




Brother Michuzi,
I hope you are fine and congrats for the impressive job. Nimeona nikutumie hizi photos za Tosamaganga, Iringa, ili wadau wapate kujikumbukusha walikotoka.
Hii ni shule ambayo waheshimiwa wengi wamepitia and it was among the best government schools( Sijui kama bado ina hiyo status!!).
Mdau Sao Paulo.
Tosamaganga one of the Golden Oldest Best Schools this country has ever had!Thanx to the Roman Catholic Missionaries wherever they may be.Indeed one of the 'Classic Old Schools'.Imetoa Wasomi wazuri wengi sana,miongoni mwao hivi sasa ni Viongozi Serikalini,Wakuu wa Idara za Serikali,Wahadhiri wa Vyuo Vikuu na Maprofesa katika Fani mbalimbali,Wataalamu wa Uhakika,Raia wema na wacha Mungu.Ilikuwa shule ya Wamisionari lakini ilipokea wanafunzi wote bila kubagua imani za kidini,ilikuwa na Waalimu wazuri sana na wachapakazi hodari,ilitoa wanafunzi waliofaulu vizuri sana katika masomo yao,ilijenga mahusiano mazuri na ya karibu sana na Sekondari nyinginezo mkoani Iringa na ulimwenguni kwa ujumla.Kijiji chenyewe cha Tosamaganga ni kama Educational and Social Comlex.Kuna shule nyingi kuanzia Chekechea,Primary,Sekondari hadi High School.Kuna Girl Schools na Seminaries.Ni mwendo wa nusu saa hivi hadi Iringa Mjini na mwendo wa robo saa hadi kijiji cha Kalenga yaliyo kuwa makao makuu ya MKWAWA aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kijadi wa Wahehe wenyeji wakuu wa Mkoa wa Iringa.Tosamaganga ndipo palipokuwepo na Kituo cha kwanza kabisa cha kuzalishia Umeme uliotumika katika baadhi tu ya maeneo ya Mji wa Iringa kwa wakati ule,mji huo ukingali mdogo sana.Kama kumbukumbu zangu hazikunitupa mkono umeme ule ulitolewa na Wamisionari kwa Mji wa Iringa sawa na Bure!Baadaye watu wakaja anza kulipia malipo madogo sana.Kwa hiyo Tosamaganga pia kwa kiasi fulani imechangia sana katika ukuaji na maendeleo ya Mji wa Iringa na Mkoa mzima wa Iringa kwa ujumla.Kilikuwa ndicho kitovu cha Elimu,Sayansi na Ustaarabu.Ipo Cathedral kubwa sana ya Roman Catholics pamoja na Hospitali ya kutegemewa.Kwa upande wa Social Life nayo Tosamaganga haikubaki nyuma.Nakumbuka wakati ule baada ya masomo mazito ya wiki nzima walimu walikuwa wakitupa muda wa kujiliwaza kidogo wakati wa wikiendi.Yalikuwepo MaBougie au Madisco wakati ule kina Jmaes Brown na Otis Redding walikuwa wakitamba kwa mitindo yao ya SOUL MUSIC na mitindo ya nywele AFRO.Siku shule za wasichana wakikataa mialiko yetu kwenye Madisco au Bougie za Wikiendi basi tuliishia kujiliwaza kwa kitu kilicho itwa BULL DANCE.Ilikuwa balaa kila mmoja akijaribu ku demonstrate His New Dancing Style.Break Dance na Ma House yalikuwepo kibao.Wengine waliofanikiwa kutoroka kidogo walikimbila kijiji cha jirani cha Kalenga kupata ULANZI kinywaji laini cha asili sometimes wakichanganya na pombe ya GUINESS,ilikuwa BALAA Mze!Lakini usiku KITABU HADI KUNAKUCHA halafu watu wanaruka na Distinction kwenye paper mze!Wakati huo kulikuwa hakuna UKIMWI na nchi ilikuwa imetulia.Hiyo ndiyo Tosamaganga kwa ufupi.Ujana mzuri ndugu zangu.Use your Time Carefully and Wisely.Time if unwiselly spent may turn out to be your BIGGEST ENEMY!Lost Time can not be bought even for a Billion Dollars,take care.Adieu!
