KWA HESHIMA NA TAADHIMA NAOMBA KWA UNYENYEKEVU KUTAMBULISHA KWENU WADAU WOTE LIBENEKE JIPYA KABISA KATIKA ANGA HIZI. LIBENEKE HILI NI LA LA VIDEO LINALOENDA KWA JINA LA:




KAMA JINA HILO LINAVYOELEZA LIBENEKE HILI NI ZAO LA GLOBU HII YA JAMII NA AMBALO LENGO LAKE LIKIWA KUWAUNGANISHA WADAU DUNIANI KOTE KWA NJIA YA VIDEO. HAPO UTAKUWA NA FURSA YA KUONA NA KUSIKIA MAMBO MBALIMBALI NA PIA KUTOA MAONI YAKO KAMA KAWA. NAKARIBISHA MAONI AMA MAWAZO ENDELEVU KATIKA KUFANIKISHA LIBENEKE HILI


KATIKA www.bongotyube.com MDAU UNAKARIBISHWA KUJISAJILI NA KISHA KUTUMA VIDEO ZA MATUKIO NA MAMBO MBALIMBALI AMBAYO UNADHANI YATAFAA KUONEKANA NA KUSIKILIZWA NA JAMII YETU, HUSUSAN INAYOTUMIA LUGHA YA KISWAHILI POPOTE PALE ULIMWENGUNI.


MCHANGIAJI MKUU KATIKA HILI NI WEWE MDAU, NA SIO MIMI PEKE YANGU.
HIVYO JISIKIE HURU KUTUNGIKA VIDEO ZAKO KWA KUFUATA MAELEKEZO NA MIIKO, IKIWA NI PAMOJA NA KUHAKIKISHA KWAMBA UNACHOTUMA HAKITOCHAFUA HALI YA HEWA NA PIA HAKINA UTATA WA HAKIMILIKI. SOMA VIGEZO KWA MAKINI KABLA YA KUANZISHA LIBENEKE.
VIDEO ZILIZOMO KATIKA http://www.bongotyube.com/ NI ZILE AMBAZO ZILITUMIKA KWA UTAFITI NA MAJARIBIO KWA MUDA WA KARIBU MWAKA MMOJA ILI KUHAKIKISHA LIBENEKE HILI HALIDODI. HIVYO ZISIKUTISHE ILA WEWE MWAGA TU VITU VYAKO ILI NASI WADAU TUFAIDI UHONDO...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2008

    MIMI SIJUI KUTUMA VIDEO.UNAFANYAJE KUANZIA KUPIGA HADI KUTUMA HADI INATOKEA KUSIKILIZWA KWENYE MTANDAO.NAOMBA MSAADA KWENYE TUTA KWA WAJUZI MNAOJUA.

    ReplyDelete
  2. kaka za Kilingala ruksa?
    Honrera sana mkubwa!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2008

    Nishatumbukia mzee Michuzi na nimeangalia klip moja ya Bulgaria music idle ni kali sana umeipata wapi?
    HONGERA SANA NA JITIHADA ZAKO
    nategemea utuwekee live ya sabasaba
    malisa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2008

    BREAKING NEWWZZZZZZZZZZZZZ
    Hjaskia habari ya Rais wetu wa ZAmbia Levy Mwanawasa ametuaga duniani mchana huu tafuta hiyo habari,Pole Mwenyekiti wa AU Mr Kikwete ni huzuni jamani,na Summit lao huko,Maana huyu ndo naskia alimpa live Jongwe sasa cjui akakimbizwa hospital

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2008

    kwa nini Mmetumia jina la YouTube???
    hamkuweza kupata jina jingine?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...