wananchi wenye hasira wakimsulubu jamaa anayesadikiwa kuwa ni kibaka baada ya mtu aliyetaka kumchomolea pesa mfukoni kumshtukia na kuanza kupambana naye sasa hivi mtaa wa samora avenue.
jamaa wakiendelea kumwadhibu mtuhumiwa huyo huku jamaa aliyepigwa poketi (mtasha, shati bluu) akijisachi
kwa kuogopa shari jamaa aliyetaka kupigwa poketi anaamua yaishe na kuanza mbele akiwaachia wadau wamalizne na kibaka ambaye hatimaye aliachiwa. siku za karibuni vibaka wamekuwa wengi sana maeneo y katikati ya jiji ambako inabidi doria iimarishwe..





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Walimwachia wa nini matairi mabovu bongo jamani muwizi ni muwizi tu ni kuchomwa moto mpaka mauti yake sioni huruma mimi kwa yoyote ambaye ni mwizi pumbavu kabisa unajua nini kesho atakuja kukuibia wewe au mtu mwingine yaani siku hizi wanakuibia mpaka kwenye mifuko ya suruali sasa siku nyingine wataingiza mkono halafu wafikiri wanavuta wallet kumbe nyeti za mtu ohhh hatari hiyo

    HILDA

    ReplyDelete
  2. Ughaibuni kuna vibaka wa kuiba mifukoni?anastahiri hicho kipigo ila wamefanya busara kutomdedisha!!
    Mdau,Arusha.

    ReplyDelete
  3. Mbona akina Karam..., Eduadi L, Gavana na wengine hawafanywi kitu hiki?

    ReplyDelete
  4. Hilda naona jamaa alitaka kumtoka dingi

    ReplyDelete
  5. Kaka Michu huyo kibaka wangemtoa macho tu asione cha kuiba ,nashukuru sana umenikumbusha hapo SAPNA hapo mambo ya simu za mkono enzi zile tulikuwa tunaenda kufungua pin, ni karibu sana na maskani kwa kaka HERI pale kwenye magazeti.
    KT ( Japan )

    ReplyDelete
  6. Mbona mnashindwa kuwakamata na kuwapiga MAFISADI wanaoiba mabilioni ya Taifa, hebu acheni uzushi wabongo. Kama mna hasira sana na wezi basi anzeni na MAFISADI. Mnaibiwa kila siku na MAFISADI lakini mmenyamaza kimya, Ikija kwenye hawa vidokozi wadogo ndio mnajifanya mna hasiiira.

    ReplyDelete
  7. Loh,vibaka bwana kama hawajakudhuru au kumdhuru mke/mme,dada/kaka/rafiki/jamaa au mzazi wako huwezi kujua ubaya wao.Lakini vile vile kuwaua kwa sheria mkononi bado 'so'fair/solution.Tatizo ni umaskini,unemployment n.k.Kuongeza doria sawa lakini serikali lazima ijiuulize hawa vijana kwa nini wanafanya hivi?Ni hobby au nini.Wadhibiti sources.#Wadau mnaoishi ulaya,America,Asia n.k vibaka wa kuchomoa wapo?If yes,serikali zinawafanyaje?Karibuni.

    ReplyDelete
  8. Hilda, Sina uhakika kama suluhisho la vibaka ni kuwachoma moto! ni suala la mkondo wa sheria tu kuchukua nafasi yake, pia sina uhakika kama nyeti zako Dada Hilda zitavutika hata kama akifanikiwa kuingiza mkono..sana sana atapapasa tu!!

    ReplyDelete
  9. Hatua kama hizi zinapasa zitumike kwa mafisadi{WEZI)Baadhi ya vingozi wa juu WEZI Mafisadi kwani mahakamani na mkondo wa sheria sio kwaoMUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  10. huyu kibaka hajaiba., amejaribu kurudisha wakoloni walichoiba wakati wa mababu zetu. Redistribution of resources! richmond ndo wezi halisi, kina EPA, Mahalu na saga ya Italy, hizo ndo kesi za kupigwa hadharani. vibaka wanaganga njaa tu.

    ReplyDelete
  11. huyo kibaka kwanini walimuachia?atarudia kuiba tena maana haikuwa chungu!!wangemkata vidole vya kulia..jamani mzungu wa watu kawa mwekunduu!!mdau norway

    ReplyDelete
  12. HAHAHAA HILDA HEBU TULIZA MUNKARI VIBAKA WA KUTIWA MOTO NI WALE WA RICHMOND, HUYU JAMAA NI NJAA TU AMBAYO IMESABABISHWA NA MAFISADI WA NCHI YETU WENYEWE MNYONGE MNYONGENI NA HAKI YAKE MPENI JAMAA ALISTAHILI KUACHIWA KWA ONYO TU NA SIO ADHABU KALI HASA KAMA ALITAKA KUMWIBIA MTASHA.......OK DADA HILDA
    MDAU SCOTLAND.

    ReplyDelete
  13. wangemkata mkono kisha wangemuachilia

    ReplyDelete
  14. Kama kawaida, mdokozi anapata kipigo cha mbwa mwizi. Wezi wa mabilioni wanaombwa kurejesha pesa walizoiba na hata hawaguswi! Kweli bongo tambarare!

    ReplyDelete
  15. Ndugu Hilda, hivi adhabu ya wizi ni mauti? hivi angekuwa wewe au mtoto wako au ndugu yako wa damu ungesema hivyo? Wahenga walisema ukicheka cha mwenzako huwa jambo hilo linajifichaga kwenye meno.

