Ikiwa imebakiza mechi mbili mkononi Tanzanite imeshashinda mechi nane nakupoteza moja mpaka hii leo. Kutoka na record hiyo mialiko mbali mbali imekuwa ikimiminika kutoka katika club mbali mbali za soka hapa Georgia na hata Alabama.
Hivi tunavyozungumza timu hiyo itajitupa uwanjani kupambana na Viet Hung SC jumapili hii. Pia tarehe 19 mwezi wa nne timu hiyo inatarajiwa kufanya ziara katika jiji la Bermingham kwa mwaliko wa timu ya Mashada FC.
Watanzania wenzetu waishio Bermingham mnaombwa kuja kwa wingi kuishangilia timu yenu!!
Pia lile tamasha la soka lilipangwa kufanyika hapa Atlanta chini ya udhamini wa Tanzanite Fc EntertainmentCo. limeshathibitishwa na mpaka sasa timu za DC, Houston na Boston zimeshathibitisha kushiriki.
Nafasibado zipo kwa timu nyingine nne zitakazopenda kushirikiikumbukwe nafasi ni nane tu.
Habari zisizothibitishwazinaeleza kuwa Malazi na Chakula vinaweza kutolewa natimu mdhamini ila kama kuna mabadiliko mtajulishwa ilatimu zijiandae kwa gharama hizo (udhamni badounatafutwa).
Pia Organization inapenda kuwaarifu wachezaji wote walio katika duties mbalimbali na timu zao wafike mazoezini kila jumamosi baada ya Indoor game.
Kwa taaarifa zaidi pitia mtandao wa timu :tanzanitefc.com.
Juu nni ni kikosi kamili cha Tanzanite Fc Indoor.
Mdau Hadjihelper
Michuzi hawa jamaa hawana lolote kabisa yaani. Wanajifagilia tu vile wanazionea timu dhaifu. Ngoja tunakuja ktk hilo tamasha lao kuwafundisha soccer.
ReplyDeletehuyo ni goal keeper au book keeping?
ReplyDeleteBaab kubwa Tanzanite FC....keep it up!!!
ReplyDeleteHassan
(Atlanta)
Vijana wamependeza. Lini mtakuja Bongo kuzifundisha mpira Simba na Yanga?? Keeep up the good work brothers!!
ReplyDeleteTunaomba majina.....
ReplyDeleteKwa waliomba majina:
ReplyDeleteMbele kushoto: Bashiri Chuma, Kassim "Don Bosco", Khamza Liganga "Liga", Sajo, Richard na John.
Nyuma kushoto: Hadji "Helper", Hudy, Elvis "Gaza" Mnyamuru, Fredy "Capten Dunga" Mburushi, Togolani Kirumbi "Mtaalam", Malik "Goal Getter" na Said "Bench warmer" Chambusso.
Hilo chama linatisha Yanga na Simba kaeni mkao wa kula!!
Vyovyote vile kila la heri bros!!
ReplyDelete