
KWANZA NAKUPONGEZA SANA KAKA MICHUZI KWA KAZI NJEMA YA KUTUHABARISHA.
OMBI LANGU KWA WADAU WOTE WA GLOBU HII NI JUU YA UTATA WA KUSHINDWA KUPATA HABARI NYETI ZA KIVITA TOKA KWA WAANDISHI WETU WALIOKO KULE KOMORO.
NASHINDWA KUELEWA JAMBO MOJA NALO HIVI KWA NINI HABARI NYINGI ZITOLEWAZO KUTOKA HUKO HUJA KUPITIA BBC NA SI KUTOKA KWA VYOMBO VYETU VYENYE WAWAKILISHI HUKO? AU WAANDISHI WETU WAMETINGWA SANA KAZI KIASI HAWANA MUDA MZURI WA KUTUHABARISHA?
SINA NIA YA KUWAFUNDISHA KAZI WAANDISHI WETU, ILA JAMANI MAMBO MENGINE YANA TATIZA KUYAELEWA NA MATOKEO YAKE LIMENIACHA NA MWASWALI MENGI MNO BILA MAJIBU NDIO MAANA NAOMBA MSAADA KWENU WADADISI WA MAMBO.
MDAU MWENZENU,CANADA
zaidi nendeni hapa bbc http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/default.stm
we waandishi wetu si unawajua au umekaa sana huko canada, computer zenyewe hata ku-type utakuta wanadonyoa hawajui IE unafungua vipi kama hakuna icon kwenye desktop hawatumii internet
ReplyDeletehiyo bbc ndo source nzuri hata picha zote unazoziona hapa za vita zinatoka huko huko bbc news
Huwezi kulinganisha teknolojia ya habari ya mashirika makubwa kama BBC, CNN, AP, REUTERS nk na zile za kwetu kama TBC. Wenzetu wana vyombo maalum vinavyo wawezesha kuwasiliana kwa njia ya satelite-internet, radio simu nk kutokea popote pale, wana sources za uhakika za habari ambazo wanawalipa vizuri pamoja na wanahabari waliobobea wakiweza kuwasiliana kwa lugha nyingi mashuhuri, na wakiwa na ulinzi maalum hasa katika sehemu kama hizi za vita!
ReplyDeletekwa maoni yangu, kuandika habari kutoka uwanja wa vita (frontline)ni hatari sana. Kwa mfano hapo juzi tu huko Kenya, baadhi ya waandishi wetu kadhaa walikuwa wanaripoti kutoka hotelini wakati BBC anajitosa kwenye tukio na risasi zasikika. Jingine ni kuwa posho nayo yaweza kuwa sababu, huwezi kujitosa kwa posho kiduchu, hata wacheza soka ulaya anajitupa mzima mzima kulinda posho yake ati. Hapa kwetu ukiumia kwa soka kina nanihii wala hawakujali,sembuse kujitosa mbele ya mtutu mjomba yahitaji moyo. tutapata habari wakirudi. Au ulitaka Michuzi aende??
ReplyDeleteNaona labda kuna haja ya kuwafahamisha wasomaji wa blog kuwa kuna waandishi toka Tanzania waliokwenda Comoro na wanaandika habari na kutuma picha.
ReplyDeletePili, nahisi msomaji aliyetuma maoni hafahamu maendeleo ya sekta ya habari na wanahabari nchini. Si kweli kwamba hawatumii kompyuta ama internet. Mwenye blog hii ni mwandishi na ni kielelezo cha waandishi Tanzania. Pengine Bwana Michuzi tuna kazi ya kuwaelimisha baadhi ya wasomaji wako.
Henry Lyimo
Nakushauri utizame habari katika Televisheni yetu ya Taifa (TVT), wanaonyesha kila kitu live. Utamsikia Malini Hassan Malin akiwahoji waandishi waliopo mstari wa mbele Comoro
ReplyDeleteNapenda mshirika uelewe kuwa katika operesheni kama hizo, umeme, mawasiliano, na vitu kadhaa hukatwa ili kuparalize eneo husika. Kwa hiyo kama mwandishi umeenda na kalamu na kamera tu basi huna jinsi, sasa nahitaji kusema waandishi kama BBC wana nyenzo nyingi kama satelite telephone, solar radios, backup batteries n.k. kuweza kuwasiliana hata mbugani au nyikani, na wana Bima nzuri sana katika kazi ndiyo maana wanatuhabarisha chap chap na kuingia msitari wa mbele
ReplyDeleteTunashukuru kwa uwazi wa taarifa za BBC, kwani waandishi wetu wa habari bado wanabanwa, uhuru wao bado upo mikononi mwa hao mafsadi.
ReplyDeleteHuu umoja wa AU kama una sababu,uwezo na nia ya dhati kuikomboa Afrika kutoka utawala wa madikteta wanaochipua basi tunaisifu kwa hilo. Kasi hii isiishie Comoro, pia tunaomba Zimbabwe itazamwe kwa macho manne, huyu babu kikongwe, anatishia raia na dunia nzima inatambua anataka afie madarakani hali watu wake wanataabika wenye uwezo wa kuiongoza nchi wapo.
Tunatoa wito kwa AU kupitia kwa waangalizi ( Observers)wa upigaji kura hapa nchini,watoe taarifa sahihi juu ya uchaguzi huru na wa haki. Tunaomba haki itendeke Zimbambwe.
Mdau na Mwanaharakati haki za binadamu.
