Rais Jakaya Mrisho Kikwete kesho tarehe 2 April, 2008, saa kumi jioni, atalihutubia taifa kupitia wana CCM na viongozi wa Jumuiya za Chama katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Rais hakuweza kutoa hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa tatu (Machi) kutokana na maafa yaliyotokea katika machimbo ya Tanzanite, Mererani katika mkoa wa Manyara ambapo ilimlazimu kwenda kutembelea eneo la maafa ili kujionea hali na kutoa pole kwa wananchi na wachimbaji wa Mererani.

Hotuba hiyo itatangazwa moja kwa moja kupitia redio na Televisheni mbalimbali hapa nchini.


Imetolewa Ikulu,
Dar-es-salaam,
Tarehe 1, April, 08

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. HOTUBA HIYO NI YA MWENYEKITI WA CCM NA WAFUASI WAKE NA SI YA RAISI AKIHUTUBIA TAIFA, WANANCHI WENGINE TUSIO WANACCM TUTAKUWA WASIKILIZAJI TU, KWANI HATURUHUSIWI KUHUDHURIA KWENYE MKUTANO HUO. KULIKONI RAISI ANAVUNJA UTAIFA NA KUINGIZA ITIKADI ZA VYAMA KATIKA UTENDAJI WAKE?

    ReplyDelete
  2. Read between the lines!Soma Mistari tafadhali!Hii Hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi ni kwa ajili ya wana CCM tu peke yake?'Atalihutubia Taifa kupitia wana CCM?'.Maana yake nini?Watanzania Siasa kwetu BADO HAIPANDI!Hatutathmini poltical implications zake,hatutathmini athari zake kisiasa!Kwa nini tangazo lisisomeke kwamba,'Rais atalihutubia Taifa kama kawaida yake kila mwisho wa mwezi katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa kumi jioni na hotuba yake itatangazwa moja kwa moja redioni na katika televisheni.Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa DSM wamealikwa.Wote mnakaribishwa kuisikiliza hotuba hiyo kupitia redio na televisheni zenu.Ahsanteni kwa ushirikiano wenu PERIOD!Tatizo hapa siyo tangazo bali lugha na msamiati uliotumika katika kulisuka tangazo hilo.Ofcourse usisahau masuala ya kujikombakomba please in politics this is acceptable to a 0.000000001 per cent,siyo mbaya,at least!

    ReplyDelete
  3. CCM ni wanafiki na dawa yao iko jikoni. Mimi nionavyo ni kama wanawanga mchana na kila mtu sasa anayaona maovu yao. Sidhani kama itakuwa easy this time CCM kujisafisha na machafu yote kama vile Richmond, EPA, IPTL, Kiwira, Mgogoro wa kisiasa Zanzibar nk. Ni mambo mengi kwa kweli JK inambidi awaeleze watanzania kama kweli anataka kuaminiwa na wananchi.
    Sometimes najiuliza je tuna kura za maoini zinazoendeshwa na magazeti au TV stastions kuonyesha ni percentage gani ya watanzania bado wanamwamini JK na serikali ya ke ya CCM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...