prezidaa wa fm academia wana ngwasuma a.k.a wazee wa pamba nyoshi el saadat akiwa na tuzo ya nyimbo bora ya mwaka mwaka jana ya 'dunia kigeugeu'. mwaka huu fm academia na ndugu zao akudo impact a.k.a 'wazee wa masauti' hawakushiriki katika tuzo hizo kwa kile waandaaji walichoita kuwa na wanamuziki wasio wazawa. wadau hii imakaaje, tujadili kwa kina....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2008

    ina a way ni ujinga tu kama mliwaita wenyewe na vijana wa watu wanaimba kiswahili ingawa kuna sehemu wanasema bana watu.....lakini wanaelimisha jamii hiyo hiyo ya ktz mimi nimesikiliza akudo songs zimetulia sana mfn kwa wenzetu mambo ya uzawa mbona siyaoni mf kule us kina rihana kila siku wanachukua awards na kadhalika sababu wamarekani wanawakubali....hii mimi michuzi naona haijatulia kabisaaa ni wivu tu wa watu wachache na wenyewe si wakawachukue hao wazaire bei poa tu wamejichokea tu huko zaire kila mtu anaimba kule na kucheza si big deal hivyooo kuliko kuleta unafiki kwenye tuzo kwanza kuna bendi gani ukiichunguza bongo kuanzia twanga na wenzake ambao hamna mzaire ndani?.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2008

    uupuzi wa ma-"looser".. Basi Ongala naye sio mzawa... Huu ujinga wa uzawa nj akili ya watu ambao wanajijua ktoweza kushinda chochote..

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2008

    Kwa kweli mi sijaona mantiki ya kutoshirikisha hizi bendi zenye asili ya congo. Hivi hizi tuzo lengo lake ni nini. Mi nilidhani kama lengo ni kuinua muziki wa tanzania, basi hata hizi bendi nazo ni za tanzania na zinapiga mziki wa dansi kama wanavyopiga TWANGA PEPETA, BAMBINO na wengineo. Tofauti ni kwamba hizi zinazoitwa bendi za kikongo zinaundwa na wacongo wengi na hizi zinazoitwa za kitanzania zina wabongo wachache. Ila ukweli ni kwamba hizi bendi za kicongo zinaimba muziki kwa lugha yetu ile ile na jumbe zao ni nzuri sana pengine kuliko hata hizi za ki-bongo.

    Sasa mi nasema, kama tunataka kuendelea kukuza muziki wetu na watu wakaendelea kupata ajira kupitia muziki lazima tukubali changamoto zinazoletwa na bendi za kicongo. Tusiogope ushindani, ila tujiandae kwa kushindana, kuwatoa hawa jamaa wa acudo, ngwasuma, diamond ni kuogopa ushindani, manake kwakweli kama wangeshirikishwa lazima mmoja wao angechukua. matokeo yake zinashindanishwa nyimbo ambazo hata hazina mvuto. Hii inazifanya hizi tuzo zikose msisimko na hatimaye zife.

    Sasa ningeshauri kwamba waandaji wajenge hoja na wawafuate hawa jamaa wa BASATA wawambie kwamba ni muhimu hizi bendi zikawapo ili tuzo ziwe na msisimko na mvuto na ziendelee kuvutia watu wengi, vinginevyo hizi tuzo zitakuja kufa kibudu. Ikumbukwe kwamba hizi bendi zina wapenzi wengi sana na wangependa nazo ziwe zinashirikishwa.

    Big Sam

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2008

    Hiyo ni sawa na kusema kwamba katika ligi kuu ya Taifa tunakubali wachezaji wa nje wasajiliwe lakini inapokuja katika kutoa tuzo ya mchezaji bora inabidi tuzo iende kwa waTZ.Sio haki na wala haileti maana yeyote. Hao wageni wanachangia kiasi kikubwa katika ukuaji na undelezwaji wa sanaa ya muziki wa TZ kwa hiyo inapokuja katika kutambua mchango wao kwa kupitia tuzo kama hizi, inabidi nao wajumuishwe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2008