    (mbarikiwa@gmail.com)

    ReplyDelete
  16. wakuchomwa ni mafisadi si hao wezi wa miambili wachapwe wakimbizwe,halafu serikali ya hao mafisadi watoe ajira kwa vijana maana tusiangalie upande mmoja wa vijana kuwa vibaka , tujiulize nini sababu inayosababisha vijana wengi wawe vibaka,nafikiri niukosefu wa kazi ama shughuli ya kufanya wanakaa maskani mwisho wanaenda kazini(kuiba)

    ReplyDelete
  17. Ndugu Michuzi mimi naomba nitofautiane na wewe kidogo! Ukweli ni kwamba uchumi ndio unatakiwa uboreshwe na sio doria! Wataalam wa uchumi wanakubali kuwa uchumi unapopanda basi crime(mtanisaidia tafsiri) hupungua.
    Kidume, USA

    ReplyDelete
  18. siku nitakayo kuwa Rais wa nchi hii nitawapeleka wizi na wauwaji na wabakaji katika maabara za kujaribia madawa badala ya kutumiwa panya ili jamii ifadike tusiwe wapumbavu watu kama hawa lazima tuwatumilie katika njia kama hii badala ya kuwaweka jela na kuwalipia malazi na matibabu huku sie tukiwa tuna umia na maisha lazima watowe mchango kwa jamii na mchango pekee wa kufaidisha taifa ni kuwapeleka maabara kwa majaribio ya madawa kama vile ya kensa ukimwi na mengi mengineyo

    ReplyDelete
  19. WEWE MDAU WA 3:15PM KUTOKA ARUSHA PAMOJA NA WEWE MDAU WA 4:53PM, NAPENDA KUWAAMBIA KWAMBA TABIA ZA BINADAMU WOTE ULIMWENGU ZINALINGANA HIVYO MSIDHANI KWAMBA VIBAKA WA PICK POCKET HAWAPO HUKU UGHAIBUNI NA NDO MAANA HUYU MZUNGU ALIAMUA KO WALK AWAY FROM THAT SCENERIO, SABABU NI KWAMBA HAKUWA NA USHAHIDI WA KUTOSHA HUWA KUNA SHERIA ZAO ZA KUMTIA M2 HATIANI KTK KOSA KAMA HILO KWANZA LAZIMA UWE NA WATU WASIOPUNGUA WATATU WALIOSHUHUDIA KWA MACHO KWAMBA JAMAA ALIKUWA ANAMUIBIA NA SIO KUTAKA KUMUIBIA...PILI UWE WEWE MWENYEWE ULIMWONA SIO KUHISIA TU VINGINEVYO KIBAKA ANAWEZA KUKUSHITAKI KWA KUHATARISHA MAISHA YAKE KUMBUKENI SHERIA NI MSUMENO MKALI...SASA NINYI KWA VILE MMEMWONA MZUNGU KASEMA BASI MNAAMINI TU. JIFUNZENI SHERIA NYEPESI ZA HAKI YA BINADAMU SIO KUKUBALI KUBURUZWA TU.... NA NDO MAANA MMEWANYAMAZIA KIMYA MAKABAILA NA WEZI WA RICHMOND.. KWA UNYONGE MNAOUTAKA WENYEWE.... THANX
    MDAU SCOTLAND

    ReplyDelete
  20. we mdau wa sckotish wacha kabisa vijisheria vyako.... hapa bwana ni ubabe mtupu kibaka atapigwa mapaka atakufi na huo ushahidi ni inshu ndogo sana.... ila ni kweli pia hawa jamaa wa richmondi tuwavizie nao tuwatwange mawe maana napo ushahidi ndio inshu...

    ReplyDelete
  21. Hayo ndiyo matokeo ya kuwanyanyasa wamachinga. Badala ya kuwapa nafasi ya kujipatia kipato chao kwa kwa kujihangaisha na biashara ndogo ndogo wanalazimisha kuwa wezi maana tumbo linalia njaa.

    ReplyDelete
  22. Mtasha anawahi maana hana makaratasi hivyo...,mambo yakizidi akatakiwa akatoe ushahidi polisi siitakuwa tabu hapo!!

    ReplyDelete
  23. KUNAMDAU MMOJA KAONGEA KWELI HAPO JUU, KUHUSU HUYO MZUNGU KUONDOKA SABABU HANAUWAKIKA NANI KAMUIBIA, TUKIACHA YOTE, TANZANIA WANAPIGA MWINZI NA KUCHOMA, SABABU MWIZI AKIIBA SIKU MBILI ANATOLEWA, HILO NDILO LINAWAUMA RAIA.

    TANZANIA - TUFATE SHERIA ZA KUKATA VIDOLE KAMA KWELI UNAUSHAHIDI KAIBA. MWISHO ATAWACHA HIYO TABIA.

    - TANZANIA HASA DAR-ES-SALAAM K'KOO AU KWENYE MSONGAMANO WA WATU UTASIKIA MWIZI KUMBE MWIZI NDIO KAMWITA AMBAYE SIO MWIZI! MWIZI! TUNARUKIA TU KUPIGA MTU SIYE.

    WEZI WAPO SERIKALINI ILA MUNGU NDIO MUHUKUMU YA WOTE KAMA USHAHIDI HAKUNA AU UPO.

    UDA=DALADALA au ni CHAMA CHA MABUS DSM ? LOL.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...