mbunifu wa mitindo anayekuja juu kwa kasi sana ally rhemtullah (pichani akiwa kabebwa na mamodo) mwezi ujao anatarajiwa kuweka rekodi katika historia ya wabunifu mitindo wa bongo baada ya kualikwa kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa ya LONDON FASHION WEEK.

akiongea na globu hii ya jamii leo, na akiwa ni mbunifu wa kwanza kualikwa kwenye maonesho hayo, ally anasema hata yeye ameshangaa kupata mualiko huo kwani ni ngumu kupata.


amesema hata wabunifu wa sauzi huwachukua miaka 10 kupata mwaliko lakini yeye amekatiza japo ana miaka miwili tu kwenye gemu.



Hilo litakuwa bao la kisigino ambalo ally atakuwa amewapiga wabunifu wote wa bongo na ist afrika mashariki na globu hii inampa hongera inamtakia mafanikio zaidi...



bofya hapa pate mwandani wa ally rhemtullah


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongera Kaka............Ila Mbona Jina Silioni
    http://www.londonfashionweek.co.uk/designers.asp?ShowAll=1

    ReplyDelete
  2. huyo mweusi anafanana na fideli Iranga.

    ReplyDelete
  3. Annon wa kwanza nafikiri uko sawa, nimejaribu kubofya kwenye website na kuchagua kila category, sijaona jina la ally rhemtullah. Kulikona labda bado jina halijawekwa.

    ReplyDelete
  4. jina la nini? mbona lady jd nae alialikwa kwa mandela?? yale yale? gia za kuombea vissa.

    ReplyDelete
  5. Eti, kwa nini suruali yake imechanika?

    Mnasema jina lake halimo! Ha! Kwani nani alisema litakuwemo? JD hakuwemo kwenye birthday ya Mandela, ile timu yetu ya vijana ilikwenda Brazil ikachukua kombe ambalo hakuna yeyote anayelijua, hata huko Brazil kwenyewe! Hii ndiyo Bongo bwana, ehe hamjui.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...