CHAMA CHA MAPINDUZI


SHINA LA READING

MKUTANO WA TATU WA SHINA LA READING

CHAMA CHA MAPINDUZI- CCM READING

WANACHAMA WOTE –CCM READING
WAKEREKETWA WOTE-CCM READING
WAPENZI NA WANAMAPINDUZI WOTE WA READING
TAREHE; 05/07/08 SAA 6 MCHANA HADI SAA KUMI JIONI

MAHALI:
UKUMBI 79 LONDON ROAD {KIJIWENI}
READING RG 1 5BY
KADI ZIPO KWA WANACHAMA WAPYA KUMBUKA KUJA NA PICHA BEI YA KADI NI POUND TATU NA POUND KUMI NA MBILI ADA YA MWAKA MZIMA.


KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHARI WASILIANA NA;
MAIRA MIGIRE- 07799212095
KATIBU WA SHINA LA READING

WOTE MNAKARIBISHWA – KUTAKUWA NA VINYWAJI, NYAMA CHOMA NA MUZIKI BAADA YA SHUGHULI ZOTE.
KIINGILIO BURE!!!!!!!!

MUHIMU: KATIBU WA T.A (TANZANIA ASSOCIATION UK) ATAKUWEPO KWENYE KIKAO.

Akhasante.


###########################################


TANGAZO KWA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA

KUTAKUWA NA SAFARI YA KWENDA KUTEMBELEA MJI WA PORTSMOUTH MUDA SAA TATU ASUBUHI HADI SAA MOJA JIONI TAREHE 09/08/2008

MCHANGO WA NAULI NI £10 KWA KILA MTU. TAFADHALI KABIDHI FEDHA YAKO KWA WATU WAFUATAO:-

JEFFER GADO- 07796923838

BONGO FLAVOUR- 07727636009

TULI NGONYA (MAMA MARIA) - 07919874182

OSANGO APOLO- 07810356096

MWISHO WA KUPOKEA FEDHA NI TAREHE 25/07/2008 SAA KUMI NA MBILI JIONI

LENGO NI KUWEZA KUJIFUNZA NA KUONA VIVUTIO MBALI MBALI VYA MJI WA PORTSMOUTH.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA MAIRA MIGIRE SIMU NAMBA- 07799212095 AU WASILIANA NA PORTSMOUTH TOURIST INFORMATION CENTRE TEL: 02392826722.

AKHASANTE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2008

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    ReplyDelete
  2. TUDOKEZEE DONDOO ZA KIKAO HATA TUCHEKE KIDOGO

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2008

    Wadau nisaidieni, hivi shughuli za kisiasa zinaruhusiwa ugenini? maana vyama vya upinzani visijekufanya hivyo ikawa matatizo!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2008

    NAONA SASA WABONGO MMESAHAU SHIDA NA NJAAA ZA JAMAA ZENU HUKO BONGO. KWELI VIPOFU WANAONGOZANA WENYEWE SIKU HIZI. HESHIMA MNGEZIPATA KAMA HUO MCHANGO WA POUND KUMI KUMI MNGEUWASILISHA KTK KITENGO KIMOJA WAPO CHA KUSAIDIA WATOTO YATIMA KULE BONGO, ACHENI KUVAA VIATU VISIVYOWATOSHA MPO UGENINI, HATA BONGO KUNA BAHARI NA SEHEMU NZURI TU ZA KUTALII.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2008

    Kusema kweli Michuzi naamini tukiamia kwenye new blog utaacha na habari hizi za politics.

    I get so board ninapo ona hizi habari, i feel ashame sababu hakuna cha maana CCM wanachokifanya. I know huwezi kuiweka hii kwenye msg, lakini i want you to be aware of this. Utapoteza watu ambao hawana imani na siasa especial CCM.

    I hope you will eveluate your strategy, and then look at the one that will give you a competitive advantage. Remember your not entitled to this, so use your mind set evaluate one need to done at the best inorder to beat down your rivals. One of the thing is CCMlization need to STOP.

    Again huu ni ushauri wa bure.

    Mdau wa US

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2008

    watanzania wahuku ughaibuni mimi wananishangaza sana bro MICHUZI vile vitu vya kijinga na vya kipumbavu ndio wanaviona vinaumuhimu sana lakini hata siku moja sijasikia wakijadili mambo ya maendeleo ya kimaisha.ndio maana siku zote tuko chinina tutaendelea kua chini hadi mwisho wa dunia.ahsante mm MDAU

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2008

    wote hao wanaon'gan'gania chama cha mafisadi na kukipigia debe ni miwani ya mbao..toeni vibanzi vya mbao machoni mwenu..mafisadi wamepitwa na wakati,chama cha mizembe na mimbumbubu wadanganyika..mpaka ulaya mnahangaika na minguo yenye rangi ya kijani na mijano..ovyooooo..wapi mmeona nyumba imepakwa rangi ya kijani na manjano..uko uk?mabwegeeeeee...20010..inakuja..dont be surprised..tutaiga mfano wa kenya ...time is over now
    msema kweli

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2008

    WATU WENGINE BWANA SISI TUNAFAIDIKA NA CCM SASA MLITAKA TUKIUNGE MKONO CHAMA AMBACHO HATUFAIDIKI NACHO? KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2008

    Safari za makundi nani anazitaka,nikitaka kwenda mahali sinajiendea tu..sasa nitoe pound kumi za nini?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2008

    kweli usemavyo wewe unafaidika na ccm..kwa kuiba na kufisadi ndio lazima uchangamkie wizi na ujammbazi....kwani mtoto wa mwizi ni mwizi.kwa lugha nyingine unafurahikia hujuma za nchi,..poa..endeleza libeneke na utafaidika sana na ccm.majambazi nyie..

