Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
We should all direct our efforts to the best of our capability in a positive ways.
ReplyDeleteYes, we are all facing economic hardship in our society, and sometimes most of our energy and effort are quelled by the government inefficiency. But the best of advice at this hard time, is to stay focus and thinking hard, finding alternative ways of making life worth living.
Food shortage is looming on our door step, the prices keep increasing, daily personal expenses are sky rocketing. What should we do ? Do we want to stay depressed and given up hope ? The answer to that is a BIG sounding NO!.
Should we resort on petty arguments/conflicts, and bring everyone on deadlock with no clear solutions at the end of it all, the answer to that is NO.
we are the only one in charge of our own life, we need to think hard enough to think of better solutions to our problems, the politicians aren't helping anyone in large extent. we are left to rot, on your own. FIGHT WHATS BEST FOR YOU, and only YOU can do that, THINK ABOUT THAT. Think positive, we are all different on our capabilities whether a physical strength, or our in our acquired Knowledge or our own way of thinking and MIND, but it get to be your STRENGTH in you, you just need to tap into it, and use it positively.
HATE COST A LOT OF ENERGY AND TIME. Keep that in mind. It is your choice.
MOVING THE DISCUSSION FOWARD, SO WHAT SHOULD WE DO ??
By Mchangiaji
Hapo Kipanya umechemka, kwa kweli swala la huyu binti aliyekatwa kichwa halihusiani kabisa na umaskini.
ReplyDeleteHata kama tunajua kuna uhuru wa msanii kutoa mawazo yake, ila kuna mipaka.
Istoshe wasanii ni lazima kuzingania pia watu walioathirika zaidi watajisikiaje eg wazazi wa mtot.
Kipanya I fully agree with you. Ni umaskini tuu na frustrations za maisha ndo zinawafanya watu wafanye mambo ambayo hayaelezeki...Hakuna Uchawi wala nini....
ReplyDeleteBig up KP...you are just on the point!
Hakuna uwiano kati ya umasikini na ushirikina tz.
ReplyDeleteAcha kutetea ushirikina we panya buku. Ushirikina ni ushirikina na Umasikini ni umasikini tu. Kuna masikini wangapi hawafanyi mambo yaajabu ajabu vipi wao bongo zao hazijapata moto? na kuna matajiri wangapi wanafanya hayo mambo hapo vipi sasa? Leo umechemsha vibaya sana! naona na wewe ubongo unaanza kupata moto!
ReplyDeleteWe kipanya acha kuandika upuuzi!!! huyo dogo mchawi. hakuna cha umasikini wala nini.
ReplyDeleteNyinyi hapo juu jiulizeni kwanza kwani ni nin kinacho futwa huko katika uchawi? jibu ninjaa ndugu zangu ndio zinazowapelkea huko na hiyo hata baado ndio kasi na ari mpya hiyo
ReplyDeletemganganga maanayake ni kuganga nini kama sio njaa?
UPOTOSHAJI UNAWAZA SSA UKAWEKWA MAMA MOJAWAPO WA SIFA ZA VYOMBO VYA HABARI
ReplyDeleteSalaam kwa wote. Well, ni jambo la kawaida sana kwa binadamu kukosea. Na mara nyingi mtu wa kawaida ambaye hana hata chembe ya kuathiri mtazamo wa umma (public opinion)akiongea hata pumba kiasi gani huwa si hoja. Lakini leo ndugu yetu Kipanya umewasilisha pumba (samahani kwa hili neno). Fani yako ni kuwasilisha mambo yanayotokea ktk jamii ktk namna ambayo inafurahisha lakini inayorekebisha pia. Lakini ulichokosea hapa kidoogo ni kwamba UMEJIVIKA UTAALAMU ambao kwa bahati mbaya huna na huwezi kuupata hata uwe popular kivipi. UMEPOTOSHA NDUGU YANGU. Umasikini hata siku moja HAUWEZI KUELEZEA CHANZO CHA MTOTO YULE KUFANYA ALICHOKIFANYA. Kwa kusema hivi nina maana hata hoja ya UCHAWI ni hoja tu za watu ambao hawana utaalamu (laymen)ktk kujua kwa nini watu wanafanya kile wanachofanya. Sipendi kuongelea uchawi, siyo kwamba siamini kuwa upo ila tu NI VIGUMU KUUTOLEA USHAHIDI kimazingira na hata kisayansi. Kwa hiyo uchawi siyo hoja kwa sababu hiyo tu; hatuwezi kuprove.
