mwenyekiti wa umoja wa afrika rais jakaya kikwete akiwa meza kuu pamoja na mwenyeji wao rais Hosni Mubarak wa misri na naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa dk. asha-rose migiro asubuhi ya leo wakati wa ufunguzi wa kikao cha 11 cha umoja huo huko sharm el sheikh.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2008

    Kwanini kiti alichokalia Asha Rose ni tofauti na hivyo walivyokalia wanaume kikwete na mubaraka? Ni bahati mbaya au ndo itifaki.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2008

    It very unfortunate that when it comes to issues of such nature yaani politics, issues which touch and impact in all our overall daily lives wadau dont have keen interest to comment. Anyways ndio hali halisi ya ulimwengu wa sasa, mambo muhimu hayapewi uzito wake. Michuzi mwanamama huyu mwanasheria mahiri, makini na wa aina yake ametoa tamko kali na kuwatafadhalisha 'madume' yote ya Africa to call a spade a spade, stand up and condenm the activities of veteran Bob Mugabe. Yanayoendelea Zim si ya kufanyiwa mzaha na kuoneana haya, nchi inaelekea katika machafuko makubwa ambayo Africa na madume yake viongozi, hawataweza kujibu lawama. Ni Odinga pekee waziri mkuu wa Kenya,aliyeweza kuunga mkono tamko hili na he went a step further kusema Africa si vema ikamtambua dictator mwehu huyu.Hivi huko kapokelewa vipi jamani? Africa my beloved continent, please wake up and stand for the truth at least kwa hili lililowazi kabisa. Haiitaji akil, macho au masikio ya kisayansi kutambua kinachoendelea Zim jamani. Dr. Asha Rose you are a woman and a half, keep up the spirits. Big uuupppp dada!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2008

    Kwa maoni yangu Wamempa kiti tofauti sababu yeye ni mwanamke.Unyanyasaji wa kijinsia tu.

    Ukumbuke pia misri ni waislamu na waislamu wanaume hawapendi mwanamke akae pamoja na wanaume hadharani hivyo .Hivyo wamempa kiti cha tofauti ili aonekane tofauti kumnyanyasa kijinsia.

    Mama Asha-ROSE usijali iko siku mfumo koko dume utatokomea tu.Hata wangekupa tofali ukalie wewe bado ni bosi wao tu kwenye umoja wa mataifa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2008

    Katika mambo tunayosifiwa waafrika ni kupoteza muda. Je kweli hao walio kiti cha mbele Mubarak na Kikwete wanaweza kumfunga kamba Mugabe. Wao na vyama vyao ndio vinara wakulazimisha matokeo na kukandamiza upinzani. Hebu ona Mubat=rak livyowashughulikia Islamic Brotherhood. AU kama ilivyokuwa OAU bado wataendelea kukaa meza moja na viongozi watakaopindua nchi zao au kujinyakulia madaraka kwa nguvu kama alivyofanya Mugabe. Siku moja kabla ya uchaguzi wa Zimbabwe, Mugabe alitamba kuwa hakuna hata mmoja kati ya viongozi wa nchi za Kiafrika anayeweza kumnyoshea kidole. Ndipo nikakumbuka lile tangazo la Ukimwi yule dada alipokuwa akisema, " Unaponinyoshea mimi kidole, vidole vitatu vinaelekezwa kwako mwenyewe"
    Hata kile kinachojiita "Jumuia ya kimataifa aka The international community" wanashindwa kumbana Mugabe kutokana na ukweli maslahi binafsi ya nchi zao hutangulizwa mbele na si demokrasia. Mfano ni Musharaf, Mubarak , na Falme za ghuba ya Uarabu.
    Kuna kazi kubwa kuletea demokrasia ya kweli Afrika na hususa katika vyama vya kisiasa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2008

    hicho kikao cha AU kama hakitalaani yanayotekea Zimbabwe nitaamini viongozi wetu wa Kiafrika ni Wanafiki tu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2008

    Wadau hii inanikumbusha IDDI AMINI kwa ANGLE ya kitofauti ,lakini results ni zile zile ,na pia nikiwa "mzenji wa bara" pia inanikumbusha KARUME (baba mtu).kwa ufupi namuunga mkono wa Dhati mdau july 1 12.15 kwamba kila mtu kajichimbia ,maana anahofu VIDOLE VITATU, Wadau imagine KARUME WA SASA anamshutumu huyu MZEE si itakuwa noma ,maana WANZENJI WANAWEZA KUMSUTA!!!AU AINUKE MUBARAK, WAIJIPSHEN SI WATAMZOMEA? NA WENGINE KIBAO WANANOMA ZAO.HAO INTANESHNO KOMUNITE WAO NDIO BOM ZAIDI, MAANA BAADA YA NOMA RWANDA, HAWAJASOMA LOLOTE NDIO KWANZA WANAADHIRIKA TENA DAFUR, NA HUYO BUSH NAE USISEME ANA BALAA LAKE LA WANTANAMO BAY ANALIJUA MWENYEWE,(WAMAREKANI WANAGOMBANA WENYEWE KWA WENYEWE KUHUSU SUALA HILO)
    SASA HAPO ATAKAINUKA NA KUJITOLEA KUMFUNGA PAKA KENGELE NANI?
    WADAU TUSIWACHE KUIOMBEA AFRIKA, KUMBUKA WIMBO WETU WA TAIFA PIA UNASISITIZA
    "MUNGU IBARIKI AFRIKA"

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2008

    Picha kubwa: Viti vingine ni sawa na hicho cha Asha. Hakuna ubaguzi wa jinsia. Kiti cha Kikwete ni kwa ajili ya heshima ya Rais wa Afrika kwa kioindi hiki. Hicho cha Mubarak ni kwa ajili ya kuwa Rais wa mkutano huo!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2008

    Huyu binti mzuri kiakili na kimwili. Viva Migiro Viva

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 16, 2008

    Mbona katika picha hiyo Hosni Mubarak anaonekana kama anamnyooshea bastola Kikwete?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...