    HIYO NDIYO MAANA YA DUNIA KIGEUGEU

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 02, 2008

    HUU NI WIVU NA UBAGUZI,SASA ITABIDI HIZO TUZO WAVIPATIE VIKUNDI VYA SINDIMBA,MCHIRIKU NA VANGA MAANA HUO NDIO MUZIKI WA KIZAWA MAANA HATA HIZO BENDI ZENYE WAZAWA ZINA IGA NA KUPIGA MUZIKI NA KUCHEZA SHOO ZA KICONGO KWA ASILIMIA 110.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2008

    Ni asili ya binadamu kutafuta sababu itakayo okoa nafsi yake kutokana na aibu ya kushindwa jambo. speaking from my own experience, mara nyingi wanamuziki wa bendi zinazojiita za "nyumbani" wamekua na utaratibu au labda niite utamaduni wa kulaumu binadamu yoyote anyepiga muziki ambao ni tishio kwa either soko (mauzo ya santuri) or umaarufu wa jukwaani particularly wa muziki wa "nyumbani". in the past, ninakumbuka wakati mwingi walikuwa wakilaumu bongo flavour eti tu kwa sababu ya tofauti za kimtazamo wa kibiashara. Wakati bongo flavour artists wanaangalia trend ya soko zaidi, hawa wa nuziki wa 'nyumbani" wanang'ang'ania maudhui yale yale ya enzi za 80's (kumekucha jama kumekucha, majogoo vijijini wanawika) ambayo sasa si relevant kabisa. Recently,wamewageukia wa Congo ambao wamedemonstrate kazi nzuri jukwaani na katika santuri. Kunani wajomba? wakati nchi inaingia katika globalization mlizani itagusa mabenki na mitandao pekee? Huu ndio ulimwengu wa kweli wa biashara ya muziki duniani kote, toa kitu chenye quality uuze large quantity na upate tuzo. Biblia inasema asiyefanya kazi na asile.
    Mr Paul. Sydney.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2008

    HAKUNA CHA KUKIJADILI HAPA!
    Uhamuzi umeshapitishwa kuwa sio wazawa sasa kuna mjadala gani wa
    kuhalalisha haramu?
    Watanzania lazima tujenge utamaduni
    wa kuheshimu mahamuzi tunayo yaamua.
    Imeshaeleweka kuwa TUZO hizo ni kwa wanamziki wazawa kwa ajili ya kuwapa changamoto hili waendeleze vipaji vyao.
    Tusijadili jinsi gani mkate wa watoto wetu !tuwamegehe wageni,huu ni utamuduni wa kijinga kila siku tunawadhulumu wasanii wetu nafasi na kuwajali wageni