ReplyDeleteKitendo alichokifanya mtoto yule kwa sasa kinaweza tu kuelezwa kwa KISAKAYATRIA (psychiatrically) na KISAIKOLOJIA (psychologically) tu.
Kuna mabadiliko mengi yanaweza kumpata mtu katika mfumo wake wa ubongo yanayohusiana na mzunguko wa kemikali ktk ubongo wake ambayo inaweza kumfanya mtu kufanya jambo la ajabu kama lile, halafu anakuwa hana utambuzi wa kuwa anachokifanya ni kibaya kama sisi tulio wazima tunavyoona. Kuna magonjwa mengi, kama 'temporal lobe epilepsy'-samahani wadau..mambo ya fani tu...ambayo yanaweza kumfanya mtu kufanya mambo kama ambayo mtoto yule alifanya. Hata kusema kuwa wapo wengi, wanapanga kuua watu darajani Manzese, zote hizo zinaitwa visual(a-kuona) na audio (a-kusikia) hallucinations. Yote haya yanasababishwa tu na kutibuka kwa uratibu wa mfumo wa chemikali ktk ubongo tu. Nenda Mirembe ukasikie watu walivyofanya mambo ya kinyama mno, lkn kumbe tatizo ni kichwani tu. Sio lengo langu kuwapa somo, ila hoja yangu ya msingi ni kwamba, ktk hili hebu siye tusubiri wataalamu wa afya na mahakama wafanye kazi yao. Mtoto yule atafikishwa mahakamani na atasomewa shitaka na atapelekwa Mirembe Dodoma kwa uchunguzi na najua kule watagundua ana matatizo tu ktk ubongo wake. Kwa hiyo bwana Kipanya leo umechemsha mno kwani unachokisema ni kwamba UMASIKINI UKIONDOLEWA BASI MAMBO KAMA HAYA HAYATATOKEA. Sii kweli. Magonjwa kama haya ya akili yapo sana huku nchi zilizoendelea na matukio ya kuteka watoto na kuwachinja, au kuua tu bila sababu si kitu cha kushitusha. Ila tu wenzetu wanatambua mapema (diagnosis) na hivyo kuwaweka watu wanaoweza kuwa wauaji katika vituo maalumu (institutions).
Naomba uendelee kutuchorea COMICS na haya mambo ya kitaalamu waachie wenyewe. Kwa katuni yako umedraw conclusion ktk namna ambayo haijaenda shule kwa kweli. Anyways, sikulaumu, you are just a cartoonist and a media lay person. Kwa taarifa yako umewatukana wazazi wa mtoto yule kwamba ni masikini mno kiasi mtoto wao alifikia kufanya vile. Mtoto wa miaka 12 anajua hata maana ya kutafuta hela hadi akafikia hatua ya ubongo wake kutoka jasho. UWE UNAFIKIRIA KIPANYA, SIKU ZOTE KUMBUKA NAFASI YAKO KTK JAMII HALAFU CHAMBUA HIVI HIKI KINA UZITO AU NI PUMBA. (naanza kuudhika sasa, ngoja niachie hapahapa)
Mdau
Japan
Hata Kama ni Umasikini lakini Hau-justify Mtu aue, tena anatoa uhai wa an innocent little Girl !! It's pathetic !! Na kutokana na habari zinazoandikwa juu ya huyu kijana, yeye binafsi haonyeshi kujuta kufanya kosa kama hilo na hii hainipi picha nzuri. He and his fellow perpetrators, if any are found, should face Justice
ReplyDeleteHivi weee kibuku !! kama maskini wote wa Tanzania wangeamua kuua ...tena worse enough watoto wadogo...Watanzania !? Hili Taifa lingekuwepo Kweli ??!! Acha Hizo !!
