Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ,Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanziabar, Aman Karume (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Pius Msekwa (kulia) na Katibu Mkuu wa CCM, Yusu Makamba wakiimba wimbo wa CCM kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo katika Kijiji cha Butiama
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara.

Kikao hicho kimeanza baada ya Rais Kikwete kuwasili Butiama tayari kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM .

Kikao cha NEC kinaanza leo ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika kijiji ambako alizaliwa Baba wa Taifa na mwanzalishi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais Kikwete aliwasili Butiama kwa barabara akitokea Mwanza ambako ndege yake ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza mapema asubuhi na akaamua kusafiri kwa gari kwenye Musoma.

Mjini Mwanza, mamia ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake, walijitokeza kwa wingi, katika baadhi ya sehemu za jiji hilo mvua ikiwa inanyesha, kumshangilia Rais wakati msafara wake ukikatisha mitaa ya jiji hilo kuelekea Musoma.

Mara tu baada ya kuwasili Butiama ambako alipokelewa na mamia ya wananchi, Rais Kikwete alifungua ukumbi mpya wa mikutano ambao utatumika kwa ajili ya kikao cha NEC.

Ukumbi huo unaitwa Joseph Kizurira Nyerere, mdogo wake Baba wa Taifa.Ukumbi huo umejengwa kiasi cha mita 300 kutoka nyumbani kwa Marehemu Joseph Kizurira Nyerere.

Mara baada ya kufungua na kutembelea ukumbi huo, Rais Kikwete aliwapokea wazee 17 ambao wametembea kwa mguu, kwa siku mbili, kutoka mjini Musoma hadi Butiama, ili kuunga mkono uamuzi wa CCM kufanyia mkutano wake wa NEC ya chama hicho katika kijiji alikozaliwa Mwalimu Nyerere. Kijiji hicho kiko kiasi cha kilomita 32 kutoka Musoma mjini.

Wazee hao pia wameeleza kuwa walitembea kutoka Musoma hadi Dar Es Salaam kuunga mkono Azimio la Arusha mwaka 1967.

Akizungumza na wananchi katika tukio hilo mbele ya jengo la ukumbi huo mpya, Mwenyekiti wa CCM ameelezea sababu za CCM kufanyia mkutano wake Butiama.

Amesema kuwa uamuzi huo ulitokana na uamuzi wa CCM kurudia utaratibu wake wa zamani wa kufanyika vikao cha NEC katika mikoa mbali mbali nchini badala ya vikao vyote kufanyika Dodoma kama ambavyo imekuwa katika miaka ya karibuni.

Amesema kuwa baada ya uamuzi wa kurudia utaratibu huo wa zamani,ulikuwa ni mkoa wa Mara uliojitolea kuandaa mkutano wa kwanza wa kawaida wa NEC, baada ya uchaguzi mkuu ndani ya chama, Novemba mwaka jana, mjini Dodoma.

“Basi mkoa wa Mara ulipojitolea kuandaa mkutano wa kesho,mimi nikasema basi kikao hicho kifanyike Butiama, kwa heshima na kumuenzi mwanzilishi wa chama chetu na taifa letu, Mwalimu Nyerere,”

“Hii ndiyo maana tuko hapa.Hiki ni kikao cha kawaida tu cha NEC.Hii ndiyo siri ya kikao kufanyika hapa. Wengine wamekuwa wanaogopa, wengine wamejijengea matumaini ambayo hayapo, lakini hiki ni kikao cha kawaida katika utaratibu wetu mpya na utaratibu huu utaendelea,” alisema Rais Kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Bwana Michuzi nakushukru sana kwa picha hizo ambazo kwa kweli kwa sisi makada wa chama tuliopo nje kwa muda kwa lengo la kuongeza uwezo,zitufanya tukumbuke sana harakati za hapa na pale zinazotokana na vikao nyeti na muhimu kwa mustakabali wa masuala mbali mbali ya nchi.Natambua kwamba kikao hicho ni kawaida kama Mh.Mwenyeketi Rais Jakaya Kikwete alivyobainisha kwenye taarifa yake.Hata hivyo,kwa uzoefu wangu sitasita kusema ni moja kati ya vikao vya NEC ambavyo wajumbe wake watakuna vichwa kweli kweli,kufoka kwa hoja,na pengine kutoleana uvivu.Na hii ni kutokana na uzito wa baadhi ya agenda zitakazowasilishwa ambazo kwa namna moja zitagusia matukio mazito ya kisiasa yaliyoikumba nchi hivi karibu.Hatahivyo,nina hakika kwa uzoefu huo huo kwamba mwisho wa siku chama kitatoka na kauli moja.WanaCCM na wote wenye mapenzi mema na chama chetu na taifa kwa ujumla, tuelekeze dua zetu Butiama ili wanaCCM wenzetu wajawe hekima, busara, na uvumilivu katika majadiliano na hatimaye maamuzi kwa manufaa na maslahi ya nchi

    ReplyDelete
  2. USTAADH ISSA HABARI ZA LEO KAKA..SHUKRANI KWA PICHA MUHIMU KAMA HIZI

    ”..TATE MWENYIKITI..”

    ..…MHESHIMIWA MAKAMBA…AKA..”..PWAGU..” SHASHA NGOJA ..TIONGEE..KISHAMBAA… ONGA MSHI..NVYEDI…HABEI ZE ..”..NDIMA..” MNGOSHINGWA..NDIMA HIYO NVITANA..DU..HEE..

    KUMRADHI JAMANI MIE NA MHESHIMIWA MAKAMBA NI NDUGU YEYE KWANGU ..NI “..MKAZA MJOMBA..”

    KWA WALE MNAOELEWA MAANA YAKE NAOMBA MUWATAFSIRIE WASIO ELEWA KWASABABU YA UTATA WA HILO.. NENO.

    MFANO: INANIBIDI NIWE MWANGALIFU KIASI KWASABABU NENO “..MTOE..” KWA KISAMBAA NI ..”..MPIGE..” KWA HIYO HALA HALA MATUMIZI YAKE, HASA PALE UNAPOENDA “..KUMCHUKUA MWALI NDANI..”..

    ReplyDelete
  3. Pamoja na mimi kumpenda Nyerere lakini hii statement yako michuzi ya kudai ni "mwanzilishi wa Taifa la Tanzania" haijaniingia hata kidogo.Ina maana kabla ya Nyerere kuongoza harakati za kugombea uhuru na Muunganisho wa Bara na Visiwani hakuna mtu mwingine aliyekuwa na mawazo yanayofanana na Mwalimu?
    Hii statement ina uwalakini mjomba.

    ReplyDelete
  4. Hivi jamani huyu Pius kazi yake ni nini maana hasikiki wala haonekani anachofanya hadi siku ya visherehe ndio anaonekana akipiga tumakofi vyake tu

    ReplyDelete
  5. NAOMBA WADAU NAOMBA Kuelimishwa.NIA NA MADHUMUNI ya kufanya hivyo ni nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...