kama nilivyotangaza juma hili mwanzoni ni kwamba kuanzia leo jumatano majira ya saa sita usiku kwa saa za bongo, anuani ya globu hii ya jamii itakuwa www.michuzi-blog.com na sio issamichuzi.blogspot.com tena.
naomba nifafanue hapa kwamba kinachobadilika ni anuani tu kwani globu itabaki na muonekano wake uleule, sema itaongezwa libeneke kwa kuwa na mapicha, habari pamoja na video kedekede tofauti na ilivyo sasa.
sababu za kuhamia www.michuzi-blog.com ni kwamba huduma ya blogger haikutosheleza kutokana na kuwa na nafasi ama space finyu kwa kuwa ni ya dezo. hivi sasa space ni ya kulipia ambapo itakuwa kubwa zaidi kama libeneke litakavyokuwa.
kwa heshima na unyenyekevu naomba niseme tena; kinachobadilika ni anuani tu toka hii ya siku zote ya issamichuzi.blogspot.com kwenda www.michuzi-blog.com na libeneke litakuwa ni lile lile na sio kubadilika kwa globu kama wengine walivyoelewa.
pia msisahau kutembelea na hata kuchangia video zenu katika wavuti dada ya globu hii ya jamii inayoanza rasmi leo:
asanteni sana wadau
nawapenda wote
MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2008

    Nipo Cardiff, Ukerewe na ni saa Nane Kasoro Robo usiku na nyumbani ni saa Kumi Kasoro Robo Alfajiri na nilitegemea kuukuta link mpya ikiwa inafanya kazi kama ulivyosema......lakini bado ujumbe wa kwamba "Iko kwenye ujenzi, tembelea baadae" umetawala.

    Vipi Mzee MITHUPU mbona hivyooooooo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2008

    MLIOSOMA NA KUBOBEA KATIKA IT YANI TEKNOHAMA NISAIDIENI
    Hivi kwani lazima site ya video iitwe tyubu? Youtube,eastafricantube,bongotyube etc? Napenda kujua. Pia Michuzi heri ukabadili hiyo BONGOTYUBE kuwa bongoTUBE. Hako ka 'Y' umekaweka ukidhani kanaleta ladha ya kiswahili kitasababisha asilimia kubwa kutoitype correctly. Tupende kupokea maoni toka wataalamu na sio maoni toka watu. Tyube ni heri tyubu kuweka kiswahili. Aminia na endeleza Mbeneke!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2008

    BREAKING NEWS,MANDELA KAONDOLEWA KWENYE LIST YA WATU MAGAID DUNIAN,
    WADAU MNASEMAJE.
    CHA AJABU BILL CLINTON ALIENDA KWENYE BIRTHDAY YAKE UKU AKIWA ANAMTAMBUA KAMA MTU GAID

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2008

    wewe anon 9:09 king punguani wa mapunguani...sasa nelson mandela ana ugaidi gani?unajua maana ya ugaidi?its terrorist..so your calling mandela a terrorrist?are you insane?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...