ReplyDeleteasante sana leo nafurahi kusikia mmeona kwa macho yenu kuwa kipanya ni mpuuzi, tukiandika comments kuonyesha upuuzi wake haziwekwi at least leo mmekuwa wawaz. Kama sio mpuuzi amechora akiwa amelewa yaani ni Mlevi
ReplyDeleteKP kama umechora hii kwa sababu ya wale makinda wa miaka 18 umechemsha. Umri wa miaka 18 siyo umri wa mtu ubongo wake tayari upate moto kwa sababu hao vijana bado ni 'kula kulala'.
ReplyDeleteKula nyama na kunywa damu ya mtu siyo kawaida ya binaadamu. Lazima kuna nguvu zingine zinazoendesha zoezi hili ndani ya hao watu. Ni rahisi mtu kuwa chizi na kuvua nguo na kutembea uchi kuliko kunywa damu ya mtu.
Soma hii: KUUKATAA UONGO KUNAUFANYA UONGO UWE UONGO lakini KUUKATAA UKWELI HAKUUFANYI UKWELI UWE UONGO!
Umasikini upo na uchawi upo vile vile.....
Wee Kipanya na wewe acha kutuletea hizo hapa, wewe ukae ukijua kipaji chako ni kuchora tuu picha na ongeaa thru hizo picha zako watu tutatafsiri wenyewe jinsi tunavyotaka. Sasa ukianza kuandika mawazo yako kwa upana na urefu kama hivi unachemsha kaka yangu. wewe kuongea na comment sio fani yako waachie wenyewe waosha vinywa a.k.a wanasiasa. Hapa Ume boili kinoma !!
ReplyDeleteMimi leo nimefurahi kaka Michuzi hajabania comment za watu ili kumsitiri swahiba wake Kipanya kwa huu mchemsho aliofanya, mana kaka Mithupu ana hizo sana za kuwasitiri maswahiba zake aliona wanashambuliwa. Anyway nisiseme sana asije akabania hii comment yangu bure !! Wewe bwana KiMouse mimi nakuomba tuu kitu kimoja , mzunge huwa ana usemi "Don't quit your day job", kwa hiyo bwana sisi tunajua wewe fani yako ni kuchora vikatuni so stick to that hii habari unaleta ya kuandika mawazo yako pumba ndani ya vikatuni Mzee Umechemsha !! kama ideas za uchoraji hafifu then pumzika kwanza!!Chonde chonde Kipanya Siku nyingine usirudie tena ufisadi kama huu!!
ReplyDeleteKP kachemsha kutokana na uwelewa wake mdogo juu ya maswala ya kitaalam lkn mimi namlaumu mhariri, hii cartoon ipo kwenye gazeti la mwananchi. Mhariri alitakiwa aignore baada ya kugundua haileti maana kwa wasomaji...ushauri wa bure kuna watu wakiwa macelebs huwa wanjifanya wanajua kila kitu kumbe mdebwedo tu na matokeo ndo kama haya ya KP kuwakilisha pumba kwa wadau.
ReplyDeleteKP umechemsha sana... hebu jiweke ktk nafasi ya wazazi wa salome...na uone katooni kama hiyo pamoja na comments zake potofu!!
