(Naomba ibandike pasipo jina langu mkuu wangu)

Habari yako kaka Michuzi,
pole kwa kazi nzito unayofanya daima kutuhabarisha habari mbali mbali kwa njia ya picha.Naomba kutumia blog yako kuwasilisha kero yangu kwa hawa ndugu zetu wa Tanesco, pamoja na kuwatetea sana hivi karibuni, lakini nao wakati mwingine wanazidi, wanalalamika sana kwamba wanabebeshwa mzigo mzito wa kulipa madeni na kadhalika, pia wanadai wana mpango wa kuongeza bei za umeme ili waweze kujiendesha, lakini sijui huko kujiendesha wanamaanisha nini ikiwa hata mambo fulani ya kawaida wanashindwa kuyafanya kwa wakati.
Pale Tabata Kimanga kuna nguzo moja imeanguka kutokana na mvua, sasa hivi ni karibu wiki moja inakatika, lakini hawajafika kubadilisha na kuweka nyingine, ndo kusema wakazi kibao wa maeneo hayo hawana umeme kwa muda karibia wiki nzima sasa hivi, kwanza kabla hiyo nguzo haijaanguka, ilikuwa imeliwa na mchwa, wakaelezwa kwamba hiyo nguzo ni hatari, hawakufanya lolote, ilipodondoka, walipoelezwa, wakaja kutoa nyaya zao, wakasema watakuja, mpaka leo ni kimya, jamaa wakifuatilia, jamaa wanaonekana kabisa wanataka mshiko ndipo warudishe huduma, sasa kwa mtaji huu tutafika kweli.
ni hasara kiasi gani wanawasababishia wananchi wanaoishi maeneo hayo? pia na wao ni kiasi gani cha pesa wanapoteza mpaka sasa hivi? hili nalo tunahitaji kusaidiwa kufikiri kwa msaada wa wawekezaji jamani? hivi nguzo moja ni bei gani ya kushindwa kununua? mbona pale Tanesco tunaziona nguzo kibao zipo tu, kuja kuweka hapa kuna tatizo gani? na siku wakirudisha umeme, kwa wale ndugu zangu wanaotumia mita zao, utasikia bili yao, mpaka unaweza kujiuliza hivi umeme huu umetumika lini na vipi?
jamaa ni mafundi sana wa kubambikia watu bili za ovyo, nakumbuka mjomba wangu wakati anatumia mita zao, kwa mwezi akiletewa bili nzuri (pesa kidogo) basi ni shilingi elfu themanini (80000/=) basi akawachoka, akaamua kuweka mita ya Luku, kila mwezi anatumia umeme wa shilingi elfu kumi na tano (15000/=) na hajabadili matumizi zaidi ya kuongeza vitu vinavyotumia umeme, sasa unaweza kujiuliza wakati ule anatumia mita za kawaida pesa nyingine alikuwa anamlipia nani?
hivyo tunaomba wahusika wanaosoma (kama huwa wanapitia blog hii) warekebishe tatizo la umeme pale Tabata, imeshakuwa ni kero sana kwa wakati wa eneo hilo.
"Be Strong and of Good Courage"
mdau tabata

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...