mdau wa kimasai akipatiwa huduma ya kwanza na wenzie baada ya kupigwa dafulao na daladala kwenye barabara ya kilwa rodi jana. hadi globu ya jamii inaondoka sehemu za tukio wanausalama walikuwa hawajafika na majeruhi alikuwa bado ana fahamu zake. sema hao jamaa zake walikataa kumsogeza ama kumkimbiza hospitali hadi trafiki waje wapime

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2008

    Uhai wa jamaa ndio muhimu kwanza kabla yakusubiri trafiki kupima.
    Hata hivyo ndio hali ya ufukara wa huduma zetu TZ. unapata ajali hakuna huduma ya haraka. polisi utasubiri masaa, ambulance nayo hivyo hivyo.
    hata kama ulikua na majeraha ambayo yanaweza kupona lakini unakufa kwa kusubiri. watu wengi wanakufa kwa kupoteza damu nyingi.

    Hivi TZ tuna huduma ya helikopta kuwawahisha mahututi hospitalini?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2008

    Rafiki yangu mmoja alikuwa akisema sote tuna ubaguzi ndani yetu. Tunawabagua wazungu, nao wanatubagua. Wanyamwezi wanaweza kuwabagua Waha nao Waha wakawabagua Wanyamwezi. Mara nyingi tunakuwa hatuuhisi ubaguzi huu hususan pale unapotokea miongoni mwetu (yaani "sisi" vyovyote utavyoichukulia). Miongoni mwa maneno yanayojitokeza bayana kwenye picha hii ni neno "Mmasai". Nafikiri Mmasai au Mnyawezi si muhimu sana kwenye maelezo ya tukio na picha hii. Fikiria kagongwa Mnyakusa karibu na Eiffel Tower na ikaandikwa kuwa ...mwafrika akiwa kagongwa... naamini mimi binafsi ningeona ajabu. Ingalitosha hapa kusema "mtu", "mwenda kwa miguu", au "mwananchi" vyote havina ladha ya ubaguzi...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2008

    yaani wewe nlikuona unazungumza mambo ya maana lakini tena naona wewe ni limbukeni kweli tena nafikiri upo nje ya nchi haujarudi nyumbani kwa miaka mingi,sasa kama unasubiri huduma kwa masaa hiyo helikopta itatoka wapi?hizo barabara zenyewe unazijua fatilia habari za nyumbani ni nyumbani tu usijisahau sana na box kisa likikuangukia helikopta itakuchukua kukupeleka hospitali unanikela kweli weee mwana

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2008

    Michuzi rekebisha usemi sio ajali barabara ya kilwa rodi badala yake ungesema ajali barabara ya kilwa au ajali kilwa rodi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2008

    anon wa 2 we mmasai tu ndio maana..wanakuwa distinguished because they are different culturally,u can tell a masai anywhere but can you tell a nyakyusa or chagga person!?i dont think so..dont attack michuzi for no reason.

    hao wanaosubiria trafiki ambao wapo vijiweni wanakunywa kahawa,mpaka mtu wawatu atapoteza fahamu na maisha in general..kha!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2008

    hivi AAR haina helikoptas?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 03, 2008

    Jamaa kanifurahisha sana anapofikiria ingefaa tuwe na helikopta kuwapeleka majruhi hospitali, good thinking for following an accident there is what is called the golden hour during which your chance of survival
    is high if you get professional help, lakini si lazima upelekwe hospitali kwa msaada wa kwanza. Hapo Dar ingekuwa bora sana kama pangekuwa na Paramedics na pikipiki
    Mjomba helikopta ya Yorkshire air ambulance (UK) baada ya kununuliwa na malipo ya marubani etc yahitaji £7200 kila siku

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 04, 2008

    Hawa jamaa nao tatizo huwa hawali wakashiba. pia unakuta kutwa wapo barabarani vingunguti mpaka mwenge kwa miguu. usikute daladala lilimpitia karibu yake tu na ule upepo ukamzoa hatimaye chali. Masai vipi kutembea napo mnaendeleza mila...!! achane ubahili pandeni daladala.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 04, 2008

    Aibu tupu Tanzania!

    malisa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 05, 2008

    sasa we malisa,aibu tupu ya nini!?we mjinga nini..ajali zinatokea hadi marekani..aibu gani sasa?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2008

    Anon wa july 3 saa 9:38. Helikopta bongo ni muhimu. Pesa si tatzo bongo... Ikiwa serikali ina uwezo wa kulipa pesa nyingi za Richmond kila siku kwa huduma isiyotolewa, inashindwaje kulipa vijisenti hivyo £7200 kwa ajili ya maisha ya wananci wake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...