ReplyDeleteUngejisikiaje? I hope wewe ni mzazi na unajuwa uchungu wa mwana.
sehemu kubwa ya watanzania niya wahali ya kawaida. Wengine hutumia jina la walala hoi. Je kila mmoja angeshiriki ushirikina ili apate utajiri tungemalizana wenyewe kwa wenyewe. Hivyo hakuna correlation kati ya umaskini na utajiri. KP umeboa sana leo. RIP Salome
ReplyDeleteUuaji wa makusudi wa binadamu mwenzio hauwezi kufananishwa au kupelekea kwamba unasababishwa na umaskini hapa kipanya umechemsha lakini kwa kuwa ni mawazo yako binafsi tunakusamehe. Tusifanye makosa au kuwatetea wanaofanya makosa kama wamachinga wanaovua nguo hadharani kwa kisingizio cha Umaskini
ReplyDeleteBado nashswishikakusema kuna watu wanajiona wana akili sana, na wanaufahamu kiasi kuwa comment zao ni final, kutoa kugha za kejeli matusi, kulaumu, wala hamna HOJA, SIJAONA HOJA HAPO JUU NA HII NI AIBU JAMANI, catroonist ameleta hoja na kueleza mtazamo wake, huku akina nyie msiojua kuchora hata ua mnasubiri comment basi mnapinga bila kujua hali halisi.
ReplyDeleteUMASKINI WA KIPANYA HAJAUELEZEA NI UPI!! NA HAPA NINAONA HATARI ya watu wengi kufedheheshwa,KWA NINI UCHAWI HUPO, CHANZO NI UMASKINI, SIO WA HELA MPAKA WA MAWAZO WEGNI WENU HUMU HAMJAWAHI KUFANYA UCHAWI KWANI HAMUAMINI, WALA WENGINE HAMJASHIRIKI, KWA SABABU UBONGO WENU UKO KATIKA MAWAZO ANGAVU YA UPEO WA KISOMI, KUNA HABARI MATAJIRI WENGI WAMEPATA UTAJIRI KWA KICHAWI, NENDA JANGWANI UONE VIBANDA VYA WAGANGA VILIVYOSHENENI.
JAMANI UMASKINI WA MAWAZO NI UJINGA, LA KAMA HATUKUBALI PIA UMASKINI WA KUTOKUWA NA HELA UNAIGUBIKA JAMII ISIYOELIMIKA YENYE VIONGOZI WANAOWAPUMBAZA, ANGALIENI MAALBINO NA WAZEE WANAVYOUAWA KANDA YA ZIWA NA KWINGINEKO, JAMII HII YA KICHAWI INAISHI KARNE YA 16! maskini hawa wangeelimika punde hata wakawa na uwezo tu wa kufikiri kidogo wangeudharau uchawi.
Na hii inathibitishwa na nchi zilizoendelea hata maada za uchawi hazizungumzwi, la kama wachawi wapo, for thei benefit sio kutafuta nyama na miili ya watu ya kula.
ningependa mtu aote hoja ya kutofautisha umaskini na uchawi, HAKUNA RAIS ALIYEPATA UMAARUFI DUNIANI KWA KUJENGA HOJA KUWA CHANZO CHA UKIMWI NI UMASKNI NA SIO VIRUSI!!!!sembuse kipanya jamani tuone hoja, ukiwa hauna huwezo wa kutoa hoja basi umefilisika kimawazo
mdau
Canada.
Unajua huyu miki maus ana upeo mfupi sana na anazidi kuwa kipanya kutokana na kupata mshiko wa duka ndiyo maana anaona issue ya huyu dogo ni umasikini.
ReplyDeleteyou must grow up bro!
Kaka michuzi kwanza napenda kukupongeza kwa kazi nzuri inayo ifanya kutu update na ishu zinaendelea nyumbani kwa sisi tulio mbali ... huku ndio watu wanabadilishana mawazo na wanatoa wanayo wasumbua moyoni ...asante ..
