miss redds 2008 angela lubala (pichani na wazazi wake) amejivua taji hilo leo kwa kile kilichotajwa kuwa ni sababu za imani ya dini. meneja wa redds george kavishe atatoa tamko kuhusu hilo wakati wowote kuanzia sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hao "wazazi" walikuwa wapi mpaka mwanao ameanza mazoezi ya u-miss, ameenda kambini, ameingia kwenye shindano, ameshinda wao bado tu walikuwa hawajashtuka ama?????? Hii haimake sense hata kidogo unless walikuwa chini ya jiwe ndio wametoka huko na kumkuta binti keshakuwa miss.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza hapo juu...nionavyo mimi ni kwamba hao wazazi walichokuwa wanakitaka na kukitegemea ni binti kunyakua tawi la juu kabisa yaani awe mshindi wa kwanza....kuja kutaharuki binti anatangaza kilevi (hivi kwani REDDS ina kakilevi kidogo??).....sasa unafiki wa wazazi wa staili hii unaishiaga na kuumbuka...........otherwise Lundenga awe anawapima akili kwanza hawa candidates wake kabla hajawanadi.......kweli kama ndo umeshaingia contract na kuchukua hela za kampuni eti unawaletea mrembo wa kutangaza kinywaji chao na mambo ndo yanakuwa kama yalivyokuwa, hivi hiyo sura utaifichia wapi mtu mzima.......

    ReplyDelete
  3. Nilidhani Redds kinywaji ni non-alcoholic au? Kama ni non-alcoholic than imani za kidini zinatoka wapi? Au ni sababu nyingine ya kidini na sio kinywaji?

    Angeanzia kukataa wakiwa Mwanza ningeona ama kweli ana/wana msimamo kama sababu ni ya kidini na ni kinywaji anachokigomea. Lakini alishiriki Mwanza kwenye preliminaries, aliposhinda during Ms TZ alifanyiwa hafla na wazazi wake walikuwepo na picha Michuzi ulituwekea humu kijijini.

    Sasa how does this come-come? Please! TZ should forget this young lady no matter how cute she is as she or her parents or both are a waste of our time!

    ReplyDelete
  4. Nadhani huyu binti hakuwa na washauri wazuri hasa inapofikia wakati wa kutia sahihi na kukubaliana na mkataba husika. Mimi kama mwanasheria na ninavyojua ni kuwa ktk hizo karatasi au MKATABA kuna kifungu ambacho kinaeleza wazi kuhusu kupata USHAURI toka kwa watu wake wa karibu hasa ikiwa ni pamoja na wazazi na kadhalika. Sasa kama alipata ushauri kabla (prior advice from the related parties) hajasaini BASI hakutakiwa kuusaini kwani SUALA la IMANI alikuwa nalo hata kabla !!!! Mimi wasiwasi ni kwamba HUENDA washauri wake kabla ya kuusaini huo MKATABA walitegemea watapata FUNGU kubwa endapo bibie angeshinda !!! Na pengine ilikuwa si muafaka kuingia kabisa ktk MASHINDANO YA ULIMBWENDE ili akijua IMANI YAKE (ya UKIRISTO) haimruhusu kufanya hivyo !!!!!! Mimi kwa ushauri wa BURE ningewaomba waandaaji wa hili TAJI la REDDS wamsamehee huyu BINTI, kwani endapo wataamua kumfungulia mashtaka BASI HUYU BINTI HATAKUWA ANA NAFASI FINYU YA KUKWEPA HASARA ITAYOMPATA kwani bila shaka waandaaji wametumia pesa nyingi kumuandaa ikiwa ni pamoja na kuwapeleka MWANZA kwa maandalizi.

    USHAURI KWA WAZAZI/WALEZI:-
    ENDAPO UNAONA MWANAO HANA VIGEZO IKIWA NI PAMOJA NA KUKINGIZWA NA IMANI ZA DINI, BASI HAWANA BUDI KUWAKATAZA WATOTO WAO KUSHIRIKI KTK ULIMBWENDE !!!!

