wachimbaji wadogo wa madini mererani maarufu kama wana-apollo wakisubiri wakati zoezi la kuwatoa wenzao waliopatwa na maafa watolewe migonini
PINDA AAGIZA MAWAZIRI WATATU WAENDE MERERANI

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewaagiza mawaziri watatu waende mara moja katika eneo la Mererani mkoani Manyara kutathimi maafa ya mafuriko yaliyosababisha vifo katika machimbo ya madini ya eneo hilo.

Mawaziri hao ni wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Philip Marmo; Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha.

Katika taarifa yake Waziri Mkuu Pinda ambaye yuko mkoani Mara kwa vikao vya CCM alisema kuwa mawaziri hao watatathimini hali ilivyo na baadaye kutoa taarifa itakayoiwezesha serikali kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na hali hiyo.

Waziri Mkuu amesema serikali inafuatilia kwa karibu tukio hilo na inawapa pole ndugu na jamaa wa marehemu na wahusika wote.

Mafuriko hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana Jumamosi Machi 29, 2008 na kusababisha maji kuingia katika machimbo ya madini.

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu, imeeleza kuwa maiti sita walipatikana kutoka katika machimbo hayo yaliyojaa maji ya mafuriko kutokana na mvua kubwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kulikuwa na watu 74 waliorodheshwa kuwa waliingia katika machimbo hayo wakati mafuriko yanatokea na 20 walipatikana wakiwa hai.

Haijajulikana hali za watu wengine 48 kati ya hao walioingia kwenye machimbo hayo, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Poleni sana wafiwa na ambao bado hamjajua hatima ya ndugu zetu tunaomba Serekali ijitahidi kuwaokoa hau ndugu zetu nasema tupo wote katika kipidi hiki kigumu kwenu Pia natoa pole kwa wanaapollo wote kwa kuondokewa na ndugu zao wapendwa.

    Katochi)

    ReplyDelete
  2. Kaka michuzi, umeshaanza kuficha comment, sasa kwangu mimi kusema serikali kupeleka mawaziri watatu itasaidia nini ?? badala ya kupeleka magreda, pump za maji, elimu ya uchimbaji na permanent base yawakumahasisha hawa jamaa wa uchimbaji kuweza kupata elimu ya kutosha katika kuendeleza fani yao ya uchimbaji. MEngine mikopo midogo midogo, Vifaa vya usalama kama ajali kama hii ikitokea, na vile vile uwekezaji wa vituo maalum kuwahisi wasiingie kwenye migodi once kukiwa na MVUA(point hii inambatana na ELIMU kwa ujumla)

    Mdau wako Mpendwa.

    ReplyDelete
  3. haya ni maafa makubwa yametukuta Watanzania me nawapa pole wafiwa kwa kipindi hiki kigumu kwako nawaombea kwa Mungu awatie nguvu kubwa wape faraja.



    NB: SERIKALI IANGALIE SANA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO KWANI WANAFANYA SHUGHULI ZAO KWA RISK KUBWA YAANI VIFAA NI DUNI NAFIKIRI HII NI MARA YA 2 KUPATWA NA MAAFA HAYA MAKUBWA WAHUZIKA WATAFUTE UFUMBUZI WA KUDUMU

    ReplyDelete
  4. PINDA umechukua ofisi juzi tu sasa unaanza kuchemsha mapema namna hii, haya ni maafa ambayo hakuna muda wa mawiziri kwenda kuangalia kutoa report halafu ndio serikali ichukue hatua za haraka, haya ni maafa yanayohitaji hatua za haraka kuchukuliwa mara moja. Kutuma mawaziri ni kupoteza muda muhimu unaoweza kuwaokoa ndugu zetu. Huna haja ya kungoja report PINDA unaanza ku-bore mapema mno...

    ReplyDelete
  5. Mungu awalaze mahala pema peponi. walikuwa wanajitafutia riziki tu kama tufanyavyo sote. kwei mwanadama hajui siku wala saa.

