wadau, hususan wapenzi wa liverpool fc a.ka bwawa la maini. kama nilivyoahidi jana tayari tumeshapata anuani ya barua pepe kurahisisha mawasiliano yetu katika kuanzisha na hatimaye kuendeleza tawi la klabu yetu tuipendayo.
anuani hiyo ni: bwawalamaini@gmail.com
unachotakiwa kufanya kama unataka kuwa memba wa bwawa la maini a.k.a BongoReds kama ambavyo tawi la liverpool la hapa nyumbani litavyojulikana, tuma maelezo yako kwenye anuani hiyo ili uweze kusajiliwa kama mwanachama wa tawi hilo.
idadi maridhawa itapotimia utaitishwa mkutano mkuu ambao utaanza na uchaguzi na kupitisha rasimu ya katiba pamoja na jina rasmi tutaloamua tujiite katika kuendeleza libeneke la bwawani.
hivyo basi
1. tuma jina lako kamili
2. shughuli uifanyayo
3. Jinsia yako na umri wako
4. anuani yako ya kawaida
5. anuani yako ya email
uanachama uko wazi kwa mdau yeyote anayeipenda liverpool

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2008

    Kenge....kuwa mwanachama wa bwala la maini unatakiwa kuwa na roho ya chuma...club linafungwa kila wakati.....kenge sanaaaa..... afadhari kuwa mwanachama wa manyema

    ReplyDelete
  2. michuzi sijafurahishwa na ushabiki wako wa "sisiem wafungua tawi jipya..." na "wale wapenzi wa bwawa la maini"
    je sisi washika bunduki, watandaza kandanda safi duniani, hasa pale landani na wapenzi wa "part of democracy and development"(chadema) tumkimbilie nani???
    Mike Massawe
    BANANA INVESTMENTS LTD-ARUSHA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2008

    BROTHER MICHUZI acha hizo,naona unajibu kuonyesha ni jinsi gani ulivyo mmbinafsi,watu wa Sinza D madukani wamefanya party ya nguvu kusheherekea ubingwa wa ligi kuu na champions league lakini hukuweza kutoa picha hata moja na badala yake unashabikia mambo ya liverpool kwa vile wewe unaipenda, sasa basi kama ni hivyo badilisha au waelekeze watu kuwa blog hii inatumika kwa wapenzi wa liverpool peke yao manake mimi ni mdau lakini sijawahi kuona habari za timu nyingine sana.

    si vizuri kuwa katikati uwe mkweli toa ile habari na zile picha mwenye kuzitoa nishai atoe mwenye kutukana atukane poa tu ila zirushe hewani kaka usiwe mbanifu wa habari usizozipenda.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2008

    sasa mithupuu....kazi yangu ya nini eboo?au utatupa vibaruaa?mi sidhani kama kazi yangu inahitajioka kwenye kujisajili na uanachama ...........wa bwawa la maini

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2008

    Nikiwa bado naendeleza libeneke la soka la Bongo napenda kuipongeza Mtibwa Sugar Fc kwa kuwa timu ya kwanza kuanzisha website iliyokamilika. Website yenu imekaa kimataifa ningeomba wapenzi wote wa soka tujiandindikishe katika Forum yao ili kuipa sapoti timu hii inayoendeshwa ki professional kuliko hata Yanga na Simba labda wao pia wataiga mfano wa mtibwa sio kila siku majungu tu! Hongera Mtibwa Sugar !! Website imetulia!! Ingia www.mtibwasugar.com

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2008

    MICHUZI, sasa kwa nini usitumie hizi nguvu kusupport timu za nyumbani? hawa jamaa wa UK watakusaidia nini? watu wengine bwana!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 11, 2008

    Badala mfikirie mtaepusha vipi vipigo vya Taifa stars na world cup qua...mnaleta oh bwawa la maini miles miangapi mpaka Liverpool IoI kweli kazi bado ipo anywa wish ya all the best...
    Londoner.
    Ealing Broadway

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2008

    Duh! kweli waafrika wameumbwa kuwa watumwa tuu. maaana yake hata nikisema ninayotaka kuyasema haitasaidia kitu.
    Kwa ufupi bwana michuzi kutokana na kazi yako nzuri ya kuendeleza ushenzi uliofanywa na akina Karl Peters na Dr. Livingstone, umepoteza mdau mmoja leo hii.