ReplyDeleteThe grety Tosamaganga!!Good old days of ours at tosamaganga!!namkumbuka head master marehemu mzee mpogole(dudu),nakumbuka by then kulikuwa na natural selection yaani ilikuwa inaaminika kila form five wanapoingia tosamaganga mmoja wao lazima afe(must be selected by nature to die) by then iliaminika kwamba hiyo ilikuwa ni moja ya defencive mechanisms za dudu ku-remain kwenye power tosamaganga!!I remember so much these guys(PCB CLASS-1991-1993),Pius Mahimbi,Peter Sanga,Ntebe Majigo,Mkuji.N.Mkuji,Ulimboka Kabage,Albert Mbukwa,Ranwel Mbukwa,Billy Haonga,Emil Yotham,Jasper Makalla,Ebrahim Mwangaraba(EGM),Tadeo Lupembe(EGM),Edward Bruno(EGM),Ephraim Helman(PCM),Mashaka Mpofu(PCM),Denis Mtatifikolo,Angel Mbugi na wengine wengi wa dalasa letu la PCB mwaka huo na wasalimia sana.Second by then Mwamvika(chipanzii)yupo wapi siku hizi?
ReplyDeleteLong live Tosamaganga!!!!Namkumbuka Huge!!Dominicus Mapunda(pcm)
Mdau,Hosea Sichone(PCB 1991-1993)
hoseasichone@yahoo.com
Ama kweli ya kale ni dhahabu!!! Picha hizo zimenikumbusha mbali sana..Half mile n.k. kwa taarifa za mwisho tu nilizokuwa nazo Mr Mwavika(CONTRA) alikuwa ni afisa elimu taaluma wilaya ya Kilolo Iringa..Story za Dudu tulizikuta pale mara baada ya kuhamishiwa Mkwawa High School na hatimaye kufariki baada ya muda. Tulimkuta Head Mr Mbanga na timu nzima imekamilika kama vile Mbilinyi,Sanga N, Sanga ASK na Mpiga picha maarufu (Mwl jina limenitoka)inawezekana hata hizo picha alipiga yeye..
ReplyDeleteBig up kwa mdau ailtuletea picha hizo..Nimekumbuka bweni langu la MAPINDUZI na MANDELA..
Mdau Abel B. Nzogela (PCM 1993-1995)
anzogera@yahoo.com
Jamani juzi kuna mdau alipiga picha za Tabora School na kuzirusha hapa. Naomba sana, tena sana kama anaweza kupiga picha za Milambo Secondary School, shule ya wanaume pale Tabora basi afanye hivyo!
ReplyDeleteInatia raha kuona shule yako japo kwenye picha baada ya zaidi ya miaka 10.
Dah! we acha tu mimi nilikuwa hapo July 1990 to May 1992, nakumbuka kipindi hiki ndio 'dudu'(Ni marehemu sasa hivi) aliondolewa madarakani kwa mgomo mkubwa sana. Nakumbuka washkaji wa class yangu EGM akina Prosper Mambo(UK), Alfred Herman(Dar), Tumaini Mgomi MTZ(USA), Hodrum Suleiman(Dar), Richard Mgonda Chair(Dar), Leonard Mgoyo(alikuwa UK, nafikiri kaisha rudi pale AR) na washakaji wengine kama Donald Herman(CBG)yuko USA, Lordwell Lugano(CBG) yuko UK, Nsajigwa Mbije yuko pale SUA lecturer. Dah Tosa washkaji mnakumbuka Half Mile? Mhavika sijui yuko wapi lakini mgunya yuko pale Arusha ni headmaster pale Arusha Sec. Dah Lyalamo, ma-partner enzi hizo Iringa girls(Zoo).
ReplyDeleteNawamisi kichizi
born2bkul@yahoo.com
nimesoma hapo mbona wadau mnamkumbuka "FUBU" na huo wimbo wa shule " Tosa Maganga" pia na wale boko kule shambani...
ReplyDeleteNAWAONEA DONGE WASHKAJI SIJUI KAMA HUKO KWETU TULIPOSOMA WALIKUA WANAJUA HATA KAMERA DAH KUDADADEKI WALAH KAMA KUNA HATA MMOJA ALIYEWAHI KU PHOTO PALE LEMBENI SEKONDARI SASA NYERERE SEC ATURUSHE NASISI
ReplyDeleteMICHUZI KAMA KUNA KOSA KUBWA UMEFANYA NI KUTOA PICHA YA TOSAMAGANGA NA KUACHA YA WAKE ZETU INAONYESHA JINSI GANI GENDER ISSUE AMBAVYO HAIJASINK KWA KICHWA CHAKO HEBU TULETEE HARAKA YA WAKE ZETU AKA IRINGA GIRLS..