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 02, 2008

    Waandaaji wa Tuzo hizo za Muziki wa Tanzania wanahitaji MSAADA ZAIDI WA KITAALAMU.Lengo lao tumelifahamu lakini utaratibu wanao utumia HAUFAI HATA KIDOGO na hakika utarudisha nyuma zaidi maendeleo ya Muziki hapa nchini badala ya kuuendeleza mbele.Utoaji wa Tuzo za aina hiyo itategemea zaidi nini malengo ya Tuzo hizo.Ikiwa lengo ni kukuza muziki nchini pamoja na kuendeleza vipaji basi KIGEZO MUHIMU ZAIDI katika kuamua au kuchagua Washindi ni KWANZA kwa kuangalia ni Tungo au Rekodi au Santuri(CD) ipi iliyo UZWA zaidi au ILIYOPENDWA ZAIDI na wanunuzi au wapenzi wa muziki nchini.Sidhani kama hao Waandaaji wa hizo Tuzo wamesha jenga uwezo huo kimtandao wa kuweza kupata takwimu sahihi kuhusu Tungo gani iliyonunulika zaidi na wapenzi wa muziki katika msimu maalamu unao shindaniwa.Muziki ni Lugha ya Kimataifa.Na Muziki haubagui makabila japo lugha iliyotumika katika kuimba inawezekana ikawa katika kilugha zaidi ya Kiswahili kinachokubalika zaidi katika Ushindani huu.Ku determine popularity ya Tungo kwa kutumia njia zinginezo kama emails,sms,simu,maoni magazetini,maoni redioni nk hakutatoa uamuzi wa haki na ulio sahihi.PILI,iwapo lengo ni kuendeleza muziki hapa nchini badala ya kubagua wanamuziki kwa misingi ya ukabila au nchi watokazo (kigezo ambacho kwangu sikubaliani nacho na ni cha kijinga)utoaji wa Tuzo hizo ni vyema ungezingatia Aina ya Makundi ya Washindani 'Music Award Categories'.Ingawa sikubaliani na wale wanaosema kuna Muziki wa Tanzania na Muziki wa Kongo,kwangu mimi miziki yote ya nchi hizo mbili inatokana na Ngoma za Kitamaduni za Makabila mbalimbali ya KIBANTU.Na ndiyo maana Uchezaji wake hautofautiani sana kati ya Kongo na Tanzania.Wanaosema kwamba Miziki ya Kongo eti ni Miziki ya Kigeni katika Utamaduni wa Kitanzania NASEMA TENA NI WAJINGA WATUPU AMBAO LAZIMA TUWAPUUZE!Hao wana sababu zao binafsi za kibiashara!Mtu akisema kwamba wanamuziki wenye asili ya Kongo wasishindanishwe kundi moja na wale watokao Tanzania KWASABABU KUBWA MOJA kwamba wanamuziki wa Kongo wametupita zaidi katika sanaa hiyo ya muziki wa Kiafrika HAPO NITAKUBALIANA NAYE.Kwa maana hiyo Tungo zilizo imbwa na Wakongo japo katika Kiswahili zishindanishwe katika kundi lake maalum ILI KUWALINDA WANAMUZIKI WETU CHIPUKIZI ambao haitakuwa haki kuwaweka kundi moja na hao Wakongwe.Lakini kama Kigezo ni Muziki gani ulionunulika zaidi na wapenzi wa muziki hapa nchini basi hapo HAPATAKUWEPO MAANA YOYOTE YA KUWATENGA WANAMUZIKI AU KUWABAGUA ETI WA KONGO HAWARUHUSIWI KUSHIRIKI.that will be very unprofessional indeed!Watanzania tusipende sana DEZODEZO AU MAMBO YA URAHISI RAHISI TU kila wakati.Lazima tujitume na tuongeze Ujasiri(creativity and hard work).Muziki siyo Kazi rahisi kama wengi wetu tunavyo fikiria.TUTENDE HAKI KWA WAPENZI WETU WA MUZIKI na tuwatendee haki wanamuziki bila kubagua kwa kuthamini vipaji vyao na kukiri kiwango wanchokubalika kwa wapenzi wa muziki wenyewe AMBAO NDIYO WAAMUZI SAHIHI NA WA MWISHO lakini siyo BASATA au TBL au PATEL au VIONGOZI WA KISIASA!Tuuache Muziki ubakie Muziki bila ya kuingiliwa na maamuzi ya wachache wanao jifanya 'mabingwa'wa fani ya muziki.Muziki utakaopendwa na kununuliwa na wapenzi wengi zaidi siyo lazima uwe ule ulio upenda sana wewe binafsi!Kuna vitu vya ajabu sana vinavyo fanya Tungo ikakubalika zaidi kwa watu wengi zaidi kinyume na matarajio ya wengi.UTARATIBU UNAOTUMIKA HIVI SASA HAPA TANZANIA KATIKA KUCHAGUA WASHINDI WA TUZO MBALIMBALI ZA MUZIKI KWA KWELI HAUFAI NA UKO CHINI SANA YA KIWANGO CHA KIMATAIFA!Kufanya makosa siyo mbaya.Tujifunze tusiyarudie tena Makosa yaleyale yaliyopita.Vinginevyo Tuzo hizo ziko hatarini kupoteza Maudhui yake na hatimaye kukosa wafuasi!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 02, 2008

