
Kwa mujibu wa habari zilizotolewa naMkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhaville, marehemu Mndolwa alilazwa hospitali ya Kairuki kwa wiki moja. Kifo chake kimesababishwa na shinikizo la damu.
Mndolwa ambaye alizaliwa Novemba9,1962 mkoani Tanga alianza kazi za uandishi mwaka 1980 katika Idara ya Habari ya Radio Tanzania (RTD) na aliajiriwa na ITV na Radio One Julai 1994.
Mipango ya mazishi inaendelea kufanyika. soma zaidi habari hii ya kuhuzunisha kwa kwenda lukwangule.blogspot.com
Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu - AMINA
Michuzi shukrani kwa kututaarifu hili, hii imenistua sana.Mungu aiweke roho yake mapumzikoni na aipe nguvu familia yake.
ReplyDeleteDu!RIP Mndolwa....Mungu awape nguvu familia yako.
ReplyDeleteBwana ametoa na Bwana ametwaa.
ReplyDeletepoleni sana Ndugu wafiwa tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu kwenu kwa kuondokewa na mpendwa wenu nyie mlimpenda Mungu kampenda zaidi
katochi
R.I.P. Brother.
ReplyDeleteSteveD.
Duh!!mungu amlaze pema peponi marehumu,, alinisaidia sana katika maswala ya uandishi
ReplyDeleteRIP John,
ReplyDeleteFaraja ya Mungu iwe pamoja na wote walioguswa na msiba huu.
Patrick Kamera.
RIP
ReplyDeleteMungu amlaze roho yake peponi
Na kama alizaliwa Nov 62 atakua na miaka 45...au ni mimi sijui kucount
Poleni sana wafiwa mimi namkumbuka sana john halikuwa lafiki sana wa kaka yangu mwandishi wa gaziti la michopo mashaka mapunda naye alisha tutangulia.
ReplyDeleteMungu ashukuriwe,Pole kwa familia,ndugu na jamaa wa Marehemu.Nilimfahamu Marehemu nimeikitishwa na taarifa za kifo chake, tumuommbee ndg yetu.AMEN.
ReplyDeleteAsante Michuzi.
Poleni sana wafiwa namkumbuka sana John enzi za Chakuwajali (chama cha kuwasaidia waliopatwa na hajali tz)alitoa mchango mkubwa sana katika chama yeye na waandishi wengine kina Khlid Mika..
ReplyDeleteMungu akuweka mahali pema peponi Amina
Poleni sana wafiwa nimesikitika kupata habahari hizi. namfahami John miaka mingi sana
ReplyDeleteRIP John.
ReplyDelete