
benki inayotembea ya crdb ikidunda kama kawa leo viwanja vya maonesho vya sabasaba. kuna mdau katuletea ufafanuzi kuhusu habari kwamba leo ni sikukuu ya mabenki na kwamba eti benki zitafungwa. soma kwa makini hapo chini
Kaka misupu,
naomba uwaweke watu sawa kuhusiana na hiyo bank holiday.
ukweli ni kwamba walengwa wa hiyo siku ni benki kuu kwa sababu leo ni tarehe yao ya mwanzo wa mwaka wao. Hivyo basi toka jana wako bize na kufunga mahesabu yao ya mwaka.
Kinachotokea kwenye mabenki mengine ni kwamba shughuli ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na bank kuu ndizo hazitokwepo ila mabenki hayatafungwa na shughuli nyingine zitaendelea kama kawa, kasoro Bank kuu tu ndio hakuna shughuli ya kibank itakayoendelea leo
Mdau mtaalamu wa vijisenti


SI KWELI MTAALAM WA VIJISENTI.LEO NIMEKWENDA STANBIC NA HUDUMA KWA WATEJA ILIKUWA HAKUNA,HUO NDIO UKWELI.ULIZA MTU YEYOTE.
ReplyDeletecrdb hongereni kwa bank inayotembea. michuzi umebania mail yangu kuirusha hewanio poa nijibu basi wewe swali langu,
ReplyDeletesweet
hii bank holiday CRDB Bank jikusanyeni upya muwape Wazalendo card zao kama ni hivyo basi ATM na hilo ligari la nini ni Show Off tuuu au maana hatuwaelewi kabisa Mr Kimei tunaomba ufafanuzi kwa hili tumechoka njoo kesho na kupanga foleni tujue moja bado tuko Zama zile za Mawe!!!!!!!
ReplyDeleteMtanzania aliyechoshwa na Nchi hiii maana watu wanaangalia kwenye 10% kam hilo ligari kuna mtu anacheka sasa
Asante mtaaluma wa Vijisent kwani maalezo yako ni kamilifu na sahihi...
ReplyDeleteEti mahesabu ya nafungwa siku ya Mwaka mpya?????!!!!!
Hakuna lolote.
ReplyDeleteBenk zote zilifungwa na msela wangu anayefanya benki alikuwa maeneo ya saba saba akienjoy HOLIDAY !!!
Nanilosoma waraka waliotoa BOT unasema ni HOLIDAY ya wafanyakazi wa BENKI.
Labda ni mapumziko BAADA ya kufunga mahesabu na siyo WAKATI wanafunga mahesabu !!!
Mbaya zaidi hawakutoa taarifa mapema !!!