    mimi nikiwa kama mshabiki wa hizo bendi za wakongo je mwaka jana mlipowaita hamkujua kama si wazawa? au mmeona acudo wameingia basi tuzo zote zitaishia kwa ngwasu na kudo hao akina twanga hamna kitu wanaiga kila kitu lakini angalia sebene wakilicheza wazawa linavyokolea na samaki mwenye vipande vitatu sasa . acheni ubaguzi wenu semeni tuzo zilikuwa hazitoshi ndio maana mkawatolea nje.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 02, 2008

    ni kawaida ya watanzania wanapoona mtu anaendelea au kufanya kitu cha maana,wanazusha ooh si mzawa,uchunguzi ufanyike na mengineyo.wakae chonjo watazushiwa kubaka kama ngunza na hao pia.
    siasa hata kwenye burudani jamani!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 02, 2008

    mhhh Sio kila mwanamke akiingia ni Malaya,sio kila mwanamke akenda baa anajiuzaa..... Wako waenda baa ni kwa starehe zao binafsi, wengine waenda baa kuwaona wazee wa Ngwasuma.... Kwenye pochi zao wana pesa zao za matumizi.Hela zakula hela za kunywa na usafiri wakurudi makwa. Nikibwagizo tu cha wimbowao mpy aachilia Dunia kigeugeu. Kwama anana kii hao wa tafiti wa michanyo ya band huu utakuwa niuonevu. Jamani wadau tuacheni kuoneana. Ngwasuma juu juuuu juuu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 02, 2008

    HUO NI UPUUZI ,TENA NI UJINGA SIO SABABU YA MSINGI MIMI NAFIKIRI WAMEONA KILA MWAKA WAZEE WA NGWASUMA NDIO WATAKUA WANAICHUKUA HIYO TUZO MANA MASONGI YAO YAMEKWENDA SHULE, NDOMANA WAMEAMUA KUWATEMA.HATA KAMA SIO WAZAWA KWANI HIZO NYIMBO ZAO SI ZINASIKILIZWA NAWAZAWA/WATANZANIA PIA?AU ZINASIKILIZWA DRC?WAANDAAJI ACHENI KUWABANIA WAZEE WA NGWASUMA KWA SABABU ZA KIPUUZI.MISS R. NYANGE.LONDON

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2008

    Mleta hoja asante sana kwa hili. Hata hivyo naomba ABC ya hiyo Kampuni au NGO au Taasisi ya waandaaji wa shindano la 'Nyimbo Bora.'Hususani Kusudi la shindano, washiriki kusudiwa ni nani na utaratibu wa kushiriki na kumpata mshindi kabla mimi sijatoa hukumu katika mahakama hii ya ustaarabu ya jamii!

    Maana mashindano hapa duniani yapo kibao na kimsingi yote (nasema yote!) yana 'ubaguzi' wa aina fulani ambao unakuwa umeelezwa waziwazi mapema sio dakika za mwisho za ushiriki. Mfano hata Olympic nayo ina 'Ubaguzi' wa kuwakataa Wote 'wanaobugia unga' na hata katika soka kuna mashindano yanayojali uraia kwanza na mengine umri na mengine usajiri tu n.k
    Zaidi ya yote naomba pia tujulishwe aina ya uandikishwaji wa bendi zetu tulizonazo kama FM Academia, Akudo sound hata hiyo ya Respect (TOT), Bambino na zingine zote maana hata unaweza kukuta nyingine hazikusajiriwa kabisa au hata zinafisadi pato la Taifa au zinafanyisha kazi wasanii wa nje bila hata work permit na au resident pemit!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2008

    huu ni upuuzi na ubaguzi usiokuwa na maana yeyote utakuta jitu hil lililotoa hiyo idea ya uzawa linaenda kwenye show zao sasa sijui manaake ni nini.kuna watu sijui wana vichwa vimejaa matope.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 02, 2008

    INASEMEKANA HUYU MHESHIMIWA ANAUNDUGU NA "CAVE MAN" NENDA GOOGLE UTAMWONA MWENZIE.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 02, 2008

    MANDELA KAONDOLEWA KWENYE LIST YA WATU MAGAID WA US LEO,CHA AJABU CLLINTON ALIENDA KWENYE BIRTHADAY YAKE UKU ANAMTAMBAU MANDELA KAMA GAID NI AIBU KUBWA KWA MAREKAN NA WASHIRIKA WAKE.
    WADAU MNASEMAJE.UKIPIGANIA UHURU BAS WE NI GAID

