Sinema ya Bongoland II ni mojawapo ya filamu kibao zitazoooneshwa katika Tamasha la filamu la Zanzibar (Zanzibar International Film Festival).
Sinema ya Bongoland II itaonyeshwa rasmi Jumamosi, July 12 saa moja na dakika 15 jioni.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa tamasha, Bwana Martin Mhando, alisema "ratiba hii imezingatia umuhimu wa kuwapatia watanzania wengi fursa ya kuiona sinema hii, ndo maana ikapangiwa jumamosi". Itaonyeshwa kwanza katika sinema zote zitakazoonyeshwa usiku huo.
Kama mnavyokumbuka, Bongoland II ilishutiwa katika jiji la Dar mwaka jana mwezi wa saba. Wasanii wote katika sinema hii ni wakazi wa Bongo. Hii ni sifa kubwa maana sinema hii itachuana na sinema nyingine nyingi kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni.
Mwezi ujao Bongoland II itaonyeshwa Chicago katika Gene Siskel Film Center katika Black Harvest Film Festival. Habari zaidi bofya hapa.


Jamani,
ReplyDeleteHizi Bongo landi ni sinema za kinazi na roho korosho. Zinashauri watu wasitafute maisha ngambo, mbona wao wamezichezea ngambo na kuzuga bongo?
Mbona wao hawarudi.
Nawambia mtumwa anayelishwa vyema ni bora zaidi ya mtu huru mwenye njaa kali, ataiba.
Mtu ambaye anatamani kuzaliwa mbwa ulaya, unmwambia asiwe mtu ulaya ambayo ni haki yake ya kuvuka mpaka wa nchi yoyote!
RUDINI NINYI BASI!!!!
ha ha ha haha hahahaaaa...
ReplyDeleteSasa wewe tena umechemsha kabisa. Hawa jamaa walikuwa Bongo na wanaonyesha hali ya Bongo...na hii ni sinema..yaani hadithi.
ReplyDeleteTukifuata mantiki yako kwa hiyo mtu akitengeneza sinema ya wauaji au malaya...lazima awe muuaji au malaya?? Halafu usiazime maoni...nunua sinema kwanza...kusudi upate ujumbe wake.
Mimi ni mdau wa kwanza.
ReplyDeleteHebu angalieni part I ya bongo land ndo mtajuwa lengo lao (kushawishi vijana wa kibongo wasiende ngambo kwamba wataadhirika).
Ya II inaonyesha kukaa bongo ni bora zaidi kuliko magharibi, hii ni kweli?
Ndo maana wanaojuwa maudhui na mantiki ya filamu hizi husema ni roho korosho. Watu wataka waishi ngambo peke yao.
KAMA WANYOHUBIRI NI KWELI BASI WAWE NA. 1 KURUDI!!!!