ReplyDeleteKitu nilichokua nakuomba ukifanye ni kuleta mjadala iliwatu wachangie hoja zao ni kuandika maswali machache kwa watu wanaopenda kuendeleza nchi yetu instead ya malalamiko nikipi wata takakuchangia kuendeleza nchi yetu . Tuanzisheni jumuia ambayo itakuwa inasaidia mambo madogo kama watu wakitaka kuadopt kituo cha watoto yatime na kuchangia chakula au vifaa maana na jua pesa zinaleta ishu kubwa sana ...maana kila siku tunatoa mavitu negative tu action speak louder than words
Asante
kweli mdau wa Cnda swala ni hoja kwa nini umaskini tuutofautishe na uchawi, KWELI MBEKI ALILETA KIHOJA CHA MWAKA PALE ALIPOSEMA UKIMWI UNALETWA NA UMASKINI, NA SIO VIRUSI AKAITETEA HOJA YAKE MPAKA LEO.SIONI TATIZO KIPANYA KUTOA HOJA KAMA HIYO, ILA KWA SABABU YA UFUPI WA UJUMBE WA KATUNI HATUNA MUDA WA KUMSIKILIZA YEYE, WALE WANAOMPINGA TOENI HOJA, KUNA MTU ANASEMA YEYE ANAJUA KIPANYA ANA MATATIZO SIKU ZOTE, HUKU AKIONA KATUNI ZAKE ANATOA MAWAZO!!!! KWA NINI MSIRUKE JAMANI, KUNA HABARI NYINGI ZA KUTOA MAWAZO HUMU!!!!!
ReplyDeleteTOENI HOJA, UCHAWI NI UMASKINI -KWISHA , ILA UMASKINI SIO UCHAWI!!!!
Nakubaliana 100% na wengi wanaposema kuwa Kipanya kachemsha. Hii inatokana na hisia za watu juu ya familia ya wahusika katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Au tuseme katuni hii sio wakati wake muafaka lakini bado inaelimisha jamii juu ya imani potufu za usakaji wa utajiri kwa njia za kishirikina.
ReplyDeleteNakubaliana vilevile na Kipanya 100%. Uchawi kwa Tanzania ni umaskini. Angalia wakati wa chaguzi zetu viongozi wetu wanavyotembelea waganga wa kienyeji.
Ona jinsi gani vikongwe, watu wenye vipara, maalbino na hata watoto wachanga wanavyokuwa hatarini kutokana na imani za kishirikina kuwa utajiri unaweza patikana kwa kuwadhuru watu wa jamii hii.
Mwisho, RIP Salome and the almighty give strength to the family to move on on this hard times
Hey Mr. Teacher KP... toka huko, umeingia ladies!
ReplyDeleteSeve
Jamani,
ReplyDeleteHuyo Mkanada katoa hoja ya nguvu sana. Mpaka huyo Daktari na sakatriki yake haoni ndani. Amedadafua kwa usahihi kabisa. Tatizo letu siku zote tunasubiri kuona udhaifu tu ili tukandie. Mimi siku moja nilisema, kuna watu humu huwa hawazielewi hizi katuni, na hawawezi kuchambua maudhui yake. I wish kama kipanya (Nimevunjika mbavu na kusikitika wengine wanamuita kimouse, kipuku, kibuku,n.k.)angepata nafasi ya kueleza mawazo yake tungemwelewa. Wengine wamejifanya wasomi na kumuona kipanya ana elimu ndogo, nyieeeeeeeeee!
Kuna wengine hata taaluma zenu mkipewa nafasi ya kuzitete kivitendo hamuoni ndani kwa kipanya. Tumheshimu tu kipanya na mawazo yake.
