agosti 25, 2006: mwanamuziki dokta remmy ongala (kati) akiwa na kikumbi mwanza mpango 'king kikii' (shoto) na ismail issa michuzi katika ofisi za copyright society of tanzania (cosota) kupokea mirabaha kwa ajili ya kazi zao zilizotumika nchini.

Bro Michuzi.

Naulizia tu kwa kutaka ufahamu.. Movie kali ya Hollywood ya 'Natural Born Killers' ilikuwa na soundtracks za Remmy Ongala ikiwemo 'Kipenda roho', na wakali wengine wenye majina makubwa kama vile nine inch nails, kwa udadisi wa haraka Movie hii ilipata kuwa Box office hit, kwa kupata mamilioni ya dollars.. sasa je huyu mzee wetu maskini hohe hahe Remmy Ongara alipata chochote kweli???????

caption ndogo chini labda zinaweza kutuongoza...

contains an edit of Remmy Ongala And Orchestre Super Matimila — "Kipenda Roho" ... Box Set: NIN On "Doing The Soundtrack For Natural Born Killers". ...

10, Remmy Ongala - Totally Hot [featuring an excerpt of "Kipenda Roho"], 0:47 .... produced the soundtrack for the Oliver Stone film Natural Born Killers. ...
rateyourmusic.com/release/comp/various_artists___
soundtracks___film_soundtracks_1990_94/
natural_born_killers/ - 65k -


Asante Mkuu

Mdau Frank Godfrey
A-taun

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Too much of anything is harmful na pia wanasema everything should be made as simple as possible but not simpler! iyo link ya jamaa inayoelekeza habari za ongala mbona imepitiliza hadi nje ya Chikilini, Michuzi najua hatukulipi ila do some repair work kwa web yako bwana, hao MK group ndio Perfection yao hiyo? Ukilala watu hawalali, hii blog sitaki iwe km Kibajaji, hata utoke Dar adi Chalinze mtu akianza na landkruza Dar atakukuta hata segera hujafika, Michuzi usilale bwana fanya mambo matamu, Hao MK nadhani wanamaanisha Cheap sio PoorQuality, shaurienu!

