Kaka Michuzi ,
mimi nipo hapa Ulaya(majuu) gudmorgani kwa kazi za sanaa.
Nipo nasafisha macho. nataka kuwatia moyo wakulima wa matunda kama machungwa,mapapai,machenza na mananasi,akina Mgosi kule Kunanii waongeze bidii maana ni dili huku majuu.
Pia nimekuta tangawizi,mihogo na viazi vitamu.Pia maboga yapo ila yaliipiga chenga kamera yangu.
Kwa bei hizi kama ni Tz ingekuwa ni neema kwa wakulima,nadhani wengi wetu tungerudi vijijini na kujikita kwenye kilimo kuliko kubanana ndani ya bongo.

2kg machenza=2.50Euros(Tsh.4,500)

1/2kg Epo=1.99Euros(Tsh.3,582)

Kumbe ulaya hata viazi vitamu vipo?1/2kilo=1.50Euros(Tsh.2,700)

Tangawizi kwa sana tu1Kg=3.50Euros(Tsh.6,300)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Asante sana mdau kwa snep nzuri kutoka huko majuu, ni chalenji kwa kweli kwa Tanzania. Muozo wa matunda kipindi cha msimu ukomeshwe kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji au njia yeyote ya kuyahifadhi Matunda.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli wenzetu wanajitahidi na utunzaji wa matunda. Ingawa mengine inawezekana kuwa yanakuwa imported ndio maana bei yake inakuwa kubwa.

    ReplyDelete
  3. Nilifanya research kidogo ya kuyaleta haya matunda uk kwani niliona ni dili. LAkini vikwazo ni vingi kwa upande wa kwetu Tz, k.m
    1.Ubora wa maandalizi wa matunda, huku U.k. kuna sheria za matumizi ya pesticide na fertiliser. Kuna madawa yamepigwa marufuku,
    2.Issue nyingine ni wastani wa ubora. Ukitaka kuleta matunda, ni lazima yatokee kutoka kwa mkulima au shamba moja kwani ukichanganya mzigo, tatizo likitokea hutajua nani wa kumlaumu. Tatizo kama wadudu, ukosefu wa wastani wa hilo zao, lingine litakua dogo lingine kubwa,

    3. Huku U.K watu wapo concious na mambo ya 'food miles'. Wanaaamini kama chakula kimeletwa na ndege kina haribu mazingira kwani ndege zinaleta pollution kwa kama yametoka kwetu sio dili kama wakenya sasa hivi wanasota ku campaign kuokoa soko lao uk. around $ 400 million kwa mwaka

    4. Tamaa ya wauza matunda tz, wanataka faida kubwa na mzigo wa kwanza!! Bei mnakosa kuelewana vizuri, pia mahitaji ya packaging wauzaji wanaona unawasumbua.

    5 Baada ya kuagiza mzigo wa kwanza, ni vigumu kupata tena mzigo mwingine wa kuagiza kuja Uk kwani unakuta labda msimu sio, mkulima hajafanya mpangilio wa kuzalisha hayo matunda kwa mwaka mzima...

    yaaaani mambo kibao na serikali ingeweza kutatua hizi issue kama itashirikiana na wakulima,

    Ningependa sana kupata muuzaji mzuri niagize tz nimsaidie kupata soko huku. matunda , karanga , etc. michuu nitakutumia email yangu.
    yankee u.k

    ReplyDelete
  4. kwa uk matunda mengi na mboga mboga ni vitu vinavyoingizwa kila siku toka nje kwa mfano ndizi,nanasi,water melon zinatoka costa rica.spinach toka spain,maharage mabichi toka kenya na dhabibu toka south africa na apple toka marekani na spain pia kwa bei za huko ujerumani ni double ya hapa uk so ni swala la kuweza kupack na kuexport tu ila wabongo hatuwazi hilo wala serikali.Kama siku hizi uk kuna population kubwa ya waafrika so vitu kama mihogo na maboga na kila chakula alisi cha mwafrika kinatakiwa ila kazi kweli kwetu sisi wa tz

    ReplyDelete
  5. mfano mwingine milungi kwa uk ni halali na sio kosa kuuza wala kutumia sasa watu wanaohuza ni sub dealer na super dealer nasikia ndio mmiliki wa mashamba makubwa ya milungi huko kenya na kila siku kuna ndege ya mizigo na cargo yake,ni swala la kuweza kupata market na kuleta huku tu

    ReplyDelete
  6. Asante mdau, angalau wadau fulani watapata picha tofauti, maana wenginewanadhani nje matunda ni ya makopo tu .

    ReplyDelete
  7. JAMAA UNASHANGAA VIAZI VITAMU MAJUU AKATI KUNA MPAKA KISAMVU KWA MZEE BUSH SIJUI KWA MALKIA HUKO LAKINI SIWEZI KUSHANGAA KAMA VIPO.

    ReplyDelete
  8. Jamani hii kali. Mdau uliyeweka picha hii umenikumbusha mbali saaana. Nilipokuja Nchi za Ulaya na Marekani miaka michache iliyopita, nilikuwa kila nikienda kununua kitu nalinganisha na TSHs, basi kila kitu naona ghali tu. Nikawa siwezi kununua kitu, hahahahah!
    Baadae nikapata elimu kidogo

    ReplyDelete
  9. poa bro lakini next time usitie bei za vyakula kuna hatari ya wauzaji wa bongo kuzidisha bei

    ReplyDelete
  10. nililetaga mananasi. Mtaji ukakata. Kisa nilipofika heathrow wakaniambia yako contaminated na mavi.!

    ReplyDelete
  11. Na nyie mlioko ulaya sasa mnakuwa malimbukeni,kwani bei ikiwa juu ni ajabu?kuna kutransport na kuifadhi viziharibike kuosha kupaki..sasa wewe unalinganisha na mahali mwaka mzima summer?tanzania tunalima wenyewe na hali ya hewa ni tambarare sasa kwa nini bei ziwe kama UK?ACHA USHAMBA BWANA...MDAU KYEKUE

    ReplyDelete
  12. Mmh watu lazima mkomae na comments. Yeye hakumaanisha kulinganisha bei ila kama nimemuelewa vema anamaanisha tuone wenzetu wanavyoweza kufaidika kwa kuwa na biashara ya mboga mboga na matunda.
    lazima tukubali na kuona umuhimu wa wafanyabiashara ndogo ndogo kama hizi za matunda na mboga mboga. Tanzania tuna rasilimali sana ikiwemo ardhi yenye rutuba lakini ndio hakuna cha kuendelea wala nini.
    Wahusika lazima wafikie mahala wajue ni jinsi gani wanaweza kuwanyanyua hawa wakulima na wafanya biashara hixo za matunda na menginey.
    Ahsante sana wee endelea kuturushia hata sie tuliopo hukutuweze kujua kiendeleacha kwenye nchi nyingine.
    Mdau Marie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...