
Nina furaha na fahari kuwafahamisha maendeleo ya mchakato wa kuundwa na hatimaye kusajili rasmi tawi la BongoReds a.k.a Bwawa la Maini ambapo wapenzi wote wa klabu ya Liverpool FC popote walipo wanakaribishwa kujiunga.
Hadi sasa wadau takriban 100 wamejitokeza kujiunga na tawi hili la Liverpool hapa bongo, na wengine ni kutoka mikoani na hata nje ya nchi. Kwa niaba ya kamati ya muda inayosimamia uasijili huu natoa shukrani kwa wale wote waliotuma majina na maelezo yao kwa azma hiyo.
Hivi sasa kamati inajiandaa kutuma huko Anfield orodha ya majina hayo ambayo yatakuwa ya wanzilishi na kisha baada ya kusajiliwa zoezi la kusajili wapenzi wengine wa Liverpool litaendelea. Mwisho wa kupokea majina ya awali itakuwa ni siku ya Ijumaa saa sita kamili za mchana kwa saa za bongo.
Hii haimaanishi kwamba wataochelewa kutuma majina na maelezo yao watakuwa wamekosa nafasi. Hayo majina ya awali ni kutimiza sharti la kuwa na majina ya wanachama waanzilishi ili kuweza kupata usajili rasmi. Baada ya hapo zoezi litaendelea ili kupata wanachama wengi zaidi.
Wanakamati ya muda wamejitolea kugharamia zoezi zima la usajili ili kuharakisha mchakato huu. maelekezo ya kujiandikisha na hatimaye kupata kadi ya uanachama yatatolewa mara baada ya kupata usajili kamili toka huko Anfield.
Anuani yetu pepe ni bwawalamaini@gmail.com
Hivyo stay tuned....
YOU WILL NEVER WALK ALONE
PS: sio vibaya tukiwachunglia Liverpool wenzetu wa Dubai wanavyoendeleza libeneke kama hili tunalotaka kuanzisha kwa kubofya hapa


Nah kweli...mawazo ya kiutumwa bado hai!!!jikomboe Mtanzania,wakati bado upo!!!
ReplyDeleteIngependeza zaidi kama mngeunda kitu kama hicho kwa Yanga na Simba.
ReplyDeleteGod will bless us more if we will join the development movements. I do understand there is no future light in economical, social and political aspects in Tanzania. So, in some extent i don't blame you guys.
ReplyDeleteMdau wa US tawi # 1
TAFUTENI KAZI MFANYE
ReplyDeleteHalafu nyie ndiyo wa kwanza kuilaumu serikali kwamba maisha bora kwa kila mtanzania haiwezekani wakati mnatumia muda wenu mwingi kufanya vitu ambavyo haviboreshi maisha ya mtanzania ila vinaendeleza utumwa. Nguvu hizi ungezielekeza kwenye SACCOS kwa mfano ya kilimo si ungewaondoa wamachniga na wapiga debe wengi kwenye umasikini? hebu tumieni akili zenu vizuri ili kuleta maendeleo na siyo kuendeleza utumwa. Wakati nyinyi mnaanzisha matawi ya vilabu vya mpira, wageni wanawekeza katika vijiji mlivyotoka na si muda mrefu mtaanza kuleta fujo kwa kudai kwamba mashamba wamepewa wageni!!
ReplyDeleteDuh!! Mi nimechoka kweli kweli!! Kila siku twashangilia mafanikio ya wenzetu. Mbona Taifa cup watu hamkushabikia hivyo Jamani. Nyumbani ni nyumbani.
ReplyDeleteJikwamueni nyinyi wenyewe kutoka utmwa wa kiakilia, hakuna wa kutukomboa akili zetu, bali ni sisi wenyewe, haya maneno yalikuwa kweli. Huwezi kuamini mpaka leo Watz tunashangilia mafanikio ya wageni? Hivyo ndivyo ilivyo. Ndio maana hata ukienda maofisini na sehemu nyingine tunawababaikia wageni kwa hisia kama hizi. Hivi Mh. Michuzi si unakuwa unasafiri? Huoni jinsi wazungu na wengine wanavyojidai na vitu vyao? Tupeleke nguvu zetu kwenye maendeleo ya nchi yetu sio kuyaendeleza ya wenzetu.
ReplyDeleteJamani hee, hizi timu za watu zina historia na wenyewe wanaozipenda hata siku moja hawataki washabiki wasiokuwa na muungano wa kihistoria "historical connection" na timu zao. Na ndo maana, kama wewe unatoka New Castle na unashabikia Liverpool, washabiki wa Liverpool wenyewe hata siku moja hawatakuona kama wewe ni mmoja wao, na kuna neno maalum kwa ajili ya washabiki kama nyinyi "Glory seekers" au "Glory hunters".
ReplyDeleteBwana michuzi, wewe ni Glory seeker tuu, na ukitaka kuamini nenda kwenye pub ya washabiki wa liverpool na jezi yako ya Liverpool hapa UK. Mwanzoni watakukaribisha kwa kudhania kuwa wewe ni mwana Liverpool. Baadaye ukishazungumza na kukutambua kwa "accent" yako ya ki-matumbi,chinga, au vyovyote, basi utaona watakavyokuchukulia kutoka hapo.
Sina haja ya kusema sana lakini kwa wale wanaoishi ughaibuni wanalielewa hili.
Charity should start at home!Tungeanza na Simba na Yanga ladba tungeweza kuboresha kiwango cha soka nchini kwetu.
ReplyDeleteHuu ni utumwa.