    SIINGII TENA KWENYE BLOG YAKO.

    MDAU KILEMELA HAPA.
    22 orde hall street
    Great Ormond street
    Holborn
    London

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2008

    Sasa hilo tawi linasaidia nini soka la tanzania? Hongera mtibwa na washabiki wake.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 11, 2008

    Bwana michuzi nimefurahi sana kuona jitihada kama hizi za kuanzisha tawi la washabiki wa bwawa la maini. Ila kuna vitu ambavyo vimenisikitisha sana kwa namna moja ama nyingine, sioni sababu ya kuhusisha jinsia au shughuli aifanyayo mtu. Naelewa kwamba hivi ni vitu ambavyo huulizwa mara nyingi hasa Tanzania lakini mimi huwa nina ona kama vile vina dalili zote za ubaguzi kwani jinsia na shughuli aifanyayo mtu havihusiani kabisa na suala zima la kuwa mwanachama. Imani.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2008

    Michuzi nakupenda sana, ila hapo sasa umechemka. Acha hayo mambo ya ajabu, kama livyosema anon hapo JP, tumia hizo nguvu kufanyia mambo ya maana bwana. Vipi na ile picha ya yule mbwa umeshaitoa? Maana juzi nilikuomba ukagoma kuitoa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2008

    Sasa jamani kuna wabongo wangapi wanaichezea au waliwahi kuichezea hiyo timu kule ughaibuni?duh huo ushabiki wakudoelea hebu tuuache!!Mungu ibariki Tanzania na vipaji vyake (kama tunazo!!!)

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 11, 2008

    Naungana na wadau wote walio laani jitihada hizi za Michuzi kushabikia timu za kigeni!Timu zetu za nyumbani bado zinahitaji uzalendo wa hali ya juu ili ziweze kufanya vizuri. Kuendelea kushabikia vya wenzetu ni utumwa wa kizalendo!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 11, 2008

    Michuzi, Hongera sana kwa kuanzisha tawi la klabu uipendayo katika ligi kuu ya uingereza.Ushauri wangu ni huu:
    1,Tumia jina litakalotoa picha halisi ya aina ya uanachama wa hii klabu kubwa duniani, mfano LiverpoolTanzaniaBranch au kwa kiswahili chake, kumbuka huna haki za kisheria kutafsiri jina la Liverpool kwa Lungha yako au Lungha nyingine yeyote kama ilivyo CCM, hata ukiandika kichina, kijapani au kiyahudi utakapotaka kuandika CCM, itabidi uandike CCM tu!.
    2, Kujiita bwawa la maini ni kujiweka katika hali ya itakayowafanya watafute tafsiri ya hilo neno, kisha ukaonekana huna maana, wakati sisi tunajua wewe ni mtu wa kazi.
    3,Waaandikie wakupe Habibu za Rejea au Memorandum of understandings(MU),kati yao na wewe ili zikupe nguvu za kisheria za kufungua tawi huku ukifuata taratibu zao na maadili yao, kwa wanachama wako.
    4,Ushirikishe Ubalozi wa Tanzania kupitia Muambata wa Utamaduni pale Ubalozini, watakusaidia, Balozi Mhe Mama Maajar ana ari kubwa sana ya kusaidia maendeleo ya michezo nyumbani, ni imani yangu kwa kuushirikisha ubalozi wetu Nchini Uingereza utakuwa umefanya jambo la maana sana, ndio maana nasema wakiulizwa nini maana ya bwawa la maini watapata tabu kuwafahamisha nini maana yake.
    www.tanzaniasports.com

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 11, 2008

    MDAU KILEMELA kila binadamu ameumwa na utashi wake na nafsi zao zintofautiana kila siku mnaubiliwa upendo kuanzia kwenye dini,reggae,hiphop hadi kwenye michezo,kama kweli hupendi vya wazungu umefata nini kwao? si ungebaki kwenu kijijini ili uwalaani vizuri hao wazungu, ni utashi wako na mapenzi yako ya kupenda maendeleo na imani yako kwamba ukienda Ulaya utapata mafanikio ndivyo vilivyokupandisha ndege,kwa hiyo acha sisi tusupport Liverpool kwani hata Waingereza wenyewe wanaipenda Brazil kwa sababu ya soka yake nzuri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...