nabandika hii nikiwa na ndito kule a-taun mahususi kwa kuwashukuru wadau wote wa globu yetu hii ya jamii kwani wasiwasi wangu wa kwamba wengi watapotea mtaa baada ya kubalika kwa anuani kwenda www.michuzi-blog ulikuwa ni wa bure.
vile vile kuna walioomba kujua kama email address yangu nayo imebadilika. jibu ni hapana. email yangu ni ile ile issamichuzi@gmail.com na naendelea kupokea picha, salamu, msaada tutani na chochote chenye kuendeleza libeneke.
pia nashukuru kwa kupokelewa vyema mwana mpya wa globu hii ya jamii anayekwenda kwa jina la www.bongotyube.com ambaye kazi yake ni kuendeleza libeneke la video za aina mbalimbali. huko pia mdau unakaribishwa kujisajili na kuweka video zako bila kupitia kwangu. fuata maelekezo nawe utafanikiwa tu.
asanteni sana wadau wote kwa kuendelea kuniunga mkono. nami nawaahidi kutowaangusha hata siku moja. hapa habari na picha ni za leo leo tu, hakuna kungoja nini wala nini
Michuzi


faza michuzi, mimi ni mmoja wa wadau waliokwama humu ndani, kwa hata ukihama mitaa inabidi asubuhi kabla ya kwenda kuendeleza libeneke, napata dozi ya kuja hapa kijiweni, na hasa msimu wa mvua humu ndani, mfano wakati wa uchaguzi, migogoro na skendo za kisiasa, bajeti, mikutano na kadhalika huwa najisikia kama nipo DAR ingawa niko huku mwisho wa dunia KANADA MZEE MISUPU ENDELEZA LIBENEKE WADAU TUPO...!
ReplyDelete