    ReplyDelete
  2. Jamani Tunataka kuona Wanamuziki wetu wanalipwa Haki yao stahili kwa Kazi ya Jasho lao!Hii COSOTA kweli bado iko hai?Na ina mtandao gani wa kufanya shughuli zake za kudhibiti Hakimiliki za wanachama wake katika mikoa na wilaya zote nchini?Njia moja wapo ni kwa kuwa na Authorised Agents wenye Nembo zao zinazo tambulika kisheria pengine katika mikoa mbalimbali nchini.Kila Mwanamuziki atakapo toa kazi yake ataingia na Authorised Agent mmoja wapo wa chaguo lake,kupitia Cosota.Kwa hiyo kulingana na makubaliano baina ya Mwanamuziki au Msanii na huyo Authorised Agent kupitia Cosota,mkataba utakuwepo wa MALIPO MAALUM kwa Mwanamuziki toka kwa Authorised Agent.Yatakuwepo ya mkupuo wa kwanza na yatakuwepo ya hatua kwa hatua.Mwanamuziki anaweza kudai ajengewe nyumba na pesa kidogo badala ya kupokea zote kama pesa taslimu kwa idadi fulani ya mauzo ya kwanza.Na kila kazi itadhibitiwa maduka ya rejareja na Authorised Agent mwenyewe kwa kudhibiti matumizi ya nembo yake mwenyewe pamoja na resiti za mauzo.Iwapo mwenye duka la rejareja atafumwa na Mwanamuziki mwenye Hakimiliki yake akiuza kazi zake zisizo kuwa na Nembo ya Authorised Agent wake moja kwa moja Madai ya Fidia yatafanyika kutoka kwa Authorised Agent ambaye litakuwa jukumu lake kumfungulia mashtaka mhusika mwenye duka la rejareja.Utaratibu huu unaweza kurekebishwa kidogo ili ukidhi mazingira yatakayo kuwepo.Wanamuziki katika umoja wao au kila mmoja kivyake wanashauriwa kuwa na Wanasheria wao watakao wasaidia katika hili.Ikibidi hata kuwaajiri Wapelelezi Binafsi(Private Detectives) wawasaidie kutafuta wahalifu hawa katika maduka ya rejareja hata ikiwa mara moja kwa mwiezi mitatu kimstukizo.Itasaidia kukomesha tabia hii.Mimi siwalaumu Watanzania kwa kufanya biashara hiyo ya kuuza kanda za muziki au VideoTapes au CDs au DVDs za wanamuziki na wasanii mbalimbali katika utaratibu ambao umekuwepo hapa nchini kwa kipindi kirefu bila ya wao kujua kwamba kwa njia hiyo walikuwa wakiwatia umaskini mkubwa wasanii kwa kazi zao halali ambazo wangestahili kufidiwa gharama walizozipata.Lakini sasa ni vyema wakatambua kwamba hali lazima ibadilike.Ili kazi ya muziki izidi kuendelea na kustawi zaidi ni lazima tuthamini michango ya wasanii na wanamuziki wetu kwa kuwalipa kile watakacho stahili kwa kazi yao.Ili hata wafanya biashara nao waendelee kuwapo katika soko.Nimejaribu kutoa ufafanuzi huu kidogo kwa sababu imenitia uchungu sana kuona Wazee wetu hawa wakitaabika kwa maisha duni wakati jitihada zao zikiwatajirisha wafanya biashara wengine bila ya kutoa jasho lolote.Hii siyo Haki na siyo Maendeleo.Vijana wetu wanao chipukia leo wataikimbia Fani hii ikiwa mambo yenyewe yataachiwa yaendelee kama zamani bila ya udhibiti wa aina yoyote.Lazima twende sambamba na wenzetu ulimwenguni kote.Ndipo Fani ya Muziki,Sanaa na Filamu itakapo komaa na kustawi hapa nchini.Pengine niliyo yasema yamekuwa yakifanyika.Lakini siyo kwa kiwango cha kuridhisha.Kila Mwanamuziki anayo haki ya kunyanyua sauti yake na kupiga Kelele akiomba msaada ili sisi Watanzania wapenda Muziki tuweze kusaidia pale itakapo wezekana.Na wenye maduka waambiwe ni marufuku kuuza kanda au videotape au DVD au CDs zisizo kuwa na Nembo za HAO AUTHORISED DEALERS PEMBENI YAKE LOGGO YA COSOTA!Good Day to all Musicians and Actors!

    ReplyDelete
  3. Kumbe karemi ongala ni kahensamu akitoa rasta ee?
    niliskia alilia sana kisa kapewa mshindi wa pili kwenye mashindano ya sura mbaya duniani, sijui kweli au ni usanii tu???

    ReplyDelete
  4. hata aliyetunga na kuimba version ya kwanza ya 'the lion sleeps tonight' (imbube), naye alidhulumiwa. Disney na wasanii wengi walitengeza mutli-million dollar fortune coz of huo mwimbo but the poor guy died with only $25dollars to his name. lakini familia yake walienda kotini kudai haki yake.

    ReplyDelete
  5. ya namfagiluia sana dr Ongala kwa nyimbo zake za kuelimisha.
    ila jamani kuuliza si ujinga,hivi wewe michuzi ni ndugu yake na waziri mkuu mizengo pinda?mbona mwafanana sana?

    ReplyDelete
  6. Jamani!Remmy Siyo mzee ni uchafu tu!na kuwa jamaa alikuwa aakigida sana Gongo na kuvuta sana ban..??
    alkini hana uzee wowote,na kwa kuwa mwaka aliozaliwa kule kijijini Kindu,Bukavu haukumbuki sawa sawa!mara nyingine anasema 1947!mara 1951 hakumbuki,lakini siyo mzee kama King Kiki au Shem Kalenga na Kassim mapili

    ReplyDelete
  7. Naomba kuuliza..kuuliza si ujinga. Hivi Remmy, Mizengo na Michuzi ni ndugu au la?

    ReplyDelete
  8. He/she is right,
    Nilikuwa nikitembelea Mtandao nikaona Mtandao wa wapelelezi binafsi, hebu waambieni hao wanamziki wawatafute ile waweze kusaidiwa... web yanina ni www.tzprivateinvestigationagency.com
    they are Private Investigators,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...