Braza Michuzi.
Naomba kuwakilisha hayo majengo mawili ambayo yamebadili kabisa sura ya mwanza. Ni jengo la PPF (juu) na lingine ni la NSSF.

Mdau Mak

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Duuh..

    inavutia sana.Huo ni uso wa mwanza.

    naomba utusaidi upige picha na miguu ya mwanza mfano ze kisesa,bugarika,Igogo na kule dampo Buhongwa.

    Mwanza kamua usafi zidishine isije kuwa kama LILE JIJI la uchafu ambalo kila mwaka kipindu pindu kama kawa.

    Wanatoka kwenye ilo jiji ...msinimeze.

    ReplyDelete
  2. We Mdau Mak uliyeleta huu mtundiko.
    Sio naomba "kuwaKIlisha" bali ni naomba kuwaSIlisha.
    Jifunzeni Kiswahili fasaha jamani!

    ReplyDelete
  3. miji mingi ktk nchi maskini duniani huwa na sura mbili; ya mbele na ya nyuma. kwa mwanza hapa ndio usoni, alafu kule mabatini na igogo ndio kibera yao.

    SHING'WENG'WE

    ReplyDelete
  4. HONGERA SANA MKURUGENZI WA MJI WA MWANZA. WASAIDIE NA KINA KANDORO DAR

    ReplyDelete
  5. Kwa mujibu wa takwimu za maendeleo afrika, jiji la Mwanza linakuwa kwa kasi sana. Aidha kwa miaka miwili mfululizo limeweza kuwa Jiji safi kabisa (No 1) katika Halmashauri zote za mji na majiji katika Tanzania....

    ReplyDelete
  6. Hayo majina mapya yametoka wapi..?? nisaidieni jamani ,, naona miji mingi imekuwa na tujina angalau tufanane na kizungu au , nchi maarufu duniani..
    Arusha- A- town
    Mwanza- Rock city
    Singida-Singapore

    Hata watani zangu washashi, na wakurya, hamkubaki nyuma eti kamji kenu ka MUSOMA kanaitwa MUSCAT....haaah sina mbavu . hivi wakurugenzi wa miji mnajua hayo..?

    ReplyDelete
  7. Nawasikitikia sana WaDanganika....Mak umesema mwenyewe majengo yanamilikiwa na nani, naona heri uje kwetu tulime uache ushadadi wa majengo ya walewalee!! Halafu kama Mnamjua Walter Rodney, kwa taarifa yenu WaDanganyika kwa Ujumla Hatuhitaji majengo yanayoparamia Anga....Hujamaliza hata robo ya ardhi yako kwanini uanze mikakati ya kwenda kuishi Mwezini?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2008

    jamani watu wa mwanza mnamjua ahmad chopa, mdau wa dodoma lakini toka aingie mwanza miaka sabini hatujamskia tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...