Zikiwa zimebaki takriban siku sita kabla ya ule mtanange wa timu mahili ya Mashariki (East Mass) kumenyana na timu kongwe ya Magharibi (West Mass) katika kusherehekea miaka saba toka tuanze shughuli hizi, masikio na macho ya wengi yamewaelekea wenyeji wa hafla hii kubwa ya mwaka katika majimbo yetu ya New England ambapo watanzania huja kukutana kuzungumza, kubadilishana mawazo na kufurahi sisi wenyewe,familia zetu, jamaa na marafiki.
Tunapenda kukumbusha tena wewe ndugu yetu kwamba, shughuli hii ya kukata na shoka itafanyika Greenfield,Massachusetts Jumapili tarehe 20 Julai, 2008 kuanzia saa tatu asubuhi (9am) mpaka saa tatu usiku(9pm). Habari zilizonifikia punde kutoka kwenye kamati maalum ya ufundi ya shughuli hii, inasema maandalizi yamekamilika na yule ngo'mbe jike kweli yupo!
Katika kuyaweka mambo sawa chanzo changu cha habari kimeitanabaishia Globu hii ya jamii kwamba yule mtaalam wa kuchoma nyama katika ukanda huu wa East Coast anawasili mapema mwishoni mwa wiki na "yuko fit" kwa kazi hiyo!
kama umewahi kula mishikaki au nyama choma ya mnadani Dodoma basi ladha ile na ya huyu jamaa haipishani hata kidogo!
Kulingana na mratibu wa shughuli hii ametonya kwamba ni bora watu wafike mapema hasa wale wenye kutaka supu ya utumbo kwa vitumbua, baada ya hapo kutakuwa na michezo ya soka kwa watoto na watu wazima, mpira wa vikapu kwa watoto na watu wazima, netball kwa kina mama na ndipo tutapumzika na kupata chakula kizuri cha mchana.
Baada ya hapo ndipo burudani ya mitindo ya mavazi ya kitanzania kwa watoto, kina mama na kina baba yatafuata. Shughuli ya ubunifu wa vipaji tofauti kama kuimba,kufoka n.k. vitakuwepo.
Bila kusahau dansi maalum ya kiafrika ambayo mwaka jana ilikonga nyoyo za watanzania wengi kuona vijana wetu wenye umri wa miaka 15 mpaka 18 pia wanaweza kucheza "pinda mgongo".
Ni muhimu uwahi mapema wewe na familia yako na jamaa zako ili uje tufurahi pamoja.
Haya ni maisha, hapa tulipo ndipo kwetu...nyumbani mbali na nyumbani, na kama ujuavyo maisha yenyewe mafupi haya njoo tufurahi.Kama kawa "Sugu"
Mr. II atakuwepo na kutupa burudani la nguvu na kijana wetu Hasheem atakuwepo kuwapa vijana muelekeo wa kucheza mpira wa kikapu.Na kama ilivyo ada namalizia kwa kusema mwakwetu shughuli ni watu na hao watu ni mimi na wewe.
HABARI NDOO HIYO!
Naomba kuwakilisha,
Isaac A. Kibodya
Kwa niaba ya wanakamati
Ukihitaji mawasiliano zaidi basi usisite kupiga simu za wanakamati ambayo baadhi yao nimeziandika hapa chini.
Shukran!
Bwana Stephen Tomi 413.658.5253
Bi. Maria Sombe 413.364.8151
Bwana Richard Mwandemani 413.262.0400
Bwana Baraka Baraka 413.364.8151
Bwana Ahmad Mkambavange 413.221.2935
Bwana Mohamed Kibodya 413.796.9761
Bwana Severine Kiputa 413.306.2109
Bwana Kawala Mgawe 413.330.1609
Kwanini hamfanyagi jumamosi hii party? wengi tungependa kuja huko lakini mtu ukisafiri ufike huko jumapili na sijui tutaweza kurudi na kwenda makazini monday...Au wenzetu hamfikiriii hilo au hamtaki wageni?
ReplyDelete