Vikosi hivyo vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania wanashiriki katika Operesheni Demokrasia Komoro yenye lengo la kumuondoa Rais aliyejipachika Bw. Mohammed Bacar.
Hivyo saa na wakati kama huu ambapo vijana wetu wako katika hali ya hatari na ambapo wanayaweka maisha yao hatarini ni kitendo cha kutokuwajibika kwa baadhi ya wanasiasa kudai kuwa Rais amevunja Katiba wakati kipengele wanachokinukuu hakihusiki na mapigano haya.
Kitendo cha kutumia mapigano hayo kujipatia pointi za kisiasa nakipinga na kinaonesha ni jinsi gani baadhi ya wanasiasa hawajui Katiba lakini wakati wanajeshi wetu wako kwenye mapigano wao wanaongoza jitihada za kuwavunja moyo.
Kama raia wa Tanzania naomba nitumie nafasi hii kutuma salamu za ushindi kwa Jeshi la Wananchi, kwa Amiri Jeshi Mkuu na kwa makamanda na wapiganaji wote huko Comoro ili hatimaye wafanye kazi tuliyowatuma kwa haraka, ufanisi na kuhakikisha kuwa maisha ya raia yanalindwa kwa kiasi chote kinachowezekana.
Saa na wakati kama huu, hakuna Chadema, CUF, CCM au SAUT Tanzania ni moja na hatima yake ni moja, na ni jukumu la kila raia kusimama na kutakia ushindi vikosi vyetu na haya mambo ya kulalamika yaje baadaye siyo wakati risasi zinarushwa.
Kwa jeshi letu, USHINDI NI LAZIMA!
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika.
NB: Kwa matangazo yangu ya leo tembelea http://www.klhnews.com na usisahau kutumia search injini yetu pale.
Title: KLH News Episode: Operesheni Demokrasia Comoro - Wangwe angekaa kimya!
Enjoy!
Kabla ya kwenda Comoro ilibidi tujiulize tulipata faida gani kiuchumi kwa kwenda kupigana Msumbiji,Namibia,Zimbabwe,Uganda na Afrika ya Kusini?
ReplyDeleteWajapani walipigwa sana vita ya dunia wakaapa kuwa vita yao watahamishia kwenye uchumi na siyo kwenye bunduki na wameshinda Toyota zuiko kila mahali hadi Ikulu dunia nzima.
Tanzania kazi yetu kuzurura na wanajeshi kupigana nje ya nchi badala ya kwenda na wawekezaji watanzania wanaokwenda kuwekeza nje ya nchi.Nje kuna sifa ya wanajeshi wa Tanzania badala ya wawekezaji watanzania wenye viwanda,biashara kubwa huko n.k.
Hii sera ya kwenda nje kupigana tuuu badala ya kuwekeza ni vizuri ifike mahali ikome tusifiwe kwa mengine siyo kwa ngumi,judo na kurusha mabomu tu kwenye nchi za watu wengine.
Ni kweli huu ni wakati wa kuwapa nguvu askari wetu na si wakati kwa wanasiasa kujitafutia umaarufu. Jana limsikia makamu m/kiti wa CHADEMA (Chacha Wangwe)kupitia BBC akinukuu sehemu ya katiba ya jamhuri lakini maeneo aliyonukuu hayaendani na mission ya vita hii, Huyu jamaa aliongea PUMBA sana na inaelekea bado anaendesha siasa za mwaka 47, zile siasa za uhasama, chuki na majungu badala ya siasa za kuwaleta wanachi pamoja ili washiriki kuijenga nchi. Inabidi wapinzani wawe wanafikiri kwanza kabla ya kukurupuka kwani haya mambo yanahatari. Kwani masula ya EPA hayana mvuto kwa sasa mpaka waache kuyazungumzia na kuanza kudandia hoja ambazo hawazifahamu?
ReplyDeletetumuombe ndugu hao ndugu zetu(jwtz)wasije wakakutana kimeo kama kile cha vijana wa bush kule iraq
ReplyDeleteHatua moja mbele , Mbili nyuma..
