni kuacha, kuondoka.

    ReplyDelete
  11. Kutoka kwenye katiba Kifungu 57 (2)(e) Waziri Mkuu Akijiuzulu serikali yote (Baraza la mawaziri) wanatakiwa wajiuzulu. Hii ndio Hoja aliyotoa Iddi Simba kuwa alijiuzulu ili kuepusha waziri mkuu (Sumaye) na serikali nzima kuvunjwa. Kwa hiyo hapo JK atavunja Baraza la Mawaziri na Kuunda upya. Sijui kwa nini Bunge bado linaendelea wakati Serikali haina kiongozi Bungeni (Waziri mkuu amejiuzulu, yeye ndio kiongozi wa serikali Bungeni)

    ReplyDelete
  12. Michuzi hili la kusema NIA KUJIUZULU mnapotosha hali halisi ukweli na mnaleta siasa za kupooza mambo. Kisheria Kama WAMEANDIKA BARUA NA KUITUMA (kUITUMA maanake ni kwamba hatua ya kuifikisha barua kwa mlengwa kwa mfano kuipeleka posta na kutumbuiza kwenye box au kumkabihi mtu aipeleke, au kumkabidhi anayehusika, nk;; yaani wakati hiyo barua inapotoka kwenye umiliki wako) basi hiyo si NIA tena bali UMESHATEKELEZA nakilichoandikwa kinakuwa na nguvu KISHERIA. Ukitaka kubadili inabidi uandike barua nyingine tena. pia katiba haisemi "Akijiuzulu na kukubaliwa" inachosema ni "akijiuzulu" ambako ushahidi ake ni huko kuwasilisha barua. HIyo kama wamepeleka barua za kujiuzulu basi tayari wamejiuzulu. lakini ni wajanja hawa wanatka kumuwekea JK mtego na ndo maana wamepeleka barua za KUOMBA KUJIUZULU. Sasa janja yake asijibu hizo barua bali atangaze wakushika nafasi zao. Full stop. atakuwa kamaliza kazi na wataondoka automatically. Haya maneno ya NIA za kujiuzulu ni katika KULINDANA tu hamna lolote. KAtiba haisemimtu "akiomba kujiuzulu" bali inasema mmtu "akijiuzulu". WAACHE JANJA YA NYANI. Soma vifungu vya 50 hadi 60 Toleo la 1998.

    Kuhusu Waziri MKuu akijiuzulu ni baraza lote ni kweli katiba inasema hivyo lakini ndo mfano mwingine wa kukosekana umakini katika maandishi yetu. Huo ni mfumo unaotumika katika nchi ambazo Waziri mKuu ndiye Mkuu wa SERIKALI mfano UINGEREZA. Nchi yetu ni jamhhuri mabapo Rais ndiye Mkuu wa nchi na vilevile Mkuu wa serikali (kisheria nchi, taifa na serikali ni vitu tofauti. Basi wataalamu wetu walikopoï bila kuwjua uhalisia na utekelezaji wake. Nadhani baada ya hapa watabadili hilcho kifungu.

    Kwa katiba hiyo hata waziri mkuu akifa hakutakuwa na baraza la mawaziri. Naamini walioweka hicho kifungu hawakuwa na dhamira hiyo japo ndio maanake.

    Kila la kheri Lowasa, Karamagi na Msabaha. Kazi iliyobaki ni namna gani bei ya umeme itashuka. HAo akina Lowassa enzi yao ndo imepita hivyo laikini ughali wa maisha uko pale pale. wabunge wajadili hilo zaidi ili kmnufaisha mwananchi na si NIA za KUJIUZULU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...