kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi mkoa wa dar afande suleiman kova wiki hii ametoa wazo kwamba ili kusaidia kupambana na uhalifu kamera za cctv ziwekwe kwenye kila gesti na hoteli ili kila anayeingia humo ajulikane na kama ni mhalifu iwe rahisi kumnasa. wadau hii imekaaje?
hakuishia hapo. pia kamanda kova ametoa hadharani namba yake ya simu ya kiganja anbayo ni +255754034224 ili wadau wampigie muda wowote kutoa taarifa za uhalifu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2008

    Suala la Kamera ni wazo zuri lakini kuwe na utaratibu ili wasi abuse privacy za wate. Haya mambo ya kutoa simu yake ya mkononi ndiyo iweje sasa? kwani hakuna namba za Polisi?

    Inaonyesha kuwa watu wengine hawajui au hawana uwezo wa kufanya kazi au hawana jipya au yote.

    ReplyDelete
  2. Hii ni vizuri sana; ili pia WAZINZI na WAASHERATI wajulikane.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2008

    ni wazo zuri ila sasa uamuzi huo uwekwe kwenye sheria za nchi kuhusu picha zitakazo dakwa na camera hizo ziwe na mipaka yake zitumike tu kwa ajili ya uhalifu iwapo utatokea,sio kesho uje uone picha za wateja zinasambazwa kusikohusika,na je atatuhakikishia vipi kwamba hizo picha zitatumika kwa kuchunguza uhalifu tu na sio vinginevyo,na je kama zikitumika vinginevyo mhusika ana haki gani kisheria ,mimi nafikiri hili suala linahitaji umakini,kidogo sio kukurupuka na kuanza kuingilia privace za watu na kukusanya info za watu ,halafu zinakuja kutumika vibaya ,na kama ni majambazi si wapumbavu si watakuja wameficha sura zao,mimi nafikiri kikubwa kusaidia na wala sio kuzuia kabisa tanzania kila mtu awe na address itasaidia sana

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2008

    Huo ni ulimbukeni na kuingilia faragha (privacy) ya raia ambayo ni haki yetu ya kikatiba. atafute njia nyingine. anaonekana asivyojua kazi na wajibu wake.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2008

    Duh, Waziri Mkuu (Pinda) kashampa ulaji mdogo wake.. Duh. Wamefanana sana, wala hamna haja ya kuuliza kama ni ndugu. Duh!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2008

    mijitu mingine mipuuzi kweli. Kama anony wa uly 04, 2008 3:19 AM hapo juu.
    Kova alikuwa kamanda wa special zone ya Dar muda mrefu tu kabla ya Pinda kuwa W. Mkuu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2008

    ilo ni wazo zuri tu,kama alivyosema mwenzangu wasikurupuke tu,iwekwe kwenye sheria ya nchi kama wenzetu wanavyofanya,wengine badala ya kutafuta majambazi watatafuta wake na waume zao,mtaleta balaaaa hapo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 04, 2008

    Safi sana Kamanda Kova, kwa wazo zuri sio tuu utapungaza ujambazi bali kasi ya maambukizi ya Ukimwi. maana watu wamezigeuza Nyumba za kulala wageni kama sehemu ya kufanyia Uasherati.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 04, 2008

    Jamani Hivi Huyo mtoa maoni wa kwanza,na hisi sio mzalendo kwani ishu ya kutoa namba haijaanza kwa KOVA bali hata kamanda mstaafu ndiye aliye uanzisha utaritibu huo na ulionekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. na hawa Eti PRIVACY za watu mbona magazeti ya udaku hamya semi kwa kuingilia hiyo namyo ita privacy. Wewe pilipili usiyo kula inakuwashia nini? Big up KOVA, OVER! tumekusoma

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 04, 2008

    Sasa ukisikia KUTAFUTANA UCHAWI ndio huku!

    We Kova wacha hizo. Sio wote tunaokwenda kule ni Majambazi. wengine tuna ISHU zetu watatuwangia bure na makamera yao.

    Sasa itabidi tumalizane kweye MAGARI tu COCO BICHI kule. Basi.

