Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, bungeni mjini Dodoma leo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongea na Waziri wa Miundombinu na mbunge wa Bagamoyo, Dk. Shukuru Kwambwa, bungeni mjini Dodoma leo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2008

    Kaka Michuzi habari za leo.
    Kwanza ninakupongeza kwa blog yenye
    muonekano mpya.

    Pili na la mihimu zaidi ni kufanya sahihisho dogo tu. Mhe. Sophia Simba si Mbunge wa Viti Maalum, yeye ni Mbunge wa Kuteuliwa na Mhe. Rais. Ni vizuri tukaelewa hivyo, kwani tofauti ipo kati ya aina hizi za Wabunge.

    Nakutakia siku njema.
    Karibu Makao Makuu - Dodoma.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2008

    hey bwan shemji yaani ugonjwa wangu ni hiiyo chupa ya ndovu hapo juu mwe!!


    kuhusu mawaziri misifagilii hata kidogo hebu watupe nafasi na sisi jamani miaka nenda rudi ni wao tu this isnt haki kabisa. sijuii tufanyeje . wkina zito walianza vizuri sasa wanatoa hoja za kujadili zimbawe badala ya kwetu hapa jamani wacheni wafu wawazike wafu wao

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2008

    hehe...bunge la tanzania linauwezo wa kutunga sheria za Zimbabwe au vipi tena jamani! Nchi inawashinda wanaanza kujadili zimbabwe bungeni!
    Waache kunifurahisha hawa...lakini hela ya kila siku bungeni wanakula tu...kwa iyo hakuna tatizo hapo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2008

    TUSIFANYE MZAHA NA SEKTA YA VIWANDA NCHINI.Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana Kikao cha Bunge Dodoma lakini bado sijaridhika na jinsi wabunge wetu walivyoweza kuyabainisha matatizo yetu ya kiuchumi hususan katika mahitaji ya msingi ya kila siku kwa kila mtanzania ambayo lazima yatatokana na uzalishaji viwandani.Shilingi yetu inayumba na imekuwa ikipungua thamani ikilinganishwa na sarafu za majirani kutokana na uzalishaji duni viwandani mwetu.Karibu kila kitu utakacho hitaji kutoka dukani kimezalishwa ama katika nchi za jirani au kutoka nchi za nje kabisa.Hakuna Mbunge hata mmoja niliyemsikia akihoji kwa nini viwanda vyetu vimekuwa vikishindwa kuzalisha kiasi cha kutosha,na kwa vichache vinavyo zalisha bidhaa zake ni ghali zaidi kuliko zile za kutoka nchi za nje.Na kwa nini sekta ya viwanda inazidi kudumaa badala ya kupanuka na kustawi zaidi.Serikali yenu mawazo na akili yake yote iko katika ukusanyaji wa mapato zaidi kupitia kodi zaidi.Lakini hakuna anayejiuliza ili viwanda vyetu viweze kuzalisha kwa faida itabidi kodi viwandani iwe ya kiwango gani na gharama za uzalishaji viwandani lazima ziwe za kiwango gani.Somo hili ni refu lakini hapa nimejaribu kuchokoza tu mjadala bungeni kuhusu kuzorota kwa sekta ya viwanda nchini,na kwa nini wawekezaji wa hapa nchini na wa kutoka nje wamekuwa wakikwepa kuwekeza katika viwanda nchini.Wengi kutoka nje wameonelea inalipa zaidi iwapo akiwekeza viwanda katika nchi za jirani lakini akilenga soko la Tanzania.Kwa njia hiyo tumepoteza fursa nyingi sana za viwanda vipya,na tumekuwa tuki 'export nje'ajira za vijana wetu na kulifanya tatizo la ukosefu wa ajira nchini kuwa sugu zaidi.Maneno kuhusu maendeleo ni mengi zaidi kuliko vitendo.TALK IS CHEAP!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...