bwana mheshimiwa misupu,samahani kwakuwa napitia njia ya panya, lakini wazolangu ni kutaka kujadili ni kwa jinsigani jamii ya wasomi inavyoweza kutumiwa kuisaidia jamii katika baadhi ya mambo haya:-
ReplyDelete1.kuwapa elimu kwa lugha na kwa ufupi na wepesi wa kueleweka watu hasa wa haliya chini sana,ikijumuisha maeneo ya vijijini,uswahilini,n.k kuhusu kuwa na mtizamo chanya wa maisha ktk nyanja za afya,uchumi,siasa,n.k
2.kuwaweka wasomi wetu hasa wa vyuovikuu [wahadhiri wakiwemo maprofesa] hasa wa fani zasayansi ya vitendo katika vipindi kama kiti moto ili waeleze kila mwezi ili waeleze nikwajinsi gani wanavyotumia uwezo wao wa kitaaluma kuleta maendeleo ktk jamii na vikwazowanavyokumbana navyo kutotimiza malengo yao, ili kama serikali inahusika ktk ukwamishaji nayo iwekwe kitimoto iseme ina mkakati gani wa kuwawezesha watimize malengo yao.
hili nalisema bwana michuzi kwasababu nafahamu na ninaamini kwamba binadamu anauwezo uliofichika ndaniyake,lakini akiwekwa ktk hali yakubanwa,kuwajibishwa iwe na watu au nature, basi hii huactivate uwezo wake na kumfanya autumie maximally na inauwa productive. mfano tu mtu wakawaida akishtuliwa na simba gafla adrenaline inatolewa na suprarenal gland na huyomtu anaweza kuruka fensi ambayo kwa kawaida hawezi kuiruka,au anweza kupandamti wenyemiiba ambao kwa kawaida hawezi kuupanda,mana nature imemuwajibisha.lakini ukimbembeleza aruke au apanda practically inakuwa haiwezekani!
tuifanye jamii yetu kilammoja wetu aache kuzuga atumie uwezo wakewote tutajikwamua.angalia wachina,wakorea,wajapani n.k nimataifa ambayo watuwake wanadiscipline ya kujituma kwa kadiri ya uwezo wao unapoishia.
NACHO SISITIZA HAPA NI HIVI BILA KUWA NA TEKNOLOJIA KTK NYANJA MBALIMBALI TUNAYO IZALISHA WENYEWE BASI TUMEKWISHA ILA TUNASOGEZA TU SIKU! bob marley aliimba "my feet is my only carriage so i've got to push on through,but while i'm gone EVERYTHING GONNA BE ALRIGHT!"
nasisi our technology is our only carriage so we have got to push on through,but while we're gone everything is gonna be alright!
naomba usiibanie hii mkuu ikiwezekana itoe front page tuijadili!chonde mkuu nikochini ya miguu ya..
MDAU-ughaibuni.
Watu bwana , wanapenda kubonya bonya keybodi, ili mradi waandike, UCHAWI NI NINI?? na umaskini ni nini?? wachawi wote ni maskini, maskini wote sio wachawi, kama mnataka nifafanue nifate sumbawanga
ReplyDeleteubishi tu utafikiri paka wa kichawi!
KAKA MICHUDHI, MIE SIONI KOSA LOLOTE AMBALO KP KAFANYA HAPO, YEYE KALETA KAZI YAKE NA WADAU WAIONE, KAMA HAWAJARIDHIKA WALETE MICHORO YAO KUELEZEA HICHO ALICHOSEMA KP, YEYE NA KAZI YAKE KAMALIZA...NAHISI WENGI WETU TUNA UWEZO MDOGO WA KUSOMA KAZI ZA SANAA NA HASA KUTOKA KATIKA UCHORAJI
ReplyDeleteBIG UP KP, TULETEE MWANANGU...TENE ZILE ZILE
NYANINGEDERE
KATIKA HILI KIPANYA UMEPOTOKA
ReplyDeleteSijui tuseme kwamba ni shule au ni busara haijatumika au la.
Kuna suala la upeo wa mtazamo, katika katuni hii kipanya kweli umepotoka na napata wasi wasi kama ni shule haiko ya kutosha au ni busara tu imepita kushoto.
Unaweza kuwa na elimu ndogo ukawa na busara na unaweza ukawa na elimu kubwa na usiwe na busara.
Na unaweza kutokuwa na elimu ya kutosha na busara pia usiwe nayo.
