baada ya kumaliza kwikwi ya blogu ya jamii nimeamua kuchukua vekesheni ndogo na kuelekea makao makuu, dodoma. nikiwa njiani nikakutana na machweo ya jua nikiwa naingia karibu na kibaigwa. nikawawaza wadau na kusimama ili nikamate machweo na kuwapa zawadi wadau kwa kuendelea na libeneke kama kawa. mdau yeyote ana ruhusa kutumia picha hizi atakavyo bila gharama wala kuomba ruhusa ikiwa ni kama zawadi yangu kwenu na shukurani kubwa kwa kuendelea kuniunga mkono maradufu ya awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kwa wasiojua utaalamu ktk kupata picha kama hizo wanaweza kuona ni kitu rahisi saana ( na anayebisha achukue ki-point and shoot chake na hata li-SLR aende aone kama hajajaza card ya 4GB bila kupata picha za hivi. Lakini nasema tena na tena Kaka unatisha na najivunia kuwa mwanafunzi wako. Naja japo kwa speed ya jongoo, lakini naamini "SIKU MOJA NDIO" (One day yes)ntafika ulipo. Hii ni zaidi ya zawadi kwa ma-rookie wa upigagi picha. Ni kama homework. Ni changamoto kwa sie na naweza sema tangu umeanza kutoa zawadi, hii ni ya ki-kwelikweli kwangu.
    Heshima kubwa kwako Kaka
    M.T.B

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi

    These are wonderful scenes captured. Umeonyesha kuwa hubahatishi na ni weledi katika sanaa ya kupiga picha. Fagiliaaaa...!!!

    Wasalaam

    ReplyDelete
  3. Hizo picha kwa mtu ambaye hana ile kitu inaitwa 'photo appreciation', basi hawezi kujua na kupata uhondo wa picha hizo.
    the photos are beautiful. good work of your camera tricks and good use of the opportunity (time of the day).
    obstruction ndogondogo (electric Pole na kichaka) ndio zimepunguza ukali wa picha lakini all in all zimekaa poa!

    ReplyDelete
  4. WOW! Kaka nimekuvulia kofia, picha nzuri sanaaaaa. Hongera

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi, hii ni kwa manufaa yangu tu ili niweze kuelewa. I love the photos ambazo hazina Milingoti na nyaya za simu/umeme(?). Zenye milingoti zinaongeza nini hasa kwenye uzuri wa picha?

    Picha namba sita ndiyo nimeipenda saaaana.

    ReplyDelete
  6. Bravo Michuudh!Mimi niliwahi kuwa Painter in those Old Good Dayz!When Artistry in this country meant nothing to our 'Politicians'!Labda Uimbe Kwaya.Hizi picha ni mali kwelikweli kwa Colour Painters nakwambia!This is a Nude Photograph of the 'Environment'!Lovely Natural Beauty of the Naked!environment ofcourse,ulidhani nini?Umesemaje? tehe tehe tehe tehe... najua nimeanza kuamsha hisia za majemedari.....tehe!Kazi nzuri Michuz na we unajua kitu kizuri.

    ReplyDelete
  7. Mimi nakushauri Michuuuz,wewe kama Professional Photographer,umeshadhihirisha Umahiri wako,basi kwa picha kama hizi na zingine pengine za wanyama na viumbe vya porini,za makazi na shughuli za watu katika uhalisia wa mazingira yao na zinginezo tele,FIKIRIA SIKU MOJA KATIKA MWAKA uwe unafanya ANNUAL MICHUZ PHOTO EXHIBITION utayaona matunda yake!This is very personal.Ukitaka ushauri vipi utavuna jasho lako nitafute kwa muda wako mjomba nimejaa tele sina hiyana!But I know for sure you can make it in Life in a very Big Way!Na hiyo itakusaidia kuwa na malengo katika upigaji wako wa picha katika mwaka!Time is so Precious Michuz dear!If you know what Um Sayiiing!Ukipanuka zaidi vivyo hivyo ndivyo utakavyoweza kufanya Photo Gallery hata za Kimataifa katika World Capitals! Na ukipata mashabiki wa picha zako ambao wana kipaji cha Oil Painting utakuja niambia!GoodLuck!

    ReplyDelete
  8. jamani kaka michuzi picha nzuri mno.

    ReplyDelete
  9. Bro Michuzi, jaribu kuwasiliana na Modern Art Museum iliyopo Amsterdam. Nina uhakika utafanikiwa mzee na siongelei picha hizi tu; una picha lukuki mzee.

    Nilipotembelea pale niliona picha chache kutoka Afrika; nyingi zilikuwa zinatoka Afrika Kusini. Lakini hakuna picha zozote kutoka East African au Bongo. Jaribu mzee..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...