ReplyDeleteSisi tunajitwaa katika vita ambayo haituhusu, na haina faida yoyote kwetu, zaidi kutuletea majambazi, trauma ya wanajeshi ambao tutashindwa kuwahudumia wakati watakaporudi nyumbani.
TUNA VITA DHIDI YA UKIMWI, MALARIA, UMASKINI, MIUNDO MBINU, na mengi mengineyo..
Sasa hili kwetu litatusaidia nini ?? tumeshindwa kuivamia KENYA, ambapo uchaguzi wake umefanyika katika misingi hii ya DHULMA, mpaka tumefikia muafaka wa kuelewana pande zote mbili..TUTASHINDWA NA VISIWA VIDOGO KABISA VYA COMORO...South AFRICA mbona inasupport maelewano na siyo vita, kwa sababu moja kuu, hakuna faida kwao wao kujiingiza katika vita itayowarudisha nyuma.
Vile vile ningependa kuuliza kwanini hatuendi kuvamia ZIMBABWE??
Hii yote ni Double Standards JK.. lazima uangalie hilo.
Tujiulize nini manufaa na faida kwa nchi yetu..Ningefurahi kupata majibu yake
kutokana na Mugabe kuonesha wazi kutawala kimabavu kwa kusema hataruhusu wapinzani kutawala Zimbabwe akiwa hai namshauri JK tukimaliza Comoro Twende kupambana Zimbabwe kumn'goa dikteta Robert Mugabe
ReplyDeleteALUTA CONTINUA...VIVA TPDF-Z
ReplyDeleteDah, mimi huwa najiuliza maswali kibao na kujaribu to think out of the box.
ReplyDeleteInaenda hivi; ukiangalia juu juu, hatuna interest yoyote Comoro. Je, hao wanaotupa misaada?? It wouldn't make sense for a first-world country to invade Conoro. Ujue, hawa viongozi wetu are just f****ng muppets and puppets. Lakini wana choice gani ukiacha kufuata matajiri wanao-control the world economy? Kwahiyo mimi binafsi - I am just experssing my own views - ninaamini kuwa kuna pressure kutoka taifa au mataifa fulani. Ukisema JK adinde, TZ itakuwa kama Zimbabwe in year...(laba).
Hata enzi za Nyerere, yale yote ya kwenda Msumbiji, Zim, Angola na SA ilikuwa call from some powerful communist contries; Cuba, Russia, Korea.
Just try to look at this from a different point of view and think for yourself. Media siku hizi inalemaza akili zetu. Jamaa wana-analyze kila kitu wakijua fika kuwa hawako sahihi na wanayosema si jibu pekee.
Anyway, ndio dunia ilivyo. Politicians run this s*%t!
Nimeiona hii toka Wikipedia:
ReplyDeleteFrance's military had already transported about 300 Tanzanian troops and 30 tons of freight to Grand Comoros Island between March 14 and March 16. According to reports a French diplomat said that France was ready to transport Senegalese troops as well, but had not yet done so. The diplomatic source said France remains "favorable" to dialogue but on condition that Bacar accepts the presence of African troops at the port and airport of Anjouan [10]. France's clandestine role was brought into the spotlight when an unauthorised French military flight carrying three people from Mayotte crashed on March 19 in the sea close to Sima on Anjouan. Reports stated that the crew survived.
Put the pieces together now. Is France part of AU? ..Ndio nilivyokuwa namaanisha kwenye comment yangu hapo juu {kama Michuzi hajaibania}.
Hii imenichekesha kusema ukweli(Wikipedia):
ReplyDeleteAnjouan is the world's primary exporter of ylang-ylang oil, an ingredient in almost all perfumes.
Sasa, naona uwepo wa France kwenye 'kuipa' tafu AU makes sense, if you know what I was talking about.
