Bro Michuzi,

Napitia uani mzee kwani kupitia mbele inashindikana itabidi labda unielekeze kwa haraka nini nakosea. Inawezekana ni setting kwenye computer yangu. Eee bwana nina issue hapa naomba iwekwe hadharani lakini tumia jina hili MPIGANIA HAKI.

Ninaandika masikitiko yangu kwa TRA Dar es alaam namna wanavyorudisha nyuma jitihada za kuinua uchumi na badala yake wanatengeneza mazingira ya rushwa. Sijui kama tutashinda vita dhidi ya mafisadi.

Nikiwa mwanafunzi huku abroad nimejibana kutuma gari huko nyumbani kwa mzee wangu lisaidie familia. Gari ni isuzu used nimelinunulia Japan kwa gharama nafuu kabisa. Kuepuka usumbufu wa kipengele cha kuingiza gari lisilozidi miaka 10, basi nilinunua gari ya mwaka 1999.
Gari ilisafirishwa toka Japan mwezi wa 11 mwaka jana na kuingia bongo mwishoni mwa desemba 2007. Jamaa zangu huko home walifuatilia kulitoa na jamaa wa TRA wakasema lilipiwe milioni 5 kwa maelezo eti ni la kifahali. Hatukubishana, pesa ilitafutwa ikalipwa.
Nikapata taarifa eti TRA wametupiga faini ya milioni 2 zaidi kwasababu wamegundua gari ni ya mwaka wa nyuma imeandikwa kwenye mikanda tofauti na ilivyoelezwa kwenye papers.
Mimi nikahisi kuna harufu ya dhuruma hivyo nikawaambia ndugu zangu wasilipe fine wafuatilie kiundani. Wakawasiliana na kampuni inayoingiza magari ya isuzu toka Japan. Jamaa wakawapa taarifa ya maandishi kuwa gari used zinazonunuliwa Japan zinafungwa vifaa vipya kuondoa vichakavu.
Kuna uwezekano mkanda uliofungwa ukawa mwaka tofauti na manufacture date ya gari. Barua ilipelekwa TRA kwa wahusika basi mpaka leo Michuzi inapigwa dana dana. Wanasema wiki hii eti kuna sekretari TRA aliipoteza barua haikuweza kuingia kwa mkubwa, hivyo wakahitaji copy ambayo tulikuwa nayo waiingize kwa mkubwa.
Sijui itachukua muda gani na gari iko bandarini muda wote huo.


Nimeona uozo huu niuanike hadharani ili kama kuna yoyote anayeweza kunisaidia anisaidie.

MPIGANIA HAKI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Katika mashirika ya umma ambayo wafanyakazi wanakula bata ni hawa TRA...yani wewe hata ukipata dili ya kufuta vioo mule ndani ni bata, sasa kumtengeneza huyo bata ndio kunaanzia huko kwenye faini zisizo na kichwa wala tako...umenisoma mkubwa, kama vp we lipa hiyo faini ukaendelee na shughuli zako la sivyo hilo gari litaozea hapo mwana

    ReplyDelete
  2. Pole mkuu. Kuna kodi za aina nyingi. Hapo ulikwepa kulipa uchakavu lakini ukasahau ukubwa wa engine (Cubic Capacity au CC). Nadhani gari yako ina cc zaidi ya 2500, hapo unalipa excise duty kadhaa.

    Lakini kuna gharama kubwa ambazo sijui utakwepa vipi, nazo ni 'storage'. Hiyo mjomba ni US$ 1 kwa siku, kuanzia siku 7 toka gari liwasili bandarini!

    Usipime kabisa usumbufu na rushwa ilivyo wazi pale TRA, nafikiri kuna ushirikiano mkubwa kati ya clearing agents na maafisa pale.

    Kila lakheri,

    Madau NY

    ReplyDelete
  3. we acha tu mi mwenyewe yamenishawahi kunikuta kama hayo bro...

    ReplyDelete
  4. Kijumla TRA Tanzania nzima ni mafisadi....walarushwa na dhuluma ni nje nje... wadhungu walisema 'if you can not beat them join them' we wape rushwa uende zako na daima waombee mikosi wao na familia zao...

    ReplyDelete
  5. Mdau pole sana kwa yaliyokupata. Lakini hupaswi kulalamika kwenye hii blog kwani itakuwa ngumu sana kupata msaada wa kutatua tatizo lako. Kinachoonekana hapa ni kuwatupia lawama wafanyakazi wa TRA. Mara nyingi lawama si sahihi. Fahamu TRA ipo kusimamia sheria za kodi ambazo Serikali kupitia Bunge inakuwa imeziweka.

    Cha kufanya ili kupata ufumbuzi wa tatizo lako nenda TRA kuna idara inaitwa Taxpayer Services and Education. Peleka malalamiko yako kwa hii idara na utasaidiwa mara moja. Wana ofisi Water Front au jengo la Makao Makuu TRA. Pia kule Customs kuna kitendo kinachoshughulikia malalamiko kama yako, kama umedaiwa kodi kubwa zaidi au la. Inachunguzwa na kama ni kweli unarudishiwa pesa zako na maofisa kuonywa au kufukuzwa kazi kama walifanya makusudi kukuibia pesa.