    Habari ndo hiyo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 04, 2008

    Kamanda Suleiman Kova Bwana!!!! VERY INTERESTING CHARACTER!!!
    Mwaka 2007 mwanzoni akiwa Kamanda mkuu wa Polisi Mbeya aliwahi kuwaita waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya kama ilivyo desturi yake akawatangazia kuwa kuna tukio (jambo) muhimu sana anataka alizindue...
    SII JINGINE ILA ANATAKA KUZINDUA TOVUTI YA POLISI MKOA WA MBEYA!!!...
    Basi mimi na waandishi wa habari wenzangu tukajimwaga kwenda kushuhudia (an innovative system to be launched ever by Police katika mkoa wowote) Basi tukakuta Desktop Computer imefunikwa na kitambaa akatayarisha wapiga picha mara akakifungua kitambaa we we weeee... Tukapiga makofi na Shangwe nyingi...
    SASA JINA LA TOVUTI HIYO MWEE MWEE MWEEEE... inaitwa policembeya@yahoo.com LOL...
    GO KOVA GO KOVA LOL

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 04, 2008

    Peleka Camera wanapoiba vitu vya magari huko shoprite na mlimani city weka kamera parking yote weka mtu anaangalia unakamata vibaka sasa kamera kwenye room uliona wapi au ndio client no 9

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 04, 2008

    we anon wa 11:07am ujatulia,umeniacha hoi kinoma kwa kicheko hadi oficn wananishangaa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 04, 2008

    huyo anon wa 11.07 ni mtu waa ajabu sana,wewe kama mwandishi wa habari kazi yako sio kudiscourage jambo la muhimu kama hilo kutoka kwa kamanda, what u were supposed to do nikutayarisha makala nzuri zaidi ya kukemea ujambazi na kuwatia moyo polisi, pia kuwahamamsiha wananchi ili wawape polisi wetu support ya kutosha,use ur brain bro!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 04, 2008

    Anon wa 11:07 mbavu zngu zinauma, sasa ulimuelimisha mheshimiwa kwamba hiyo si tovuti? au ulipiga makofi ukaenda kucheka mbele? bado nacheka.

    ReplyDelete
  16. anony wa July 04, 2008 11:10 AM umeniacha hoi, hahah, "Client #9"


    na tena ma-Eliot Spitzer Bongo wapo wengi sana

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 04, 2008

    hehe...comments za watu zimenifurahisha sana humu! CCTV zipo sehemu nyingi sana! As long as they dont put them chumbani au vyooni mimi sioni violation ya privacy ya mtu yeyote maana kwanza upo public area. La maana ni kuhakikisha utumiaji wake usiwe wa kuonea watu. Ijulikanee kabisa, nani ana access na hizo video, nk. Ndo kupiga hatua huko. Nyie mnaosema kuwa wahalifu watakuja wakiwa wameficha sura...utashangaa ulaya watu wangapi wanakamatwa na hizi camera. Zinasaidia sana...hasa katika ku-retrace hatua za wahalifu!

    Lakini sheria lazima iwepo.
    hapa kweli inaonyesha jinsi tulivyo nyuma katika uelewa wa kazi za serikali na bunge. Pia inaonyesha nguvu polisi waliyo nayo tanzania. Hili swala lingetakiwa kuanzia bungenlitungiwe sheria...sio mkuu wa polisi anaamka asubuhi na kuamua mwenyewe tu kitu kinachogusa maisha ya wananchi! Tuko nyuma sana!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 04, 2008

    Wee annon wa July 04, 2008 8:30 AM, kabla ya kuwaita watu wengine wapumbavu uwe unajaribu kutafakari wenzako wanayoyaandika, maana wengine wanaweza wakawa wana-joke then wewe unakuja malizia stress zako za maisha humu kwa michuzi. Cool down ndugu yangu na enjoy maisha.. That was just a silly joke... Kicheko ni afya.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 04, 2008

    Tumechelewa sana, huku mamtoni ni kila sehemu cctv hata viduka uchwara, barabara zote cctv, hata polisi wanatembea na kamera walizovaa kama sare kunasa matukio ya kihalifu, any way ni level ya maendeleo. Big up Kova

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 04, 2008

    HIZO HOTELI NA GUEST HOUSE ZINAINGIZA SHILINGI NGAPI KWA SIKU HADI WAWE NA UWEZO WA KUFUNGA HIZO KAMERA ZA CCTV?

    AU POLISI WATATOA RUZUKU?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 04, 2008

    Mi nashauri kamera hizo ziwekwe mpaka kwenye milango ya kuingilia vyumbani ili tujue wanaoiba wake/waume za watu! Kwa hili tutaweza pia kupunguza kasi ya maabukizi ya ukimwi! Go Kova go go go!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...