Msanii mahiri katika fani ya muziki aliyejiengua katika kundi la Parapanda Arts, Richard Mziray amekamilisha albamu yake inayojukalam kwa jina la nafsi yangu ambayo ina jumla ya nyimbo nane.

Mziray ambaye alikuwa moja kati ya wasanii mahiri waliowika na kundi la Parapanda amesema tayari amshatengeneza video ya baadhi ya nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ambayo ameitoa akiwa msanii wa kujitegemea baada ya kutoka Parapanda Arts.

“Nimekamilisha albamu ambayo ina jumla ya nyimbo nane, na nimetengeneza video ya nyimbo tatu, albamu yangu inaitwa Nafsi Yangu ikiwa na nyimbo zenye maudhui mbalimbali yanayomlenga Mtanzania na Mwafrika,” alisema.

Msanii huyo aliyekuwa nguli katika uandaaji wa muziki katika maonyesho ya kikundi cha Parapanda amesema katika albamu hiyo pamoja na wimbo wa Nafsi yangu, ambao umebeba jina la albamu yake, pia kuna nyimbo zingine kama vile Nimehangaika, Kuna Mapambano, Ni Simulizi, Panga la Shaba, Mama Dori, Salam Bibi na Nishike mkono.

“Nyimbo zote zipo katika mahadhi ya kiasili isipokuwa wimbo mmoja ambao nimeupiga katika mtindo wa kimagharibi wa Blues, na pia nyimbo zangu zimebeba maudhui muafaka sana kwa jamii ya watanzania katika maisha yanayotuzunguuka,” amesema Mziray.

Amesema lengo la kuamua kujikita katika muziki hivi sasa ni kutaka kuinua fani ya muziki wa asili hapa nchini. “Tanzania tuna aina nyingi sana za muziki ambazo zinavutia sana, hivyo kama mtaalamu wa masuala ya muziki nimeamua kijikita ili kutoa msukumo wa uhakika katika fani ya muziki wa Kitanzania,” alisema.

Mziray amesema kuwa albamu hiyo itaingia sokoni hivi katibuni baada ya taratibu za kimsingi kukamilika na kwamba itapatiokana CD na kaseti za kawaida ambapo pia itapatikana katika video kwenye DVD, VCD na VHS. Tayari baadhi ya nyimbo zake zimeanza kusikika na kuonekana katika baadhi ya vituo vya redio na Televisheni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana kijana, I am sure mwaka huu tutakunywa bia kwa Nzari au Uplands! Unaionaje hiyo?

    ReplyDelete
  2. Asubuhi na mapema,kabla jua kuzaliwa,ndani machinjioni panga la shaba n´gombe kashikiliwa.hayo yalikuwa ni maneno ya kwanza wakati tulipoanza kutunga wimbo huu,nafikiri richard atakumbu huyu anayeongea ni nani.nakupongeza sana richard kwa kupakuwa album,niko nyuma yako na unaweza kunipata pia katika www.yangoyo.blogspot.com ukiona picha yangu utanikumbuka bila shaka.nifikishie salam bwana michuzi.Rich anapatikana pale changanyikeni karibu na kwa mzee matemba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...