Shindano la Miss Tanzania EU 2008 MZUKA!

Lucy (pichani akiwa na ali kiba) mwenye miaka 18 alishinda katika upinzani mkali na warembo wengine. Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Sabrina Bashir, ya pili na Jacquline Sabanya.
Ali Kiba aliwarusha warembo na washabiki wa Miss Tanzania EU Ujerumani Mwanamuziki wa kizazi kipya ambaye alipagawisha mashabiki kibao kutoka sehemu mbali mbali za Ulaya.

Ali kiba na vibao vyake vikali; Cinderella, Mac Muga, Nakshi nakshi nk. Viliwarusha washabiki toka mataifa mbali mbali usiku huo.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa Ngemera alifungua shindano hilo kwa kusisitiza waandaji wa shindano hilo kutoishia hapo bali liendelee tena na tena.

Katika ufunguzi wa shindano hilo ambalo lilidhaminiwa na shirika la ndege la Ethiopia, wimbo wa taifa uliimbwa na Godlove Muliahela mtanzania anayeimba Gospel jiji la Mülheim nchini Germany.

Maelezo na picha kwa wingi zaidi nenda www.malumbosjr.blogspot.com ambaye kaleta habari hizi na picha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2008

    mmmm!!! no comments,tumekosa mitu kabisa???

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2008

    Mshindi wa kwanza ni Sabrina Bashir au Lucy Mwiza Fundikira?

    Bado hii habari inanichanganya

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2008

    afadhali ya wewe uliyechanganyikiwa, lakini habari ndo hiyo kwamba Lucy ndo wa kwanza.

    imebidi niende kwenye hiyo site ili nione alioshindana nao wanafananaje, lakini sikuona kitu cha maana. anyway, ngoja niendelee kuhifadhi maoni yangu maana nisije nikaitwa ni muosha kinywa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2008

    sasa karatasi ni mrundi,hao IND kweli hizo picha hawaoni?na ukibahatika kuwa Miss Tanzania inakuwaje?utaukana urundi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2008

    Tanzania mabinti wazuri kuliko huku hakuna UK wala EU in general sijaona ushindi bongo hivi nguo zinatokea huku sasa mbona bongo mademu wao wanapiga pamba kwenye hizo show kuliko show za huku nimechanganyikiwa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2008

    kulikuwa na matangazo ya kushiriki mnaojiona warembo hankuenda sasa watu wameshinda mnatoa malalamiko. ndio haiwezi tena ku rewind ,imetoka ikirudi pancha..tusubiri mwakani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2008

    jamani kuna MSHINDI halafu anyefuata ni mshindi wa kwanza (1st runner up) akifatiwa na mshindi wa pili yaani 2nd runner up...habari ndo hiyoo

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2008

    Hongera sana. You deserve it. Nakutakia Kila la kheri Nyumbani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2008

    WEWE ANON4 HUO NI WIVU TU NA CHUKI BINAFSI KWANI NYIE WABONGO WA HOLLAND MNASIFA HIYO HAMPENDI MAENDELEO YA WENZENU NA SASA MNAKOELEKEA NI KUCHOMANA TU KAMA WABONGO WA UK. KUWENI NA WIVU WA MAENDELEO SIO WIFU WA KICAWI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 02, 2008

    ww anonymous july 01,2008 2:51 pm hiyo comment yako kama ninani au nani ww hayakuhusu nyie ndio msiopenda maaendeleo ya wa2 kama umeshindwa kumpeleka demu wako huko ww 2lia usubiri huye demu wako mwenye karatasi ya kibongo akashiriki ww mwenye unakaa kwenye maisha ya yaho ya IND alafu unataka kusema nn m2 kama kashindi acha ashinde,tuweni na maendeleo sio majungu 2.NAKUPA ONGERA MREMBO LUCY MWIZA UTAWAKILISHE HUKO VIZURI UWENDAKO.take care na wazushi hao walishaanza majungu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 02, 2008

    hayo ya kweli mnayosema anonymous 9 na 10.
    wivu umewajaa mpaka wanataka kuwa rangi ya green. mnayotakiwa ni kumpa hongera zake na mafanikio zaidi na sio midomo mirefu.
    pendaneni jamani wabongo wa ulaya. chuki binafsi haina maana yoyote.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 02, 2008

    am sorry but the gal who won aint pretty at all...not hatin or anythin, but yeah thats my opinion..

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 02, 2008

    Kwa warembo wa EU mimi nasema: No Comment.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2008

    urembo sio kila kitu jamani. inatakiwa awe na kichwa pia na pia hao majaji kwani hawana akili?
    wana akili nido maana wanafanya hivyo.
    tuache majungu... mkiona hivyo huyo kashinda mjue maswali alijibu vizuri kuliko hao warembo wengine.
    kama ingekunguwa hivyo afrika mbona warembo kibao lakini nini kimewachanganya?
    kichwa jamani. wanaulizwa hivi wanajibu hivi. nasema tena jamani kichwa...
    kichwa

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2008

    Kweli hakuna kitu kabsaaaaaa, bora wakaa hukohuko wasije poteza pesa zao na hata hivyo vijikaratasi bandiaba

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 02, 2008

    Haya Ali Kiba,peta tu tutawasalimia kule Kigoma!Ila usije ukasahau ukaenda Railway Station,huko hakuna Kigoma Mze au vipi?Kama mmeishiwa Mawese huko tuma email kwa Konoooz haraka,tufanye mambo huku!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 03, 2008

    hehehe..kiswahili chawashinda sasa. mshindi wa kwanza ndo 1st runner up?huo uongo sasa....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...