ReplyDeletekhamsini mwalimu wa namba na sura mbaya kuliko wote mlimuacha?Double life je?Half mile kwenda usiku noma.Mama mingoi alitutoa sana.Masela kuna watoto wenu mliozaa na wanakijiji wanaendelea vizuri wanaomba mwatembelee
ReplyDeletehiyo ndo shule ya wanaume, ukimwona mwanamke sister (watawa) au watoto wa lyalamo ila nawasifu sana vijana maana hakukuwa na kesi za kubaka watoto hongereni sana vijana. hope ukimwi utawapitia mbali baada ya ile conditining ya Tosa! Ila tabia ya kutaja watu walipo siyo ya wanafunzi wz tosa nadhani hyou aliyeswataja wenzake wako us, uk dar alikuwa mwanafunzi wa kalenfa sec pale chini wanaume si mnakumbuka wale vijana kwa kujinadi?
ReplyDeleteAnonymous wa 7.51pm umenena jambo la maana hebu Michuzi fanya jambo la kuwatafuta Iringa Girlz A.K.a Jangwani wa Iringa.maana nakumbuka enzi hizo ukisikia Disco Tosa Mabwenini hakukali basi ilimradi shughuli ya kwenda kuwaona wachumba.Hivi Jamani Mama Mgonja bado yupo?alikuwa na mikwara naye sometimes.DJ Imma bado anaendeleza libeneke la Disco kati ya Tosa na Iringa gilz?
ReplyDeleteAnonymous wa Thursday, April 3, 2008 7:51:00 PM EAT.....umenigusa kumoyo....yaani mamsapz wa Tosa tumesahaulika naona. i remember disco la Tosa kusema kweli kulikuwa hakukaliki pale iringa girls a.k.a Zoo.... viroho vinapwita. Mkwawa nao walikuwa hawaachi kuzamia....basi alimradi. Hivi yule Shabba alikuwa Mkwawa au Tosa?
ReplyDeleteMMESAHAU MAMBO YA ULANZI HALAFU WAKATI WA DISCO MNASUUZIA NA BEER ILI WALAU MNUKIE MJINI.....HAKI YA NANI!
ReplyDeletewoooow nimefurahi kuiona tosa ila mimi nilikuwa mkwawa 1999-2001nakumbuka nilienda tosa mara moja kwenye easter conference,pametulia ila kwenye msosi wa tosa ni ugali na ndondo tu daily siwapatii picha maana sie mkwawa tulizoea kununua mboga mboga kwa wake za walimu wa mkwawa ukichanganya na ndondo inakuwa mwake babaake kwa nguna ila tulipoenda tosa hamna anaeuza mboga ya majani ndondo tu kwa kwenda mbele labda walikuwa wakiuza maandazi tena yanaisha mapema sana,tuliinjoy mazingira ya tosa ila tulimiss mikate ya mkwawa aka vimgimwa na mboga za majani.
ReplyDeleteMmmmh weka na picha ya dining pale tulipokuwa tunapata 'sifongo' dah bonge la kumbukumbu.
ReplyDeleteKudadadake!sema wazee wa msiwasisi, hivi nani anakumbuka yale mawe waliyorushiwa Highland pale msiwasi 1991? jamani we adolff malembeka, morgani chaulaya mko wapi? kilato na Aswile je mpo?
ReplyDeleteMi nimefarijika sana kuiona Tosa Boys...... ila mmesahau mabanzi haya ni maandazi ambayo tulikuwa tukichanganya na uji ili kupata mchanyato na matokeo yake ni mwendo wa kusinzia class! ila cha ajabu vijana tulikuwa tukipasua kwa sana National
ReplyDeleteNakumbuka mafuta ya taa yanawekwa kwenye ndondo kila Iringa Girls aka Zoo wakija pale kwa disco hivi wadau ilikuwa kwanini? mi nimesahau nikumbusheni
Wewe Dada anon Frid 5:39 unayetaka kufahamu kuhusu Shabba nadhani itasaidia ukitaja miaka uliyosomea pale Zoo, unajua katika kijiji hiki kuwa waliosoma miaka 60,70,80, 90 na karne hii ya 21. Kama ulisoma miaka ya 70 basi utakumbuka yale mabasi ya RAB. Tosamaganga ulikuwa mfano mzuri sana wa Technology village inasikitisha kuona kama nchi tumeshindwa kupanua sehemu mbalimbali na badala yake kuacha pazolote. Hayo mabati hayakuwepo enzi zetu na uniform ilikuwa kaptura na kibaridi cha Tosa hatari.