    ReplyDelete
  6. kwanza kabisa poleni sana kwa wafia wote na taifa zima la tanzania kwa ujumla hio ndio mitihani,m,mungu atupe uvumilivu na nguvu na wale wote waliofiliwa wake na moyo wa subra.

    ReplyDelete
  7. Naanza kwa kuwapa pole watanzania wenzetu wafiwa. Watanzania tuungane pamoja katika kipindi hiku cha majonzi.
    Lakini kinachonishangaza ni hao waheshimiwa wabunge waliotakwa na mheshimiwa waziri mkuu waelekee mererani. Hivi kwani wao hawajui wajibu wao mpaka waziri mkuu awatake waelekee huko? Waziri wa madini, waziri wa mambo ya ndani walikuwa wanasubiri waambiwe wajibu wao? Hawa waheshimiwa,hawajui wajibu wao? Mheshimiwa Rais, hawa ndio watu uliowaamini wafanye kazi kwa niaba yako bila ya kusubiri kusukumwa? Tutafika kweli watanzania kwa kasi hii?

    ReplyDelete
  8. JAMANI MBONA VIONGOZI WA HIYO MIGODI HAWAANGALII VIPINDI VYA HALI YA HEWA WAKAJIWEKA SAWA NA MAZINGIRA YA KAZI ZAO: SISI TUKO HUKU MBALI LAKINI KILA SIKU TUNAJUA NINI KITAKUWEPO TANZANIA KAMA SASA TUNAJUA MVUA NA UPEPO MKALI
    TUJIWEKEE TAHADHARI NA MAJANGA KWA KUANGALIA HALI YA HEWA HASA CNN:

    ReplyDelete
  9. TANZANIA HAIFAIDIKI .."...INAVYOPASWA...".NA "..TANZANAITI, DHAHABU..ALMASI NA MADINI MENGINE MENGI.."..NCHI JIRANI NDIO WAUZAJI WAKUBWA KATIKA SOKO LA DUNIA NA...SERIKALI CHUKUA MIGODI HIYO YOTE..WAPENI VIJANA KAZI YA KUCHIMBA KUTUMIA MBINU NA ZANA ZA KISASA...TANZANITE NA DHAHABU ZOTE TANZANIA ZIENDE KWENYE HAZINA YA SERIKALI...MAUZO YAFANYIKE KWA UTARATIBU UTAKAOPITISHWA NA BUNGE...."..KUMBUKENI MADINI YANAONGEZEKA THAMANI HALAFU ..."..TANZANITE HAITAKUWEPO MILELE..."

    ReplyDelete
  10. MUHESHIMIWA PINDA, UMEANZA KUNIKATISHA MOYO MAPEMA SANA, NA RAIS JK VIPI TENA MBONA UMEKUWA SLOW NA MAJANGA MAKUBWA KAMA HAYO JAMANI??? HIVI HUKO SERIKALINI KUMEPITIWA NA NINI?? YAANI WATU 75 WAMEPOTEZA MAISHA, MUHESHIMIWA PINDI UNATUMA WATU WAKAANGALIE KWANI NI HARUSI HIYO? UNATUMA WATU BILA VIFAA INASAIDIA NINI? PINDA, UMESHEMSHA MAPEMA HIVI KWELI TUTAFIKA? WACHIMBAJI HAWA WANA SAIDIA UCHUMI WA TANZANI KWA KIASI CHA ASILIMIA KUBWA SANA, TENA MNO, SASA INAKUWAJE HAWAANGALIWI? HAWATENDEWI HAKI? SERIKALI YA TANZANIA INABIDI VIONGOZI WAAMKE WALIKOLALA HAYA SIO MAMBO YA MZAA. PINDA YOU MUST DO SOMETHING AS SOON AS POSSIBLE, YOU ARE MOVING WAY TOO SLOW. MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI MAREHEMU HAO. AMEN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...