    Yangu ni hayo kwa leo. Otherwise, I stand to be corrected if and ONLY if am NOT along the rightful lines !!!

    ciao

    ReplyDelete
  5. Hakika hii ni picha nzuri ya familia yenye furaha. Sometimes you can judge the book by its cover. Na kuhusu binti kikubwa ni kuhakikisha you are in the same page and that she is ok.

    ReplyDelete
  6. You know what? Hapo ndio bongo tunahitajika kuelimika na kuwa na malawyer. Hivi hawakupewa mikataba hawa wakazoma na wakajua ni kipi kitakuja baada ya hapo? Yeye alipokua anava tembezwa huko mwanza na kote huko hakujua kuwa payback ni ipi na kwa muda gani?> this is just wastage of other time.
    Kwani alikua hajui redds ni nini kabla hajaingia hayo mashindano.

    Ni mimi waandaaji wa hayo mashindano tungemsue mpaka watu wajifunze.

    Hamna mikataba bongo mpaka leo.

    ReplyDelete
  7. mtu mwenye imani za dini asingeshiriki u miss,ila kama anayake

    unaambiwa kuwa kwa MUNGU hakuna mbaya wote tuko sawa sasa alianza vipi kujiona yeye mrembo?

    hata hivyo wamemsaidia tu ila yeye anafanana sana na baba yake mbona baba yake hajashiriki urembo?

    wazazi acheni tamaa!!

    ReplyDelete
  8. Ondoa uanasheria wako. Si kila mkataba una hicho kifungu chako. haya ndiyo matatizo ya elimu yetu Tanzania. Huyu msichana ni mzuri, kwa hiyo msifuatefuate, ana haki yake kufanya kila atakalo bila kuvunja sheria. Mtoto mzuri weye wasikutishe.

    ReplyDelete
  9. HAPO NDIPO MNAONA KIWANGO CHA ELIMU CHA HUYU DADA.
    DINI NI HISTORIA, VITABU NA HADITHI ZOTE ULIMWENGU VINAANDIKWA NA MAPAPARAZI KAMA MICHUZI VILE.
    POLE SANA DADA WAZAZI WAKO INABIDI WAKULIPIE SANA UENDE HATA ELIMU YA WATU WAZIMA WALLAH!

    ReplyDelete
  10. JAMANI HAWA WATOTO WANATUCHEZEA AKILI INABIDI WASHIKISHWE ADAMU.TUWASHITAKI GHARAMA ZOTE ZILIZOTUMIKA ZILIPWE NA CHAJUU PIA. KAMA WALIOTOA PESA ZAO KUMGHARAMIA HAWANA UCHUNGU NA HIZO PESA ITABIDI TUCHUNGUZE SOURCES YA MAPATO YAO KAMA WANALIPA KODI ZOTE NA KUPATA ZIADA YA KUCHEZEA. HAIINGII AKILINI MTU KAPITIA STAGES ZOTE THEN SASA ANASEMA DINI. AMEWAZIBIA WENGINE AMBAO WANGEPATA HIIYO CHANCE. HIYO PICHA ALIYOPIGA NA WAZAZI WAKE NI YA LINI?KAMA NI SIKU HIYOHIYO KWANINI WALIPIGA PICHA NAYE?

    ReplyDelete
  11. Please please nyie hamna dini??UPAKO hauchagui muda.Amebahatika amepata UPAKO sasa.
    Mrembo uamuzi wako wa Kumtangaza YESU itakujengea HAZINA KUBWA MBINGUNI.Pombe ni dhambi.Ubarikiwe

    ReplyDelete
  12. Jamani this lady was on S&C magazine sikumbuki mwezi ila ni ya 2006 tena on the cover with subject "Future Tanzanian model". By that time alikuwa na 16 years only na alivyoandika maelezo yake ni kwamba alipokuwa na miaka 2 yeye na familia yake walihamia USA ambako alikaa huko mpaka alipokuwa na miaka 16 ndo akarudi bongo. Alitaka kugombea umiss ili awe Miss Tanzania na amtangaze yesu kwa kutumia taji lake. Na wazazi wake walikuwa wanam-support for that. Kwahiyo alikuwa anasubiri afikishe miaka 18 ndo aingie mashindanoni. So jinsi naweza judge here ni kwamba matarajio yake ya kuwa Miss Tanzania hayajafikiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...