Hata kama tunapiga vita umaskini mtazamo huu wa kipanya ni budi ukemewe mara moja. Hakuna uhusiano wa aina yoyote ile kati ya uchawi na umaskini.
MGEMA AKISIFIWA TEMBO HUTIA MAJI
NA WEREVU MWINGI MBELE GIZA
Naona nisiende mbele zaidi maana ntaonekana namchagiza kipanya.
Mwaushe Ohiwa,
Mdau wa Sweden
Nikweli nakubaliana na wewe anonny wa 2:02AM kwa jina la mdau wa ugaibuni. kwani umaskini wetu hauwezi kufukuzwa[kumalizwa]kwa njia ya misaada.
ReplyDeletemaana chakuomba hakisitiri matakwa!! namaanisha kuwa tufikie mahali bajeti yetu tujitosheleze wenyewe!sio kilamwaka lazima tujitahidi kuwapendeza mabwana wakubwa ilimradi tu waweke mkono wao wa baraka kwenye bajeti yetu,na wasipoweka basi balaa limeingia!
nikweli wachina,wakorea,wajapani na hata wahindi sikuhizi wanakujajuu sana na technolojia yao na hii inawapa nguvu ya kiuchumi.
lazima wasomi wetu waonyeshe kwa vitendo maana ya elimu yao,isiwe tu kufundisha basi,kisha waliofundishwa nao wanakwambia vifaa hatuna bwana,sasa wewe si msomi wa fanihiyo ya kuvitengeneza unasubiri nani aje akutengenezee?au tutanunua hadi lini?
kununuwa kweli siodawa ya kutusaidia,nisawa na mtu anayetumia siku30 kwendakazini kisha analipwa 60,000/= anaitumia kwa mwezi unaofuata inakwisha kwa basic needs.
wakati mtu mwingine anaefuga kwa kitaalam ng'ombe,mbuzi,kuku, analima mbogamboga na matunda, atajikuta hahitaji mahitaji yake mengi toka dukani,hivyo atakuwa bora kuliko hata mfanyakazi huyo nilomsema hapo juu.
tungekuwa na vifaa vyetu wenyewe hata wagonjwa wasingekuwa wanapanga foleni kusubiri vipimo maana vifaa havitoshi,na vilivyopo vingi sio electronised,ni mechanical. pia hata wanapelekwa india na kweingineko huwa ni vifaa tu havipohuku kwetu. sasa watalaamu wetu wange kuwa wana fanyakazi kama timu iliyokuwa coordinated nadhani tungepiga hatua.
kwa mfano tuseme dactari atahitaji majibu ya vipimo haraka ili amtibu mgonjwa na kunusuru maisha yake,mtu wa maabara iliatoe majibu haraka atahitaji kifaa kinachoweza kupima sample za wangonjwa wengi kwa muda mfupi,tuchukulie mfano malaria, badala ya kuchungulia kwenye darubini, angeweza ku detect specific antigen ya mdudu wa malaria kwa kutumia kifaa kinachotumia miale yenye wavelength fulani,hapa mtu wa ELECTRONICS nahitajika akitengeneze, na labda kuweza kupata usahihizaidi wa kuipata hiyo antigen inaweza kuhitajika kemikali fulani ambayo ita combine na antigen ili iweprecipitated[kutua chini] hapa tahitajika mtalaam wa kutengeneza kemikali.
kwa ufupi timu hiyo ikicheza vizuri tutajikuta hakuna tena msongamano wa wagonjwa,vifo visivyo vya lazima kwa kuchelewa matibabu,nk
sasa kama hilo ni moja tu je vipi na mengine kama vile usalama,kilimo,ufugaji,n.k tutajikuta tunapiga hatua kwa kasi na tunacho zalisha hatukitumii kuagiza badala yake tunakuwa na surplus na huu ndio utajiri maana uko self sufficient.sio kuwa na pesa lakini kilakitu lazima ununue,pesa ikiisha you are done!!
nimtizamo tu nawakilisha!