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2008

    sio mbaya kuwa katika c.c.m
    mimi nawachukia sana mafisadi lakini nampenda sana mwalimu nyerere mwanzirishi wa chama hicho

    kidumu chama cha mapinduzi!!
    zidumu fikra za mwenyekiti wa chama
    na adumu RAIS JK ninamaana KIKWETE
    kwani yeye ni jk kama nyerere yaani JK kambarage ninamatumaini atakuwa na busara kama mwalimu

    mimi sifaidiki na c.c.m ila amani na upendo nimuhimu ktk nchi si wote
    tutafaidi matunda ya nchi ila amani tu pia ni muhimu

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2008

    JAMANI MNAJUWA HAWA WALIFIKAJE HUKO UGHAIBUNI? ASILIMIA KUBWA UNAWEZA KUKUTA NI WATOTO WA WALEWALE!!!!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2008

    mdau wa USA ni vyema ungeandika kwa kiswahili maana lugha ya wenyewe huiwezi!sasa board una maana bored?
    kuhusu safari za vikundi ni nzuri tu pamoja na kufahamiana inakupa wasaa wa kujua na kujionea maana mbalimbali badala ya kubeba box kila siku.
    vilevile wadau ni vyema tuelewe CCM imebadilika na hao jamaa wa ughaibuni nao tunawaomba watuletee mawazo mapya na utendaji au uendeshaji mzuri wa nchi na chama.sitaungana na wadau wengine kutaka kujua waliendaje huko au ni watoto wa wakubwa kwani hiyo si hoja na watu hatuwezi kulingana
    nzehe

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2008

    Jamani haya mambo naona sasa yamezidi mlishaona wapi chama kikafungulia nje ya nchi maana nauliza sijaona TAWI LA DEMO au REP VYA USA nje ya nchi AU CHAMA CHOCHOTE CHA NCHI YOYOTE DINIA KILICHO FUNGULIWA BONGO sasa nashangaa kuona haya mambo ya CCM sasa yame zidi kama mmnataka nendene mkawasaidie kufanya ufisada kule kule bongo kama manaipenda sana ccm mbona mnafungilia matawi nje tu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2008

    Wewe Mdau wa US kwa kweli umenimaliza na lugha yako hata sijui hiyo ni lugha ghani sana sana kizaramo.
    I get so "board" ninapo ona hizi habari.
    Utapoteza watu ambao hawana imani na siasa "especial" CCM.
    Remember "your not" entitled to this.
    Rudi tu nyumbani CCM ikupe elimu ya bure na michuzi hapa afanyii mashindano kama unataka kuondoka wewe anza tu. Msaada kwenye tuta ni bure wewe leta tu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 02, 2008

    Safi sana Wanaccm. Tujitume halafu mtuletee huo ujuzi mlio nao huko na nchi itaongozwa vema. Wenye wifi wachinyonge sasa. CCM Oheeeeeeeeeeeeeee. Wapnzani chiniiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!
    Mimi mwanamapinduzi halisi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 02, 2008

    Aisee watu wengine bwana! Michuzi una haki kufichanri kwenye nyanja zote za kijamii mradi usivunje sheria. Wenye kupenda politics na waseme wasiopenda basi waache kusome taarifu hiyo. Pili kumbukeni kuwa CCM kama chama haki shida. Wewe unayesema ccm mbaya ndio mbaya kwani hata wewe ukipewa uongozi nafikiri utakuwa mfisadi wa kulipwa. Acheni bwana. Michuzi dumisha uhusiano wa kijamii popote duniani na ktk nyanja zote

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 02, 2008

    watu tupo ccm kwa kuvutiwa na sera zake na katika sera hizo hakuna kipengere kinachohamasisha ufisadi,sasa kama kuna wafisadi ni baadhi ya watu na sio sera ya chama hicho,kijijini kwangu asilimia tisini na tano ni wanaccm na hakuna fisadi hata mmoja wanasaidiana kwa hali na mali.jamani siku nyingine watanzania tuamke tuwe positive.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 03, 2008

    Cool Maaan!The only thang these Numskullz have ever been taught and known in their entire life is worshipping CCM the godfather!Hakuna anaye ona aibu kwa nini Tanzania haitajwi kabisa katika soko la hisa za kimataifa na hakuna anaye hangaika kuitaja thamani ya shilingi yetu katika soko la kimataifa HATA INAPOKUJA katika kuzidurusu nchi za Afrika peke yake!Sarafu za nchi zote zinazo tuzunguka zimesha ipiku thamani ya shilingi yetu,ukianzia Burundi,Rwanda,Zambia,Malawi,Msumbiji,Kenya na hata Uganda!Thibitisha hilo katika mitandao,katika habari za biashara kupitia TV Channels za Kimataifa,na katika Forums mbalimbali za Kimataifa.Tanzania tutalazimika tuanze upya kwa Vijana wetu!shamefull indeed!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 03, 2008

    anonymous july 02,2008 11:24 inaonesha baba yako ccm watu wankufu na njaa una sera sera gani hizo wa2 wanalinda mpaka wazungu wanawatoa nishai huko UK kwa ficha pesa nyingi na mapka leo wanalinda hawataki kuwakamata wa2 tuambie hiyo ya mwizi kuridisha pesa ndio waangalie kumfungulia mashata na mwizi wa kuku au bata anahukumiwa bla hata kuambiwa arudishe hivyo vitu kwanza hizo ni siasa za uongo hizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...