Hi Bro Michuzi,
Natumaini u mzima! Mimi ni mdau wa blog hii (yaani imekuwa kama dose kwangu) daily mara 2 (asubuhi na jioni)

Nimeona leo blog hii imefikisha visitors 3,762,102 (since 2006) kama kila mmoja angekuwa anachangia Tsh. 10/- kwa ku-visit, sasa hivi Bro Michuzi ungekuwa na Lexus kali …
Naomba ku-share na wenzagu takwimu hizi kuhusu “Internet Usage”, duniani na hata nyumbani TZ. Pia angalieni watani wetu wa East Africa Federation, tusipoangalia tutamezwa wazima wazima!!
Tanzania kwenye “data” hizi tuko chini kama nafasi ya 18 hivi.
Hizi data ni halali/ halisi kutoka Miniwatts Marketing Group, ambapo ni updated December 31, 2007
please please email kapuni!!
thanks,
good day,
Mdau wa Durban Zitto (Not Kabwe!)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ombi la Msaada
    Pamekuwa na promotion kubwa ya mkutano wa wafanyabiashara wa kutoka Marekani wa sulivan. Sisi tumeambiwa tujitayarishe lakini hakuna hata siku moja tumeambiwa wafanyabiashara wanaokuja ni akina nani ama ni wa aina gani ili katika kujitayarisha tujue tunakutana na watu wa aina gani na matayarisho yetu yalenge uwiano wa maslahi. Ama sivyo watakuja na pasiwe na chochote. Nani atakuwa wa kulaumu kwa kuua fursa hiyo? Hebu tuwe makini kidogo!

    ReplyDelete
  2. Dah naona Wanigeria wanaongoza kutumia mtandao.Hii inadhihirisha zile email za wizi(scams) wanaotumia watu.Inaelekea wanakesha kwenye cafe kutuma haya ma-email kwa watu mbalimbali duniani.

    ReplyDelete
  3. watu ukiwaambia andika email au njoo online anasema piga simu au anakubeen mnakaa kutajirisha hizo phone firm tu mdandao ni sawa na bure use it ukiweka computer yenye speed kijijini watu wote wataongea na kuwasiliana na hiyo computer ila seems bongo bado kila mtu anafancy simu sijui kama tutafika kweli watu bado wanaogopa computer una email address ujafungua wiki mbili unaishi vipi jamani??
    Londoner

    ReplyDelete
  4. Duh...hata Waarabu wametuzidi...'elimu ni mali'!!!

    ReplyDelete
  5. mi nafkiri kwa hapa kwetu tanzania gharama za internet ziko juu kiasi ndio maana watu wanaogopa kuunga , pia connection mara iwepo mara iko down mfano voda bei zao juu, zantel wako slow,sijaelewa provider wengine

    mi naona tatizo hapa ni gharama za mtandao wenyewe ziko juu kiasiukilinganisha na uk

    ReplyDelete
  6. wa nigeria ni wezi tu

    ReplyDelete
  7. Its not about how often we use internet jamani.. Its How u benefit from it.
    Kuna watu hawafanyi kazi za kuajiriwa wanapata hela kwenye internet.. kama mimi nauza vitu daily ebay kama part time job hapa mtoni.. sasa Bongo tumieni fursa hii kupata kipato halisi na halali.. sio kukalia rushwa tu.. NB sijasema muuze ebay kama mimi manaake najua kabisa africa minada ya mtandaoni watu wataibuwa mpaka wakome.. lakini njia ziko nyingi sana.. Mfano ukiwa na site tu ukaweka vijitangazo viwili vya voda na kampuni nyingine una uhakika dola mia kwa mwezi hukosi wakati bei ya kuweka site hewani ni kama vile hela ya kwenda rose garden kulewa... nimekumbuka niweke wazi.. JAMANI WABONGO MNALEWA SANA sijui hela mnapata wapi?? HIVI MNAFIKIRIA KUINVEST KWELI ILI MLEWE MILELE KAMA KWELI MNAPENDA POMBE?? AU NDIO rushwa.. manaake madili yote huko naskia yanapangwa baa mpaka makamba akapiga marufuku kukaa baa na kucheza pool mchana.. lol..
    All the best jamani.. Mkitumia internet vizuri mnaweza kuwa matajiri au hata kuongeza kipati.. TAHADHARI: TENA KALI SANA... MSITUMIE INTERNET KUIBIA WATU.
    NB2: Kuna mdau kasema hata waarabui wametushinda.. Hivi unajua kama misri wanatumia mfereji mmoja tu kwa matumiozi ya maji domestic na industrial?? na kila siku maji safi yapo na viwanda kama kawa?? Nyie mna maji mpaka hamjui myafanyeje na bado kila siku umeme mgao.. maji taka bombani nk.. Waarabu sio wenzetu... sisi wenzetu burundi na rwanda bwana..Angalieni GDP zao ndio mtajua kama wao ni matajiri so kuafford internet ni kitu cha kawaida.

    Ndimi Mchangiaji.

    ReplyDelete
  8. computer ni bure kuingiza tatizo wanunuaji hakuna kila mtu anaogopa computer na kama ipo kuweka net ni deal kubwa sana so inabaki kuwa pambo tu na kufunikwa so serikali lazima ipange bei watu waweze kuweka net la sivyo tutakuwa wa mwisho.

    ReplyDelete
  9. acheni wivu kuhusu wanigeria.
    Kwanza mjiulize ni watanzania wangapi wenye umeme? au mnafikiri hizo komputer zitawashwa kwa vibatari?

    ReplyDelete
  10. nyie mnahesabiwa hizo takwimu na IP adress, huku bongo kwa taarifa yenu IP moja kama ya cafe wanakaa watu mia na upuuuzi, nakataa hizo takwimu ni feki, IP zetu hazijawa mapped kwaio si kweli watu wangu, inazidi waliyoweka (mi nimeona eti 380000 tu ndio wanatumia net walau mara moja kwa mwezi, si kweli. Afu kuhusu hit counter kama ya mchuzi ni inasoma page ikiload, kwaioa ata wewe ukikaa ukirudiarudi idadi inaongezeka tu, na pia km inatumia IP inachemsha maana nikikaa mimi, nikiinuka akija mwingine km sijaexit inaonesha ni mimi mimi naendelea, takwimu feki hizo!

    ReplyDelete
  11. Wewe unayesema takwimu ni feki, wabongo tunaelekea kwenye milioni 40. naomba unipe asilimia kidogo tu ya wabongo wanaotumia umeme, tena weka asilimia ya wenye umeme tu na sio watumiaji wa pc.

    Ukija na hizo asilimia utakuja kuona kwamba wabongo we have a long way to go.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...