Tanzania kwa kimbelembele!! watu wanakufa njaa dawa hakuna mahospitali badala ya kushughulika na wananchi wao, wana shuulika na wananchi wa wenzao, Tanzania nchi ya ajabu sana sijui tumelogwa na nani!!!
ReplyDeleteWe Paul Kabewa nafikiri huangalii vitu kwa undani unaangalia hapa karibu u dont know issue ya Zimbabwe. Mugabe anakuwa sabotage na nchi za magharibi thus all mwafrika yeyote mzalendo asiefuata mkumbo wa media za western hawezi kumkandia mugabe kama wewe. Soma vitu analyse usikurupuke tu oh mugabe dictator he is man, a real patriot,Tatizo la uchumi wa zimbabwe limeanza mara tu ya kuwafukuza wazungu wanyonyaji basi ikawa oh anavunja haki za bindamu wewe unwaweza kupewa ardhi ukawa settler England thubutu yako hata ungekuwa una hela kama Bill Gate as you are a black you are nothing to them so be careful unachoongea LONG LIVE MUGABE LONG LIVE PAN AFRICANISM LONG LIVE ZANU PF ALUTA CONTINUA.
ReplyDeleteWAKISHAMALIZA HUKO SASA NA WAENDE SOMALIA PIA WAKATULIZEE GHASIA
ReplyDeleteKumbe zile ziara za Rais wa Comorro kuja bongo zilikuwa na lake,mimi nilidhani ni ziara za kisiasa kumbe alikuwa anakuja kuomba apewe tafu na Rais JK.Siasa ni mchezo mchafu sana.Cha ajabu hizi news agency zetu hazikugunduwa haya.
ReplyDeleteWabongo acheni jazba! ni kweli nchi ina matatizo mengi ambayo pia tumeyatangazia vita kama vile umasikini, ukimwi, malaria n.k lakini tusiseme mambo kwa kukurupuka bila kuajua undani wa jambo lenyewe!! ulizeni kwa wahusika wawaeleweshe then ndiyo muwapinge kwa hoja. Naona vyombo vya habari vya magharibi vinaharibu uwezo wetu wa kufikiri na kufanya kila wanalozungumza ni sahihi na hii ilianza tangu tulipoanza kuziita tamaduni zetu za kishenzi, za wazungu ndiyo bora. Hivi leo wazungu kunyang'anywa ardhi zimbabwe ndiyo uvunjifufu mkubwa wa haki za binadamu wakati weusi wengi waliopo kwenye hizo nchi za weupe wananyanyaswa ila hawasemi.Bush alituambia Sadam ana silaha za maangamizi, redio za magharibi ziimba huo wimbo na waafrika kila kona tukaimba na mwishowe tumeumbuka. Leo mataifa makubwa yanaipiga vita china na wanataka kuichafua kwa kisingizio cha tibeti hali Uingeereza na Marekani nao wanawanyima watu uhuru wao kama ilivyo tibet kwa china lakini leo wote wanaisakama china na siajabu wanaharakati wa Tz nao wakaandamana kuipinga china kwa sababu tu wanafadhiliwa na magharibi!!!! WAFRIKA inabidi tuzaliwe upya, tuwe na fikra mpya otherwise tutakuwa watu wa kutumiwa na kusimangwa na wazungu. Tutachafuliwa na tutafanywa kama wanyama wa majaribio kwa sera zao. Siyo kila wanalosema na wanalofanya lina manufaa kwa afrika kwani dunia hivi sasa ipo kwenye vita ya uchumi na vita inayohitaji akili zaidi, ukilemaa tu umeachwa feri!.Maafande piganeni na mungu atawajalia.