ReplyDeleteKwa taarifa picha hizo zilipigwa na Dr Marchini kati ya Sept 1995 na sept 1998 picha zaidi tembelea
ReplyDeletehttp://www.stats.ox.ac.uk/%7Emarchini/vsopics.html Aliyekuwa Gavana BOT Balali alisomea hapo Tosa bila kumsahau Waziri wa sasa wa Elimu
Anonymous wa Friday, April 4, 2008 2:49:00 PM EAT....mie nilimaliza pale zoo 1994, kuna mkaka pale Tosa alikuwa anafanana na Shabba Ranks akawa hadi ana panki kama la Shabba Ranks, na akawa anajiita Shabba. I never knew his real name, ila alikuwa ananyanyasa
ReplyDeleteduh washkaji na mi nilikua pale tosa mwaka huohuo 1993 nikiwa PCM3 Nakina mwakilasa,shaib uyagilo,andrew undule,robert lulandala,robert mgombela,marehem stanley mdogolo,koomkoom,petro njamas (ustazz),mpooo njamas upo wapi?mashaka ngunyale upo wapi? mzee wa ipamba,shamsi iddi wa pcb,mkujimkuji, jamani nawakumbuka sana mi nipo dar namaliza chuo DIT mwaka huu 2005.tuwasiliane jamaa mi mliniita MNYAMWEZI jackson francis,jackson_francis2000@yahoo.com,tell 0753 965501.
ReplyDeleteMan kweli apo ni kama Gutenamoo... duh... kuanzia mambo ya sifongo... j4 mambo ya manya na ugali...ukimi wewe afyaa mbayaaaa... kama kawa mama mingoii kwa kanteen aliwatoa watu sanaa kibaolojiaaa...huuu kina zuena...baba wachaaa bila kusahauu mabit ya kusoma kina Ka 50 na mzee sikaaaa....sitasahauu iyoo kamp man...nilimaliza apo 2002..PCB. KWA sasa niko finland
ReplyDeleteTeacher mlwale yuko wapi jamani, ndie alikuwa anatuphotoa miaka ya 1991 to 1992, kuna waziri mmoja kwenye serikali hii ya sasa nae alikuwa anatuphotoa miaka hiyo.
ReplyDeleteAAh Michuzi asante sana kwa blog hii, comments za wana-Tosa zimenikumbusha mbali sana, about 18 yrs ago (1991- 3)nilipokuwa pale. Vipi wazee hasa wale wa 1991 - 3 mnakumbuka mapambaano ya kung'oa utawala wa kibabe wa dudu? watu waliwakimbia polisi, walilala mt ruparama hadi asubuhi wakinyeshewa na mvua, wengine kwa mahindi karibu na half mile!! mmh it was a big war, sisi tulikuwa summit wala polisi wasituone tukidhani wajanja, vumbi la kule siri yetu.
ReplyDeleteThank to roman catholics kwa kujenga Tosa na kuweka summit.
Jamani natoa wito kwa wanatosa wote (hata tukianzia wale ninaowafahamu 1991-3) kupitia blog hii, nafikiria baadae tuanzishe TOSA ALUMNI TRUST FUND kwa ajili ya kusaidia orphans na watoto wenye shida wasome japo kwa msaada wetu, si kwa shida sana kama sisi tulivyosoma. Japo leo si kwamba tuna raha sana lakini we can at least afford to live a day wala siyo kunywa sifongo na na kula nyali za kubeep na maharage ya kuloweka.
Nakumbuka siku ya kwanza nilivyokuwa dissappointed kufika Dinning hall kuchukua uji nikidhani una sukari, ooh salale ilikuwa balaa, maana chumabani kwetu ni mtu mmoja tu alikuwa anaweza kuja na sukari toka kyela/Tukuyu mmmh omba uone atakavyokulima. Mungu bariki wanatosa hawakuwa wezi tungemaliza mahindi ya wanakijiji na kuacha shule.
Mnawamkumbuka hawa jamaani, Furaha, Elias nyunja, Bigger kipemba, kandonga, kantalamba, ooh no it all about Tosa boys where are they?
Back to the TRUST FUND, I am ready to organize this with your support. Najua wanaTosa kwa umoja wetu we can make a change and set an example in this country. For sure the trust fund will at the near end grow into a very successful financial organization in view of starting to lend loans to members at low interest rates.
mbukwa@yahoo.com
duh,safi, wapi wengine pcm3? mnyamwezi pcm3 1993
ReplyDeletejamani huyo mdau alietoa wazo la wanatosa waliomaliza kuanzia miaka ya 1991 up 2 now ange organise ki2 kupitia hii blog mbona yuko kimya fanya hivyo basi
ReplyDeletemichuzi umenikumbusha mbali sana miaka hiyo tosa ilikuwa tosa boy kweli sio leo kama vipi hii picha iweke tena maana inaonekana ya kitambo ili uendeleee kutuunganisha wadau tukumbuke wapi tumetoka na ni namna gani tutaanzisha TOSA ALUMNI
ReplyDelete