    Nakushauri nenda huko peleka malalamiko yako na yatafanyiwa kazi mara moja.

    Steve,
    Dar es Salaam

    ReplyDelete
  6. Bro kama kweli una uchungu na nchi yako wakamatishe hao jamaa kwa PCCB. Mimi nawaomba wadau kwamba tusiwe wanafiki wa kulalamika kwenye vyombo vya habari kwamba TRA kuna rushwa wakati tunaweza kuitokomeza kwa kuwalengesha hawa jamaa na pia kwa kutumia camera za siri ili tuliondoe hili tatizo. Rushwa za wafanyakazi wa TRA zinatokana na ulafi na ubinafsi na siyo mishahara midogo kwani mishahara yao ni mizuri sana. Pia baadhi ya watu wanashirikiana na watu wa TRA ili kufanikisha haya mambo. Tuwafichue hawa watu ili nchi iendelee badala ya kuleta unafiki hapa kwenye blog, chukueni mfano wa waamerika walivyomuumbua rais wao, Clinton kwa kashfa ya ngono na tuache woga wa kuwashughulikia hawa watu wadogo sana wa TRA. Kama sisi tunakuwa waoga, ni nani atakuja kuondoa ufisadi au ndiyo ile hali ya kusubiri ipaka mambo yaharibike na waitwe wakaguzi wa nje then tupige kelele? (mfano EPA): PREVENTION IS BETTER THAN CURE

    ReplyDelete
  7. (PCCB) ILIFICHA YANAYO ENDELEA (EPA)NA NDIO MAANA WANAFICHA YANAYOENDELEA (TRA) MPAKA TUWASILIANE NA (WABUNGE)WACHAPAKAZI WENYE UCHUNGU WA NCHI NA WANANCHI.

    ReplyDelete
  8. wewe unayesema kuleta UNAFIKI KWENYE BLOG unakosea sana. vyombo vya habari ni kimbilio la jamii. bila jamii blog haifanyi kazi ama bila jamii chomba cha habari hakina umuhimu.
    kwa taarifa yako mdau anahaki ya kuweka hadharani uovu wa TRA, huu ni wakati wa uwazi na ukweli.
    TRA ni wezi, walarushwa na mafisadi.
    kwani gari ikiwa ya kifahari ndio nini si kila mtu anajikuna panapowasha.

    nashangaa.

    ReplyDelete
  9. TRA ni pamoja na kusema kuwa wanasimamia shria za kodi zilizotungwa na Bunge letu, kwa kifupi ni kwamba katika kutekeleza hilo jukumu hawa jamaa ni wala rushwa wakubwa sana wakishirikiana na makampuni ya Clearing ambayo mengi ya hayo yanamilikiwa na wafanyakazi waliofukuzwa TRA kwa mazingira ya Rushwa au kwa Uonevu tu. Hiyo kanuni ya kuangalia mwaka gani gari limetengenezwa kwenye Seat Belt label ni ya kijinga na inaonyesha ni jinsi gani kulivyo na vihiyo humo TRA!Ni wajifunze na kuelewa:
    1.Makampuni yanayotengeza magari hayatentengezi kila kitu yenyewe.
    2.Ili kupunguza gharama za uzalishaji huwa wana- Subcontract baadhi ya parts kutoka makapuni mengine.
    3.Mojawawapo ya hizo parts ni Seat Belts.Hivyo basi orders za Seat belts huwa zinatolewa in advance ili ku-meet demands na hii inatokana na manufacturing schedulles.
    4.Unweza kukuta Seat belt iliyoandaliwa mwaka 1995 au 1996 inafungwa kwenye magari ya mwaka 1999 na hata ya 2002.
    5.Kinachosema gari ni ya mwaka gani ni chasses Number na si vinginevyo.SEAT BELT siyo GARI. GARI NI CHASSES NA ENGINE yake.
    TRA msiwe ma-layman kiasi hicho! STOP this UNJUST TO the PUBLIC!

    ReplyDelete
  10. Mkuu pole sana!! inawezekana kabisa ikawa sio wanataka rushwa ila umekuwa na bahati mbaya ukakuta malengo hayajafikiwa(ya kukusanya kodi ya siku au robo mwaka) kwa hiyo limekulipukia wewe,kuna target ambazo serikali wameweka ambazo mwisho ni kuumiza tu wananchi.kwa kweli wananchi tumegubikwa mizigo sio mchezo tukianza kuoengea patakuwa hapatoshi! ushauri lipa, toa gari then baadaye kama ushauri uliopwe na ndugu hapo juu basi rudi na doc. and the anza kulalamika!! pole sana! kwa taarifa yako, hiyo iko kwenye sukari,unga, usafiri nk masikini watanzania.

    Ndugu yenu wa mwanza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...