Kamera za waandishi wa Tanzania ni zile za kupiga picha halafu unasubiri urudi Dar es salaam uende studio ya Michuzi ukasafishe ndiyo upeleke gazetini au Chombo cha habari na ili zitoke chombo cha habari inategemea huyo mhariri kama siku hiyo kafurahishwa na hawara yake au la au kama ni ndugu yako.
ReplyDeletePicha Zingine kama hizo za vita inabidi ukishasafisha uzipeleke kwa mhariri ambaye na yeye kabla ya kuzipeleka gazetini inabidi awapelekee bosi fulani anayejiita mhakiki wa habari nyeti azipitishe kuwa sawa zitoke ndiyo zitoke.BBC ukiritimba huo hawana mtu akitwangwa hata risasi vitani saa hiyohiyo picha inarushwa bila kufanyiwa SENSORING.
Nchi zetu hata Askari polisi akitwanga jangili ukipiga picha utaambiwa ni kosa na waweza tiwa matatani maana huna kibali na kupiga picha polisi wakiwa kazini na utaambiwa picha kama hiyo unahitaji kibali maalumu cha afisa mkubwa sana!!!!! ambaye ukimwendea atasema naye atasema nenda kapate kibali kwa mkubwa zaidi,na ukienda kwa mkubwa zaidi utaambiwa nenda kwa mkubwa zaidi hadi unachoka na kuamua kutupa na kikamera chenyewe dampo na kuacha kazi ya uandishi wa habari na kuomba kazi ya kuwa afisa uhusiano wa kampuni ya mhindi.
HEBU JARIBU WEWE KWENDA KUFANYA KAZI YA UANDISHI SEHEMU KAMA HIYO..HALAFU UTAONA KWANINI HAWAWEZI KUKUPA HABARI...OK..?
ReplyDeleteMADAU
MIMI
Please please post this "FOOD FOR THOUGHT" from
ReplyDeletehttp://africa.reuters.com/top/news/usnBAN628930.html
*******************
Critics say the AU picked a soft target. With a history of assassinations, mercenary invasions and some 20 coups or attempted rebellions since independence from France in 1975, Comoros is notorious for its political instability.
France and the United States backed the assault on the tiny island of 300,000 people, but it was criticised by continental power South Africa.
President Thabo Mbeki said on Tuesday the military action took Comoros "back to this history of force instead of resolving matters peacefully".
Comoros was "particularly disappointed" by Mbeki's position, government spokesman Bacar said.
"It goes against the decisions of the African Union, especially the Peace and Security Council, and resolutions from foreign ministers in the region, of which South Africa is a part."
He accused the Anjouan leader of setting up a dictatorship and said Bacar would answer for his crimes in court.
"We have reports and witnesses about people being tortured, people being raped, even killed," he said.
"We had a physical education teacher whose arms and legs have been broken by Bacar's men. They have to answer for that. We have to take him to court."
WACHENI KUJITETEA KITOTO ENYI WAANDISHI WA NYUMBANI. IKIWA KWELI MNAZIDIWA KI ZANA NA MASLAHI NA HAO WAANDISHI WA MASHIRIKA YA NJE, SASA KWA NINI MLIKUBALI KWENDA HUKO COMORO? NI WAPI MLIONA WATU WANAKUBALI KAZIWASIOKUWA NA UWEZO NAYO KUIFANYA HALAFU UMA UKAWAELEWA? JE, MLIPO ONGEA NA WAZIRI MEMBE JUU YA MPANGO WA KUWAPELEKA KOMORO MLIGUSIA LOLOTE JUU YA ZANA? NAOMBA MUIRUDIE HOTUBA YA MUHESHIMIWA MEMBE NA WAANDISHI NA MTAONA UMUHIMU WENU HUKO NA IMANI YA SERIKALI NA WATANZANIA KWA UJUMLA JUU YENU KUWEPO HUKO ILA SASA IMEPOTEA KABISA KUWA HAMUWEZI KAZI AU HAMJUI JUKUMU LENU. NASEMA HIVYO KWAKUWA NAJUWA HABARI NI USHINDANI, NA HABAR NZURI NI ILE INAYOWAFIKIA WATU KWA WAKATI MUAFAKA.
ReplyDeleteWanafanya shopping...si unajua tena trip hii ni lazima mtu arudi na plasma TV....I am kidding!!!!
ReplyDeleteLakini unakumbuka wale walienda kwenye Olympic wakachelewa kwenda kwenye mashindano siku hiyo waliyotakiwa sijui walikua shopping ...walivyorudi tuliwalaki kwa shangwe pamoja na kuwa hawakushindana ......nakumbuka nikiwa mdogo hiyo issue
but kwa hawa waandishi labda mazingira magumu wanayofanyia kazi...huwezi jua labda wao wanatumia ile njia za zamani...kuandika kweney note book....kutafuta simu wapige bongo...saa ngapi...?????
Sasa jamani mbona hela tulizopewa na USA zinaenda kutumika kwenye vita badala ya kujenga barabara?
ReplyDeleteMaswali..karibu yote ya wna blogu yamejibiwa na ...
ReplyDeletemakala hii...
"Mbeki, Tanzania isingewasaidia Nelson Mandela angekuwa huru?"
Jamanani someni wenyeweeeeeeeeeee...
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=siasa&habariNamba=6091
michuzi asante, na wewe mdau wa canada wasalimie wabongo wengine uko.
ReplyDelete