    ReplyDelete
  18. Yaani Michuzi kwanza kabisa mimi nakushangaa wewe hapa. Yaani na uzalendo wote ulishindwa hata kutuwakilisha sie tuliopo mbali mapema ili tukupe dondoo zetu. Haya mambo yaliyofanywa na Kili Awards ni upuuzi mtupu. Hawa jamaa wanapiga muziki wa kitanzania, kama walitaka kutoa hizo awards kwa wanamuziki wa Bongo tu basi hata wasingeweka category ya Bongo Flava kwani huo si muziki wetu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 03, 2008

    Huu ni U-mugabe. Watu wameshindwa na hawana mapya kichwani lakini bado wanataka kutawala na kuharibu vitu bila msingi wowote. Kama ni hivyo tu, basi hata wasingeweka Bongo Flava kwani ule si muziki wetu. Beats za Computer from US na Europe, mtu hana kipaji chochote anawekewa beats yeye anatia sauti halafu mnaita muziki wa Bongo? Kili acheni ubaguzi usio na sababu. Yaani hapa mnabaguana hivi hivi. Msije kukuta ni Asha Baraka anafanya hivi ili bendi yake ishinde. Yule Mama naye ni Mugabe.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 03, 2008

    Nikisikiaga hizi tuzo huwa napata kichefuchefu kabisa.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 03, 2008

    Sasa mzawa ni nani na muziki wa kizawa ni upi?Labda Msondo na DDC Mliman park.Bongo flava mnaita muziki wa watanzania?wanaiba beats kutoka kwenye miziki wa watu na internet,ndio sababu sasa hivi hampigi miziki ya nje kwa sababu hao mnaoita maproducer wanajua wataazirika. Twanga pepeta na wenzie mnasema wanapiga muziki wa kitanzania?lile si bolingo linaimbwa kiswahili,tuache wivu watanzania, wote tunajua FM Academia ni mwisho wa maneno,waliowazuia wanajua kuwa wanamuziki wetu wanaiga,sasa kuwaruhusu FM ACADEMIA ni sawa na kutangaza mshindi kabla ya shindano

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 03, 2008

    Ninavyojua mimi kuwa kili Music awards ni kwa ajili ya muziki wa Tanzania, sasa hapa flava inakujaje? Ngwasuma wanapiga muziki wa Tanzania na huimba kwa kiswahili kuelimisha jamii, leo hii hamuwatambui?

    ReplyDelete
  23. Mbona wanatoa award kwa wanamuziki wa nje ya nchi kama,uganda na kenya?? jamani mbadilike jamani, hakuna uzwa kwenye globalisation.wakongo,bongo flava, taarabu, bluzi zote sio ngoma zetu zimetofautiana tu ni nani aliwahi nani alichelewa. MIZIKI YETU NI NGOMA ZA UTAMADUNI, NYAKATI ZA MAVUNO, WALA MSIJIONE MKO SAHIHI.

    PAPII YUKO WAPI?? JE HAKUWAHI KUCHUKUA TUZO????

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 03, 2008

    wanasema nimekunywa bia, nasema sijakunywa bia....hizi ni siasa tu jamani, acheni ujinga nyie waandaaji..ufisadi hadi kwenye mziki??? ngwasuma na acudo tupeni raha bwana achaneni na hao wapuuzi, ni kuwasusia tu ma-award yao, vi-award vyenyewe uchwara tu hamna lolote..