ReplyDeletewaje kwa mgambo na wamachinga wanaovua nguo,machangudoa pale joly na kinondoni pia
ReplyDeleteWewe anon March 25, 2:49 PM unae mtetea Mugabe kuwa ni real Patriot..mbona ana silence upinzani? Patriot gani ana loot nchi yake kwa personal gains zake mwenyewe? Angekuwa patriot wa kweli angesimama pembeni baada ya kuona vision yake imeleta maafa (inflation, njaa, rushwa) kwa watu wake. Angekuwa real patriot angeruhusu mawazo ya wananchi wengine "wazawa" sio tu wanamtii' Yes man" na wale pia wanaom challenge katika kubuni namna ya kuipeleka mbele Zimbwabwe. Mbona Gaddafi wa Libya aliwekewa sanctions na mataifa ya magharibi lakini wananchi wake wakasimama nyuma yake mpaka leo? Tofauti hapa ni kwamba wewe focus yako ni very minute..usiangalie suala la kuwafukuza settlers tu. Kwani alifanya hivyo kujipatia umaarufu wa kisiasa. Utagawaje ardhi kwa wananchi waliozoea kilimo cha Peasantry bila, elimu, na mtaji. Hayo ma tretka na farm equipment nyingine watazinunua na nini? Halafu unatoka kwenye surplus ya chakula mpaka kwenye deficit na watu wanakufa njaa..unatetea ni strategy nzuri. Kuchapisha hela na ku devalue thamani ya dola ya Zimbabwe ni nzuri? Leo hii Zimbabwe kwa sababu ya weak economy..hakuna kazi, hakuna political stability, corruption iko juu. Unategemea investors gani wataenda kuwekeza kwenye hayo mazingira?
ReplyDeleteEti "ushindi ni lazima".Huyo anashangilia vita kama ni kitu cha kujisifia.Vita ni "shame" kwa nchi yeyote inayojiingiza.If the purpose is to restore order then thats understandable, but even then we shouldnt sound fanatical about it.Eti "ushindi" ni lazima!,wait until your family is caught up in the middle of it,then you will think twice about your remarks.
ReplyDeletendugu zangu, hata kimya ni jibu pia. wengi mmeandika mawazo yenu ila naona hakuna anayeelewa anaandika nini, tulia tafakari maisha yako kwanza sio kulalamika na kuanza kutoa mifano ya kufikirika, hakuna mchumi hapa wala mwanasiasa wote ni sawa ni mara 100 tuulize maswali kuliko kukurupuka kama kocha anayetoa mchezaji afadhali ana muingiza mchezaji ili mradi- Bube
ReplyDeleteKwa wasiojua watu wa comor walikuwa wanateseka na maharamia wanafanya watu wakimbilie nchi zingine za Africa,wakati tumelemewa na wakimbizi.Comoro kukiwa shwari,that is one tambarare done in Africa.Watu wa comoro ni washiriki sana wa nchi yetu ila kinachowazuia ni magaidi.Kwahiyo nchi moja baada ya nyingine kuweka usalama sawa. Majeshi ya umoja wa Africa yanapigana na magaidi na sio majeshi ya comoro wala wananchi wa comoro.JWTZ inaongoza majeshi mengine ya Afica katika mapambano yaani kama marines wa tanzania kwa wale wasioelewa.Hayo ni majeshi ya umoja wa Africa kwa wale wapumbavu wanasioelewa.Uganda wametoa wao,kenya,south na wengineo.Sasa msiparuke tu bila kujua.Tanzania imo kama kiongozi ili kusiwe na ufyatuaji usio na mpango.Kwa mfano lete wahutu waongoze hili jeshi uone watu watavyouwawa kiholela au lete waliberia waongoze,akili si nzuri.TZ imechaguliwa kuongoza kwa hekima na sio kwa ubabe.Tuwaombee wanajeshi wa Africa warudi salma na sio TZ pekee,mshaanza ubaguzi.Nyoooooo
ReplyDeletembona hatuendi kusaidia somalia,magaidi? nasikia somalia ndio wamejaa sio comoro, kuhusu wakimbizi wa somalia wamejaa kila mahali, marekani,umoja wa ulaya wamesema watagharamia umoja wa afrika wakituma majeshi somalia.jwtz wamevamia kisiwa kidogo jamaa mnatamba hebu jaribuni kwenda mogadishu, tutaanza kusema a lutta discontinua !!!
ReplyDelete