    Kuna huyo anayewakandia wazawa, kiswahili chenyewe hajui, ni walewale tu watoto mama wa lidaz!!!!ha ha ha ha ha ha...ale mwanangu bado mdogooo...kizuri kinajiuza aaah..!!! wivu sinaaa ila roho inauma beibeee....kamueni wanangu, achana na hii mizawa ishachanganyikiwa!!! kudadadeki!!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 03, 2008

    UPUUZI MTUPU, MWAKILISHI WA MASHINDANO YA NANI HINO ..................NANI VILE RIDHA KAENDE KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MAONYESHO YA DUNIA. TUZO AMBAZO NI ZA NDANI YA TANZANIA MNATUMIA SABABU YA UZAWA...ACHENI ZENU MNAFAHAMU KWAMBA WATACHUKUA WAO TENA NDIO MAANA AMUWATAKI SIO.TANZANIA TUNAKWENDA WAPI? KAMA TUNABAGUANA NAMNA HIYO BASI WAFUKUZENI WAHINDI WOTE BUNGENI WASISHIRIKI KWANI HUKO NDIO SEHEMU MUHIMU ZAIDI KUSHINDA HATA HUO MUZIKI.

    NAAMINI KABISA KAMA KUNGEKUWA KUNABENDI YA WAZUNGU WASINGELETA MAMBO YA UZAWA.

    NANI MZAWA HASWA? KWANI MENGI YA MAKABILA YA WATANZANIA NI WAHAMIAJI TU UKIANGALIA HISTORIA NZIMA YA NCHI YETU.INAONEKANA HATA HAO WANAOLETA UZAWA LABDA NI WAHAMIAJI KAMA WENGINE WENGI.TUACHENI UBAGUZI WAKIJINGA KWANI TUKIFUFUA HISTORI 50% SIO WAZAWA.

    MJUSI

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 03, 2008

    MLETA MADA KAPOTOSHA UKWELI WA TUZO HIZO. SIYO KWELI KUWA BENDI KAMA FM WANA NGWASUMA ETI HAIKUWEMO KWENYE TUZO KWANI YENYEWE INAO WABONGO WAKUTOSHA NA NDIYO MAANA MWAKA JUZI WALIPATA TUZO YA DUNIA KIGEUGEU. MWAKA JANA NGWASUMA HAWAKUTOA ALBUM MPYA NDIYO MAANA HAWAKUWA ONE OF THE NOMINEES JAMANI.WAO WAMEBAKIA NA ILE ILE DUNIA KIGEUGEU, TOFAUTI NA WENZAO WA AFRICAN STARS- TWANGAPEPETA AMBAO WANATOA ALBUM MPYA KILA MWAKA.BENDI ILIYOSEMEKANA KUWA NA WACONGO WATUPU NI ACUDO TUU. YENYEWE NDIYO HAIKU QUALIFY. NA HATA WANGEIWEKA ISINGEAMBULIA KITU KWANI WAO WAMETOA ALBUM YAO YA KWANZA MWAKA HUU. SO WASUBIRI MWAKA KESHO LABDA NDIYO WATU WAZOZE. AUTHORITY

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 03, 2008

    hahahah anon 12:57 nimecheka mpaka basi walahi! HAHAHAHAH ... u mugabe tu huu...wivu tuu na udiktetaa waacheni bwanaa!!!!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 04, 2008

    baada ya kubrowse kwangu nilikutana na huyu jama anatengeneza beati kali.....huyu jama ni mbongo..au yuko bongo? luna mdau yoyote anafaham anapatikana wapi? mcheki hapa:
    http://ilike.com/artist/baraka+bk

    Mgosi

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 04, 2008

    Watu wengine bwana. Kama hamana cha kusema simkae kimya tuu. Kwa taarifa yenu ni kwamba wanaoidhinisha nominees kwa ajili ya TUZO za Kilimanjaro Music Awards ni BASATA ambao kazi yao ni kuimamia sanaa ya Kitanzania. Sasa chombo cha serikali kama hicho nyie mnafikiria kinaweza kuwafagilia hao Wacongo wa FM wanaobadili nyimbo za Kina Werrason kutoka kwenye kilingala na kuwa za Kiswahili?. Halafu wa wa nominate kwenye Album bora ya Dansi ya Kiswahili kweli?. Kama huko nyuma walfanya makosa nadhani mwaka huu wameamua kujisahihisha. Safi sana BASATA kwa kuwastukia. Kwanza swahili yao ni mbofu mbofu mtawapaje ushindi wa album bora ya kiswahili wakati wanatamka DI Siukuje?,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...